FULL TEXT: Hotuba ya Mwenyekiti na KUB Mhe. Freeman Mbowe kwa umma kuhusu Janga la Corona

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)

TAARIFA KWA UMMA

JANGA LA CORONA NA YANAYOENDELEA BUNGENI

1.0 UTANGULIZI

Ndugu zangu Watanzania,

Kamati Kuu ya Chama chetu CHADEMA, ilifanya kikao chake cha kwanza kwa mfumo wa kidigitali kupitia jukwaa lake la CHADEMA Digital, siku ya Jumamosi tarehe 9 Mei na Jumapili tarehe 10 Mei 2020.

Kufuatia kikao hicho, Kamati Kuu imejadili kwa kina, miongoni mwa agenda mbalimbali, Janga la Corona na athari zake kwa taifa letu, mataifa ya jirani na dunia nzima katika ujumla wake.

Kamati Kuu, ilijiridhisha kuwa janga hili halihitaji masihara, mzaha wala usiri katika kulikabili. Ilitambua kwa mara nyingine umuhimu wa kuweka tofauti zetu pembeni na kutoruhusu chuki za kisiasa, hodhi za kisiasa, kiburi cha madaraka na mamlaka katika kupambana na vita hii.

Kamati Kuu ilitambua kutokana na ripoti mbalimbali za kisayansi za tafiti za kimataifa kuwa, Janga la Corona siyo jambo la kuisha haraka. Ni janga ambalo Taifa linatakiwa kujipanga kuishi nalo kwa muda mrefu. Hakuna njia ya mkato (quick fix) na sisi taifa nzima tunalazimika kuanza kufikiria kwa mawanda mapana (thinking out of the box).

Kamati Kuu iliona athari kubwa za watu wetu kupoteza maisha (kama ambavyo tayari tumeshaanza kushuhudia) na huduma za afya katika nchini kwetu kushindwa kuhimili ongezeko kubwa la mahitaji. Ilijiridhisha kuwa tupende tusipende, uchumi wa nchi yetu utaporomoka na kutakuwepo na ugumu mkubwa kwa Serikali kutekeleza bajeti yake ya kawaida.

Hakika, biashara na mipango ya mashirika na makampuni yetu ya ndani na hata ya wawekezaji wa nje itayumba kimitaji, kimapato na hivyo kusababisha makampuni mengi kufilisika. Watumishi wengi wa sekta binafsi watapoteza ajira zao na hivyo tatizo la kuongezeka kwa wasio na ajira kuwa mara dufu.

Uvutiaji wa mitaji mipya toka nje (FDI: Foreign Direct Investments) itakuwa vigumu sana kupatikana. Sekta za Utalii wa kimataifa na usafirishaji, yaweza kuchukua si chini ya miaka 2 kurejea katika level tuliyokuwa tumefikia.

Kamati Kuu imetambua kuwa athari za kijamii na kisiasa nazo haziepukiki. Familia zitaathirika na maisha ya kila mmoja wetu yataguswa. Umasikini utaongezeka na maisha tuliyoyazoea (lifestyle) hayatakuwepo tena.

Jack Ma, Bilionea wa China, mmiliki wa Alibaba Group amebashiri kwa kusema, nanukuu: “For people in business, 2020 is really a year for just staying alive. Don't even talk about your dreams or plans. Just make sure you stay alive. If you can stay alive, then you would have made a profit already,” mwisho wa kunukuu.

Kwa tafsiri ya Kiswahili: “Kwa watu walio katika biashara, 2020 hakika ni mwaka wa kuyapigania maisha. Huhitaji kufikiria ndoto na mipango yako! Pigania kubakia hai. Kwa kubaki hai, utakuwa tayari umetengeneza faida!

Huyu, ni tajiri mkubwa aliyetoa msaada mkubwa kwa mataifa kadhaa ya Africa, Tanzania ikiwamo, ya vifaa tiba mbalimbali kusaidia kupambana na janga hili.

Huu ni ukweli mchungu ambao inawezekana bado hatujaukubali. Wakati Taifa linapambana na vita yenyewe sasa, vita ya pili itafuata pale wimbi la janga hili litakapotulia. Hakika, viongozi na watu wetu wanastahili kulielewa hili na kujitayarisha nalo kuanzia sasa.

Kamati Kuu imesikitishwa na namna ushauri wowote unaotolewa na Chama cha CHADEMA kwa Serikali na Bunge unavyopokelewa kwa hisia hasi na kuzua malumbano yasiyo na tija kwa taifa letu.

2.0 TULISHAURI NINI?

Ndugu Watanzania wenzangu,

Itakumbukwa, tarehe 28 Aprili 2020, nilizungumza na Watanzania kwa niaba ya chama chetu cha CHADEMA, na kuelezea kwa kina tunachokiona kuhusiana na Janga la Corona linavyoitesa dunia na kipekee nchi yetu Tanzania. Tulitoa mapendekezo kadhaa na ushauri kwa Serikali, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wote kwa ujumla wao:

Tulitoa wito wa kuwepo ushirikishwaji, uwazi, ukweli na umoja katika vita hii.

