Hotuba za Rais kila mwezi

Hotuba za Rais kila mwezi

Je unaridhika na hotuba za Rais Kikwete?

  • Ndio

    Votes: 13 15.5%
  • Hapana

    Votes: 71 84.5%
  • SIJUI

    Votes: 0 0.0%
  • Sina jinsi

    Votes: 1 1.2%

  • Total voters
    84
  • Poll closed .
Kamanda soma vizuri, Mwananchi wa kawaida anasumbuliwa sana na Malaria. Juhudi zilizofikiwa katika kupambana na ugonjwa huo ni habari njema kwa mwananchi wa kawaida na watz wote kwa ujumla...

Matengenezo ya barabara ni matumaini makubwa kwa wananchi wa kawaida,

vita dhidi ya ukimwi ni tumaini kubwa kwa mwananchi wa kawaida..

Na utafutaji wa vyanzo vingine vya umeme kwa mji wa Kigoma ni habari njema mno kwa wakaazi wa huko... zaidi watu wengi wa Mafia watafarijika kwa kuwa na uwanja wenye taa

Habari ni njema na hazitofautini na zile tunazozipata wakati wa bajeti ya serikali kule bungeni. lakini kwa wakati huu ambapo wananchi wamepoteza imani na utendaji wa serikali na wanahitaji kujua majina na nini kitafanyika dhidi ya wale ambao wameyafanya maisha ya wananchi kuwa magumu zaidi. Si jambo la kushangaza kupanda kwa gharama za maisha na mfumuko wa bei matokeo ya Richmond,Downs,IPTL na BOT scandal. Sasa sijui mkubwa wa nchi anatueleza habari ya bajeti ya pesa za bush,wakati hatuna imani na watakaosimamia pesa hizo,sijui hii inakaaje
 
..and i wonder,when reading western news,he is not mentioned anywhere,hata kwa neno moja tu.

..annan ndio anaonekana shujaa.

DAR si LAMU,

Watu mnanifurahisha kweli kweli, JK akisifiwa na watu wa West, mnasema who are they? JK ni kibaraka.

Asipoandikwa na wao kuhusu amani ya Kenya, mnasema kwenye magazeti ya West
hawamtaji.

Where is the consistency?
 
DAR si LAMU,

Watu mnanifurahisha kweli kweli, JK akisifiwa na watu wa West, mnasema who are they? JK ni kibaraka.

Asipoandikwa na wao kuhusu amani ya Kenya, mnasema kwenye magazeti ya West
hawamtaji.

Where is the consistency?

Mtanzania...

umeanza kuzeeka sasa ..lol..

wanaouliza haya maswali ni memba tofauti.
Kuna consistency moja tu hapa JF - ukiona raisi wa nchi masikini ameanza kusifiwa na media za west pamoja na makampuni yao ya kijasusi mf WB and IMF, basi ujue kuna kitu kikubwa sana kiko wrong na huyo raisi.
 
Mtanzania,

Hapana mkubwa wangu hujanipata kabisa kwani umeshindwa kutofautisha kati ya dira ya kitaifa, mrengo wangu, mawazo ya Mwalimu na reality.
Mkubwa umetoa mifano ya nchi kama Marekani, Uingereza jinsi zinavyoendesha Biashara zake na nchi kama Saudia na China. bahati mbaya ni kwamba Tanzania hatuendeshi biashara ila tunaomba msaada..
Tofautisha kati ya yule maskini anayekaa mlangoni msikitini akisubiri kuomba na mbangaizaji (mlalahoi) anayechapuka kila asubuhi kuingia mitaani ktafuta deal iwe ktk maofisi ama hata Machinga.
Tanzania kwa kukosa mrengo tumekuwa kama masikini anayesubiri mitaani akipiga gita na kucheza sana mnenguo akisubiri kusikia sauti za sarafu zaikimwagika ktk kopo lake. Yaani kifupi ni kwamba aidha milango ya uchumi wa nchi yetu ni ile ya Kitalii na kufanywa ma Charle Chaplin, nchi nzima tunacheza ngwasuma na kutegemea kuwa kivutio kwa nchi za Ulaya. Ama sisi ni sawa na jamaa zetu nyumbani ambao kila siku hutegemea sisi tulioko Ulaya tutawatumia mallioni ya fedha wapate kuendesha maisha yao ya kila siku.
Na kwa bahati mbaya mfano yetu wenyewe tumeiona sana kuwa hata siku moja huwezi kumkomboa ndugu ama jamaa yako kwa kumtumia dollar, atakufilisi wewe na yeye bado ataendelea kuwa maskini...
Haya ndio maisha tunayoishi na kweli nakubaliana nawe kuwa ndio reality ya Tanzania. Ni reality inayoppatikana Tanzania tu wala sio nje ya mipaka yake. Tanzania hata ukimkopa mtu kurudisha hizo fedha ni ngoma, yaani wengi hutegemea kupewa msaada zaidi ya kukopeshwa. Na reality ni kwamba unapoombwa fedha basi ni vizuri kufikiria kumpa bure usitegemee malipo kuliko kumkopa mdanganyika... utakesha!..
Hii ndiyo reality ya Tanzania (only in Tanzania) reality ambayo haiwezi kutuvuta hata hatua moja isipokuwa kutuweka ktk utumwa na kutudidimiza zaidi ktk dimbwi la Umaskini.

Nasema hivi kwani hata Kitaifa, viongozi wetu na wananchi kwa ujumla hutegemea kuona hiyo mikopo yetu tumesamehewa kiasi gani!.. na tunaposiukia tumesamehewa hupiga makofi na kumpa hongera kiongozi wakati tunashindwa kujiuliza hizo fedha zilijenga kitu gani?...
Hivyo basi mkuu wangu kwa mzee Bush nasema hivi,
Ni ujinga mkubwa kuendelea kumpa fedha mvuta unga ukitegemea utaweza badilisha maisha yake, hizo fedha zitaenda nunua unga zaidi na kumfanya awe teja la kutupwa...Misaada ya Bush ya vyandarua utakuja sikia vimeuzwa kwa wananchi. Na huwezi kuondoa maleria kwa viandarua mkuu wangu hilo halina reality!... ni ujuha wetu kujisifia kupata viandarua tunashindwa kufukia madimbwi ambayo hayana cost kubwa kama huduma na jitihada zote zinazofanywa kuzuia Maleria...
 
TAARIFAKWA VYOMBO VYA HABARI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete keshotarehe 2 April, 2008, saa kumi jioni,
atalihutubia taifa kupitia wana CCM na viongozi wa Jumuiya za Chamakatika ukumbi wa
Diamond Jubilee.

Rais hakuweza kutoa hotuba yake yamwisho wa mwezi wa tatu (Machi) kutokana na maafa
yaliyotokea katika machimboya Tanzanite, Mererani katika mkoa wa Manyara ambapo
ilimlazimu kwendakutembelea eneo la maafa ili kujionea hali na kutoa pole kwa
wananchi nawachimbaji wa Mererani.

Hotuba hiyo itatangazwa moja kwa mojakupitia redio na Televisheni mbalimbali hapa
nchini.


ImetolewaIkulu, Dar-es-salaam,
Tarehe1, April, 08
 
Last month it was all around George Kichaka visit to Tz, Siasa za Kenya!
I don't expect anything new!🙄
 
Alipohutubia bunge alisema kwamba katika vitu ambavyo atavishughulia ni mpasuko wa kisiasa Tanzania visiwani.
Swali ambalo ningependa JK alijibu katika hotuba yake.... "Baada ya uamuzi wa CCM kuhusu mazungumzo ya muafaka, je, anaonaje maendeleo ya utafutaji wa suluhu ya kisiasa Tz visiwani? Je, yalipo maendeleo ya suala hili ndipo alitaka yawe? Anaridhika na maendeleo ya kutafuta suluhu ya matatizo ya Tz visiwani?"
Otherwise blah blah nyingine hazivutii!
 
Mimi nimepoteza matumaini na huyu mheshimiwa. Naona yuko weak mno na anaogopa kuchukua maamuzi magumu ambayo yanatakiwa ili kulisogeza mbele taifa letu.

Labda sasa ni kuanza kuelemisha watu ili wajaribu kumn'goa mwaka 2010. Kwa speed hii, jamaa akiongoza miaka 10 itakuwa balaa kubwa kwa nchi.

Kenya waki solve matatizo yao, wataanza kutuacha tena kwa mbali.
 
Mimi nimepoteza matumaini na huyu mheshimiwa. Naona yuko weak mno na anaogopa kuchukua maamuzi magumu ambayo yanatakiwa ili kulisogeza mbele taifa letu.

Labda sasa ni kuanza kuelemisha watu ili wajaribu kumn'goa mwaka 2010. Kwa speed hii, jamaa akiongoza miaka 10 itakuwa balaa kubwa kwa nchi.

Kenya waki solve matatizo yao, wataanza kutuacha tena kwa mbali.

Bahati mbaya umechelewa sana kukosa naye imani huyu bwana. The bad news ni kuwa kuna kila dalili kwamba tutakwenda naye hadi 2015. Hapa naona JK amejenga mazingira ya watu kumkumbuka na kumpenda Mkapa.
 
The UEFA Champs league is my priority today... nangoja tu kandanda, hotuba za mhe. JK zimenikifu!
 
Kwa nimuonavyo sivyo alivyo anaweza kusema hili akafanya lile ni mtu wa ajabu ajabu tu haeleweki ,ila kinachoendela naona kama anazidi kupoteza nguvu si kama wenye viti wengine waliopita ambao wakisema watatekeleza basi hakuna anesubutu kupinga ila huyu naona mwisho wake watakuwa wakipigiana dana dana kama mpira wa makaratasi uliofungwa na kusukwa kwa kambaza mnyaa vizuri.
 
Jamaa alianza kwa mbwembwe nyingi na hotuba ya ufunguzi wa bunge ambayo ilikuwa na ushawishi wa akili karibu kwa kila MTZ,Lakini leo amepeleka Taifa ktk ufukara kwa kuwa tu mamlaka aliyopewa na wananchi/katiba ya maamuzi ameshindwa hata kuthubutu.

Nafurahi kuwa nitakuwa EMIRATES STADIUM,kuliko kujipa huzuni kusikiliza hotuba zilizopambwa kama makaburi yaliyopakwa chokaa kumbe ndani mifupa ya marehemu.
 
Kwa nimuonavyo sivyo alivyo anaweza kusema hili akafanya lile ni mtu wa ajabu ajabu tu haeleweki ,ila kinachoendela naona kama anazidi kupoteza nguvu si kama wenye viti wengine waliopita ambao wakisema watatekeleza basi hakuna anesubutu kupinga ila huyu naona mwisho wake watakuwa wakipigiana dana dana kama mpira wa makaratasi uliofungwa na kusukwa kwa kambaza mnyaa vizuri.

Nasikia kwamba Mkapa alisha mjua na ndiyo maana hakuna la kuendea kule Butiama .The guy I mean Mkapa despise this guy maana hata uwezo wa kujenga hoja kama rais hana .Jamaa anasema hata kuweka sahihi it took him ages hadi Bush akawa amekaa anangoja amalize kuweka sahihi .
 
Nasikia kwamba Mkapa alisha mjua na ndiyo maana hakuna la kuendea kule Butiama .The guy I mean Mkapa despise this guy maana hata uwezo wa kujenga hoja kama rais hana .Jamaa anasema hata kuweka sahihi it took him ages hadi Bush akawa amekaa anangoja amalize kuweka sahihi .

Hii ya kuweka sahihi imekuwa inasemwa chini chini naona sasa imekuja juu... kwi kwi kwi, mitomingi issue ya Kikwete na Mkapa inazidi kukua day after night na sijui itaisha vipi. Ngoja nione hii hotuba itakuwa na nini kipya!
 
ameshaanza 'kuunguruma' TBC. ameanza na uvamizi comoro, atazungumzia pia maafa ya mererani, na maamuzi ya nec ya ccm kuhusu muafaka
 
Hii ya kuweka sahihi imekuwa inasemwa chini chini naona sasa imekuja juu... kwi kwi kwi, mitomingi issue ya Kikwete na Mkapa inazidi kukua day after night na sijui itaisha vipi. Ngoja nione hii hotuba itakuwa na nini kipya!

JK kuweka sahihi namna kuliwaaca wengi wanashanaga na hata Bush akawa anashangaa jamaa.Yaani kila kitu kwake ni kulemba hata kuweka sahihi jamani ?

Comoro kasemaje ? Tunataka kujua pesa za vita ni zipi .Tupeni habari zaidi hapa JF.
 
JK kuweka sahihi namna kuliwaaca wengi wanashanaga na hata Bush akawa anashangaa jamaa.Yaani kila kitu kwake ni kulemba hata kuweka sahihi jamani ?

Comoro kasemaje ? Tunataka kujua pesa za vita ni zipi .Tupeni habari zaidi hapa JF.

Kuhusu Comoro anasema kuwa ulikuwa ni uamuzi wa AU. Kanal Bacar alikuwa mbishi na alikataa kuutambua utawala wa gnad comoro na kuitisha uchaguzi kwa kutumia madaftari ya wananfunzi baada ya kukosa vifaa vya kupigia kura.
Anasema gharama za vita zinalipwa na AU na fedha ambazo TZ imezitumia au itazitumia zitarudishwa na AU.
Anasema kazi imekamilika, kisiwa kimepata uongozi na uchaguzi utafanyika mwezi ujao.
Askari wa TZ watarudi kwa awamu 2, ya kwanza mwishoni mwa mwezi huu na ya pili mwezi wa tano baada ya uchaguzi
 
JF members,kama mtakumbuka miezi ya mwanzoni kabisa ya utawala wa JK,kuna ghorofa lilidondoka kule Chang'ombe hadi kusimamishwa kwa mhandisi aliyehusika na jango lile.Hatua zilizochukuliwa zilimfariji kila mtanzania kwamba sasa viongozi tunao.Lakini wadau wasiasa walisema isije ikawa nguvu ya soda,hili alilikanusha JK mwwnyewe kwamba wanaodhani ni nguvu ya soda wameumia.Hapa alikua na maana kwamba ni kazi kwa kwenda mbele.

Katika hotuba yake ya Dom alisema hivi samahani kama nitakua nimekosea baadhi ya maneno kwamba THOUGH I'M SMILING FACE BUT I'M FIRM IN ISSUES.Mtanirekebisha kama nimekosea.Mimi kwa mtazamo wangu I think Salma is more firm than his Husband.

Kuhusu hotuba ya leo sitegemei kama JK akuja na jipya zaidi ni vicheko vingi kwa kwenda mbele.Kwako BabaH,sio kwamba JK anakua hana cha kusema,kinachokera ktk hotuba za JK ni kwamba hotuba zake nje ya wakati na mara nyingi hazina maslahi kwa mtanzani wa chini.Kwa mfano ktk hotuba hiyo usitegemee kwamba ataongelea juu ya BOT,Muafaka,Richmond,hana huo ubavu.Ameshindwa kuunguluma Butiama yaaaaaaaani Jk amekwisha.2010 ni bora mama salma akachukua form za urais may be we may achieve something not from JK.
 
Back
Top Bottom