Huenda Mwenyezi Mungu sasa katuchoka Wanaume na ameamua kuwainua Wanawake katika nyadhifa kubwa za kiuongozi Duniani ili tujifunze kwao

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,877
Huko Marekani kwa mara ya Kwanza katika Historia yao Makamu wa Rais wa sasa ni Mwanamke Kamala Harris.

Nchini Tanzania kwa sasa na haikuwahi kutokea Rais wa nchi ni Mwanamke Mama Samia Hassan.

Huko nchini Kenya pia katika Historia yao kwa mara ya Kwanza leo imempata Jaji Mkuu Mwanamke Martha Koome.

Katika Maisha ya sasa (tena huku Vyuma vikiwa Vimekaza) ila cha Kushangaza Wanawake wanazidi tu kuwa na Uchumi mkubwa na Sisi Wanaume tunadidimia tu.

Huenda kuna mahala Wanaume tumefeli na huenda hata Baba Muumba (Mwenyezi Mungu) nae katuchoka vile vile hivyo anatukomesha sasa Kiaina.

Nawapongeza Wanawake wote duniani.
 
Toka muda imekuwa hivyo labda hukufuatilia mapema! Wamekuwepo.

Theresa May, Dilma Rousseaf, Sheikh Hasina Wazed, Tsai Ing-wen, Jacinda Kate Laurell, Bidhya Devi Bhandari, Kolinda Grabar-Kitarović, Angela Merkel, Ana Brnabić, Saara Kuugongelwa, Hilda Heine, Zuzana Čaputová kwa uchache na wengi wao wamefeli vibaya mno.
 
Toka muda imekuwa hivyo labda hukufuatilia mapema! Wamekuwepo,

Theresa May, Dilma Rousseaf, Sheikh Hasina Wazed, Tsai Ing-wen, Jacinda Kate Laurell, Bidhya Devi Bhandari, Kolinda Grabar-Kitarović, Angela Merkel, Ana Brnabić, Saara Kuugongelwa, Hilda Heine, Zuzana Čaputová kwa uchache na wengi wao wamefeli vibaya mno.
Ila kwa sasa wameibuka kwa Kasi sana.
 
Next US President atakuwa mwanamke, Nikki Haley

Tunzeni hii post
Kwa Marekani ukisikia mwanamke si lazima awe biological female yaani si lazima awe ni mwanamke wa kuzaliwa! Ni midume imeamua kuwa mijike na kufanyiwa upasuaji na kunyweshwa hormone za kike.

Kuna dume moja lilikuwa linaitwa Michael, likaamua kuwa jike na likaolewa na MTU aliyekuja kuwa mtu mkubwa sana!
 
Kwa marekani ukisikia mwanamke si lazima awe biological female yaani si lazima awe ni mwanamke Wa kuzaliwa!! Ni midume imeamua kuwa mijike na kufanyiwa upasuaji na kunyweshwa hormone za kike.
Kuna dume moja lilikuwa linaitwa Michael, likaamua kuwa jike na likaolewa na MTU aliyekuja kuwa MTU mkubwa sana!!
Acha uongo, alizaa vipi wale mabinti.
 
Mungu aliwapa wanaume kazi ya kutawala kwa niaba yake lakini hatutawali kwa niaba ya Mungu bali yetu. Tumekuwa majizi, wabinafsi, waongo, wazinzi, na wakatiri. Kazi yetu ni kuzalisha wanawake na kukataa mimba na kuligeuza tendo la ndoa kuwa starehe. Tuko bize kutafuta nguvu za kiume, uchi imekuwa ibada yetu.

Tunawatawala watu kwa nguvu bila kujali utu, hata kumwasi Mungu.
 
Back
Top Bottom