Tuliisihi Serikali isihodhi janga hili kwani linahitaji nguvu na mshikamano wa pamoja kwani ni suala la uhai na kifo (life and death) kwa kila mmoja wetu.

Tulilisihi Bunge lione umuhimu wa kuitaka Serikali ilete Bungeni mkakati mahsusi wa namna ilivyojipanga kukabiliana na janga hili pamoja na bajeti yake, kisha Bunge lijadili kwa kina na kuidhinisha mpango huo maalum.

Tulihoji iwapo ni sahihi kuendelea na vikao vya bajeti bila kwanza kujiridhisha kuwa maoteo ya mapato ya Serikali yataweza kuathirika kiasi gani.

Tulisisitiza umuhimu wa utengemano na ushirika na mataifa mengine ya Africa Mashariki, SADC, Africa (AU) pamoja na nchi nyingine zilizo washirika wetu wa maendeleo.

Tulishauri mkakati makini wa kufanya mashauriano na mashirika ya fedha duniani kama World Bank, International Monetary Fund na Mashirika na Taasisi za Kimataifa kama CDC (centre for Disease Control), Global Fund na mengineyo mengi yanayoweza kutusaidia kuipunguzia Serikali yetu mzigo huu.

Tulisihi kuheshimu maelekezo na Itifaki za Shirika la Afya Duniani (World Health Organization). Hii ni pamoja na njia zilizo bora zaidi za kupima na kuhudumia waathirika.

Tulisihi kuwepo kwa mpango wa wazi na wa salama wa mazishi yenye staha kwa wenzetu watakaopoteza maisha na kutangulia mbele za haki.

Tulisihi mkakati wa haraka na wa makusudi wa kuwa kinga wapiganaji walio mstari wa mbele tukimaanisha Madaktari, Wauguzi na wahudumu wote katika huduma za afya, wa hospitali za umma na za binafsi kwa kuwapatia PPE na motisha.

Tulisisitiza sana umuhimu wa kupima kwa haraka na kwa upana zaidi ili waathirika waweze kujulikana na kutengwa kama njia muhimu ya kupunguza kasi ya maambukizi.

Tuliamini katika kujifunza kwa wenzetu yale yanayoweza kuwa ya msaada kwa mazingira yetu.

Tulishauri sana Serikali kuacha “kuficha” au kupunguza idadi ya waathirika na hatimaye vifo, tukiamini ukweli wa ukubwa wa janga hili kujulikana kutaongeza ufahamu na umakini katika kukabiliana nalo.

Tulionya kuhusu dalili za wazi za kuporomoka kwa uchumi, kutokana na kudorora (slowdown) isiyothibitiwa licha ya serikali kukaidi ushauri wa “lock down” au “partial lockdown” kwenye maeneo maalum yaliyoathirika zaidi.

Tulikumbusha Watanzania wote kuwa, mstari wa kwanza kwa mtu yeyote kujikinga ni yeye mwenyewe. Ni matendo na mwenendo wake.

Tulisisitiza elimu na kampeni kubwa ya ufahamu na uelewa.

Tulionya kuwa tunaona ufa mpana unaoelekea kuparaganyisha Taifa letu kama hatutaweka Utaifa wetu mbele.

Naam, tulilazimika kusema na kutoa ushauri huu hadharani baada ya juhudi zetu za ndani kupitia kamati mbali mbali za Bunge na mawasiliano ya moja kwa moja na viongozi wa Bunge na Serikali kuonekana kupuuzwa au kutokupewa uzito uliostahili.

Watanzania wenzangu,

Kutokana na kasi ya kusambaa kuwa kubwa zaidi hata kuutingisha Mhimili wa Bunge; na baada ya kuona ushauri wetu hautiliwi maanani; tarehe 1 Mei, mwaka huu, Chama chetu, baada ya mashauriano na makubaliano ya ndani, kilifanya maamuzi ikiwemo kuwaagiza wabunge wake wachukue hatua za kujilinda na kulinda wengine kwa kujitenga kwa siku 14, huku tukisihi Bunge zima ikijumuisha watumishi kutafakari uwezekano wa kujiweka karantini na kupima.

3.0 MAPOKEO YA USHAURI NA WITO WETU

Watanzania wenzangu,

Tunasikitika kwa namna ambavyo ushauri wetu huo, uliokuwa kwa ajili ya nia njema kwa taifa letu, ulivyopokelewa hususan na Viongozi wetu Wakuu wa Mihimili ya Bunge na Serikali na kugeuzwa kuwa uhasama wa wazi!

Tangu nilipotoa hotuba ile Aprili 28, mwaka huu na baadaye chama chetu kushauri Wabunge wetu kujitenga, kama inavyoshauriwa na WHO kwamba, pale ambapo ndani ya kundi lolote panapotokea hisia za kuambukizwa mmoja wenu, ushauri ni kundi zima kujitenga kwa muda wa siku zisizopungua 14 au kupima.

Kuanzia hapo, Kiongozi wa Mhimili Mkuu wa Bunge, Mheshimiwa Spika Job Ndugai ametumia majukwaa mbalimbali, nje na ndani ya Bunge kunishambulia na kuniandama mimi binafsi, viongozi wenzangu, Wabunge wa Chadema na Chama chetu kwa ujumla kwa lugha zisizo za staha.

