Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,231
- 113,609
Lakini NN si wote wenye uwezo wa kupeleka watoto daycare na sehemu nyingine hizo daycare hakuna.
Natambua hilo. Lakini kama una uwezo wa kuajiri mwangalizi wa mtoto/ watoto nyumbani basi nadhani hata gharama za daycare utaweza kuzidumu. Au pengine hutaweza.
Hapa kuna tatizo kubwa sana la kimfumo zaidi ya hili. Hebu fikiria, hapa Tanzania hatuna utaratibu wa kuwafanyia waombaji kazi background checks. Kama upo utaratibu kama huo basi mimi siujui.
Sasa fikiria, unaajiri mtu ambaye hujui hata chembe ya background yake ikoje. Hujui kama ni sexual predator kama huyu anayesemwa hapa. Unaajiri tu kichwa kichwa na matokeo yake ndio haya sasa. Kungekuwa na mfumo na utaraibu mzuri wa kuwafanyia watu background checks mambo kama haya kwa kiasi kikubwa yangekuwa yanaepukika.
Unajua kwa mfano ile mibaba inayorubuni vitoto vidogo vya shule...ile yote ni mi-sexual predator/ sex offendors. Ilitakiwa iwe ndani au kutengewa maeneo yao maalumu mbali kabisa na watoto wadogo. Lakini sasa hivi ipo tu inajichanganya uraiani na kuendelea kuharibu watoto wetu.
Kwa hiyo tatizo kubwa kuliko yote hapa ni ukosefu wa utawala wa sheria. Utawala wa sheria ni kitu muhimu sana kama tunataka kujenga jamii inayolinda na kutetea haki na maslahi ya watoto. Ngoja niishie hapa kwa sasa.