MAKOSHNELI
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 932
- 1,569
ubarikiwe
ubarikiwe
Kwanini uliandika kwa lugha usiyoielewa?We ni mjinga nenda arusha na moshi kuna mafly catcher wengi wanajua kingereza lakin hakuna wanajua zaid ya kula unga. Unafikiri kujua kingereza ndo akili sikufahamu unapeo Mdogo hivi
Kujua kingereza sio kipimo cha akili kama unavyotaka kutuaminishaKwanini uliandika kwa lugha usiyoielewa?
Ulimaanisha nini kwa Kiswahili Hilo bichwa lako la habari?
1.Nianze na swali la pili ambalo nadhani litajibu na swali la kwanza naomba uwe unasoma na biblia haya ninayoyajibu kujihakikishia zaidi kama ni kweli imeandikwa au najitungia tu,Umejibu vizuri mkuu
Nina maswali kwanini alichomwa mkuki ubavuni na wale askari?
Siku ya tatu Yesu alifufuka but we umesema roho ambae ni Mungu aliondoka mara baada ya Yesu kufa pale msalabani je yule aliyerudi kwa manabii baada ya ufufuko alikuwa ni nani?
Je bikira Maria aliendeleza familia I mean kuwa na watoto wengine baada ya Yesu au aliishia uzazi wa Yesu?
Nijib maswali yangu tafadhali
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana mkuu nashukuru mnoo1.Nianze na swali la pili ambalo nadhani litajibu na swali la kwanza naomba uwe unasoma na biblia haya ninayoyajibu kujihakikishia zaidi kama ni kweli imeandikwa au najitungia tu,
>Pale msalabani kipindi Yesu katundikwa kuna mambo Mengi yalitokea nitaelezea haya... Jambo la kwanza Yesu,Yesu alipaza sauti akalia "Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha" (Mathayo 27:46)" Kwanini alisema Mungu wangu Mbona umeniacha??,Nikweli Mungu alimuacha, Kwakuwa Mungu alikuwa ndani ya Yesu,au roho wa Mungu alikuwa ndani ya Yesu alitoka,ROHO YA MUNGU ILIYOKUWA NDANI YA YESU ILITOKA,Pale Yesu akabakia na pumzi tu kumbuka Roho ya Mungu ina kazi mbili kazi ya kwanza ni kuleta Pumzi/Uhai kwa Mtu ndiomaana imeandikwa Mungu alipomuumba Adam halafu ili awe hai Mungu alimpulizia Pumzi (Mwanzo 2:7),kwahiyo kila binadamu aliye hai na ana Pumzi ana Roho ya Mungu ndani yake,Na kazi ya pili ya Roho wa Mungu ni kuleta uzima wa milele,Hii ndio Roho mtakatifu,ndio ile roho ya milele, ndio ile imeandikwa mwili bila roho umekufa (Yakobo 2:26,Warumi 8:9-17)
Kwahivyo mwanzo Yesu alivyolia mara ya kwanza kuwa "Mungu mbona umeniacha", Roho mtakatifu (Mungu) alitoka ndani yake akaenda wapi? Roho wa Mungu alienda kuzihubiria zile roho zilizokuwa mateka KUZIMU,Kumbuka wale wafu watu woote waliokuwa wamekufa kuanzia Adam hadi kipindi cha Yesu iliwapasa nao pia waisikie injili kusudi siku ya mwisho woote tuhukumiwe kwa kipimo sawa asiwepo wakusema hakuisikia injili!! kipimo ni injili,ndio maana hata petro alisema kwa sababu hii hata wafu walihubiriwa injili(1 Petro 4:5-6)!!
Sasa na Yesu alipolia kwa sauti tena Mara Ya Pili akaitoa Roho yake akafa (Mathayo 27:50) then pazia la hekalu likapasuka katikati kuonyesha kuwa hekalu halina maana tena sasa hekalu ni katika miili yetu (1 Wakorinto 6:19-20) ,then Makaburi yakafunuka,ikainuka miili ya watakatifu waliolala (Mathayo 27:52-53),(ndio hawa Roho ya Mungu ilienda kuwahubiria injili huko walikokuwa)!,sasa Pale msalabani ukabaki mwili wa Yesu bila Uhai (fresh and bones),Baadaye ukachukuliwa ukawekwa kaburin.
