How GOD is smart


1. Tatizo lako maneno mengi halafu huelewi unachokiongea. Sasa hayo maelezezo uliyotoa juu umethibitisha kuwa yesu alikuwa ni binadamu tu ila Mungu ndiye alikuwa ndani ya Yesu ili Yesu aweze kufanya jambo.

2. ili Yesu nae awe Mungu inabidi ukiri ya kwamba kulikuwa na Yesu wawili kwamaana aliyekuwa duniani kufundisha waisrael na kisha akafa kifo cha laana alikuwa ni Yesu, na pia aliyekuwa mbinguni kipindi Yesu akiwa duniani ambapo Yesu alimwita kuwa ni baba; naye alikuwa ni Yesu huyo huyo kwahiyo Yesu alikuwa anajiomba mwenyewe.

3. Nimekwambia utoe andiko linalosema Yesu ni Mungu tangu mwanzo wa dunia. Umenipa 1wakorintho (10:1-4) kwenye hilo andiko hakuna mahali paliposema kuwa Yesu ni Mungu tangu mwanzo wa dunia.
Andiko lako hilo hapo ulilotoa
1 Wakorintho 10:1-4

1 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;

2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;

3 wote wakala chakula kile kile cha roho;

4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu alishagawa rizki kwa kila kiumbe hadi panya na kiroboto na alisha gawa uhai mpaka muda maalum alioamua yeye ufe. Haijalishi ni jambazi au padri au mchawi
 
Kwas sababu kila neno lake ni sheria nimependa iyoo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida unachukulia concept ya Mungu ki-binadamu
1.Yesu alikuwa Mungu na ni Mungu sasa lakini mwana wa Adam hakuwa Mungu ila Mungu alikaa ndani yake,Yule mwana wa adamu aliyeitwa Yesu Kristo alirithi Jina,nguvu,uweza,mamlaka,nk kutoka kwa baba yake ambaye ni Mungu,ndiomaana hata sisi tukifanyika kuwa wana wa Mungu basi tunarithi hivyo vyoote

2.Hapa ndio unachukulia Concept ya Mungu kibinadamu,Mungu mwenyewe kasema yeye sio mwanadamu!,Yohana anasema Mungu ni Roho (Yohana 4:24),kama ni Roho inamaana Yuko kila mahali kwa wakati mmoja,(Yeremia 23:23-33,mithali 15:3,zaburi 139:7-10).Angalia maajabu mengine ya Mungu kipindi Yesu kristo kaenda kubatizwa na Yohana mbatizaji ,
>Mungu huyo huyo alikuwa ndani ya Yohana Mbatizaji (Sababu yohana mbatizaji alizaliwa tayari kajaa roho mtakatifu Mungu alikuwa ndani yake),
>Mungu huyo huyo alikuwa ndani ya Yesu kristo (sababu imeandikwa Mungu alikuwa ndani ya kristo kuupatanisha ulimwengu na yeye)
>Mungu huyo huyo alisikika mbinguni akisema "Huyu ni mwanangu mpendwa nimependezwa naye"
Shughuli zoote hizi alikuwa anazifanya mwenyewe kwa njia mbalimbali,umeniuliza kama Yesu alikuwa anajiomba mwenyewe
inamaana hujui Yesu alikuja dunian kufanya nini!,biblia inasema hivi Yesu alikuja duniani kuacha mfano wa sisi wanadamu kuufuata (Yohana 13:13-16,1wakolinto 11:1).Alibatizwa na sisi tunabatizwa,alimuomba Mungu na sisi tunamuomba Mungu,hakutenda dhambi na sisi tunatakiwa tusitende dhambi,alifunga na sisi tunafunga,alishiriki meza ya bwana na sisi pia tunashiriki,alijawa na roho mtakatifu na sisi pia tunatakiwa kujawa na roho mtakatifu,nk ,kwahiyo alikuwa anamuomba Mungu ambaye alikuwa ndani yake,na Muda huo alikuwa mbinguni!

3.Hilo andiko nimekupa umeliandika na huo mstari wa 4 inamaana haujauelewa au ulitaka waseme Yesu kabisa na sio kristo??,ngoja nikupe na hili,umesahau Yesu mwenyewe aliulizwa yeye ni nani na akajibu Kabla ya Abraham kuwako alikuwako (Yohana 8:58) na hii (1 Wakorintho 10:1-4) huo mstari wa 4 unasema Mwamba wa Roho uliokuwa umewafuata akina Musa ni Kristo! (Yesu),
Kinacho kuchanganya ni huyu Yesu aliyekuwapo kabla na yupo sasahv na yule Yesu aliyezaliwa na bikira mariam wewe unawaona ka Yesu wawili tofauti wakati ni mmoja isipokuwa alipokuja duniani alitengeneza mwili akakaa ndani ya huo mwili ambao ulipewa jina lake YESU,Hujawahi kujiuliza kwanini hakuitwa Emmanuel kama Isaya alivyosema?
>Isaya alisema ataitwa Emmanuel (lakini akaitwa Yesu) isaya 7:14 kwanini?
>isaya huyo huyo alisema Ataitwa "Mshauri wa ajabu" "Mungu mwenye nguvu" "Baba wa milele" "Mfalme wa amani" (lakini akaitwa Yesu) kwanini hakuitwa hata moja kati ya hayo majina yoote aliyoyasema isaya?(isaya 9:6)
Jibu nikwamba Yesu hakuitwa hayo majina yoote sabau hayo sio majina bali ni Title (vyeo) au kazi za Mungu ambazo angezitenda kupitia huyo mtoto wa Kiume,badala yake Malaika alivyomtokea mariam alimwagiza mtoto aitwe YESU,kwanini Yesu kwasababu Yesu ndilo Jina la Mungu,kwahivyo kwakuwa yeye alikuwa ni mwana wa Mungu alirithi Jina la Baba yake,Kwa hivyo Jina Yesu ni jina la urithi alilopewa mwana wa Adamu "Waebrania 1:4",wafilipi 2:9-11,sasa kazi ya Yesu Kristo duniani ilikuwa ni nini? kuzaliwa,kutuonyesha binadamu kuishi maisha ya kitakatifu bila ya kutenda dhambi mpaka kufa,then pale msalabani kutolewa kafara ili kuukomboa ulimwengu kupitia ile damu na maji vilivyo mwagika pale! Biashara ikaishia hapo aliyefufuka hapo ule mwili alikuwa ni Mungu(Yesu) sasa Yule aliyekuwa ndani ya yule mtu kabla hajafa akiwa na mwili wa utukufu wake,ndio huyo atakuja tena kulichukua kanisa lake na kuhukumu Ulimwengu na ndio huyo huyo MUNGU!!

