How the Dreamliner is Killing Tanzanians dream?

Serikali ya awamu ya tano itachagua la pili
 
Hatujui kuendesha nchi, licha ya shirika.

Ndiyo maana hatujui kama nchi ni ya kijamaa au kibepari.

Bila hili kueleweka, hata habari ya kama mashirika haya yawe mikononi mwa serikali au mwa sekta binafsi ni vigumu kuamua.

Ndiyo maana tunaenda tunaweweseka, mara akiingia rais huyu anauza mashirika, akiingia mwingine anayarudisha serikalini, akiingia rais huyu anamuahidi Dangote deals za kuvutia uwekezaji, akiingia rais mwingine anakataa kuzikubali deals hizo.

Kati mazingira kama hayo, kuwekeza hela nyingi katika biashara yenye high risk kama ya usafiri wa anga ni kujitakia mabaya tu.
 
Hizo nchi za ndege ulizozitaja, Qatara, Emirates, Germany, kugeza mambo yao ni kugeza tembo kunya, tutapasuka msamba.

Mimi kiujumla napendelea maendeleo yanayowagusa watu wengi, tena wengi wa hali ya chini, kwa mpigo.

Kiuchumi, unaweza kutengeneza mzunguko wa hela vizuri zaidi kwa kuongeza purchasing power ya watu wa chini, halafu watu wa chini wakaongeza consumption, halafu enterpreneurs wakaongezeka, halafu wakajikusanya nguvu mpaka kuanzisha mashirika ya ndege yao, bila kuhitaji serikali ichukue risk kubwa.

Serikali inakuwa na jukumu la kuweka legal framework nzuri tu, kuweka amzingira ya biashara mazuri tu, kuweka level playing field, kuweka misingi ya free trade inayoendana na no barrier to entry or exit the market etc.

Sasa hivi serikali imejiingiza kwenye biashara kwa mabavu, imefanyia mpaka fitina mashirika binafsi. Hili linasababisha monopoly. Monopoly itapandisha bei halafu biashara ikose innovation.

Pia, hata shirika likipata hasara, vitabu vitapikwa, CAG atakatazwa asikague vitabu, zitaletwa figisu kibao. Kwa sababu shirika lishakuwa project ya kisiasa ya rais, na rais akitaka kuadhirika lazima asitiriwe by hooks or crooks.

Ndiko tunakoelekea.
 
Honestly ni kwa sababu ya korosho ambazo zimeshusha traditional exports kwa nusu from almost 1bn usd to 500mil usd ..ila kiukweli Tz inabid tu imporve sana kwenye fishing na holticulture hizo zote ni 1Billion usd industires kwa mwaka na sisi tunazilalia...Kama hizi priorities zingepangwa vizuri...tununue Deep Sea Fishing Vessels to empower wavuvi wetu na fish processing industiries ..pia tuongeze kulima mboga mboga na matunda...ingawa naona tunaendelea ila mwendo inabid uongezeke..viwanda kama Eat fresh, Rungwe avocado ..viwe hata 100 ili hizi dreamliner ziwe zina mzgo wa kutosha wa matunda ,mboga ,maua na samaki ...itakuwa tumeua ndege wa wili
 
Serikali lazima ianzishe national carrier , mambo yakishatengemaa ndo wataachiwa ATCL wajiendeshe. Lazima mtoto umlee akue ajitegemee ndo unamwachia.
 

Utateuliwa tu ... kaza
 
Mimi sipingi ununuaji wa ndege..ninaona tu imefanyikwa kwa pupa sana...lets say Hizi dreamliner moja ni 250mil usd ...wakati hizi airbus moja ni 82mil usd ..hii inamanisha kwa dreamliner moja unapata airbus 3 ...ambazo range yake sio kubwa ofcourse ila zitatutosha lu focus lu connect african cities na middle east huku far east ikisubir ... Hyo usd 250 mil ya dreamliner ya pili ..ninge empower wavuvi kwa kununua fishing vessels na kujenga viwanda vya ku process samaki...na pia nningetoa mikopo na elimu kwa watu wajifunze kilimo cha maua ,mboga na matunda...na kujenga cold storage rooms airport ..ili kuongeza export za holticulture
 
Mawazo hayapigwi rungu!!
Nimeona nikujibu kizungu.