Badala ya kujadili ushauri tuliotoa; badala ya kuhurumia maelfu na pengine mamilioni ya wahanga wa janga hili; badala ya kujihoji kama kweli wametekeleza wajibu wao kwa weledi uliopaswa; badala ya kuiona nia njema kwa nchi yetu na Watanzania wenzetu wote; wametumia mamlaka yao ya ofisi za umma na nguvu kubwa kutudhalilisha, kutubeza huku Taifa likiendelea kushuhudia roho za watu wasio na hatia zikiendelea kupotea kwa kasi!!

Mheshimiwa Spika amedai, CHADEMA tunageuza kila kitu siasa. Sisi tunakiri wajibu wetu ni wa kisiasa na ndiyo uliotupeleka Bungeni na unaotupa uhalali wa kuitwa Chama cha siasa.

Amechagua kumuandama mbeba ujumbe badala ya kuutafakari ujumbe wenyewe. Tunapenda kuwakumbusha viongozi wetu kuwa siasa ni maisha ya kila siku na inagusa kila binadamu. Hata wao, kila wanalofanya ni siasa. Tofauti yao watawala na sisi watawaliwa ni kuwa maamuzi yao, yasipokuwa makini huumiza wengi na hatimaye huua wengi bila hatia.

Mwanafalsafa Socrates alisema miaka mingi iliyopita. Nanukuu: “The prize a wiseman pays for neglecting politics is to be ruled by fools.” Kwa tafsiri isiyo rasmi ni: “Gharama anayolipa mtu mwerevu kwa kupuuza siasa ni kutawaliwa na wajinga.” Mwisho wa kunukuu.

Sina hakika huyo mjinga anayemzungumzia Socrates ni aliyetoa ushauri akapuuzwa au ni aliyepewa ushauri akatukana, akang’aka na kuvunja Katiba! Hiyo kila mmoja ajitafakari. Ni busara sisi wanasiasa tusiruhusu tunaowaongoza wasituone wajinga!

Watanzania wenzangu,

Ukweli utabaki kuwa ukweli milele. Bunge hadi leo linaelekea ukingoni ilhali halijapitisha bajeti maalum ya kupambana na vita dhidi ya Covid-19 na halijapokea mpango mahsusi wa Serikali wa namna ilivyojipanga kukabiliana na Janga la Corona.

Mipasho, matusi na udhalilishaji wa Spika dhidi ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni, akisaidiwa na baadhi ya “wapiga debe wake” vyote vitapita lakini roho za marehemu wa COVID-19 zitawalilia milele!

Mateso na machozi ya familia zao nayo yatawatesa kwani walishindwa kutumia kwa hekima na busara muda wa Bunge kujadili namna ya kuwalinda, lakini wakatumia masaa kadhaa kuwashambulia Wabunge wa CHADEMA.

Mheshimiwa Spika ni Baba na Mzazi, kama tulivyo wengi anaokazana kutupaka sifa bandia za uovu. Anajua tulikutana Bungeni miaka 20 iliyopita na tumefanya kazi pamoja Bungeni kuanzia mwaka 2000 chini ya Mheshimiwa Spika Pius Msekwa. Anatambua namheshimu na sijawahi kumshambulia binafsi.

Tumekuwa wote katika Kamati za Uongozi wa Bunge kwa miaka 10. Kwanza akiwa Naibu Spika chini ya Spika Mheshimiwa Anna Makinda na kisha yeye akiwa Spika kamili. Tumehudumu wote Kamati ya Kanuni za Bunge na Tume ya Huduma za Bunge kwa miaka 10 sasa.

Nawiwa kuliomba Taifa kumwombea Mheshimiwa Spika anayemaliza muda wake Job Ndugai. Sisi tumechagua kufikiria haki ya uhai ya Watanzania wote bila kuomba kibali kwa yeyote. Yawezekana wenzetu wanawaza uchaguzi ujao, sisi tumechagua kuwaza kizazi kijacho.

Kiti cha Spika ni muhimu sana katika kujenga utengemano kwa Taifa. Bunge ni chombo cha muhimu sana kinachohitaji weledi usiotia shaka. Bunge la vyama vingi linahitaji Spika asiyekuwa na “double standard” katika kulisimamia na kuliunganisha.

Haitegemewi Spika akawa wakala na dalali wa kurubuni Wabunge wa vyama vya upinzani na kupandikiza utovu wa nidhamu, uasi, chuki na uchochezi miongoni mwao. Bunge halipaswi kuwa jukwaa la propaganda bali jukwaa la hoja za kuifanya Tanzania yetu kuwa nchi bora zaidi ya kuishi kwa kizazi chetu na zaidi kwa vizazi vingi vijavyo.

Bunge si tu kwamba linawajibu wa kuisimamia na kuishauri Serikali kwa njia mbalimbali, bali linatunga sheria zinazoweza kuwasaidia wananchi au kuwaumiza. Tunapohubiri “uzalendo” hatupaswi kufikiri uzalendo ni utii kwa Serikali iliyopo madarakani, bali ni utii na dhamira safi yenye kusimamia utu na haki kwa Taifa lako na watu wake wote bila ubaguzi wa aina yeyote.

