how to get the ring.

how to get the ring.

u niliulizwa kabla hata sija-settle kwenye mahusiano, yaani mimi naona nayaanza mahusiano tu naulizwa kuolewa, na juzi tu nimeulizwa kuolewa naye tena.....
.
natamani nijue ulijibu vipi?
 
mie panaponichosha ni wadada tu wapo desperate na ndoa, wakaka walaaa, nina mdada hapa ofisini natamani hata dk hii ajibiwe ombi lake la kupata mume jamani, mana tukimaliza huu mwaka bila-bila atachizika, na wakaka wameshajua shida yake ni ndoa wanamtumiaje sasa? yeye anabaki labda nimeandikiwa huyu, kesho hamuoni na ameshafanya nae yote, then wanakuja kulalamika "wanachezewa" hawachezewi wanajichezea wenyewe, ndoa si kamari jamani useme "ngoja nijaribu" labda nitafanikiwa.
yaani nilipokuja hapa lengo langu ilikuwa kukushtua ili uje utuambie mawazo yako kuhusu hili.
 
nadhani hapo kwenye red ndo haswa binadamu tunapokosea, tunadhani kwa sababu miaka inabadilika basi hata life style zetu zinatakiwa zibadilike....
kwani kuna shida gani kusubiri mwanaume akuulize kukuoa? kwanza mimi naona ndo kama nitajisikia nahitajika sana naye akiniuliza kuliko mimi kumwuliza.

na ukimuuliza, hata kama alikuwa ana nia hiyo tayari ataichelewesha avute subira afikirie ni kwanini umemuuliza! wadada subirini muulizwe, juzi kati nilikuwa njoro, mdogo wangu alituita kutupa chakula kidogo na kutupa habari za kuleta mchumba, huyu mdogo wangu aliikuwa na mwanaume ambae kila mtu kwenye familia alijua ndio atakaemuoa, kilitokea cha kutokea wakashindwana, haijapita hata mwezi tunaitwa kwenye chakula, mie namuuliza wewe huyu bwana mpya umemjuaje ghafla hivyo, nikajibiwa dada haya ni mambo ya "backup" nani anataka kuabika mjini hapa? nilichoka kabisaaa, mapenzi ya kisasa full vituko.
 
Kama mdada amemzimia BF wake kiasi vha kumuona anafaa kabisa kufunga naye pingu za maisha kwanini asubiri BF ndio awe wa kwanza kutangaza ndoa!? Badala ya kupoteza muda chungu nzima huku ukiendelea kusubiri "Labda leo labda kesho" funguka moyoni na umueleze kwa kina nia yako ya kuwa mke mtarajiwa badala ya kutaka mambo kama yawe ya mwaka 47. Najua hili wengine wanaliona gumu sana.



................. jana nilikuwa nachungulia kitabu cha steve harvey cha ACT LIKE A LADY THINK LIKE A MAN.ni kitabu kizuri sana ila sie wengine uvivu wa kusoma vitabu tunakosa mengi.

steve anasema wanaume wanajua kabisa kuwa wanawake wanataka ndoa. wanawake wanatakiwa kujiondoa katika mentality ya kizamani ya kusubiri mpaka mwanaume atangaze ndoa. tunatakiwa kuset timeline for the ring, mwambie mpenzi wako unachotaka na matarajio yako. haina maana kuwa katika mahusiano ambayo hayakupeleki kule unataka kwenda, kwa case hiyo tafuta mtu ambaye mna direction moja. wanawake wengi huwa wanashindwa kufunguka kwa wapenzi wao kuhusu ndoa vile wanaogopa au wanahisi ni vigumu lakini ni ngumu zaidi kudate na mtu mpaka mnazaa watoto na hana mpango wa ndoa (wakati wewe intention yako ni kuwin pete).

muoneshe mwanaume thamani yako na asikutumie kama vile amekodi nyumba mwisho wa siku akipata sehemu nzuri anahamia huko. set standards zako na angalia kama anafit huko.

"the
number one cause of failure in this country is the fear of failure.
Fear paralyzes you from taking action. Don’t be afraid to lose
him, because if a man truly loves you, he’s not going
anywhere"

tujadilini jamani, tuanze kuset timeline au twende na zama zetu za mwaka 47 za kusubiri kuambiwa.lol.

nawasilisha.
 
Last edited by a moderator:
la enzi hizo
ha haaaa, nilikubali kwa sababu kuu moja....
enzi hizo sikuwa naingia mwenye mahusiano na mtu ambaye sikujiridhisha kuna natamani kuishi naye kwa maisha yangu yaliyobaki. yaani kama mkaka ananitokea hata kama nampenda lakini siridhishwi kuishi naye huwa nilikuwa nakataa, siwezi kuwa naye kabisa. kitendo cha kukubali mahusiano naye ilikuwa clear kwangu kuwa napenda kuishi naye, sikupata shida kujibu hilo.
 
Kama mdada amemzimia BF wake kiasi vha kumuona anafaa kabisa kufunga naye pingu za maisha kwanini asubiri BF ndio awe wa kwanza kutangaza ndoa!? Badala ya kupoteza muda chungu nzima huku ukiendelea kusubiri "Labda leo labda kesho" funguka moyoni na umueleze kwa kina nia yako ya kuwa mke mtarajiwa badala ya kutaka mambo kama yawe ya mwaka 47. Najua hili wengine wanaliona gumu sana.



tupo pamoja BAK, sijui watu wanaona kuna ugumu gani kuulizia uelekeo hapo.... tena unakuta mdada hamu ya ndoa inamkereketa ila ndio anasubiri kuambiwa. ya mwaka 47 tuyaache huko huko jamani.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
na ukimuuliza, hata kama alikuwa ana nia hiyo tayari ataichelewesha avute subira afikirie ni kwanini umemuuliza! wadada subirini muulizwe, juzi kati nilikuwa njoro, mdogo wangu alituita kutupa chakula kidogo na kutupa habari za kuleta mchumba, huyu mdogo wangu aliikuwa na mwanaume ambae kila mtu kwenye familia alijua ndio atakaemuoa, kilitokea cha kutokea wakashindwana, haijapita hata mwezi tunaitwa kwenye chakula, mie namuuliza wewe huyu bwana mpya umemjuaje ghafla hivyo, nikajibiwa dada haya ni mambo ya "backup" nani anataka kuabika mjini hapa? nilichoka kabisaaa, mapenzi ya kisasa full vituko.
ha haaaa, mambo ya backup........
ila wanayaweza
 
ha haaaa, nilikubali kwa sababu kuu moja....
enzi hizo sikuwa naingia mwenye mahusiano na mtu ambaye sikujiridhisha kuna natamani kuishi naye kwa maisha yangu yaliyobaki. yaani kama mkaka ananitokea hata kama nampenda lakini siridhishwi kuishi naye huwa nilikuwa nakataa, siwezi kuwa naye kabisa. kitendo cha kukubali mahusiano naye ilikuwa clear kwangu kuwa napenda kuishi naye, sikupata shida kujibu hilo.

ulikuwa na expectations zako na standards zako kabla hujaingia kwenye mahusiano, una bahati mpenzi wako alilijua hilo, vipi kama asingekuuliza miaka nenda rudi? nawewe ungeuchuna? kumbuka awali ulikuwa unataka mtu wa kuishi nae maisha yako yote. be honest, ungenyamaza unasubiri akuambie?
 
Kama mdada amemzimia BF wake kiasi vha kumuona anafaa kabisa kufunga naye pingu za maisha kwanini asubiri BF ndio awe wa kwanza kutangaza ndoa!? Badala ya kupoteza muda chungu nzima huku ukiendelea kusubiri "Labda leo labda kesho" funguka moyoni na umueleze kwa kina nia yako ya kuwa mke mtarajiwa badala ya kutaka mambo kama yawe ya mwaka 47. Najua hili wengine wanaliona gumu sana.
ha haaa, rafiki hebu tuambie ukweli wako kabisa.....
hivi utajisikiaje kama mdada unayemtokea akakuuliza umuoe? reaction yako itakuwa vipi?
 
ulikuwa na expectations zako na standards zako kabla hujaingia kwenye mahusiano, una bahati mpenzi wako alilijua hilo, vipi kama asingekuuliza miaka nenda rudi? nawewe ungeuchuna? kumbuka awali ulikuwa unataka mtu wa kuishi nae maisha yako yote. be honest, ungenyamaza unasubiri akuambie?
ndo maana nikasema tangu mwanzo kuwa mimi siyo mfano mzuri sana....
unajua ni rahisi sana kuisemea situation ambayo haupo ndani yake. sababu sikupitia hilo naweza kusema kirahisi kuwa ningesubiri mpaka aniulize ili nijue kama naye ana-feel ninavyo-feel mimi, lakini je ningekuwa kwenye hiyo situation ningejibu hivyo hivyo? sijui....
I am trying to be honest here
 
Back
Top Bottom