Hukumu ya Lengai Ole Sabaya yaahirishwa hadi Juni 10, 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,456
Sabaya.jpeg

Hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita inatarajiwa kusomwa leo Mei 31, 2022 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Kesi hiyo imeendeshwa tangu ilipoanza Julai, 2021.

Hukumu hiyo inatarajiwa kuamua hatima ya kiongozi huyo wa zamani na wenzake endapo wataachiwa huru, kwa kuwa baada ya kesi hii hawana nyingine iliyosalia Mahakamani.

UPDATE: HUKUMU YAAHIRISHWA HADI JUNI 10

Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha imeahirisha hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita kutokana na Hakimu kuwa na majukumu mengine.

Akiahirisha kesi hiyo leo Jumanne Mei 31, 2022, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Fadhil Mbelwa amesema shauri lilipangwa kwa ajili ya hukumu ila hakimu aliyekuwa akiisikiliza amepangiwa majukumu mengine ya kikazi nje ya ofisi.

"Shauri linakuja kwa ajili ya hukumu na liko kwa Hakimu Mkazi Mwandamizi, Patricia Kisinda lakini siku ya leo amepangiwa majukumu mengine ya kikazi nje ya ofisi hataweza kutoa hukumu leo hadi Juni 10, 2022," amesema Hakimu huyo

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27/2021, mbali na Sabaya watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Leo Jamhuri iliwakilishwa na Mawakili wa Serikali waandamizi Janeth Sekule, Felix Kwetukia, Wakili wa Serikali Neema Mbwana na Mwendesha Mashitaka wa Takukuru, Jacopiyo Richard.

Utetezi uliwakilishwa na Mawakili Mosses Mahuna, Fridolin Bwemelo, Edmund Ngemela na Sylvester Kahunduka ambao wanawatetea washitakiwa sita isipokuwa Mwahomange ambaye anajitetea mwenyewe mahakamani hapo

Chanzo: Mwananchi
 
Kwa double standard za hii nchi, haitashangaza akiachiwa huru! Na wakati dogo alikuwa ni haramia na jambazi sugu.
 
View attachment 2245261
Hukumu ya kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita inatarajiwa kusomwa leo Mei 31, 2022 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Kesi hiyo imeendeshwa kwa muda wa miezi saba tangu ilipoanza Julai, 2021.

Hukumu hiyo inatarajiwa kuamua hatima ya kiongozi huyo wa zamani na wenzake endapo wataachiwa huru, kwa kuwa baada ya kesi hii hawana nyingine iliyosalia Mahakamani.
Dua yangu ni kumuombea aachiwe huru.
 
Kumbukeni Sabaya alikuwa nani kabla ya kuwa mkuu wa wilaya, Baada ya hapo utapata jibu la kinachoenda kutokea kwenye hukumu ya leo.
Kilichotafutwa tayari kilishapatikana, hivyo basi si ajabu sana Sabaya akiachiwa huru.
 
Mahakama ndio yenye mamlaka ya kutoa hukumu baada ya kupitia all vivid evidence,

Tuheshimu Maamuzi ya Mahakama.
 
Yule aliibia nchi kupitia watawala wa wanasiasa wa ccm. Sabaya amewaibia raia wenzake wanao pambana kila siku juani kujitafutia riziki.
Kwaiyo kuibia nchi siyo kubaya zaidi ya kuibia raia mmoja mmoja isijekuwa baba yako aliuza ng'ombe kukusomesha kumbe kauza ng'ombe kusomesha ng'ombe
 
Back
Top Bottom