Hukumu ya Lengai Ole Sabaya yaahirishwa hadi Juni 10, 2022

Arusha. Swali kuu leo ni je, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita watashinda kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili na kuachiwa huru?

Majibu ya swali hilo yanatarajiwa kutolewa leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha pale itakapotoa hukumu yake baada ya kusikiliza kesi hiyo dhidi ya Sabaya na wenzake sita, kwa muda wa miezi saba tangu ilipoanza Julai, 2021.

Hatima ya Sabaya inasubiriwa kwa hamu na watu wengi kufuatilia umaarufu alioupata wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro na hata baada ya kutenguliwa na kushtakiwa.

Hukumu ya leo inatarajiwa kuamua hatima ya kiongozi huyo wa zamani na wenzake endapo wataachiwa huru, kwa kuwa baada ya kesi hii hawana nyingine iliyosalia mahakamani.

Sabaya alikamatwa Mei 27, mwaka jana wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, na kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani Juni 4, 2021 na kufunguliwa kesi mbili tofauti.

Katika kesi ya kwanza walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, hukumu ambayo Mei 6, 2022 ilitenguliwa na Mahakama Kuu na kuwaachia huru baada ya kubaini dosari zilizojitokeza katika mwenendo wa kesi ya msingi katika mahakama ya chini.

Rufaa hiyo ilikatwa na Sabaya na wenzake wawili, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, wakipinga hukumu ya kifungo iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma aliyekuwa akisikiliza rufaa iliyokatwa na Sabaya na wenzake, alisema mahakama inabatilisha mwenendo wa kesi ya msingi na kutengua hatia dhidi ya warufani hao na adhabu iliyotolewa dhidi yao inatupiliwa mbali.

Katika kesi ya uhujumu uchumi inayotarajiwa kutolewa hukumu leo, mbali na Sabaya watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2021, Jamhuri ilikuwa na mashahidi 13 huku upande wa utetezi ukiwa na mashahidi nane.

Washtakiwa hao walikuwa wakitetewa na jopo la mawakili watano huku mmoja wa washtakiwa, Mwahomange akijitetea mwenyewe.

Machi 31 mwaka huu Hakimu Mkazi Mwandamizi Patricia Kisinda aliyekuwa akisikiliza shauri hilo la jinai, alisema atatoa hukumu hiyo leo baada ya pande zote kuwasilisha hoja zao za majumuisho.

Chanzo: Mwananchi

====

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Leo Mei 31, 2022 imeahirisha Hadi tarehe Juni 10, 2022 hukumu ya Kesi ya Uhujumu uchumi Namba 27 ya Mwaka 2021 inayomkabili Aliyekuwa Mkuu Wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na Wenzake sita kutokana na Hakimu Aliyekuwa akiendesha Shauri Hilo kupangiwa Majukumu Mengine ya kiofisi nje ya Mkoa.

Uamuzi huo umetangazwa na Hakimu Mfawidhi Wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Fadhil Mbelwa na Kueleza kuwa Hakimu Aliyekuwa anasikiliza Shauri Hilo yupo kwenye Majukumu Mengine.

Shauri Hili lipo Chini ya Hakimu Mkazi Mahakama hiyi Dkt Patricia Kisinda. Katika Shauri hili Sabaya ameshtakiwa na wenzake kwa Makosa ya kuomba na Kujipatia Rushwa ya Kiasi cha Shilingi Milioni 90 kutoka kwa Mfanyabiashara Francis Mroso Makosa ambayo yanadaiwa kutendeka Januari 22 Mwaka 2021 Jijini Arusha.
 
Arusha. Swali kuu leo ni je, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita watashinda kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili na kuachiwa huru?
Majibu ya swali hilo yanatarajiwa kutolewa leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha pale itakapotoa hukumu yake baada ya kusikiliza kesi hiyo dhidi ya Sabaya na wenzake sita, kwa muda wa miezi saba tangu ilipoanza Julai, 2021.
Hatima ya Sabaya inasubiriwa kwa hamu na watu wengi kufuatilia umaarufu alioupata wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro na hata baada ya kutenguliwa na kushtakiwa.
Hukumu ya leo inatarajiwa kuamua hatima ya kiongozi huyo wa zamani na wenzake endapo wataachiwa huru, kwa kuwa baada ya kesi hii hawana nyingine iliyosalia mahakamani.
Sabaya alikamatwa Mei 27, mwaka jana wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, na kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani Juni 4, 2021 na kufunguliwa kesi mbili tofauti.
Katika kesi ya kwanza walihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela, hukumu ambayo Mei 6, 2022 ilitenguliwa na Mahakama Kuu na kuwaachia huru baada ya kubaini dosari zilizojitokeza katika mwenendo wa kesi ya msingi katika mahakama ya chini.
Rufaa hiyo ilikatwa na Sabaya na wenzake wawili, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, wakipinga hukumu ya kifungo iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.
Jaji Sedekia Kisanya wa Mahakama Kuu Kanda ya Musoma aliyekuwa akisikiliza rufaa iliyokatwa na Sabaya na wenzake, alisema mahakama inabatilisha mwenendo wa kesi ya msingi na kutengua hatia dhidi ya warufani hao na adhabu iliyotolewa dhidi yao inatupiliwa mbali.
Katika kesi ya uhujumu uchumi inayotarajiwa kutolewa hukumu leo, mbali na Sabaya watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.
Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2021, Jamhuri ilikuwa na mashahidi 13 huku upande wa utetezi ukiwa na mashahidi nane.
Washtakiwa hao walikuwa wakitetewa na jopo la mawakili watano huku mmoja wa washtakiwa, Mwahomange akijitetea mwenyewe.
Machi 31 mwaka huu Hakimu Mkazi Mwandamizi Patricia Kisinda aliyekuwa akisikiliza shauri hilo la jinai, alisema atatoa hukumu hiyo leo baada ya pande zote kuwasilisha hoja zao za majumuisho.
Source: Hukumu ya kina Sabaya leo | Mwananchi
Insideten vipi?
 
Je
20220210_042641.jpg

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
wadau tunaisubiri hii hukumu isomwe kwa hamu,wapo tunaomtakia kheri bwana sabaya ,na wapo tunaomtakia abaki rumande ,Kama tu ilivyokuwa kwa mbowe !!

Waisome jamani ili hili nalo lipite,maisha yaendelee !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu shetani apite na wewe ili ufanye kosa uwe kama jamaa

Usifurahie mateso ya mwenzio muombee mema
Hukumu anatoa Mungu tu
 
Back
Top Bottom