Watanzania wenzangu,

Mheshimiwa Rais ndiye Mkuu wa Mhimili wa Serikali. Bado tunahitaji kumpa moyo na kumshauri tukimkumbusha kuwa uamuzi wowote anaofanya unaweza kwa kiwango kikubwa kuokoa maisha ya wengi au kupoteza vilevile. Namwombea kwa Mungu awe mwepesi wa kusikiliza na awe mzito sana wa kufungua kinywa chake.

Kwa vioja vinavyoendelea Bungeni, ni dhahiri hajasaidiwa ilivyopasa kwenye vita hii ya Corona hata na Bunge lililojaza Wabunge wa Chama chake na kadhaa wa “kukodisha”. Wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Mheshimiwa Rais, watu wengi wa Chama na Serikali yako wanakuogopa. Akuogopaye hakuambii ukweli. Wengi wao hukudanganya ili wapate “miradi yao” na wakiwa mafichoni husema na kukiri hivyo. Wako tayari kupasuka kinywa Bungeni wakiamini wewe mwenyewe au wasaidizi wako mnawaona.

Unafiki haujawahi kuliacha Taifa lolote salama. Viongozi wasiokuwa na “principle” ni hatari kwani huchagua kuzilaza akili zao na kujibebesha akili za watakaye kumdanganya.

Mheshimiwa Rais, lawama zote za Janga la Corona zitakuangukia. Wanaopinga ushirika wa Taifa katika vita hii, wanawaza uchaguzi na kuomba huruma yako katika uteuzi. Mungu akuongoze, utafakari tena kama ushauri kadhaa uliopewa mpaka sasa ni sahihi au hapana.

Mimi na chama changu, tuliamini Bunge lilikuwa jukwaa sahihi la kuunganisha Taifa kwa maana ya Serikali, Wabunge na Wananchi wote katika vita hii. Nafasi hii imepotezwa. Sijui kwa faida ya nani.

Bunge linaishia baada ya wiki mbili. Mzigo wote unabaki Serikalini. Daraja muhimu limevunjika bila kutekeleza wajibu wake mkubwa! Upande wa pili, Serikali inapambana kupata uhalali wa maamuzi yake (legitimacy) kuhusiana na janga la Corona kupitia wapambe wengi, walioko katika mfumo wake na wasiokuwemo, kujitetea dhidi ya lawama za wahanga, wakiwamo wafiwa.

Ni jambo la ajabu sana kwamba, Serikali sasa inategemea nguvu ya dola na “manabii” kuitetea kwenye jambo la kisayansi ambalo linahitaji kujitambua, mikakati na mifumo shirikishi, rasilimali fedha na mwisho rasilimali watu.

4.0 HALI YA JANGA LA CORONA BAADA YA MIEZI MIWILI

Ndugu zangu Watanzania,

Jana tarehe 16 Mei, tumetimiza miezi miwili tangu mgonjwa wa kwanza wa Corona kugundulika Tanzania tarehe 16 Machi, 2020. Tuliyoyazungumza mwanzoni kama nadharia, sasa tunaweza kuyapima na kuona hali halisi. Sisi washauri tumejifunza. Sijui watawala na serikali wamejifunza kiasi gani.

Madaktari na wauguzi wameumizwa sana. Jamii inayojali imejifunza kwa njia ngumu ya vifo na mateso mengine yanayoambatana na janga hili.

Jambo moja muhimu ni kuwa sasa kila mmoja anakubali Corona ipo, inasambaa kwa kasi na inaua, tena sana.

Tuligoma ku-“lock down,” tukashindwa kufanya “partial lockdown,” tukaruhusu ugonjwa kuenea mno na kuua wapendwa wetu. Tulidhani tunalinda uchumi wetu. Tulisahau kulinda uhai wa watu wetu. Corona imeendelea kula vyote - uchumi na uhai.

Siku nyingi huko nyuma, niliwahi kutoa tahadhari kuwa tusipokubali kufanya ‘lock-down’, tutakuwa ‘locked out’. Inawezekana watawala hawakuelewa wakati ule au wengine waliona tunazungumza nadharia. Lakini hatimae vitendo vimeshaonekana. Kuwepo kwa taarifa za nchi jirani kufunga mipaka yake dhidi ya nchi yetu na hata kuzuia watu wetu kuingia katika nchi hizo au watu wetu kuwekewa taratibu mpya za masharti ya kuingia/kupitia katika nchi hizo ama wakuu wa nchi ambazo ni wanachama wa jumuiya ambazo sisi pia ni wanachama (EAC, SADC) kufanya mikutano huku nchi yetu ikiwa haina uwakilishi, ndiyo mwanzo huo wa ‘locked out’ na nchi zingine, tuliotahadharisha mapema sana.

Mwanzoni tulizungumzia kujifunza kutoka uzoefu wa nchi nyingine, sasa tunazungumzwa na wengine kama kielelezo hasi cha vita dhidi ya Janga la Corona Africa na duniani.