complicated eeh? Jawa na roho mtakatifu utanielewa
 
Senkiyuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Astaghafulahi...hizi kufuru ebu zitubie kiongozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kunipata tarehe na mwaka wa hayo matukio
 
Umesema kweli lkn hayo matukio Mungu aliyafanya wakat gani unaweza kunitajia mwaka ? na kwann vitabu vitakatifu havitaji miaka ya matukio mbalimbali yaliyotokea wakati huo?
 
Umesema kweli lkn hayo matukio Mungu aliyafanya wakat gani unaweza kunitajia mwaka ? na kwann vitabu vitakatifu havitaji miaka ya matukio mbalimbali yaliyotokea wakati huo?
Sijui Ni kwa sababu gani miaka haijaandikwa Wala Sijui Ni mwaka gani MUNGU MWENYEZI aliyafanya haya.Wanaojua watasema.
Ninachoweza kusema Ni kuwa hayo matukio yalitokea kipindi ambacho Adam anaumbwa.
Nimetumia source niliyonayo kufafanua kwa nini hatuwezi kumwona MUNGU MWENYEZI kwa macho yetu(Kumwona live).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini uliandika kwa lugha usiyoielewa?

Ulimaanisha nini kwa Kiswahili Hilo bichwa lako la habari?
Na we sasa unakuwa mtoto wakati ni bibi, soma maelezo yake inatosha, Kwan mtu akisema Arusa badala ya Arusha unashindwaje kuelewa kuwa alikusudia Arusha!!?
 

Hakuna ulipojibu maswali yangu zaidi ya kuleta mahubiri tu tena yote pumba tupu eti nijawe na roho mtakatifu nitakuelewa, hakuna swala la kujawa roho mtakatifu bali ni huko ni kujilazimisha kuamini bila kuhoji.

Hapa tunazungumzia uungu wa Yesu wewe umesema "
"Yesu alikuwa Mungu na ni Mungu sasa lakini mwana wa Adam hakuwa Mungu ila Mungu alikaa ndani yake,Yule mwana wa adamu aliyeitwa Yesu Kristo alirithi Jina,nguvu,uweza,mamlaka,nk kutoka kwa baba yake ambaye ni Mungu,ndiomaana hata sisi tukifanyika kuwa wana wa Mungu basi tunarithi hivyo vyoote"

Ndio maana nakwambia huelewi unachokiamini bali umekariri juu ya uungu wa yesu bila kufanya reasoning eti kisa tu eti unajawa roho na mtakatifu.

Mpaka hapo kwenye bold umeshaonesha kuna wawili tofauti (kuna Yesu na pia kuna baba yake Yesu ambaye ni Mungu)



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kunipata tarehe na mwaka wa hayo matukio
Kama kalenda tunaotumia ni ya warumi, fahamu kwamba kila jamii ilikua na kalenda yake mfano waislamu wana kalenda yao, sawa Kwa wachina, waethiopia, na jews na hata wanascience na jinsi yao ya kuhesabu siku. Kwa hy kukutajia mda exactly ni ngumu sababu hata Mungu ana kalenda yake tofauti na sis
 
Aliyeleta hizi habari za Adam kuumbwa ni nani ?
 
Sawa tutumie basi hiyo ya Mungu
 
Mbona haujamjibu? Why aumbe huo mti wa ubaya ilihali anajua fika kuwa Adamu atauchagua huo wa ubaya? Na kabla ya hapo why amuumbe shetani aliejua kabisa atamsaliti one day?
 
Mfumo aliochagua Adam ndo umeleta vurugu zote hizi tunazoziona
Why alaumiwe Adamu wakati alieumba vitu hivyo ni Mungu mwenyewe? Na hata kabla ya kuviumba alijua fika mwisho vitaleta shida na akaandaa na Jehanam kabisa.

Yaani hii ni sawa na unampa mtoto mtihani unaojua fika ataushindwa ili mwisho wa siku umuadhibu.
 

hapa umejibu tofauti na ulichoulizwa, acha mahubiri jenga tabia ya kujibu maswali kulingana na ulichoulizwa, unaulizwa yesu alikuwa anajiomba mwenyewe wewe unazunguka zunguka kwa mahubiri. ili mimi niweze kukubaliana na wewe ya kwamba Yesu ni Mungu, naomba ukiri ya kwamba aliyekuwa duniani kuokoa wana wa Israel alikuwa ni Yesu, na pia aliyekuwa mbinguni, kipindi hiko hiko Yesu akiwa duniani alikuwa ni Yesu huyo huyo. Na aliyeingia ndani wa mwili wa Yesu na Yohana alikuwa ni ni huyo huyo Yesu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…