Huawei tayari wamekamilisha Operating System (OS) yao

Huawei tayari wamekamilisha Operating System (OS) yao

Karibia kila kampuni kubwa za uzalishaji wa simu Duniani zina Operating Systems zao na zipo sokoni. Issue ya kuja na OS mpya na kuiweka sokoni si kitu kirahisi kama wengi wanavyozungumza hapa. Ni jambo linalohitaji uwekezaji mkubwa sana hasa katika issue ya App Ecosystem. Kutengeneza OS tu bila kuwa na Support ya Apps na Developers wa kutosha hilo ni tatizo kubwa sana. Unapomuona Xi Jinping anahangaika kwenda Urusi kutafuta App Store mbadala ama unapowaona Huawei wanakwenda Ureno huko kushughulikia App Store mbadala kwa ajili yao usidhani kuwa ni jambo rahisi tu la kusema "OS imekamilika".

Unasema kuwa Serikali ya China itazifanyia figisu kampuni za ndani zitakazogoma kuachana na Android;

Hilo la 'Figisu' unalosema halijaanza leo na lipo. China wameshazipiga 'Ban' kampuni nyingi tu za Kimarekani nchini humo na hata zilizopo humo mfano hata Apple wameshasumbuliwa vya kutosha na wako tayari hata kuhamisha viwanda vyao na kuvipeleka mahali pengine, ikibidi. Katika mazingira kama hayo ya kuzibana kampuni za nje na kuweka upendeleo ndani ya China pekee unafikiri ni App Developers wangapi wa Kimataifa watakaofanya kazi katika mazingira hayo kwa ajili ya hiyo OS yao na waachane na Android? Unafikiri hali ya kampuni hizo za ndani itakuwaje katika soko la kimataifa licha ya kuwa soko lao la ndani ni kubwa?

"Mazingira ya soko yanategemea Android" ?? Sidhani kama hii 'Statement' niliisema na pamoja na hilo bado haipishani sana na ukweli wenyewe sababu Android si OS tu peke yake. Kuna watu wanachanganya hapa na pengine hawafahamu nyuma yake kuna kitu gani. Android kama OS nyuma yake kuna App Ecosystem (yenye Apps za kutosha, App Developers wa kutosha) iliyojijenga kwa muda mrefu na imejitosheleza kwa ujumla wake kwa kiasi cha kufikia kuliteka soko la Dunia. Ni kwamba tayari walishatengeneza mazingira ambayo hata kama kuna kampuni zitakazoibuka na kuanzisha uzalishaji wa simu 'leo hii' hawana budi kujiunga katika 'Ecosystem' yenye nguvu zaidi kwa sasa.

Huawei wanadai kuwa wamekamilisha OS yao hiyo (Harmony). Well, Huawei wamekuwa wakifanyia kazi OS yao muda mrefu na hata sasa wana kazi ya kuhakikisha kwamba inafanya kazi ndani ya soko la China kwanza na ndicho kitakachofanyika na hata hivyo bado kama nilivyosema awali, wanahitaji kuja na kitu bora zaidi cha kuitikisa Android na kuwashawishi App Developers kutoka sehemu mbalimbali Duniani kufanya kazi nao, hicho si kitu rahisi. Na hata wanachosema Huawei ni kuwa hiyo OS haitatumika kwenye simu (Smartphones) bali katika vifaa vinginevyo kama vile Smart Displays, Watches n.k.

Na kama unavyosema, endapo Serikali ya China ikiziendeleza hizo 'Figisu' kwa sura nyingine, huenda ndipo tutakaposhuhudia uhalisia wa 'vita' yenyewe ya kiuchumi itakayo muathiri hata China mwenyewe kuliko kilichopo hivi sasa. Wachina wanalifahamu hilo na hawatopenda 'kukurupuka' na kuachana tu na Android kisa wana OS yao na ndiyo maana wanasema hivyo kwamba hawataachana na Android na wataendelea nayo kama kawaida mpaka hapo mazingira yatakapokuwa magumu kwao kuendelea kufanya hivyo.
wakati ww unapiga kelele kuitetea android kwamba inajiweza. Huyo android naye anapiga kelele kuiomba serikali ya US ilegeze kamba ili google wafanye biashara na Huawei
 
Uwezo wa China kupambana na US kwa muda mrefu ni mdogo. Wakienda hivi say kwa miaka mitano, China will collapse.
Sasa nani atanunua simu yenye OS ya mchina kwa mfano?
Mkuu biashara ina mbinu zake, unapoingia kwenye soko ambalo tayari lina watu, mbinu makini huwa ni lulu kwako kupenya sokoni na kuwapiku wenzako uliowakuta. Endapo Huawei au Kampuni za kichina zikaja na simu zenye ubora kama wa simu za Mmarekani ila zinatumia OS yake na kuziuza kwa bei nafuu unadhani watu hawatazinunua ?. Jaribu kukumbuka namna Samsung na Nokia zilivyokuja kupitwa na ujio wa TECNO.
 