Na tuliposema “lockdown,” hatukumaanisha “lockdown milele.” Wala hatukumaanisha kufunga kila kitu kabisa, bali kuweka mkakati wa kuzuia mwingiliano wa watu usio wa lazima, ili kupunguza kasi ya kuenea kwa maambukizi, na kuipa serikali na wadau wa afya fursa ya kutibu wachache walioambukizwa, huku ikitafuta suluhisho la kimfumo itayowafaa wananchi baada ya lockdown.

Ndivyo wenzetu walivyofanya, na wengine wameanza kufungua mipaka. Waliowahi kufunga mipaka wamefanikiwa kudhibiti maambukizi. Lockdown imesaidia nchi nyingi.

Kwa mfano, Rwanda hadi jana walikuwa na wagonjwa 287, hakuna aliyekufa, wamepona 177.

Uganda ina wagonjwa 160, hakuna aliyekufa, wamepona 63.

Seychelles ina wagonjwa 11, hakuna aliyekufa, wamepona 10.

Lesotho ina mgonjwa mmoja, hakuna kifo
. Sisi tulishindwa nini? Tumeacha ugonjwa ukaenea. Sasa, badala ya utaalamu, tunatumia siasa kujadili tiba.

Wenzetu waliwahi kuchukua hatua, wakafunga mipaka na maeneo nyeti. Wametumia kipindi hicho kutafiti, kujifunza na kujizatiti kimfumo, na sasa wapo tayari kuishi na ugonjwa wakiwa na tahadhari iliyojaribiwa na inayoratibiwa.

Hapa kwetu kuna viongozi bado wanaogopa kukiri kwamba kuna Corona na kwamba tayari imeleta madhara makubwa, ingawa wameshuhudia watu wao wa karibu, au hata wao wenyewe, wakitikishwa na Corona. Uongozi unatudai tuwe wakweli, maana ukweli utatuweka huru.

Mwanangu Dudley ni miongoni wa wahanga wa kwanza wa janga hili. Namshukuru Mungu kuwa hatimaye amepata majibu “negative” baada ya yeye na familia nzima kuishi kwenye karantini kwa siku 57. Tumejifunza mengi. Tunawashukuru sana madaktari, wauguzi na wahudumu wengine wote Tanzania nzima. Unapoathirika ndipo unapata fursa ya nyongeza ya kutambua thamani ya wahudumu hawa wa afya.

Miezi miwili ni siku chache katika mazingira ya kawaida. Kwa Corona, ni kipindi kirefu chenye madhara makubwa ya kimaisha, kitabibu, kijamii, kisiasa na hata kiuchumi. Serikali inapaswa kufanya tathmini ya kila wiki kujiridhisha na hali halisi badala ya kutumia mwezi au miezi kutafiti!

Ni kipindi kifupi mno lakini kinachoweza kusambaratisha maisha ya watu wengi, kubomoa kwa kiwango kikubwa mifumo ya huduma za jamii katika nchi hususan katika nyanja za kitabibu; ni kimbunga kinachoweza kujenga au kubomoa mahusiano muhimu ya mataifa na taasisi.

Ni kipindi kinachohitaji utulivu mkubwa wa akili kukabiliana nacho. Ni janga linalohitaji “Full time dedication team” ya kuhamashisha utoaji wa elimu na kamwe haipaswi kufanywa kama “part time duty.” Hii ndiyo sababu serikali inashindwa kudhibiti kasi ya janga hili. Ni kwa sababu hii, nimesisitiza mara zote umuhimu wa serikali kushirikisha wadau wengine nje ya viongozi na watendaji wake.

4.1 Serikali kusitisha upatikanaji wa takwimu za waliopimwa, maambukizi, wagonjwa na vifo.

Watanzania wenzangu,

Katika hotuba yake kwa taifa, tarehe 3 Mei, mwaka huu, Mhe. Rais John Magufuli kwa mara nyingine tena alituingiza taifa kwenye sintofahamu kubwa katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Corona. Siku hiyo alitutangazia taifa zima kuwa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, ilikuwa ina tatizo. Rais hakuwa na imani na wataalam wake wala vifaa vilivyokuwa vinatumika kupima Virusi vya Corona.

Kufuatia hotuba hiyo ya Rais, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alichukua hatua za kuwasimamisha kazi watendaji wakuu wa maabara na kuanzisha uchunguzi. Tangu siku hiyo kumekuwa na shida ya upimaji na upatikanaji wa takwimu kuhusu mwenendo wa Ugonjwa wa COVID-19 nchini.

Katika kukabiliana na mlipuko wowote wa ugonjwa unaoambukiza, silaha ya kwanza ya kuwezesha kupanga mikakati na mipango ya kudhibiti kusambaa ni upatikanaji wa takwimu. Bila takwimu, ni vigumu kudhibiti usambaaji wa mlipuko na kutathmini ukubwa wa tatizo.

Miezi miwili ya kuingia na kuanza kusambaa kwa virusi vya Corona imesababisha taharuki kubwa. Ni vigumu hata hivyo, kuweza kufanya uchambuzi wowote kwani takwimu rasmi ambazo zinastahili kutolewa na serikali hazijatolewa kwa muda wa wiki mbili sasa.

Takwimu ninazozungumzia hapa ni za idadi ya waliopimwa, walioathirika, waliofariki na waliopona. Watu wanaendelea kuugua, wengine wanakufa. Mazishi yanaendelea. Takwimu hakuna.

Kibaya zaidi ni kwamba takwimu hizi zilisitishwa ghafla kwa maagizo ya kisiasa ambayo ukiyatazama kwa jicho la tatu utagundua kuwa shabaha yake ni kulazimisha wataalamu watengeneze taarifa zinazovutia watawala. Tunajidanganya!

Upungufu huu, ambao wengine tunaamini ni wa makusudi na wenye kulenga kuipunguzia Serikali shutuma za kuchelewa kwa uzembe kujishughulisha na maandalizi ya kisayansi kukabiliana na janga hili, yanasababisha ombwe kubwa linalozua taharuki mkanganyiko miongoni wa jamii.

Ndiyo maana jamii imekuwa inajisambazia yenyewe taarifa zinazotokana na vyanzo visivyo rasmi kama wagonjwa wenyewe, idadi ya vifo na mazingira ya mazishi ambayo wana jamii wanashuhudia. Serikali isiposema, wananchi watasema.

Mazingira ya kijamii, sasa yanatuaminisha kuwa serikali inaelekea kuzidiwa nguvu na kasi ya kuenea kwa maambukizi haya. Kwamba kupuuza kwa Rais Mhe. John Magufuli na Serikali yake maelekezo ya WHO ya namna bora zaidi za kisayansi kukabiliana na janga hili;

Mazingira haya yamesababisha changamoto na taharuki nyingi kwa wananchi na Taifa.

Changamoto ya kuongezeka kwa vifo vinavyopimwa na visivyopimwa,

Changamoto ya kuenea kwa kasi kwa maambukizi,

Changamoto ya kukosekana kwa mavazi ya kuwalinda madaktari na wauguzi na maambukizi yaani PPE,

Changamoto ya kufungwa kwa mipaka na mataifa majirani (Kenya, Rwanda, Zambia).

Athari za kiuchumi zinazosababishwa na Covid-19.

Watanzania wenzangu,

Japo janga hili limedumu kwa muda mfupi, athari zake kiuchumi ni kubwa sana. Ni bahati mbaya sana kuwa, pamoja na kulishauri Bunge kuitaka serikali kuwasilisha taarifa rasmi ya utafiti kuhusu madhara ya COVID-19 kwa uchumi wa nchi yetu, jambo hili halikufanyika.

Ukweli ni kuwa sekta kadhaa zenye mchango mkubwa kwenye pato la taifa, zimeathirika vibaya. Hizi ni pamoja na utalii na ukarimu, usafirishaji na maghala, fedha na bima, biashara za ndani na za uuzaji na uagizaji nje, ujenzi na uchukuzi na kilimo ikishirikisha uvuvi. Sekta hizi pamoja na mlolongo wake wa thamani unachangia zaidi ya asilimia 65 ya pato la taifa na kuzalisha zaidi ya 60% ya mapato ya fedha za kigeni kwa taifa.

Kuporomoka huku kutasumbua sana utekelezaji wa bajeti ya serikali na hivyo kukwamisha mipango mingi ya taifa na hata uchumi wa kaya moja moja.

5.0 NI NINI USHAURI WA CHADEMA?

Watanzania wenzangu,

Ni wajibu wetu kuendelea kushauri, hivyo tunapendekeza yafuatayo;

Tunaishauri serikali isione aibu kushirikisha wadau wengine kupata muafaka na nguvu ya pamoja kwenye vita hii. Serikali isihodhi janga hili kwani linahitaji nguvu na mshikamano wa pamoja kwani ni suala la uhai na kifo (life and death) kwa kila mmoja wetu.

Tunasisitiza umuhimu wa utengemano na ushirika na mataifa mengine ya Afrika Mashariki, SADC, Africa (AU) pamoja na nchi nyingine zilizo washirika wetu wa maendeleo. Tunashauri, kipekee ushirikishwaji wa marais wetu wastaafu ili wamsaidie rais wetu ambaye kwa kweli tayari anabeba mzigo mzito na Serikali yake kulisukuma jambo hili.

Serikali ione uwezekano wa kutunga kwa haraka Sheria ya Bunge itakayosimamia utekelezaji bora wa vita dhidi ya Corona. Hii itaepusha maelekezo mbalimbali yasiyo rasmi ambayo sasa yanatolewa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

Tunadhani kuwa si busara sisi kama taifa kushambulia na kubeza washirika wetu wa maendeleo, bali tunapaswa kurejesha kwa nguvu na umakini uhusiano wetu na washirika wetu wote, badala ya kuwaona kama maadui na kuwaita majina ya kebehi huku bado tunaomba na kupokea misaada kutoka kwao.

Rasilimali fedha na utaalam ni muhimu katika vita hii. Wataalam katika masuala ya fedha washirikishwe ili wasaidiane na viongozi waliopo serikalini kuweka msukumo mkubwa zaidi. Tunatambua juhudi kadhaa zinazofanywa sasa na Serikali chini ya Waziri wa Fedha kuzifikia taasisi hizi; hata hivyo vita hii inahitaji wigo mpana kuliko wa serikali peke yake. Waziri wa Fedha na walioko serikalini wako na majukumu mengi.

Viongozi wastaafu wakiwemo magavana wa zamani wa Benki Kuu na watendaji makini na wazoefu wa zamani katika wizara ya fedha wanaweza kuisaidia serikali sana kama hatutaendekeza ubinafsi, chuki na visasi. Wakati wote tukumbuke: watu wetu wanakufa kwa kukosekana msukumo wa kutosha.

Tunaendelea kushauri mkakati makini wa kufanya mashauriano na mashirika ya fedha duniani kama World Bank, International Monetary Fund na Mashirika na Taasisi za Kimataifa kama CDC (Centre for Disease Control), Global Fund na mengineyo mengi yanayoweza kutusaidia kuipunguzia Serikali yetu mzigo huu.

Uhusiano wetu na Shirika la Afya Duniani (World Health Organization-WHO) unatia shaka. Hawa ni wadau muhimu katika vita hii. Sisi si kisiwa. Hatupaswi kuwakwepa wala kuwabeza. Hata kama kuna mambo haturidhiki nayo, lugha tunayotumia kuyajadili lazima ifanane na ilingane na ustaarabu wetu uliotukuka miaka mingi, na aina ya diplomasia inayotupa heshima katika dunia ya watu wastaarabu. Tumeze viburi vyetu tutafute amani kwa kuheshimu maelekezo na istifaki za WHO.

Tunaendelea kusisitiza serikali iweke mkakati wa haraka na wa makusudi wa kuwakinga wapiganaji walio mstari wa mbele tukimaanisha madaktari, mauguzi na wahudumu wote katika huduma za afya, wa hospitali za umma na za binafsi. Tusiwalaumu wapambanji walio mstari wa mbele, bali tuwatie moyo na kuwaongezea motisha na vitendea kazi salama.

Serikali ifanye mawasiliano ya haraka na nchi rafiki zetu ikiwemo Cuba kupata msaada wa wataalam na vifaa vya kupima waathirika badala ya kuendelea kutegemea kituo kimoja kilichopo Dar es Salaam na wataalam wa ndani ambao ni wachache. Tunasisitiza sana umuhimu wa kupima kwa haraka na kwa upana zaidi ili waathirika waweze kujulikana na kutengwa kama njia muhimu ya kupunguza kasi ya maambukizi. Hii ni pamoja na njia zilizo bora zaidi za kupima na kuhudumia waathirika.

Tunaendelea kusisitiza kuwepo kwa mpango wa wazi na wa salama wa mazishi yenye staha kwa wenzetu watakaopoteza maisha na kutangu

Serikali iepuke mtego wa ‘kuficha’ au kupunguza idadi ya waathirika au vifo, kama ambavyo tayari tumetuhumiwa na dunia. Tusitumie mabavu kuzuia taarifa sahihi, kwani hata tukisema hakuna wagonjwa au hawafi, wananchi wenyewe ndio wanaouguliwa na ndio wanaofiwa, na mazishi yanaongezeka. Hata nchi kubwa zimepigwa. Corona si aibu. Tuwe wakweli. Kadiri tunavyokuwa wawazi ndivyo tutakavyokuwa makini katika kutambua ukubwa wa janga na jinsi ya kulikabili.

Tunapongeza hatua za awali zilizotangazwa na Benki Kuu ya Tanzania, za kujaribu kunusuru uchumi. Hata hivyo, bado serikali haijaonyesha mchango wake katika kuokoa kampuni binafsi zinazochangia pato la taifa, ambazo kiukweli zimeathirika vibaya kutokana na janga la Corona.

Serikali itambue kuwa Sekta ya Utalii imeathirika sana, na itachukua muda mrefu kuinuka. Itahitaji angalau miaka miwili kurudia nusu ya uhai wake. Ishirikishe wadau wa utalii nchini katika kuweka mikakati mahususi ya kunusuru sekta hii.

Huu si wakati wa kuunda “tax task force” iliyojaa watu kutoka vyombo vya dola na kuwatuma kwenda kuwabana wafanyabiashara wa utalii ambao makampuni yao tayari yako taabani kwa asilimia mia moja. Kitendo hiki kitaua kabisa sekta ya hiyo. Sekta ya Utalii inahitaji “stimulus package,” haihitaji “Tax Task Force.”

Serikali itafute na ijenge uhusiano mwema na sekta binafsi. Viongozi wa serikali watambue na kuheshimu utamaduni na nidhamu ya kufanya biashara, na wajue kuwa kufanya biashara Tanzania hakuhitaji hisani ya Serikali, na kwamba ni kosa kubwa kuhisi kuwa kila mfanyabiashara ni 'mwizi'.

Elimu na kampeni kubwa ya ufahamu na uelewa iendelee ili kusaidia watu wetu wabadili tabia na mwenendo wa maisha, wajilinde na kulinda wengine. Tuwaeleze ukweli kuwa Corona si gonjwa la kupita kwa siku mbili tatu, bali wajifunze kuishi na ugonjwa kwa tahadhari kubwa, huku mifumo ikiendelea kuboreshwa, na utafiti za dawa na chanjo zikiendelea kutafutwa. Pale inapobidi, kila mmoja au kila familia au serikali, ichukue hatua kali za kujikinga ili kupunguza kasi ya kuenea kwa ugonjwa.

