Unaiona wapi ndoa miaka 50 ijayo

Dr criminal

JF-Expert Member
May 16, 2022
2,278
4,273
Niajeeeeeee

Naskia rangi ya majani mabichi na manjano wameanza kukusanya magaidi uko mtaaani,,wataenda kujibu kwa mwenyezimungu siku moja wallah!


Kuna vitu vya kuogofya sana vinasemwa au kufanywa na watu wakaidaaa sana mpaka unajiuliza "hili wazo la kishetani namna hii huyu kalitoa wapi",,kuunda hoja against the mighty we ni jasiri au mpumbavu kiasi gani?

Nilikuwepo wakati mwanamke alikuwa yupo tu nyumbani analea familia, baba mtaani anaitafutia familia, watoto shuleni wanaelimika, jioni wanakutana baada ya hadithi, story na homework Kila mtu anaenda kulala.

Nilikuwepo wakati mwanamke ananyanyua sauti yake kusema "mwanamke sio chombo cha starehe"," mwanamke hakuumbwa hakae tu nyumbani",,"haki sawa"

Nilikuwepo wakati serikali inatunga sheria ya kumkingia kifua mwanamke na kumpa namna nyepesi zaidi yakuifikia dola ikiwa kanyanyaswa na mwanaume

Na juzi wakati napeluzi katika moja ya mtandao wangu pendwa wa kijamaa nikakutana na bango linasomeka "Tunafanyia kazi sheria ya mwanamke kulipwa na mumewe"

Yani kufumba na kufumbua tu ndoa sio makabiliano ya watu wawili na familia zao tena, ndoa ni kazi kwa mwanamke kama kazi zingine

Naanza kuhisi kwamba Kuna siku yaja ambayo mimi nawaeza kuwepo au nisiwepo ila hii ndoa hii haitokuwepo na nna uhakika sio mbali sana kutoka leo

Lakini ukiwa makini kwenye hili wimbi linalotingisha meli kwa jina la ndoa ni kama linatingisha vitu vingi sana kwa pamoja, yani kama mafuriko ambayo hayaachi kitu.

Mapenzi ya jinsia moja, kubadili jinsia, ndoa za jinsia moja, watoto wa kujiamulia jinsia zao wakishazaliwa, shule za vindagateni kufundisha watoto wetu ufuska,,,huu ugonjwa wa mlipuko no body is safe.

So, unaweza ukae ukajiuliza, haya mambo yote yametokea wapi?, nani yupo nyuma ya haya yote? nani anafaidika nini kwenye haya yote? unataka kusema viongozi wa mataifa makubwa ndo wamelukwa na akili hivi? unataka kuniambia wanawake wetu ndo vipofu hivi? unataka kuniambia serikali zetu ndo zinaongozwa na machizi kiasi hiki?

Mi siioni ndo miaka 50 ijayo kwa sababu

Unachotakiwa uelewe aliyeko nyuma ya jambo hili lengo lake sio kumkomboa mwanamke, hapana yeye lengo lake na kuifuta hii taasisi ya ndoa na sababu ni moja tu, tupungue "depopulation"

Sasa kwenye hizo harakati since day one huwaga hapitii kwa mwanaume kwasababu ni ngumu kumlang'ai mwanaume kwahiyo alipitia kwa mwanamke jana atapitia kwa mwanamke Leo na atapitia tena kwa mwanamke kesho

Muda wote huu mwanaume ameendelea kusimama imara kuhakikisha ndoa haipotei, tumeendelea kupoteza mali nyingi sana wanaume kwa sheria za kijinga za ndoa, wamefungwa wanaume wengi bila hatia kwa sheria za kijinga juu ya mwanamke

Kuna siku wanaume watachoka, Kuna siku yaja wanaume wataona imetosha, na hiyo siku sio mbali sana kutoka leo.

Ushauri wangu
Mkipata wasaha kaeni na wanawake muwaelimish e kwamba wanachokipigania sicho wanachokiitaji, wamepelekwa vitani kama vipofu hawajui wanampiga nani.


 
Maelezo ni mengi sana ila ingesema tu hakuna jipya chini ya jua, yote yanayofanyika alikuwepo sema tu kila jambo na wakati wake, upo wakati wa mama mkwe kuvaa chupi na sindiria mbele ya mume wa binti yake.

Upo wakati wa hao kupiga French kiss hadharani. Hayo yote tunayaona hapa hapa ktk nchi ya Samia hivyo hakuna jipya.
 
Una hakika Wanaume Wamesimama Kuitetea ndoa..?

Haya Makampeni ya 'Kataa ndoa Unayaelewa'..!

Kuna baadhi unaeleweka Kuna nguvu Kubwa Sana inatumika Kuhakikisha hii taasisi ya ndoa inasambaratika Juu ya uso wa Dunia...!

Shetani mbaya Sana...!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom