Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,560
- 5,249
Yule Mwana wa mariam (YESU) alikuwa ni chombo tu cha Mungu kufanyia kazi zake hapa duniani yule alikuwa na Vyeo (TITLES) Mbalimbali ndio-maana aliitwa Nabii,Mwana wa Adam,Mwalimu,Mtume,mwana kondoo,Mwana wa Mungu,Kristo,masihi wa bwana,
,Pia hujawahi kusoma andiko linasema atazaliwa mtoto mwanaume jina lake ataitwa Emmanuel maana yake ni "MUNGU PAMOJA NASI" ? (Isaya 7:14,Matayo 1:23),kivipi Mungu pamoja nasi??,inamaana bikira mariamu alimzaa MUNGU?? HAPANA! kwanini Hapana? kwa sababu
> Mungu hazaliwi (Yesu kristo alizaliwa),wala
>Mungu hana Baba wala hana mama (Yesu kristo alikuwa nao)
>Mungu Hakui kiumri na maarifa(Yesu alikua kiumri na maarifa Luka 2:52)
>Mungu Hana mwanzo na hana Mwisho(Mwana wa adamu mwanzo wake alizaliwa na mama yake na mwisho wake alisulubiwa msalabani)
>Mungu Alikuwepo kabla ya vyoote(mwana wa adamu alikuja baadaye),
>Mungu Ni wa milele na milele (mwana wa adamu alikufa msalabani)
>Mungu hafi (Mwana wa Adam alikufa)
Sasa KIVIPI EMMANUELI MUNGU PAMOJA NASI?? Jibu lipo 2 Wakolinto 5:19 inasema hivi "yaani, 'Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho"
kumbe Yule mtoto aliyezaliwa na Bikira mariamu akaitwa Yesu hakuwa Mungu ila Mungu alikaa ndani yake,Mungu alijificha ndani yake,Mungu huwaga anajificha (ISAYA 45:15)!,
Yesu alisema "ukiniona mimi Umemuona Mungu" (Yohana 14:9) Kivipi umemuona Mungu wakati Mungu ni Roho na haonekani?,kivipi wakati Mungu sio mwanadamu Yesu alikuwa mwanadamu??,alikuwa anamaanisha Kupitia Kazi anazozifanya sababu yeye hafanyi chochote isipokuwa Mungu ambaye yupo ndani yake ndio anafanya!,yeye anatumika tu kama chombo (Yohana 14:10)!,
>Kwahiyo Mungu akiingia kwa kitu hicho kitu hakiwi Mungu bali Mungu anakuwa kajidhihirisha kupitia hicho kitu
>Yesu ni Mungu sasa na alikuwa Mungu kabla ila yule binadamu aliyezaliwa na Bikira mariam akaitwa Yesu hakuwa Mungu bali alikuwa Mwana wa Mungu ,kwakuwa alikuwa mwana wa Mungu alirithi jina la Mungu Baba ambalo ni Yesu,Mungu alikuwa ndani yake
>Hiyo yohana 17:3 ,nikweli Yesu alitumwa na Mungu kivipi? ndio nimekuelezea hapo juu,sasa ili umjue Mungu unatakiwa ukubali matendo ya mwili ya mwanaye wa pekeealiyoyafanya hapa duniani kwasababu yalikuwa kama mfano kwetu namna gani tufanye hapa duniani ili kuurithi ufalme wa Mungu,ndiomaana tunabatizwa,sababu Yesu alibatizwa,tunajawa na roho mtakatifu sababu Yesu alijawa na roho mtakatifu nk..
1. Tatizo lako maneno mengi halafu huelewi unachokiongea. Sasa hayo maelezezo uliyotoa juu umethibitisha kuwa yesu alikuwa ni binadamu tu ila Mungu ndiye alikuwa ndani ya Yesu ili Yesu aweze kufanya jambo.
2. ili Yesu nae awe Mungu inabidi ukiri ya kwamba kulikuwa na Yesu wawili kwamaana aliyekuwa duniani kufundisha waisrael na kisha akafa kifo cha laana alikuwa ni Yesu, na pia aliyekuwa mbinguni kipindi Yesu akiwa duniani ambapo Yesu alimwita kuwa ni baba; naye alikuwa ni Yesu huyo huyo kwahiyo Yesu alikuwa anajiomba mwenyewe.
3. Nimekwambia utoe andiko linalosema Yesu ni Mungu tangu mwanzo wa dunia. Umenipa 1wakorintho (10:1-4) kwenye hilo andiko hakuna mahali paliposema kuwa Yesu ni Mungu tangu mwanzo wa dunia.
Andiko lako hilo hapo ulilotoa
1 Wakorintho 10:1-4
1 Kwa maana, ndugu zangu, sipendi mkose kufahamu ya kuwa baba zetu walikuwa wote chini ya wingu; wote wakapita kati ya bahari;
2 wote wakabatizwa wawe wa Musa katika wingu na katika bahari;
3 wote wakala chakula kile kile cha roho;
4 wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
Sent using Jamii Forums mobile app