Wanaojihisi kuwa na afya isiyo na uhakika, wajitenge wenyewe kabla ya kutengwa, huku wakiendelea kujihudumia kwa kufuata ushauri wa kitaalamu. Kadiri tunavyozidi kuambukizwa, miili yetu nayo inaendelea pia kujenga kinga, lakini ili maambukizo hayo yasiwe na madhara makubwa sana, inabidi mifumo ya huduma iendelee kuboreshwa ili wanaozidiwa wasipoteze maisha.

Familia nyingi zimepoteza ndugu zao kwa janga hili. Idaidi halisi haijulikani. Hata uhai wa mtu mmoja ukipotea ni hasara kubwa kwa taifa. Tusisubiri wafe wengi zaidi ndipo tujue ubaya wa janga hili. Tuendelee kulikumbusha Taifa la Watanzania wote kuwa hatua ya kwanza ya kuepusha janga hili ni kila mmoja wetu kujikinga.

Uchunguzi wa timu iliyoundwa na Waziri Ummy Mwalimu uwekwe wazi hadharani haraka kwa sababu muda uliotangazwa kuwa itakuwa imemamaliza kazi umepita siku 3 sasa. Sambamba na hilo, Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii, irejee kufanya kazi mara moja.

6.0 CHADEMA TUNAFANYA NINI?

Ndugu Watanzania wenzangu,

Kwa kuwa,

Sisi kama familia pana ya CHADEMA, tunatambua na kuheshimu sana kazi kubwa inayofanywa na madaktari, wauguzi na watumishi wote wa Kada ya Afya;

Na kwa kuwa,

Tunatambua kwa unyenyekevu mkubwa, utayari wao wa kuhatarisha maisha yao ili kuokoa maisha ya wengine;

Na kwa kuwa,

Tunatambua madaktari, wauguzi na watumishi kadhaa katika sekta ya afya nao wamepoteza maisha yao na baadhi ya ndugu zao;

Na kwa kuwa,

Tunatambua kuwa baadhi yao ni waathirika na wanapigania maisha yao sasa kutokana na kuambukizwa wakiwa katika huduma bila kuwa katika mavazi rasmi ya kinga ya kutosha yaani, PPE

Na kwa kuwa,

Wengi wao wameendelea kutoa huduma bila PPE, na serikali imejikongoja katika kuweka wazi mpango kamili wa kutoa vifaa hivi maalum vya kuwakinga;

Hivyo basi:

CHADEMA tunatafakari namna bora ya kuja na mkakati shirikishi utakaloenga KUOKOA WAOKOZI wetu.

7.0 HITIMISHO

Watanzania wenzangu,

Wajibu tuliouchagua, unatokana na dhamira ya mioyo yetu. Ni utume ambao hauwezi kupindishwa kwa kiwango chochote cha fedha, mali au cheo. Mapigo na misukosuko tunayopitia kwa kuthubutu kusema ukweli mnayaona. Tunalazimika kukubali kuteswa katika kupigania tunayoyaamini. Yawezakana tukawa wachache kwa idadi lakini tu wengi kwa dhamira zetu.

Mabadiliko yoyote makubwa, hasa ya mifumo, hayaji hivi hivi kimzaha. Dira ya mabadiliko huhitaji watu kujitoa mhanga, tena kwa muda mrefu. Na kadiri maumivu yanavyozidi kuwa makali, ndivyo tunavyozidi kutambuana. Silaha yetu tunaitambua. Tutaendelea kuitumia ili kukamilisha jukumu zito na adhimu tuliloanza kwa pamoja. Watakaostahimili hadi mwisho tutafika nao Kanaani.

Hakika, ndoto ya taifa letu ya Uhuru wa Kweli na Mabadiliko ya Kweli, inamuhitaji kila mmoja wetu kwenye siasa na nje ya siasa. Hatuhitaji kupangiwa ratiba ya uhuru wetu.

Nawashukuru sana kwa kunisikiliza! Mungu Ibariki Tanzania! Mungu Ibariki Africa

NO HATE! NO FEAR!

Freeman Aikaeli Mbowe, (Mb-HAI)

Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni

17 Mei, 2020
 
Baada ya kuipitia hotuba hii nimeelewa kwanini Spika Ndugai alikuwa mkali kwa Mbowe.

Huwezi kukidharau kiti cha Spika na kukiita " mjinga".........hizi siyo lugha za kibunge na kiuongozi!
 
Tena Mbowe kamheshimu sana Ndugai , huyu Ndugai ni zaidi ya alivyoitwa humo
 
Hakika Israel mtoa roho kafika sijui mwenye siku yake atafurukutaje na tayari kashaharibu.🤣🤣
 
Ndio msilie lie sasa anavyotekeleza huo " ujinga"

Siasa ni sayansi!
Kabla hajafa ndugai ni lazima afungwe , hilo ulijue , Dunia haijawahi kuwa na spika duni kama huyu , kuna wakati nilidhalilika sana London kwa kujulikana kuwa mtanzania kwa sababu ya Upuuzi wa Ndugai
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom