Huawei tayari wamekamilisha Operating System (OS) yao

Huawei tayari wamekamilisha Operating System (OS) yao

Akili za watu zimefinywa zikafinyika. Wanachodhani wao it's all about kutengeneza na kuuza, hizo other factors wala hawaziangalii. Nakumbuka tangu miaka ya katikati ya tisini katika report yao, CIA walisema kwa hali ilivyo kama mchina hatapigana vita yoyote ile basi itamchukua miaka nane (8) kuwa namba tatu kiuchumi Duniani. Then, miaka ya elfu mbili CIA walisema kabla ya 2016 kama hali itabaki hivi basi China atakua namba 2 kiuchumi duniani.
Hii najaribu kuonyesha jinsi watu wanavyofuatilia mambo, mbinu na mikakati ya mchina watu wanaijua, yote ipp mikononi maana wanajua exactly pale itakapo mfikisha. Hivyo hawakuwa mafala, walitengeneza nikakati ya kufaidika naye halafu baadaye waje ku m contain na kumfifisha kabisa. China hataweza kufika anakodhani anaelekea, Uingereza hakuwa fala alipomkabidhi Hong Kong ambao hadi leo hawataki kujiona kuwa wao ni sehemu ya China.
Kuna Macau, kuna Taiwan kuna Tibet. Hizi zote ni special projects dhidi ya Mchina, ni timing bombs.
Mchina amesha kuwa contained, hana tena ujanja.
Watu si wajinga wanapo invest heavily kwenye maswala ya Research and Intelligence, si wajinga hata
Mkuuu kwenye nyanja za ujasusi mambo hayapo linear hivyo, kunawakati mnachukua maamuzi mkitegemea atafanya hivi ili akwame badae anatoka kitofauti. Mimi nadhani wachina watatoboa tu kwa maana nao kuchukua maamuzi ya kugoma kuwapigia magoti USA wamepiga mahesabu yao ya Inteligensia yao. Nakukumbusha kuwa USA kumuwekea vikwazo mchina kutamgarimu sana kwa sababu nae sasa anafanya nae kazi kwa jeuri na anaungana na maadui wake wengine hadharani na kufanya nao biashara bila kufuata vikwazo walivyowekewa kama North Korea, Iran, Russia na hii block itaitesa USA sana.
 
Mradi mkubwa madini ya rare minerals wa Austrail umenunuliwa na China pia kwa asilimia 70. May be Brazil but na yeye technology anategemea ya mchina
Haya madini Marekani anayo kwa asilimia ndogo sana. Pentagon wamewaambia mashirika ya kutengeneza zana za kivita kama sijakosea, watafute mahali pengine ili wasiwe wenye kutegemea nchi nyengine(China).

Marekani kaangukia kwa Brazil na Australia na kuwataka wazalishe kwa wingi ili walete ushindani kwa China. Lakini hawawezi kwani ki asilimia ynapatikana kiuchache na licha ya hivyo uchimbaji wa hayo madini unahitaji ardhi kubwa, na mwenye ardhi kubwa kuhusu hayo madini ni China. Licha ya hivyo, China ndipo wanayo shehena ya hazina ya hayo madini kwenye ardhi yake.
 
Ni ngumu kwasababu watu wengi hata android hawaijui ila akienda kununua simu anauliza ina whatsapp na facebook na instagram? Kumbuka hayo makampuni ni ya kimarekani which means hutoyakuta kwenye OS ya mchina kama Marekani atayapiga ban. Mchina ana wechat je ni watz wangapi anaitumia?
Kwamba Infinix,Tecno,Huawei,Itel,VIWA, ni ya kimarekani? au
 
CHINA HAWATO IWEZA
Mkuuu kwenye nyanja za ujasusi mambo hayapo linear hivyo, kunawakati mnachukua maamuzi mkitegemea atafanya hivi ili akwame badae anatoka kitofauti. Mimi nadhani wachina watatoboa tu kwa maana nao kuchukua maamuzi ya kugoma kuwapigia magoti USA wamepiga mahesabu yao ya Inteligensia yao. Nakukumbusha kuwa USA kumuwekea vikwazo mchina kutamgarimu sana kwa sababu nae sasa anafanya nae kazi kwa jeuri na anaungana na maadui wake wengine hadharani na kufanya nao biashara bila kufuata vikwazo walivyowekewa kama North Korea, Iran, Russia na hii block itaitesa USA sana.
 