Samsung
HTC
Google Pixel
Motorola
Nokia
Sony
One Plus
LG
N.k

Kumbuka kuna zaidi ya device 24.000 zinatumia android. Za china hazifiki hata nusu ya hiyo.
We upo dunia ya wapi? One plus ni kampuni ya China. Tena ni Subsidiary company ambapo parential company ni Oppo.

Hao waliobaki hakuna hata mmoja anatia mguj kwa huawei, xiaomi, one plus, oppo au vivo
 
Soko kubwa la iPhone lipo China na si US au Europe.

Inaonesha jinsi gani wachina wenyewe hawakubali bidhaa zao hasa Huawei.

Hiyo OS itawavuruga wachina na hawataitumia kama mnavyofikiri.

Ni ngumu kuacha kutumia bidhaa za US kwa jinsi walivyozifunga na Eco system zao.

Itakuwa ngumu ku-intergrate hiyo OS na products nyingi tu toka US.
Boss hizi data umetuletea za mwaka gani? Maana once upon the time ni kweli soko kubwa la iphone lilikuwa china. Lakini hivi sasa apple anapumulia mashine kwenye soko la china.
 
Sio kuisoma nimetumia blackberry os nimetumia Microsoft mobile os zote zimefail kwenye soko mkuu usiangalie unauwezo wa kutumia vitu tofauti africa wengi maisha wamekariri maisha kwenye android na ukwel android wamefanya kaz kubwa sana tena mno kwa muda kidg inabidi huawei ajipange vizur najua vita hii mmarekani dhidi ya technologia nae ajiangalie amesomesha maadui zake wengi hunaweza kuona huawei amefanya kitu hammony os alafu ikija wekwa kwenye devices features zinafanana na android we angalia tu huawei p series muonekano wa iphone x means wanajua soko likoje watulize akili vizur lkn wanaweza kupiga atua

Hivi unajua ni kwanini TECNO anafanya vizuri AFrica?
Jiulize mchina akitengeneza simu kila kitu kinatoka kwake itakuwa BEI gani?
Otherwise asikuongopee mtu hao facebook na whats app watakuja wenyewe kuomba platform kwa Hammony Os.
 
Mkuu labda we umeanza kuijua huawei juzi tu hata nokia alitumia pia microsoft na soko likamtema sasa yuko na android kabla ya android karibu kila sim ilikua na operation system yake mkuu tena blackberry alifanya vizur mno kuliko Microsoft shida mkuu sio nn ni soko labda mwenzangu ujanielewa jitafakari punguza hasira atulipwi lkn ni story tu hizi za kijiwe mkuu
Hao wote uliowafananisha na Huawei, Os zao wakuwa wamezimonopolize.
 
Huna uwezo kununua vitu toka US ni ghali mno ndiyo maana mnakimbilia vya CHINA bei rahisi na havina ubora hata kidogo
Vitu vya China havina ubora?? Labda wewe mwnyewe umetaka kununua vitu visivyo na ubora
 
Huawei ni Bigger Company. They are not stupidy on what they are doing. Ni moja kati ya makampuni ambayo yaliinvest sana kwenye research.

Yeye kasema Os yake iko 60% faster kuliko android na ios. Me nakuhakikishia kwamba kama hiyo os yake iko only 20% faster kuliko android na ios. Basi tutashuhudia maajabu

Ngoja tuone maajabu ya story za mfanyabiashara blackberry sio company kubwa microsoft je mkuu hata msanii anaweza akakwambia ana nyimbo kali alafu ikitoka inafanya vibaya mno nakumbuka mi ni moja wa watu niliekua natumia android ila nikafatilia toleo la lumia matangazo yake dah microsoft os version yake ilinivutia sababu nilikia natumia windows 8 sasa ilipokuja mkononi nadhani unajua kilichotokea
 
Mkuu umeongea kama vile huijui serikali ya china. Back in time Iphone ndo alikuwa anaongoza kwa mauzo china na pia china pekee ilikuwa inachangia 1/5 au kwa lugha rahisi 20% ya mauzo yote ya iphone duniani. Lakini hivi ninavyoandika hapa, tukisema tulist top 5 ya makampuni ya simu yanayouza zaidi nchini china basi huyo iphone hutomuona kwenye list. Hebu fikiria leo hii huawei, xiaomi, oppo, one plus, vivo, zte, tecno, infinix, itel na wengine tusiowajua wote wahamie Harmony Os nini kitatokea?.

Kwenye makampuni makubwa duniani apple 2 2018 and 2019 na hizo story nimezifatilia mno sasa ngoja niweke nilichopata sio china tu hata marekani ni hivi iphone ni simu kwa sasa duniani ndo most expesive na oppo na oneplus wamecompare na iphone kutoa samsung na huawei kwa sasa mana nazo gharama iko juu ni zina nafuu ya bei na uwezo inaweza kulingana pengine hata kidg kuwa juu ya iphone lkn bei yake iko poa sasa wanasema kama unaweza kuwa na uwezo kidg ingia huawei mana hata wameifananisha hata muonekano wake na iphone na p20 lite nimetumia mpk hata functionality zake au kama unajiweza tena kdg ingia kwa samsung sasa izo zote ni android wasi wasi wetu ni je bila android tumeona blackberry os alisumbua sana duniani leo amepotea anakuja na android os nw kama nokia
 
Hivi unajua ni kwanini TECNO anafanya vizuri AFrica?
Jiulize mchina akitengeneza simu kila kitu kinatoka kwake itakuwa BEI gani?
Otherwise asikuongopee mtu hao facebook na whats app watakuja wenyewe kuomba platform kwa Hammony Os.

Mkuu tecno africa atafuta soko la kujiendeleza kwa africa nw hata ulaya anauza tatizo sio tecno kwani win mobile hakuwa na facebook alakuwa na social media zote nini ameshindwa lumia zilikua na jina sana zilipotoka duniani hapa kuna os nyingi sana tena mno nyingine hata sio official announced in public sasa mi naongelea tecno bila android os tunaongelea bado iko mikononi mwao na pia android wanazidi nao kudevelop sio kama ndo mwisho kwanza china awawezi zuia android itakuwepo china na pia lazima wachina wataendelea tumia android pia alafu developer wa android kibiashara wako wengi mtu awezi sema mi app developer niache kudevelop kisa huawei vs usa pls jmn tuipe mda ije sokon mana tunashindanisha vitu ambavyo mmoja ajaonekana mikoni mwa watu ikija na mi ntatumia nione tofauti izo ni business mkuu aje ashindane ona mitandao leo kinachotokea so huawei afanye vizur alete changamoto ili sisi tupate nafuu ila sio kwa chuki hizi atapotea very soon navyojua tabia za os sorry ukwel mi nimejaribu nyingi ila android wame customized sana os yao ndo mana wengi wakitumia android akienda ios wenye wanarudi android coz ios command nyingi
 
Hao wote uliowafananisha na Huawei, Os zao wakuwa wamezimonopolize.

Na ye huawei je inakuja kama nani mana tujue ni open source itakua ngoja niichimbe zaidi nione kama ya kuitia mkononi mkuu dunia ya bos win mob os kipindi kile ni tofauti na sasa
 
You are genius bruh
FED na Trump wana mpango wa kushusha dollar ili waanze export zaidi.

Yuan imeshuka na hii itawasaidia Wamarekani kununua zaidi
Ni wachache sawa wameliona hili hasa kwenye nchi zetu...Beijing inavuta pumzi na kupanga mashambulizi....Yuan imeshuka kwa kiwango cha kutisha na hii itawasaidia sana kuongeza reserve yao ya $
FED imeshtuka ndo maana hapa tunajiandaa na fall ya $ ambayo itakuwa neema kwa wote ikiwemo kina sisi
 
Boss hizi data umetuletea za mwaka gani? Maana once upon the time ni kweli soko kubwa la iphone lilikuwa china. Lakini hivi sasa apple anapumulia mashine kwenye soko la china.
Na hii ni baada ya Google kuwazingua Huawei ndio balaa lilipo anzia vile wachina wana ushirikiano na wapo kama 1Billion iv na point zake while mmarekan ana tumilion ata mia tano hatufiki..What do u expect
 
iyo ni muhimu mzee fursa iyo
Hivi unajua ni kwanini TECNO anafanya vizuri AFrica?
Jiulize mchina akitengeneza simu kila kitu kinatoka kwake itakuwa BEI gani?
Otherwise asikuongopee mtu hao facebook na whats app watakuja wenyewe kuomba platform kwa Hammony Os.
 
Usi kariri..china anatumia Stratergy kibao kwenye biashara zake especially Low-cost leader kwa Africa coz anajua Africans what they like na ndio maana katoboa...mda uo U.S wanaringa na Differentiation strategy kwa Africa hawez teka soko...

Mind you China Vitu genuine vipo tena sana tu...sema inaonekana huvijui na huwa unapigwa sana
Vitu vya China havina ubora?? Labda wewe mwnyewe umetaka kununua vitu visivyo na ubora
 
Back
Top Bottom