How GOD is smart

We ni mjinga nenda arusha na moshi kuna mafly catcher wengi wanajua kingereza lakin hakuna wanajua zaid ya kula unga. Unafikiri kujua kingereza ndo akili sikufahamu unapeo Mdogo hivi
Kwanini uliandika kwa lugha usiyoielewa?

Ulimaanisha nini kwa Kiswahili Hilo bichwa lako la habari?
 
1.Nianze na swali la pili ambalo nadhani litajibu na swali la kwanza naomba uwe unasoma na biblia haya ninayoyajibu kujihakikishia zaidi kama ni kweli imeandikwa au najitungia tu,
>Pale msalabani kipindi Yesu katundikwa kuna mambo Mengi yalitokea nitaelezea haya... Jambo la kwanza Yesu,Yesu alipaza sauti akalia "Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha" (Mathayo 27:46)" Kwanini alisema Mungu wangu Mbona umeniacha??,Nikweli Mungu alimuacha, Kwakuwa Mungu alikuwa ndani ya Yesu,au roho wa Mungu alikuwa ndani ya Yesu alitoka,ROHO YA MUNGU ILIYOKUWA NDANI YA YESU ILITOKA,Pale Yesu akabakia na pumzi tu kumbuka Roho ya Mungu ina kazi mbili kazi ya kwanza ni kuleta Pumzi/Uhai kwa Mtu ndiomaana imeandikwa Mungu alipomuumba Adam halafu ili awe hai Mungu alimpulizia Pumzi (Mwanzo 2:7),kwahiyo kila binadamu aliye hai na ana Pumzi ana Roho ya Mungu ndani yake,Na kazi ya pili ya Roho wa Mungu ni kuleta uzima wa milele,Hii ndio Roho mtakatifu,ndio ile roho ya milele, ndio ile imeandikwa mwili bila roho umekufa (Yakobo 2:26,Warumi 8:9-17)
Kwahivyo mwanzo Yesu alivyolia mara ya kwanza kuwa "Mungu mbona umeniacha", Roho mtakatifu (Mungu) alitoka ndani yake akaenda wapi? Roho wa Mungu alienda kuzihubiria zile roho zilizokuwa mateka KUZIMU,Kumbuka wale wafu watu woote waliokuwa wamekufa kuanzia Adam hadi kipindi cha Yesu iliwapasa nao pia waisikie injili kusudi siku ya mwisho woote tuhukumiwe kwa kipimo sawa asiwepo wakusema hakuisikia injili!! kipimo ni injili,ndio maana hata petro alisema kwa sababu hii hata wafu walihubiriwa injili(1 Petro 4:5-6)!!
Sasa na Yesu alipolia kwa sauti tena Mara Ya Pili akaitoa Roho yake akafa (Mathayo 27:50) then pazia la hekalu likapasuka katikati kuonyesha kuwa hekalu halina maana tena sasa hekalu ni katika miili yetu (1 Wakorinto 6:19-20) ,then Makaburi yakafunuka,ikainuka miili ya watakatifu waliolala (Mathayo 27:52-53),(ndio hawa Roho ya Mungu ilienda kuwahubiria injili huko walikokuwa)!,sasa Pale msalabani ukabaki mwili wa Yesu bila Uhai (fresh and bones),Baadaye ukachukuliwa ukawekwa kaburin.
Sasa nikirudi kwenye swali lako Yule aliyerudi kwa manabii alikuwa ni nani? Ulikuwa ni mwili wa Yesu uliotukuzwa,mwili wa kiroho soma (1 wakorinto 15:35-49,1 Petro 3:18,) ndiomaana Ule mwili wa Yesu ulikuwa na uwezo wa kutokea na kupotea,ule ulikuwa mwili wa kiroho,Yule sasa alikuwa MUNGU na ni Mungu hadi leo hii na atakuja tena kwa mara ya pili

2.Swali la kwanza kwanini alichomwa mkuki ubavuni halafu ikatoka DAMU NA MAJI?
>Yesu kabla hajapaa kwenda mbinguni alitoa amri kwa wanafunzi wake waende ulimwenguni koote wakawafanye mataifa kuwa wanafunzi wake kivp ?,kwa kuwabatiza kwajina la Baba,la mwana na roho mtakatifu,sasa Yale maji yaliyotoka pale msalabani yalikuwa yanamaanisha Ubatizo,ilikuwa ni ishara ya vile vitu vitatu ambavyo wanafunzi wa Yesu walianza kufanya baada ya kupokea roho mtakatifu ile siku ya Pentecoste,petro mara baada ya kupokea Roho mtakatifu na kuanza kuwahubiria watu alisema hivi "Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu " kwahiyo hatua ya kwanza ni TOBA,unatubu dhambi zako,then hatua ya pili ni UNABATIZWA KWA JINA LA YESU KRISTO (sio kwa jina la baba,mwana na roho mtakatifu),halafu unapata ondoleo la dhambi,unakuwa umetakasika huna dhambi,halafu ili sasa roho yako iokolewe lazma upokee Roho mtakatifu,utakumbuka hapo mwanzo ili utakasike upate ondoleo la dhambi ilikuwa lazima utoe kafara ya mnyama,sasa kwakuwa kafara ilishafanyika pale msalabani na Damu ilitoka unachotakiwa wewe ni kutubu(kutambua kifo cha Yesu pale msalabani) ndio ile Damu ya Yesu iliyotoka baada ya kuchomwa ubavuni ,then Ubatizwe ,ndio yale maji yaliyotoka ubavuni kwa Yesu halafu Upate roho mtakatifu,ndio Yesu alivyofufuka katika wafu!
Ndiomaana mitume walisema ubatizo ni ishara ya kuzikwa na kufufuka pamoja na Yesu (Warumi 6:3-5),Na pia ondoleo la dhambi ni lazima damu imwagike (Waebrania 9:22-28) ndiomaana pale msalabani alipochomwa ubavuni ilitoka Damu na Maji,Tunapata Damu yake kwa kukiri kifo chake pale msalabani,halafu tunapata maji kwa kubatizwa kwa jina la Yesu hivi vitu viwili tunapata ondoleo la dhambi,then unapokea kipawa cha Roho Mtakatifu
Ndiomaana kipindi cha Musa wana wa israel walikuwa wanabatizwa lakini haikuwa effectively sababu Damu ilikuwa bado haijamwagika pale msalabani,hata kipindi cha Yohana mbatizaji bado ubatizo wake haukuwa umetimia sababu Yesu alikuwa hajafa bado pale msalabani,ila alivyokufa msalabani ndiomaana wanafunzi wake walipewa maagizo "TUBUNI,MKABATIZWE KWA JINA LA YESU KRISTO ,HALAFU UPOKEE ROHO MTAKATIFU"

3.Swali la tatu kuhusu mariam kuendeleza Familia
>Jibu ni ndio Mariam na Yusufu waliendeleza familia walizaa watoto wengine baada ya Yesu kuzaliwa kwa uweza wa roho ,majina ya watoto wao yalikuwa ni (wakiume na usichanganye majina ya hao watatu wa mwisho na ya wale wanafunzi wake 12) Joseph,Yakobo,Yuda na Simon (Mathayo 12:46,Mathayo 13:55,Marko 6:3) na pia mary alikuwa na watoto wa kike majina yao hayakutajwa kwenye biblia
 
Asante sana mkuu nashukuru mnoo


Una kipaji cha kumuelewesha mtu, japo nasoma biblia ila kuna vitu vingi vinapiga chenga!

Swali la mwisho...

Kila binadamu huwa kuna ile unataka kufanya jambo fulani especially baya na nafsi inakukataza hata ukilifanya but huwa ishakuonya!

Na hapohapo ukifanya jambo jema nafsi inafurahi au inakupongeza!

Hiki kitu ni mimi peke yangu au ni kila mtu? Na je hiyo nafsi ni ipi? ....natanguliza shukrani




Sent using Jamii Forums mobile app
 
tulisoma moja ya mfano wa nomino za dhahania (abstract noun) ni Mungu
 
Kwa nin ni Mungu Baba na Sio Mungu Mama??
Kuna tatizo gani hapa??

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mwanadamu alipowekwa pale bustani ya Eden (Adam na Hawa) walizuiliwa wasile mti wa ujuzi wa mema na mabaya,Adam kupitia mkewe wakala kwahiyo wakapata ujuzi wa kutambua jema na Baya lakini madhara yake nikwamba kifo kikaingia ( (Mwanzo 2:17, 3:22),huoni baada ya kula lile tunda Biblia inasema macho yao yakafunguka wakajiona wapo uchi!
(Mwanzo 3:7-19)
Kwahiyo kila binadamu anajua analolifanya kama ni jema au ni baya,kama ni jema Nafsi yake itamshuhudia kuwa ni jema na kama ni baya pia nafsi yake itamshuhudia kuwa ni baya,Yohana anasema kila anayefanya baya anachukia mwanga ndiomaana anafanyia mafichoni (Yohana 3:20)
Huu utashi wa kutambua jema na baya ndio unatutofautisha binadamu na Viumbe wengine
 
Kwa nin ni Mungu Baba na Sio Mungu Mama??
Kuna tatizo gani hapa??

Sent using Jamii Forums mobile app
Neno "Mungu Baba" ni cheo (TITLE)" kinachotumika kuelezea shughuli za Mungu,kwanini aitwe Baba na sio Mama,Anaitwa Baba kwanza kwasababu Yeye ndio muumba wa vitu vyoote vinavyoonekana na visivyoonekana (1 wakolinto 8:6),Pili anaitwa Baba kwasababu hapo mwanzo aliumba mtu kwa mfano wake na aliumba Mwanaume kwanza na sio mwanamke,sasa kama aliumba mwanaume kwa mfano wake hawezi kuitwa Mama inamaana yeye ni Baba.
 

Unaongea bila kujua unachokiongea

1. Unaposema "Yesu hakuwa Mungu kipindi yesu alivyokuwa duniani ila Mungu alikuwa ndani ya Yesu. Unazungumzia Mungu yupi tena tofauti na Yesu? Hivi unauelewa wa kutosha kuhusu Uungu? Umeshasema Mungu kaingia kwa X kwahiyo huyu X hawezi kuwa Mungu bali Mungu atabaki kuwa Mungu na huyu X atabakia vile vile kuitwa X . Je Roho ikikuingia wewe @MAKOSHNEL tutasema @MAKOSHNEL ni Mungu?

Kumbe Yesu sio Mungu bali Mungu mdiye aliyekuwa ndani ya Yesu kwa mantiki hiyo basi Mungu alikuwa ndani ya mitume na manabii wote. Hata wewe Mungu anaweza kuwa ndani yako pia ukitaka.

Kwahiyo Yesu ni Yesu na Mungu ni Mungu.

Yohana 17:3

Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.


Matendo 3:26

Mungu, akiisha kumfufua mtumishi wake Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabariki kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angalau wewe umeniuliza kwa kuweka na vifungu vya biblia tunaweza kuelimishana kwa maandiko na sio maneno matupu,

>Swali la kwanza,Yule mwana wa mariam hakuwa Mungu bali Mungu alikuwa ndani yake anafanya zile kazi,,
"YESU ALIKUWA MUNGU TANGU MWANZO WA DUNIA, NA NI MUNGU SASA LAKINI YULE MTU ALIYEZALIWA NA BIKIRA MARIAMU AKAITWA JINA YESU HAKUWA MUNGU ILA MUNGU ALIKAA NDANI YAKE"
Yule Mwana wa mariam (YESU) alikuwa ni chombo tu cha Mungu kufanyia kazi zake hapa duniani yule alikuwa na Vyeo (TITLES) Mbalimbali ndio-maana aliitwa Nabii,Mwana wa Adam,Mwalimu,Mtume,mwana kondoo,Mwana wa Mungu,Kristo,masihi wa bwana,
,Pia hujawahi kusoma andiko linasema atazaliwa mtoto mwanaume jina lake ataitwa Emmanuel maana yake ni "MUNGU PAMOJA NASI" ? (Isaya 7:14,Matayo 1:23),kivipi Mungu pamoja nasi??,inamaana bikira mariamu alimzaa MUNGU?? HAPANA! kwanini Hapana? kwa sababu
> Mungu hazaliwi (Yesu kristo alizaliwa),wala
>Mungu hana Baba wala hana mama (Yesu kristo alikuwa nao)
>Mungu Hakui kiumri na maarifa(Yesu alikua kiumri na maarifa Luka 2:52)
>Mungu Hana mwanzo na hana Mwisho(Mwana wa adamu mwanzo wake alizaliwa na mama yake na mwisho wake alisulubiwa msalabani)
>Mungu Alikuwepo kabla ya vyoote(mwana wa adamu alikuja baadaye),
>Mungu Ni wa milele na milele (mwana wa adamu alikufa msalabani)
>Mungu hafi (Mwana wa Adam alikufa)
Sasa KIVIPI EMMANUELI MUNGU PAMOJA NASI?? Jibu lipo 2 Wakolinto 5:19 inasema hivi "yaani, 'Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho"
kumbe Yule mtoto aliyezaliwa na Bikira mariamu akaitwa Yesu hakuwa Mungu ila Mungu alikaa ndani yake,Mungu alijificha ndani yake,Mungu huwaga anajificha (ISAYA 45:15)!,
Yesu alisema "ukiniona mimi Umemuona Mungu" (Yohana 14:9) Kivipi umemuona Mungu wakati Mungu ni Roho na haonekani?,kivipi wakati Mungu sio mwanadamu Yesu alikuwa mwanadamu??,alikuwa anamaanisha Kupitia Kazi anazozifanya sababu yeye hafanyi chochote isipokuwa Mungu ambaye yupo ndani yake ndio anafanya!,yeye anatumika tu kama chombo (Yohana 14:10)!,
>Kwahiyo Mungu akiingia kwa kitu hicho kitu hakiwi Mungu bali Mungu anakuwa kajidhihirisha kupitia hicho kitu
>Yesu ni Mungu sasa na alikuwa Mungu kabla ila yule binadamu aliyezaliwa na Bikira mariam akaitwa Yesu hakuwa Mungu bali alikuwa Mwana wa Mungu ,kwakuwa alikuwa mwana wa Mungu alirithi jina la Mungu Baba ambalo ni Yesu,Mungu alikuwa ndani yake
>Hiyo yohana 17:3 ,nikweli Yesu alitumwa na Mungu kivipi? ndio nimekuelezea hapo juu,sasa ili umjue Mungu unatakiwa ukubali matendo ya mwili ya mwanaye wa pekeealiyoyafanya hapa duniani kwasababu yalikuwa kama mfano kwetu namna gani tufanye hapa duniani ili kuurithi ufalme wa Mungu,ndiomaana tunabatizwa,sababu Yesu alibatizwa,tunajawa na roho mtakatifu sababu Yesu alijawa na roho mtakatifu nk..
>Matendo 3:26 sasa huyo Yesu aliyefufuka sio yule aliyekufa,hata mwili wake ulikuwa tofauti ulikuwa na uwezo wa kutokea na kupotea,ulikuwa ni mwili wa kiroho au mwili uliotukuzwa,ndio huo mwili tutakuwa nao tutakapokuwa mbinguni (Wafilipi 3:20-21)
 

1.Kwanza umejichanganya sana,
Kwa maelezo yako uliyotoa umedhihirisha ya kwamba Yesu hakuwa Mungu ila Mungu ndiye aliyekaa ndani ya Yesu hivyo hili linadhihirisha ya kwamba hakuna Mungu anayeitwa Yesu. Halafu Kwenye hitimisho yako umehitimisha yesu ni Mungu nawakati umeshatoa maelezo ya kutosha juu, ya kwamba Yesu hakuwa Mungu na sababu umetoa za kutosha kwa Yesu kutokuwa Mungu.

2. Toa andiko linalosema Yesu alikuwa ni Mungu, tangu mwanzo wa dunia ili kuthibitisha kauli yako ili tuijadili hapa hilo andiko.

3. Unaweza kuniambia Kuna yesu wangapi?

4. Kwa kusema kwako kuwa Yesu ni Mungu, naomba utoe andiko likionesha huyu Yesu kuja kwake duniani kajituma/kajiagiza mwenyewe badala ya kutumwa na Mungu ili tuone Yesu yupo juu ya daraja ya Uungu au yupo chini ya daraja ya Uungu.

Yohana 14:28

28 Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba, kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sema hujaelewa sio nimejichanganya,vifungu vyoote nilivyokuwekea bado unasema nimejichanganya,concept ya Yesu sio wewe pekeyako inakuchanganya,imewachanganya wanaojiita wasomi wa theolojia,wachungaji na maaskofu na wakaishia kusema Mungu kagawanyika sehem tatu (Baba,mwana na roho mtakatifu) sembuse wewe,inahitaji uwe na roho mtakatifu ndani yako kuweza kupata maana za kwenye biblia,biblia haisomwi kama Gazeti na kwa utashi wa mwanadamu,
Ndiomaana Yesu kabla ya kupaa aliwaagiza wanafunzi wake waende Yerusalemu na wasitoke mpaka watakapopokea zawadi ya Roho mtakatifu,Na baada ya kupokea roho mtakatifu ile siku ya pentekosti (Matendo 2:1-47) Huoni upeo wao uliongezeka?,huoni sasa ndio walianza kuelewa yoote yesu aliyokuwa amewafundisha mwanzo?,Ni sawa na wewe mimi naweza kukupa mistari na mistari ya biblia nikithibitisha hoja zangu na hutanielewa
Kukusaidia hayo maswali yako uliyoniuliza sitayajibu kwa kina sana sababu nimeshajibu hapo juu,labda sasahivi nikujibu kwa Ufupi tu,
> Andiko linalosema Yesu alikuwa Mungu Tangu mwanzo
"1Wakolinto 10:1-4",sasa mstari wa 4 unasema "wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo" ooh kumbe kristo alikuwepo tangu mwanzo hata kile kipindi cha akina Musa Kristo alikuwa nao ambaye ni Mungu sababu Mungu ndio aliwatoa akina musa tokea misri akawa nao muda woote hadi kanani!,
"Yohana 8:54 "Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambia, Yeye Ibrahimu asijakuwako, mimi niko."
>Kuna Yesu wangapi?
Ni sawa na kuniuliza kuna Mungu wangapi,Yesu ni mmoja na Mungu ni mmoja,Jina la Mungu ni Yesu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…