Hivi kuna Mtanzania mzalendo kama Humphrey Polepole?

Huyu jamaa ni mzalendo kweli wa nchi yake japo ni chama cha mapinduzi lakini ni mzalendo

Hawa ni aina ya CCM ya kina Nyerere yaani wale wanaccm wenye uzalendo na utaifa na walobaki nchini

Kiukweli I declare interest kwamba namkubali Polepole sana

Hii nchi inahitaji kina Polepole kama 50 hivi

Huyu alitakiwa awe Waziri kabisa au mshauri wa Rais

Kwa hizi hoja kuna wa kumpinga huyu Jamaa? Anzia dk ya 14 hapo l's ?

Namheshimu kwa kuhifadhi msimamo. Sio wengine waliyobadilika kama vinyonga. Mwanzo tu pale kuona sabaya akitemwa wakashikwa na ganzi na kumtafsiri mama kwa kubahatisha au kwa uhakika. Wengine wakaanza kuomba msamaha etc mradi wasije fukuzwa mezani kula. Polepole anakeep on fighting kwa ideas za kutukuka na kubeba juu bendera ya ccm ya siasa ya ujamaa na kujitegemea bila hofu.
 
Hivi kuna Mtanzania mzalendo kama Humphrey Polepole?

Huyu jamaa ni mzalendo kweli wa nchi yake japo ni chama cha mapinduzi lakini ni mzalendo

Hawa ni aina ya CCM ya kina Nyerere yaani wale wanaccm wenye uzalendo na utaifa na walobaki nchini

Kiukweli I declare interest kwamba namkubali Polepole sana

Hii nchi inahitaji kina Polepole kama 50 hivi

Huyu alitakiwa awe Waziri kabisa au mshauri wa Rais

Kwa hizi hoja kuna wa kumpinga huyu Jamaa? Anzia dk ya 14 hapo l's ?

Tatizo la Polepole ni kwamba alijiwekea doa jeusi sana kwenye mchakato wa katiba mpya!! Kabla ya hapo alikuwa anang'aa sana kwenye harakati za jukwaa la katiba. Lakini baadaye akakubali kuuza uaminifu wake kwa bei ya "kukubalika" kwenye chama!! Vinginevyo kama atakuwa ameligundua kosa lake, na kujisahihisha kama inavyoelekea watanzania watamsamehe japo kwa sasa bado sana!! Polepole alitusaliti!! Tuko tayarj kumsamehe kama tukijiridhisha kuwa kwa sasa anatambua kuwa mtaji wake kubwa ni wananchi wala siyo chama!! Haimaanishi kuwa atoke ccm la hasha, ila inapotokea mgongano kati ya maslahi ya chama na maslahi ya wanananchi aegemee kwenye maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla!! Kama alivyoonesha msimamo wenye kufikiria maslahi ya Taifa kwenye suala la chanjo za covid19. Yaani kutumia mabilioni ya shilingi kwenye chanjo isiyoweza kumkinga mtanzania hata kwa mwaka mmoja tu haina maslahi kwa taifa!!! Ni wizi sawa na wizi mwingine tu!!
 
Back
Top Bottom