Sasa nikirudi kwenye swali lako Yule aliyerudi kwa manabii alikuwa ni nani? Ulikuwa ni mwili wa Yesu uliotukuzwa,mwili wa kiroho soma (1 wakorinto 15:35-49,1 Petro 3:18,) ndiomaana Ule mwili wa Yesu ulikuwa na uwezo wa kutokea na kupotea,ule ulikuwa mwili wa kiroho,Yule sasa alikuwa MUNGU na ni Mungu hadi leo hii na atakuja tena kwa mara ya pili
2.Swali la kwanza kwanini alichomwa mkuki ubavuni halafu ikatoka DAMU NA MAJI?
>Yesu kabla hajapaa kwenda mbinguni alitoa amri kwa wanafunzi wake waende ulimwenguni koote wakawafanye mataifa kuwa wanafunzi wake kivp ?,kwa kuwabatiza kwajina la Baba,la mwana na roho mtakatifu,sasa Yale maji yaliyotoka pale msalabani yalikuwa yanamaanisha Ubatizo,ilikuwa ni ishara ya vile vitu vitatu ambavyo wanafunzi wa Yesu walianza kufanya baada ya kupokea roho mtakatifu ile siku ya Pentecoste,petro mara baada ya kupokea Roho mtakatifu na kuanza kuwahubiria watu alisema hivi "Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu " kwahiyo hatua ya kwanza ni TOBA,unatubu dhambi zako,then hatua ya pili ni UNABATIZWA KWA JINA LA YESU KRISTO (sio kwa jina la baba,mwana na roho mtakatifu),halafu unapata ondoleo la dhambi,unakuwa umetakasika huna dhambi,halafu ili sasa roho yako iokolewe lazma upokee Roho mtakatifu,utakumbuka hapo mwanzo ili utakasike upate ondoleo la dhambi ilikuwa lazima utoe kafara ya mnyama,sasa kwakuwa kafara ilishafanyika pale msalabani na Damu ilitoka unachotakiwa wewe ni kutubu(kutambua kifo cha Yesu pale msalabani) ndio ile Damu ya Yesu iliyotoka baada ya kuchomwa ubavuni ,then Ubatizwe ,ndio yale maji yaliyotoka ubavuni kwa Yesu halafu Upate roho mtakatifu,ndio Yesu alivyofufuka katika wafu!
Ndiomaana mitume walisema ubatizo ni ishara ya kuzikwa na kufufuka pamoja na Yesu (Warumi 6:3-5),Na pia ondoleo la dhambi ni lazima damu imwagike (Waebrania 9:22-28) ndiomaana pale msalabani alipochomwa ubavuni ilitoka Damu na Maji,Tunapata Damu yake kwa kukiri kifo chake pale msalabani,halafu tunapata maji kwa kubatizwa kwa jina la Yesu hivi vitu viwili tunapata ondoleo la dhambi,then unapokea kipawa cha Roho Mtakatifu
Ndiomaana kipindi cha Musa wana wa israel walikuwa wanabatizwa lakini haikuwa effectively sababu Damu ilikuwa bado haijamwagika pale msalabani,hata kipindi cha Yohana mbatizaji bado ubatizo wake haukuwa umetimia sababu Yesu alikuwa hajafa bado pale msalabani,ila alivyokufa msalabani ndiomaana wanafunzi wake walipewa maagizo "TUBUNI,MKABATIZWE KWA JINA LA YESU KRISTO ,HALAFU UPOKEE ROHO MTAKATIFU"
3.Swali la tatu kuhusu mariam kuendeleza Familia
>Jibu ni ndio Mariam na Yusufu waliendeleza familia walizaa watoto wengine baada ya Yesu kuzaliwa kwa uweza wa roho ,majina ya watoto wao yalikuwa ni (wakiume na usichanganye majina ya hao watatu wa mwisho na ya wale wanafunzi wake 12) Joseph,Yakobo,Yuda na Simon (Mathayo 12:46,Mathayo 13:55,Marko 6:3) na pia mary alikuwa na watoto wa kike majina yao hayakutajwa kwenye biblia


wapi imeandikwa kwenye biblia?tulisoma moja ya mfano wa nomino za dhahania (abstract noun) ni Mungu
Kwa nin ni Mungu Baba na Sio Mungu Mama??Hakuna binadamu anayefikia u-smart alionao Mungu, kwanza kabisa Mungu hawezi vunja sheria aliyojiwekea tofaut na mwanadamu, pili Mungu sio muongeaji ongeaji hovyo, huwa ana maneno machache Kwa sababu kila neno lake ni sheria.
