Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,845
Mimi msimamo wangu utakuwa ni kama ulivyo. Sigeuki nyuma nikawa jiwe. Hawa watu wanaubaguzi wa hali juu tena kibaya zaidi wanaufanya kwetu dhidi ya wazawa, lakini watu hawataki kuuona huo wala kuuzungumzia wanataka kuzungumzia ubaguzi aliofanyiwa yeye tu!
Ubaguzi kivipi Bro?
Hatutibiwi kwenye hospitali "zao", i.e Aga Khan, Hindu Mandal, Burhani, TMJ etc?
Walituzuia kwenye majumba "yao" ya sinema? Empire, Odeon, Empress, Drive inn etc?
au kwenye mahoteli "yao" Seacliff, White sands, The courtyard etc?
Tataizo "letu", kujieleza ndio shughuli, kubaguliwa kivipi?
Sidhani kama tunaweza kuwaita Azim Dewji & Mohammed Dewji-Simba, Mar Abbas Gulamali-Yanga, Shaffi & Moh'd Bora-Majimaji, Naushad Moh'd -Malindi (tena huyu ana mke Mswahili), etc kuwa hawa jamaa walikuwa wabaguzi...
Kuna watanzania wenye asili ya kihindi-wagoa wanaojihusisha na mambo ya dini, si wabaguzi, kuna wagoa wanaojihusisha na muziki mf; INAFRIKA Band, si wabaguzi...
Kuna watanzania wenye asili ya kihindi-masinga singa wanaojishughulisha na ufundi pale gerezani, si wabaguzi...
Ubaya wa wachache wetu (watanzania wazawa-wabantu) ni tabia za utoro kazini & uvivu, udokozi, fitna & majungu , na kukubali Rushwa (tena za kipuuzi i.e fulana, kofia, na wale vibosile kwenda kwenye maduka "yao" kuomba tv, mafriji etc) ndio maana hawa jamaa wanatudharau, sio kutubagua.
Hapa nilipo, kuna wahindi nane kutoka East africa, wana heshima na adabu, tena wanasema "wewe ndugu yetu, tumetoka wote nyumbani!", na kiingereza hawataki kukizungumza, kiswahili tu!.