You are indeed very stupid!!!!

Writing this article in English does not give it an academic or any intellectual edge. It's just horrendous!!!!
 
Ninyi hamjui ndege inaleta faida na ile faida itaenda kwenye madawa barabara nk halafu shida hazitakaa ziishe fikiroa wewe mbona wewe unakula raha mjini wakati ndugu zako wengi wanashindia mlo mmoja tu
 
Hizi ndege ni vizuri tujue kuzitumia na matumizi yatapatikana kama ifutavyo

1.Tuongeze kunitangaza kwenye nchi mbali mbali
2.Tuvutuie wawekezaji kwenye sector ya kilimo cha maua,matunda na mboga (horticulture )
3.Tu empower wakulima wadogo ku form vikundi watavyoweza kulima vitu vya ku export
4.Tuongeze export procesiing zones za vitu hasa Nguo, Na Electronics

Ili watu waweze kusafirsha bidhaa kutumia hizi hiz dreamliner na pia waongeze kipato chao kitachoweza kuwafanya wasafir na wao
 
Ninyi hamjui ndege inaleta faida na ile faida itaenda kwenye madawa barabara nk halafu shida hazitakaa ziishe fikiroa wewe mbona wewe unakula raha mjini wakati ndugu zako wengi wanashindia mlo mmoja tu
Unaposema "faida" unamaanisha nini?

Una "cost benefit analysis" kuhusu manunuzi haya ya ndege?

Una projected "Return on Investment"?

Unajua ndege zimenunuliwa kwa gharama gani?

Unajua kuendesha ndege kuna gharama gani kwa mwezi?

Unajua ndege ikikaa bila kuruka ina gharama gani?

Unajua revenue ya ATCL kwa mwezi ni kiasi gani?

Unajua expenditures za ATCL kwa mwezi ni kiasi gani?
 
Serikali ya awamu ya tano itachagua la pili
Hilo la pili ni hatari sana, ni kujaribu kujaza maji kwenye ndoo ambayo haina sakafu.

Ila siasa zikitamalaki, tutapigwa propaganda mpaka watu wakubali.
 

Kama Ethiopia [nchi uliyoitolea mfano] wameweza, na wao kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla inalingana au kufanana na sisi, kwa nini sisi tusiweze kuwa na shirika letu wenyewe?

Sioni kabisa sababu ya sisi kushindwa.
 
Mimi nimegundua kitu, Magu ana invest kwenye utalii kupitia ATCL. Tulipiga kelele issue ya watalii kupanda Ndege za Kenya na kuletwa bongo na magar yao, huu ulikuwa upuuzi ulioitaji maamuzi kama haya
 
Magufuli aliambiwa anaharibu biashara ya korosho, kama kawaida yake mbishi.

Sasa tumeangukia pua, ripoti ya BOT ya Septemba 2019 inasema kwamba katika mwaka unaoishia Agosti 2019, mapato ya mauzo ya nje ya bidhaa za kilimo yameshuka kwa 55%.

That's more than a half!
 
Kama Ethiopia [nchi uliyoitolea mfano] wameweza, na wao kiuchumi na kimaendeleo kwa ujumla inalingana au kufanana na sisi, kwa nini sisi tusiweze kuwa na shirika letu wenyewe?

Sioni kabisa sababu ya sisi kushindwa.
Ethiopian Airlines yenyewe ina matatizo kibao, licha ya kuonekana ni kinara.

Pia, ukifuatilia maneno ya CEO wa Ethiopian Airlines, utaona serikali kujiingiza kwenye biashara ya ndege kisiasa kutaua shirika. Hii ni risk kubwa sana kwa ATCL. Watafanya kazi anavyotaka Magufuli, si wanavyotaka wataalamu.

Soma hapa uone vinara wanavyosuasua.

Halafu sisi serikali yetu iliyoshindwa kufanya buashara ya korosho inajiingiza kwebye biashara ya ndege kichwakichwa.

Mtaliwa kichwa mlie hapo.

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…