Watu wengi tumekua tukijiuliza Kwa nin Mungu aliruhusu shetani amdanganye hawa, jibu ni kwamba Mungu alimpa mwanadamu option mbili ya kumkata au kumkubali, bahati mbaya Adam akamkataa Mungu, na Mungu bila hiana akakubaliana na adamu kwa-sababu angeingilia angevunja sheria aliyojiweka yeye. Na shetan anamjua Mungu Kwa sababu ameshakaa naye ndo maana alijiamini alivyomfuata hawa.
Ndo maana hata wanadamu wanamtukana Mungu na haingilii, jibu ni kwamba hawez kukulazimisha umtumikie/umfuate, yaan wanafamu tuna Uhuru wa kumkataa Mungu, ndo maana ni Hatar sana kulazimisha watu kumfuata Mungu.
Mungu hawez kuja kuishi duniani Kwa sababu in roho (spirit), ili uishi duniani lazima uwe na mwili (dead body), ndo maana hata majini lazima yamwingilie MTU yaishi ndani yake Kwa sababu ili uishi dunian ni lazima uwe na mwili.
Shetani ilimbidi amuombe nyoka mwili ili autumie mwili wake kumdanganya Adam na hawa Kwa sababu na yeye ni roho
Hata binadamu akifa kinachokufa ni mwili na sio roho, ndo maana baada ya kufa roho haiwez ishi duniani Kwa sababu ni illegal Kwa roho kuish duniani, kwa hy lazima iondoke, ndo maana Mungu alimtuma YESU aje na mwili wa binadamu ili atimize lengo lake.
Ndo maana dhana nzima ya maombi ikaja, Kwa sababu ukitaka kitu lazima umuombe Mungu Kwa sababu ana uhakika unataka jambo fulani au hulitaki, Kwa sababu kabla ya mwanadamu kuasi kulikua na fellowship na sio maombi.
Asante sana mkuu nashukuru mnoo
Una kipaji cha kumuelewesha mtu, japo nasoma biblia ila kuna vitu vingi vinapiga chenga!
Swali la mwisho...
Kila binadamu huwa kuna ile unataka kufanya jambo fulani especially baya na nafsi inakukataza hata ukilifanya but huwa ishakuonya!
Na hapohapo ukifanya jambo jema nafsi inafurahi au inakupongeza!
Hiki kitu ni mimi peke yangu au ni kila mtu? Na je hiyo nafsi ni ipi? ....natanguliza shukrani
Sent using Jamii Forums mobile app
Neno "Mungu Baba" ni cheo (TITLE)" kinachotumika kuelezea shughuli za Mungu,kwanini aitwe Baba na sio Mama,Anaitwa Baba kwanza kwasababu Yeye ndio muumba wa vitu vyoote vinavyoonekana na visivyoonekana (1 wakolinto 8:6),Pili anaitwa Baba kwasababu hapo mwanzo aliumba mtu kwa mfano wake na aliumba Mwanaume kwanza na sio mwanamke,sasa kama aliumba mwanaume kwa mfano wake hawezi kuitwa Mama inamaana yeye ni Baba.Kwa nin ni Mungu Baba na Sio Mungu Mama??
Kuna tatizo gani hapa??
Sent using Jamii Forums mobile app
maswali yako ni mazuri na nitayajibu kama ifuatavyo
1.Nature/Asili ya Mungu ni ROHO na ipo kila mahali
>Mungu hakujigawa vipande vipande,na wala Mungu huwa hajigawi yeye Alikuwepo mwanzo,Yupo sasa na Atakuwepo milele na milele,Mungu ni wa MILELE (EVALASTING) (ISAYA 40:28),
>Mungu yupo kila mahali (YEREMIA 23:23-33),Dunia na Mbingu hazimtoshi kukaa ndani yake (1 WAFALME 8:27,ZABURI 139:7-12)
2.swali la pili Kuhusu Mungu YESU
Naweza kuandika kitabu kizima kuhusu Uungu wa YESU kwakuwa ni maada pana sana na inahitaji uelewa wa hali ya juu wa ki biblia kwa mtu kuelewa hapa nitajitahidi kwa Ufupi,
YESU NI MUNGU SASA NA YESU HAKUWA MUNGU KILE KIPINDI YUPO DUNIANI ILA MUNGU ALIKAA NDANI YAKE!
Kumbuka tuna Mungu mmoja tu! narudia Tuna Mungu mmoja tu na ambaye hajagawanyika kwa namna yoyote ile,hana Baba wala hana Mama na hana Wasaidizi,Hakuumbwa,Alikuwepo,Yupo,na atakuwepo! MUNGU NI MMOJA Soma (Kumbukumbu 6:4,Marko 12:32,Wagalatia 3:20, nk.....)
Sasa kwa ufupi nianze kuelezea kwanini Yesu alikuja duniani ,chanzo cha Yesu kuja duniani ni Adam na hawa kutenda ile dhambi pale bustani ya eden Uhusiano wa mwanadamu na Mungu ukavurugika wanadamu woote tukawa tunarithi ile dhambi ya ADAM NA HAWA (Warumi 5:12-15),kutokana na ukaidi wa Adam na Hawa dhambi iliingia kwa vizazi vyoote vya Wanadamu sasa ili kurejesha uhusiano na Mungu,Mungu mwenyewe aliweka Sheria,kanuni na taratibu kwa wanadamu wa kufanya na kuzifuata ili wawe safi machoni pake(wajitakase) utaratibu huo ilikuwa ni Kutoa kafara ya mnyama (MWANAKONDOO AU NG'OMBE nk ALIYENONA),hii iliitwa KAFARA YA MNYAMA ndio hii ilianza kifanywa na ABELna KAINI ndugu yake mmoja kafara yake ilikubaliwa na mwingine ilikataliwa sababu alitoa wanyama ambao hawakunona nadhani story unaijua vizuri ipo (MWANZO 4:4),sasa hizi kafara za mnyama ziliendelea kufanyika kwenye Agano loote la kale kuanzia kitabu cha Mwanzo mpaka Malaki utakutana na kafara za aina hii ambazo zilikuwa ni kama ishara(SYMBOLISM) tu ya kurejesha mahusiano kati ya Mungu na wanadamu na Yule mnyama anayetolewa kafara ndio alikuwa anawakilisha kubeba dhambi za hao wanadamu waliomtolea kafara kupitia damu yake,na ndiomaana kafara zoote mnyama alikuwa anachinjwa au anachomwa moto ili damu itoke ifanye upatanisho kati ya wanadamu na Mungu
Sasa kwa miaka Mingi Mungu alianza kuwaambia wanadamu kupitia manabii na mitume wake kuwa kunakafara Halisi atakuja kuifanya Duniani,MUNGU ATAFANYA KITU KIPYA DUNIANI! (ISAYA 43:19,ISAYA 11:1,ISAYA 7:14,ISAYA 9:6,HESABU 24:17) ,sasa hikikitu kipya ni Kuzaliwa kwa Yesu Kristo na hadi kufa kwake,haya tukija agano Jipya sasa tunaona unabii unatimizwa Mwanamke Bikira anapata Mimba kwa njia ya uweza wa Roho mtakatifu anazaa mtoto wa Kiume jina anaitwa YESU!
> Sasa nirudi kwenye swali lako Je Huyu mtoto wa kiume aliyezaliwa akaitwa Yesu alikuwa ni Mungu??! Jibu ni HAPANA hakuwa Mungu,ukisema yule mwana wa YUSUFU NA MARIAMU aliyeitwa YESU alikuwa ni Mungu utakuwa unapingana na maandiko inamaana kuna Miungu zaidi ya wawili! na wakati biblia yoote inasema Mungu ni mmoja na hajagawanyika!.
> Na pia ukisema Yesu mwana wa Yusufu alikuwa ni Mungu unakosea Sababu utakuwa unaweka Umri Juu ya Mungu wakati Mungu hana umri nimeandika juu hapo kuwa Mungu ni wamilele aliumba vyoote pamoja na MUDA!,Yesu alizaliwa na mwanadamu ila Mungu hakuzaliwa alikuwepo kabla ya mwanadamu na aliumba mwanadamu,Yesu aliitwa Mtume/mwalimu na Nabii (WAEBRANIA 3:1) lakini MUNGU sio mtume wala sio nabii kwasababu hatumwi na kitu chochote lakini nabii na mitume ni watumwa wa Mungu!
>Sasa Yesu ni nani kile kipindi yupo Duniani? Aliitwa MWANA WA MUNGU,kwanini aliitwa mwana wa Mungu sababu kuja kwake hapa duniani ni Mungu mwenyewe alimfanya,kumbuka bikira mariamu alipata mimba kwa uweza wa roho mtakatifu na si kwa kukutana na mmewe YUSUFU! ndiomaana aliitwa Mwana wa MUNGU,mtu mwingine aliitwa mwana wa MUNGU ni ADAMU sababu ADAMU hakuzaliwa na binadamu naye kuja kwake hapa duniani aliumbwa na MUNGU moja kwa Moja (Luka 3:38) ndiomaana kuna mitume walisema na kuandika kuwa YESU alikuwa ADAMU WA PILI (1Wakolinto 15:22)
>Biblia inasema wazi kuwa kabla ya Mungu kuamua kuja duniani kupitia Yesu Kristo ili kufanya upatanisho baina yake na wanadamu alitafuta wa kumtuma ,MBINGUNI,DUNIANI,ULIMWENGUNI NA CHINI YA DUNIANI hakuona anayefaa kwenda kuwakomboa wanadamu (UFUNUO 5:3) hapa inakupa mwanga kuwa kumbe alishuka mwenyewe kuja duniani kufanya upatanisho kati yake mwenyewe na wanadamu sasa alishuka kivipi????, Aliingia kwenye ukoo wa Daudi kama ilivyotabiriwa na Manabii (ISAYA 11:1-2,ZAKARIA 3:8,6:12) then akatengeneza mwili ambao ukazaliwa na mwanamke bikira Halafu Mungu akajificha ndani ya huo mwili (2 Wakorinto 5:17-21),ndiomaana Yesu kazi zoote alizokuwa akifanya hapa Duniani alikuwa anampoint Mungu aliyekuwa ndani yake,aliweza kufufua wafu,kutembea juu ya maji,kuponya wagonjwa na vilema,kulisha maelfu ya watu,vyoote hivyo alivifanya kama chombo tu lakini mfanyaji mkubwa alikuwa ndani yake (YOHANA 5:17-27,Yohana 14:10),Yesu nje alikuwa MTU kwa asilimia 100 halafu ndani alikuwa MUNGU kwa asilimia 100!
>Sasa Muda wa kufanyika kafara ukafika pale masalabani (Hapa ndipo pana akili sana),Mungu mwenyewe alitoa kafara pale msalabani ili kujipatanisha yeye na Wanadamu,wayahudi walipomsulubisha Yesu pale msalabani kuna vitu muhimusana vilifanyika kwenye maisha ya wanadamu Cha kwanza Yesu alisema imekwisha akaisalimisha Roho yake(Yohana 19:30),kimsingi Mungu aliyekuwa ndani ya Yesu akatoka sasa kwenda wapi?,kwenda kuhubiria roho zilizokuwa mateka kuanzia kizazi cha Adamu hadi wakati ule wa Yesu woote walihubiriwa injili kusudi siku ya mwisho woote tuhukumiwe kwa hukumu moja!, then cha pili wayahudi walipokuja mara ya pili kuwavunja Miguu wale watu watatu akiwamo Yesu pale msalabani yeye Yesu hakuvunjwa mahalipopote kumbuka hukomwanzo nimesema mnyama aliyekuwa akitolewa kafara hakutakiwa awe kilema wala mwenye mawaa,ndiomaana Yesu hakufunjwa mguu wowote pale msalabani ili kafara yake iwe parfect! (Yohana 19:32-34) ila wale askari walimchoma ubavuni mwake then ikatoka DAMU na MAJI!!!! Ndio hii kafara ilifanyika pale msalabani na wanadamu tulikombolewa kwa damu ya Yesu kristo na Maji,(nitakufafanulia kwanini ilitoka Damu na Maji kwenye topic zijazo)
Hebu tuandikie wewe tuone ukomavu wakoKijana wewe ni mchanga sana kwenye hili swala.
Mpumbavu Kasema hakuna Mungumaswala ya mungu ni chai tu hana lolote
Bonge la point, wanadhani Mungu anavaa sutiMungu amewapa ruhusa ya watu kama nyingi kumkataa, na kama unafikiri utamjua Mungu kwa akili za kibinadamu utasubiri sana
Mungu siyo Binadamu so stop challenging himIf God is perfection kwanini ameumba viumbe ambao ni imperfection
iPhone 7plus
Unaweza kuthibitisha walau kwa kifupi kuwa Mungu yupo na si hadithi za wanadamu?
Ili kuthibitisha upumbavu wake, mwonyeshe kuwa huyo Mungu yupo isije kuwa wewe ndio mpumbavu namba moja
Angalau wewe umeniuliza kwa kuweka na vifungu vya biblia tunaweza kuelimishana kwa maandiko na sio maneno matupu,Unaongea bila kujua unachokiongea
1. Unaposema "Yesu hakuwa Mungu kipindi yesu alivyokuwa duniani ila Mungu alikuwa ndani ya Yesu. Unazungumzia Mungu yupi tena tofauti na Yesu? Hivi unauelewa wa kutosha kuhusu Uungu? Umeshasema Mungu kaingia kwa X kwahiyo huyu X hawezi kuwa Mungu bali Mungu atabaki kuwa Mungu na huyu X atabakia vile vile kuitwa X . Je Roho ikikuingia wewe @MAKOSHNEL tutasema @MAKOSHNEL ni Mungu?
Kumbe Yesu sio Mungu bali Mungu mdiye aliyekuwa ndani ya Yesu kwa mantiki hiyo basi Mungu alikuwa ndani ya mitume na manabii wote. Hata wewe Mungu anaweza kuwa ndani yako pia ukitaka.
Kwahiyo Yesu ni Yesu na Mungu ni Mungu.
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
Matendo 3:26
Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabariki kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.
Sent using Jamii Forums mobile app
Angalau wewe umeniuliza kwa kuweka na vifungu vya biblia tunaweza kuelimishana kwa maandiko na sio maneno matupu,
>Swali la kwanza,Yule mwana wa mariam hakuwa Mungu bali Mungu alikuwa ndani yake anafanya zile kazi,,
"YESU ALIKUWA MUNGU TANGU MWANZO WA DUNIA, NA NI MUNGU SASA LAKINI YULE MTU ALIYEZALIWA NA BIKIRA MARIAMU AKAITWA JINA YESU HAKUWA MUNGU ILA MUNGU ALIKAA NDANI YAKE"
Yule Mwana wa mariam (YESU) alikuwa ni chombo tu cha Mungu kufanyia kazi zake hapa duniani yule alikuwa na Vyeo (TITLES) Mbalimbali ndio-maana aliitwa Nabii,Mwana wa Adam,Mwalimu,Mtume,mwana kondoo,Mwana wa Mungu,Kristo,masihi wa bwana,
,Pia hujawahi kusoma andiko linasema atazaliwa mtoto mwanaume jina lake ataitwa Emmanuel maana yake ni "MUNGU PAMOJA NASI" ? (Isaya 7:14,Matayo 1:23),kivipi Mungu pamoja nasi??,inamaana bikira mariamu alimzaa MUNGU?? HAPANA! kwanini Hapana? kwa sababu
> Mungu hazaliwi (Yesu kristo alizaliwa),wala
>Mungu hana Baba wala hana mama (Yesu kristo alikuwa nao)
>Mungu Hakui kiumri na maarifa(Yesu alikua kiumri na maarifa Luka 2:52)
>Mungu Hana mwanzo na hana Mwisho(Mwana wa adamu mwanzo wake alizaliwa na mama yake na mwisho wake alisulubiwa msalabani)
>Mungu Alikuwepo kabla ya vyoote(mwana wa adamu alikuja baadaye),
>Mungu Ni wa milele na milele (mwana wa adamu alikufa msalabani)
>Mungu hafi (Mwana wa Adam alikufa)
