Huku ndoa yake ikipumulia mashine, Jack Wolper apata bwana mpya!

Nifah

JF-Expert Member
Feb 12, 2014
31,530
65,286
IMG_4163.jpeg
Ndoa ndoano! Mambo sio mambo!

Muigizaji aliyegeukia biashara, mwanadada Jackline Wolper Massawe ‘Wolper’ inaripotiwa kupata bwana mpya baada ya ndoa yake kukumbwa na sintofahamu nyingi.

Ikumbukwe Wolper alifunga ndoa takatifu na aliyekuwa baba wa mtoto wake Richard ‘Rich Mitindo’ 19/11/2022.

Wawili hao walioonekana kuwa na huba la moto, shatashata lililokolea nazi enzi za uchumba wao uliopelekea Wolper kufikia uamuzi wa kumzalia kabisa mtoto Rich hata kabla ya kufunga ndoa.

Mara nyingi walionekana wenye furaha na mapenzi tele, wakipop champagne kila uchwao na kushona sare!
Wambea na wenye husda walinyanyasika vya kutosha!

Jinamizi liliyasogelea mapenzi yao baada ya kufunga pingu za maisha, na Wolper kubarikiwa mtoto wa pili.

Ilianza kuripotiwa ndoa kuingia mdudu baada ya mumewe kuonekana akila maraha China, mbaya zaidi kwa kipindi kirefu aliendelea kubaki huko bila kurejea nchini ilipo familia yake kitendo kilichozua minong’ono!

Wolper alishindwa kujizuia, akaanza kuongea mengi ya uchungu hata alipopata nafasi ya kuhojiwa na waandishi aliongea ambayo wengi waliyatafsiri kama alama nyekundu ktk ndoa yao.

Baada ya kipindi kirefu cha mumewe kuwa nje ya nchi, ni wazi Wolper uvumilivu umemshinda nae kaamua kujipa ‘raha’ kwa kutoka kimapenzi na mwanaume anayefahamika kama Vincent Azrone almaarufu G Nex.

Mwanaume huyo imebainika kuwa ni meneja katika ukumbi maarufu wa starehe, Havoc Night Spot uliopo Masaki jijini Dar Es Salaam.

Wapenzi hao wameonekana mara nyingi pamoja, hadi katika sherehe ya kuzaliwa kwa mwaume huyo, wawili hao walikaa pamoja bila kificho!

Taarifa za uhakika ni kwamba G Nex yeye bado hajaoa, na kiumri anaonekana mdogo kuliko Wolper.
Mara nyingi ameonekana akiwa anaendesha gari yake Toyota Crown nyeusi.

My take; Wolper, najua ilivyo vigumu kuishi ktk stress za mapenzi na ndoa kwa mwanaume asiyeeleweka.

Sitaki kukuhukumu kwamba ulikosea kuolewa na kijana mdogo kwako kiumri ambaye damu bado ya moto anahitaji kufanya mengi kama ambavyo wewe ulifanya kwa wakati wako…

Nakuombea kheri, haya yawe ni mapito mpate kuyaweka sawa na mumeo, ndoa na iheshimiwe na watu wote!

Pichani ni mpenzi mpya mjini wa Jack Wolper, Vincent Azrone ‘G Nex’

Wenu katika ubuyu,

Nifah.
 

Attachments

  • c3c7f4fc-df22-4532-8a5e-ff5e1d0fe602.jpeg
    c3c7f4fc-df22-4532-8a5e-ff5e1d0fe602.jpeg
    70 KB · Views: 18
  • e3018bc4-9fa5-4e6a-b981-ef15cc5f5f33.jpeg
    e3018bc4-9fa5-4e6a-b981-ef15cc5f5f33.jpeg
    65 KB · Views: 9
  • 0b71a258-b44b-4655-ad9f-90ffbedd8402.jpeg
    0b71a258-b44b-4655-ad9f-90ffbedd8402.jpeg
    52.7 KB · Views: 15
Baada ya kipindi kirefu, nimeweka thread hii ya ubuyu katika jukwaa hili kama sehemu ya kumuenzi rafiki & binamu yangu warumi

Endelea kupumzika kwa amani binamu, niko hapa kuendeleza kile ulichokuwa unakipenda zaidi hapa JF.

Hadi tutakapoonana tena, RIP!
 
Hivi akitafuta kamtu 'kyake' kamemzidi umri kiasi, akapendwa vizuri, akadekezwa, mtu ambaye hana umaarufu wowote, hatopata amani kweli..??
Una akili sana!
Hili ndilo swali huwa najiuliza hadi kwa Jokate…

Wanawapendea nini watu maarufu wenzao? Wote ni wazuri, lazima kuna wanaume decent kibao wanawataka, kwanini wasichague kutulia wakaachana na hizo hekaheka za wanaume maarufu?

Siku wakija kuzijua raha tunazozipata kwa hawa wanaume low key, waliotuzidi umri kiasi watalia kwa kuchelewa!
 
Back
Top Bottom