Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,447
- 7,832
Leo kutoka ofisi za chama cha mapinduzi Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi, Humphrey Polepole anaongea kuhusu mambo yaliyojadiliwa kwenye kikao cha kamati kuu kilichoketi jana mjini Dodoma, kuwa nami..
=======
Polepole: Sisi kama chama mapinduzi tunawaahidi watanzania tutachapa kazi kuliko hata muhula uliopita, CCM kiko mstari wa mbele kuisimamia Serikali kuhakikisha yote tuliyowaahidi tunatekeleza. Tuna siku 1825 na hatuna muda wa kupoteza.
Siku ya jana iliketi kamati kuu ya halmashauri kuu Taifa ya CCM chini ya uenyekiti wa John Magufuli jijini Dodoma makao makuu ya chama na Serikali. Kwanza imetoa pongezi nyingi sana kwa ndugu Hemedi Suleiman Abdullah, makamu wa pili wa Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.
Pia siku ya jana uteuzi wa baraza la mawaziri na kama kauli ya Rais ya Magufuli ameendelea kusisitiza , tuna kazi moja tu kwa watanzania kwa kipindi hiki, kuchapa kazi, kuwapatia utumishi uliotukuka ili tuweze kulipa deni kubwa ambalo watanzania wametupatia katika uchaguzi huu wa mwaka 2020.
AGENDA
POLEPOLE: Ndugu watanzania msihangaishwe na kauli za hapa na pale, vikauli kauli hivi vya kuonesha kana kwamba, haya mambo ni ya kupuuza, sasa hivi tunataka tuchape kazi. Tuna kazi ya kuzalisha ajira nyingi(Milioni 8). Tuko vizuri mno, tunathamini marafiki wetu wote kama Taifa la Tanzania, tunawaheshimu na kuwapenda na tunatarajia na wao pia watuheshimu na kutupenda sisi kama Taifa huru na linalojitegemea.
Tutaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kama ambavyo tumeainisha kwenye ilani ya CCM katika eneo la mahusiano ya kimataifa, tuna kazi kubwa ya kuimarisha sekta binafsi, kujenga uchumi imara, himilivu lakini pia jumuishi kwa maana hiyo mahusiano ya kimataifa kwetu jambo la msingi sana lakini tunafanya hivyo tukiangalia maslahi mapana ya Tanzania kwanza na yasiyokwenda kinyume na tamaduni zetu, taratibu zetu na desturi.

- Kuthibitisha wa uteuzi wa wagombea wa nafasi za Meya wa jiji, Tanzania bara majiji sita
- Meya wa manispaa 20 za Tanzania Bara
- Wagombea wa nafasi za uenyekiti wa halmashauri za wilaya 137 za Tanzania Bara
- Kuthibitisha uteuzi wa nafasi za wagombea wa wenyeviti wa halmshauri za miji 22 Tanzania bara