It's a matter of priorty Mr...Kama Tecno waliweza Wakiamua Kwa Huawei hawashindwi i'ts only the matter of Strategic positioning and Strategy kameza sekta kibao itamshinda Huawei? Not that hard u'll tell me trust me or not.
Africa is a tiny market. It doesnt even account to 20% of Huawei sales!
 
Umenikumbusha kuna mzungu alikuja bongo kaniachia linux open source kwa kweri ipo free na inaingiliana na microft os

Na sasa iko more advance than before na virus awasumbui na iko strong kwel kwel
 
Kwamba Infinix,Tecno,Huawei,Itel,VIWA, ni ya kimarekani? au
Mkuu zote hizo zina run android na watu wengi wanataka whatsapp, insta, fb na apps utitiri ambazo ni za kimarekani ndo maana os ya kichina haiwezi fua dafu mbele ya hawa. Au hujui kuwa hizo simu zina run android?
 
Akili za watu zimefinywa zikafinyika. Wanachodhani wao it's all about kutengeneza na kuuza, hizo other factors wala hawaziangalii. Nakumbuka tangu miaka ya katikati ya tisini katika report yao, CIA walisema kwa hali ilivyo kama mchina hatapigana vita yoyote ile basi itamchukua miaka nane (8) kuwa namba tatu kiuchumi Duniani. Then, miaka ya elfu mbili CIA walisema kabla ya 2016 kama hali itabaki hivi basi China atakua namba 2 kiuchumi duniani.
Hii najaribu kuonyesha jinsi watu wanavyofuatilia mambo, mbinu na mikakati ya mchina watu wanaijua, yote ipp mikononi maana wanajua exactly pale itakapo mfikisha. Hivyo hawakuwa mafala, walitengeneza nikakati ya kufaidika naye halafu baadaye waje ku m contain na kumfifisha kabisa. China hataweza kufika anakodhani anaelekea, Uingereza hakuwa fala alipomkabidhi Hong Kong ambao hadi leo hawataki kujiona kuwa wao ni sehemu ya China.
Kuna Macau, kuna Taiwan kuna Tibet. Hizi zote ni special projects dhidi ya Mchina, ni timing bombs.
Mchina amesha kuwa contained, hana tena ujanja.
Watu si wajinga wanapo invest heavily kwenye maswala ya Research and Intelligence, si wajinga hata
Ww ulikuwa unajua kama Huawei anatengeneza OS yake? Wameitengeneza kimyakimya siku ya siku US amekuja kuropoka. Mchina akatoka mafichoni.
 
Sio kuisoma nimetumia blackberry os nimetumia Microsoft mobile os zote zimefail kwenye soko mkuu usiangalie unauwezo wa kutumia vitu tofauti africa wengi maisha wamekariri maisha kwenye android na ukwel android wamefanya kaz kubwa sana tena mno kwa muda kidg inabidi huawei ajipange vizur najua vita hii mmarekani dhidi ya technologia nae ajiangalie amesomesha maadui zake wengi hunaweza kuona huawei amefanya kitu hammony os alafu ikija wekwa kwenye devices features zinafanana na android we angalia tu huawei p series muonekano wa iphone x means wanajua soko likoje watulize akili vizur lkn wanaweza kupiga atua
Huawei ni Bigger Company. They are not stupidy on what they are doing. Ni moja kati ya makampuni ambayo yaliinvest sana kwenye research.

Yeye kasema Os yake iko 60% faster kuliko android na ios. Me nakuhakikishia kwamba kama hiyo os yake iko only 20% faster kuliko android na ios. Basi tutashuhudia maajabu
 
Kuna safari ndefu sana hata wachina sio wote wataunga mkono iyo os pia
Mkuu umeongea kama vile huijui serikali ya china. Back in time Iphone ndo alikuwa anaongoza kwa mauzo china na pia china pekee ilikuwa inachangia 1/5 au kwa lugha rahisi 20% ya mauzo yote ya iphone duniani. Lakini hivi ninavyoandika hapa, tukisema tulist top 5 ya makampuni ya simu yanayouza zaidi nchini china basi huyo iphone hutomuona kwenye list. Hebu fikiria leo hii huawei, xiaomi, oppo, one plus, vivo, zte, tecno, infinix, itel na wengine tusiowajua wote wahamie Harmony Os nini kitatokea?.
 
Ni kitu gani kitazitoa kampuni za simu kutoka Android?