Sasa KIVIPI EMMANUELI MUNGU PAMOJA NASI?? Jibu lipo 2 Wakolinto 5:19 inasema hivi "yaani, 'Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho"
kumbe Yule mtoto aliyezaliwa na Bikira mariamu akaitwa Yesu hakuwa Mungu ila Mungu alikaa ndani yake,Mungu alijificha ndani yake,Mungu huwaga anajificha (ISAYA 45:15)!,
Yesu alisema "ukiniona mimi Umemuona Mungu" (Yohana 14:9) Kivipi umemuona Mungu wakati Mungu ni Roho na haonekani?,kivipi wakati Mungu sio mwanadamu Yesu alikuwa mwanadamu??,alikuwa anamaanisha Kupitia Kazi anazozifanya sababu yeye hafanyi chochote isipokuwa Mungu ambaye yupo ndani yake ndio anafanya!,yeye anatumika tu kama chombo (Yohana 14:10)!,
>Kwahiyo Mungu akiingia kwa kitu hicho kitu hakiwi Mungu bali Mungu anakuwa kajidhihirisha kupitia hicho kitu
>Yesu ni Mungu sasa na alikuwa Mungu kabla ila yule binadamu aliyezaliwa na Bikira mariam akaitwa Yesu hakuwa Mungu bali alikuwa Mwana wa Mungu ,kwakuwa alikuwa mwana wa Mungu alirithi jina la Mungu Baba ambalo ni Yesu,Mungu alikuwa ndani yake
>Hiyo yohana 17:3 ,nikweli Yesu alitumwa na Mungu kivipi? ndio nimekuelezea hapo juu,sasa ili umjue Mungu unatakiwa ukubali matendo ya mwili ya mwanaye wa pekeealiyoyafanya hapa duniani kwasababu yalikuwa kama mfano kwetu namna gani tufanye hapa duniani ili kuurithi ufalme wa Mungu,ndiomaana tunabatizwa,sababu Yesu alibatizwa,tunajawa na roho mtakatifu sababu Yesu alijawa na roho mtakatifu nk..
>Matendo 3:26 sasa huyo Yesu aliyefufuka sio yule aliyekufa,hata mwili wake ulikuwa tofauti ulikuwa na uwezo wa kutokea na kupotea,ulikuwa ni mwili wa kiroho au mwili uliotukuzwa,ndio huo mwili tutakuwa nao tutakapokuwa mbinguni (Wafilipi 3:20-21)
Sema hujaelewa sio nimejichanganya,vifungu vyoote nilivyokuwekea bado unasema nimejichanganya,concept ya Yesu sio wewe pekeyako inakuchanganya,imewachanganya wanaojiita wasomi wa theolojia,wachungaji na maaskofu na wakaishia kusema Mungu kagawanyika sehem tatu (Baba,mwana na roho mtakatifu) sembuse wewe,inahitaji uwe na roho mtakatifu ndani yako kuweza kupata maana za kwenye biblia,biblia haisomwi kama Gazeti na kwa utashi wa mwanadamu,1.Kwanza umejichanganya sana,
Kwa maelezo yako uliyotoa umedhihirisha ya kwamba Yesu hakuwa Mungu ila Mungu ndiye aliyekaa ndani ya Yesu hivyo hili linadhihirisha ya kwamba hakuna Mungu anayeitwa Yesu. Halafu Kwenye hitimisho yako umehitimisha yesu ni Mungu nawakati umeshatoa maelezo ya kutosha juu, ya kwamba Yesu hakuwa Mungu na sababu umetoa za kutosha kwa Yesu kutokuwa Mungu.
2. Toa andiko linalosema Yesu alikuwa ni Mungu, tangu mwanzo wa dunia ili kuthibitisha kauli yako ili tuijadili hapa hilo andiko.
3. Unaweza kuniambia Kuna yesu wangapi?
4. Kwa kusema kwako kuwa Yesu ni Mungu, naomba utoe andiko likionesha huyu Yesu kuja kwake duniani kajituma/kajiagiza mwenyewe badala ya kutumwa na Mungu ili tuone Yesu yupo juu ya daraja ya Uungu au yupo chini ya daraja ya Uungu.
Yohana 14:28
28 Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.
Sent using Jamii Forums mobile app