Kilichopo na kinachoendelea ni kwamba kampuni hizo zitaendelea kutumia Android kama kawaida sababu ndiyo mazingira ya soko yalivyo, hilo halina ubishi na kukaa nje ya mfumo huo ni kujiumiza kibiashara kwa sasa. Unless otherwise.

Ndiyo maana hata Huawei wenyewe wanasema hawatoiacha Android na wataendelea nayo kama kawaida mpaka hapo watakaposhindwa ama watakapowekewa zuio la moja kwa moja na Marekani.
Serikali ya China ndio inacontrol kila kitu.

1. Huawei alipigwa ban. Hivi kwa akili yako unadhani hayo makampuni mengine ya simu ya kichina yatajiona yapo salama na mmarekani?

2. Kikichowapata iphone China kinadhihirisha kwamba hakuna kinachoshindikana. Siyo muda mrefu tulisikia kwamba na kampuni zingine za simu china zinatest Os ya huawei. Unadhani walikuwa wanatest kwa bahati mbaya?
 
Mkuu zote hizo zina run android na watu wengi wanataka whatsapp, insta, fb na apps utitiri ambazo ni za kimarekani ndo maana os ya kichina haiwezi fua dafu mbele ya hawa. Au hujui kuwa hizo simu zina run android?
Bas Naona hatuelewani Take your Time
 
Tatizo kubwa kwa OS hiyo ya China ni soko na kama ilivyo ambapo Android ndiye aliyelikamata na kampuni karibu zote kubwa za uzalishaji wa simu ziko upande wake na hata Huawei na mafanikio yake, kwa namna moja ama nyingine yametokana na Android.

Kwa maana hiyo, hiyo OS inahitaji muda mrefu tu wa kuweza kuingia sokoni na kuzoeleka lakini wakati huo Dunia haitakuwa imesimama bado kutakuwa na swala lile lile la ushindani kama ilivyo hivi sasa na kampuni za uzalishaji wa simu hazijakoma kuanzishwa ukizingatia kuna kampuni za simu ambazo bado ni changa na zipo nje na ndani ya China pia.

Ninachomaanisha ni kuwa wakati Huawei ikijijenga na OS yake, italazimika kujitoa kutoka katika ushindani uliopo sasa katika soko la simu maana Android na iOS ndiyo vinara sokoni na wakati Huawei inajijenga itazipa nafasi kampuni zingine ambazo ni miongoni mwa washindani wake kama vile Xiaomi na Oppo kukamata nafasi yake na hivyo inaweza kuwa hatari zaidi kwa Huawei

Na pia kuna lingine la msingi sana hapo, ndani ya China kuna kampuni nyingi tu za uzalishaji wa simu na zinafahamika sana tu na hizi zote zinashindania soko ikiwemo ndani ya Uchina na pia kimataifa na nyingi zina uhusiano na Android kwa sasa. Je, Huawei itawezaje kuwashawishi hawa wengine waihame Android waende kwake ilhali yeye mwenyewe Huawei ni mshindani wao mkubwa katika soko la simu?

Hapo itaibidi Huawei kwanza ipambane kuanzisha Ecosystem yake mwenyewe na kisha iteke soko la Dunia kwa kiasi cha kufikia kuiondoa Android sokoni vinginevyo hizo kampuni nyingine kutoka China ambazo ni mahasimu wake kwenye soko itakuwa ngumu sana kumuunga mkono. Hizo ni Biashara na penye faida zaidi ndipo hutazamwa zaidi.
Tofautisha China na marekani. Kwa mchina serikali ndo inacontrol kila kitu. Hivi unadhani ile taarifa kwamba kuna makampuni mengine ya simu nchini china kama Xiaomi, Vivo na Oppo yanatest os ya huawei, unadhani hiki kitu kilikuwa kinatokea kwa bahati mbaya?
 
Mkuu humu utaumia, unajadiliana na mataahira ambayo hayajengi hoja badala yake yanaleta ushabiki na mapenzi kwenye mambo ya kitaalam. Hapa utaumia. Kuna mengine humu yanatamani yanatamani marekani ife kwa sababu zao za kidini, hayo unafikiri kuna chochote yanachowaza cha maana?

Utaumia kujadiliana na wavaa vipedo na mataahira wengine inapokuja swala la Marekani.
wewe mwenyewe umetanguliza mapenzi na marekani halafu unawaita wenzio maahira. Mnasikitisha sana.
 
Mkuu zote hizo zina run android na watu wengi wanataka whatsapp, insta, fb na apps utitiri ambazo ni za kimarekani ndo maana os ya kichina haiwezi fua dafu mbele ya hawa. Au hujui kuwa hizo simu zina run android?
Embu soma hii myb utanielewa kwa kivingine
C360_2019-08-13-15-20-53-015.jpeg
 
US walianza kwa ZTE, wakaja kwa Huawei!! Hivi bado unaamini kampuni zingine za China zitaendelea kujihisi zipo salama dhidi ya US kwa kuona hayo yaliyowakuta ZTE na Huawei wao hayawezi kuwakuta?!

Kukujibu swali lako kitakachofanya waachane na Android ni kwa sababu hakuna hata mmoja anayeweza kujiona yupo salama kibiashara ikiwa ataendelea kutegenea US Tech kwa 100%!!

Aidha, serikali ya China pia inaweza kutoa incentives kubwa kwa kampuni za ndani zitakazotumia Chinese made OS na kuzifanyia figisu zile zitakazoendelea kutumia Android!! Kwa serikali ya China hilo linawezekana kabisa unless Huawei waamue hiyo OS waitumie peke yao kama ilivyo kwa Apple, jambo ambalo sitarajii kwa sababu nadhani wanafahamu kwamba hii vita si ya kupigana peke yao halafu watarajie ushindi!

Kwamba mazingira ya soko yanategemea Android sio sahihi bali usahihi ni kwamba, majority ya Smartphones zinaingia sokoni zikiwa na Android! Ni kama hoja aliyoileta mdau mmoja hapa kwamba Waafrika hatuelewi na matokeo yake tumeng'ang'ana na Windows wakati kuna Linux! Huyu amesahau kwamba majority ya PCs zinakuja na Windows, na kwavile majority ya watumiaji wa PCs ni watu wa kawaida (contrary to watu wenye ABC za IT), there's no way hao watu wanaweza kuhangaika ku-install Linux bila kujali kama muhusika ni Mwafrika, Mchina, Mzungu or whoever! Na ndivyo ilivyo kwa Android! Leo hii inaonekana Android haikwepeki kwa sababu majority ya smartphones zinakuja na Android! Endapo Apple wasingekuwa wanaibania iOS, probably the story could be different now!!

So, it's up to kwa Huawei. Ikiwa watafanikiwa kutengeneza OS iliyosimama, keep this post, within 5 years, Android itaanza kupumulia mashine hasa kwa kwa kuziangatia manufacturers wakubwa wa affordable smartphones (by units produced) wapo China, na wataendelea kuibuka kila mwaka!

Kwamba Huawei wamesema wataendelea kutumia Android; kumbe ulitarajia waanze kuwa na nyodo kabla OS yao haijasimama?! Hivi hata mpangqji aliyeamua kujenga baada ya kuchoka manyanyaso ya Baba/Mama Mwenye Nyumba, unadhani ataanza kumletea nyodo mwenye nyumba wakati nyumba anayojenga ndo kwanza ni boma tu?! Hiyo kauli ya Huawei ni lugha tu ya kibiashara ili waendelee ku-maintain customers' confidence. There's no way Mchina ataacha kuhangaika kutafuta OS ya kwake mwenyewe wakati anafahamu, there's no way Mchina atakuja kuongea lugha moja na Mmarekani at least in the next 25 years!!
Huawei walishasema kwamba os hawaitumia pekeyao. Ni open source na yoyote anaweza kuitumia. So kampuni zingine kuhamia kwenye os yake wala haitakuwa ishu.
 
Yaani kwanza ww mwenyewe ni Mdini, 2) Uache kushabikia ushoga 3)Us anakutambua ww kama Nyani tu juu ya kua unashobokea 4)Uache kupanic usidandie mada kama umekurupuka, maana umeandika kama unatoka usingizini, 5)Jifunze kuwa na heshima
Naona umempa za uso mkuu
 
Afrika nayo ya kutegemea hata chupi tu na brezia wananunua mitumba (Kafa Ulaya) leo waje wanunue simu ya laki nne.

Uchumi wa China baada ya September 2 wakishawekewa zile tariffs ndio utaanza kuelekea rasmi makaburini. China hawezi ku-survive economically kwani kutegemea masoko ya nje kwa asilimia 70 ndio itakuwa kifo chake.
China anategemea masoko ya nje??? Hivi ww unajua kwamba iphone 20% ya mauzo yake yalikuwa yanatoka china kabla ya ile movement ya kugomea kununua iphone nchini china?

Unadhani mauzo ya iphone hivi karibuni yamedorora kwa sababu ipi?
 
Haisaidii google na apple walikuwa wa kwanza first to arrive first to be served na ubaya wa wachina wanaiga sana na ni wawivu kwenye kufanya research. Sasa hivi big westerners wanafanya research on Artificial Intelligence na Big Data analysis
China mvivu kufanya research??? Hivi unajua kwamba huawei ni moja ya makampuni ambayo yaliinvest sana kwenye research?
 
Karibia kila kampuni kubwa za uzalishaji wa simu Duniani zina Operating Systems zao na zipo sokoni. Issue ya kuja na OS mpya na kuiweka sokoni si kitu kirahisi kama wengi wanavyozungumza hapa. Ni jambo linalohitaji uwekezaji mkubwa sana hasa katika issue ya App Ecosystem. Kutengeneza OS tu bila kuwa na Support ya Apps na Developers wa kutosha hilo ni tatizo kubwa sana. Unapomuona Xi Jinping anahangaika kwenda Urusi kutafuta App Store mbadala ama unapowaona Huawei wanakwenda Ureno huko kushughulikia App Store mbadala kwa ajili yao usidhani kuwa ni jambo rahisi tu la kusema "OS imekamilika".

Unasema kuwa Serikali ya China itazifanyia figisu kampuni za ndani zitakazogoma kuachana na Android;

Hilo la 'Figisu' unalosema halijaanza leo na lipo. China wameshazipiga 'Ban' kampuni nyingi tu za Kimarekani nchini humo na hata zilizopo humo mfano hata Apple wameshasumbuliwa vya kutosha na wako tayari hata kuhamisha viwanda vyao na kuvipeleka mahali pengine, ikibidi. Katika mazingira kama hayo ya kuzibana kampuni za nje na kuweka upendeleo ndani ya China pekee unafikiri ni App Developers wangapi wa Kimataifa watakaofanya kazi katika mazingira hayo kwa ajili ya hiyo OS yao na waachane na Android? Unafikiri hali ya kampuni hizo za ndani itakuwaje katika soko la kimataifa licha ya kuwa soko lao la ndani ni kubwa?

"Mazingira ya soko yanategemea Android" ?? Sidhani kama hii 'Statement' niliisema na pamoja na hilo bado haipishani sana na ukweli wenyewe sababu Android si OS tu peke yake. Kuna watu wanachanganya hapa na pengine hawafahamu nyuma yake kuna kitu gani. Android kama OS nyuma yake kuna App Ecosystem (yenye Apps za kutosha, App Developers wa kutosha) iliyojijenga kwa muda mrefu na imejitosheleza kwa ujumla wake kwa kiasi cha kufikia kuliteka soko la Dunia. Ni kwamba tayari walishatengeneza mazingira ambayo hata kama kuna kampuni zitakazoibuka na kuanzisha uzalishaji wa simu 'leo hii' hawana budi kujiunga katika 'Ecosystem' yenye nguvu zaidi kwa sasa.

Huawei wanadai kuwa wamekamilisha OS yao hiyo (Harmony). Well, Huawei wamekuwa wakifanyia kazi OS yao muda mrefu na hata sasa wana kazi ya kuhakikisha kwamba inafanya kazi ndani ya soko la China kwanza na ndicho kitakachofanyika na hata hivyo bado kama nilivyosema awali, wanahitaji kuja na kitu bora zaidi cha kuitikisa Android na kuwashawishi App Developers kutoka sehemu mbalimbali Duniani kufanya kazi nao, hicho si kitu rahisi. Na hata wanachosema Huawei ni kuwa hiyo OS haitatumika kwenye simu (Smartphones) bali katika vifaa vinginevyo kama vile Smart Displays, Watches n.k.

Na kama unavyosema, endapo Serikali ya China ikiziendeleza hizo 'Figisu' kwa sura nyingine, huenda ndipo tutakaposhuhudia uhalisia wa 'vita' yenyewe ya kiuchumi itakayo muathiri hata China mwenyewe kuliko kilichopo hivi sasa. Wachina wanalifahamu hilo na hawatopenda 'kukurupuka' na kuachana tu na Android kisa wana OS yao na ndiyo maana wanasema hivyo kwamba hawataachana na Android na wataendelea nayo kama kawaida mpaka hapo mazingira yatakapokuwa magumu kwao kuendelea kufanya hivyo.
App developer anapoamua kutengeneza app kwa ajili ya Harmony os siyo kama anaachana na Android na ios. Yeye anachoangalia ni wateja.
 
Back
Top Bottom