Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 14
Sasa sirikali mbali na Bush ina mpango wa kuwaleta hao wakimbiaji kidogo Tanzania itajwe na kuwaona wakiona kwenye luninga ?
Tutakuwa tunatoka nje ya mada.
Sasa sirikali mbali na Bush ina mpango wa kuwaleta hao wakimbiaji kidogo Tanzania itajwe na kuwaona wakiona kwenye luninga ?
Katika uchambuzi wangu wa hotuba ya JK, nimekiona kipengele hiki ambacho kidogo kimenipa taabu sana kukielewa.
Mheshimiwa Jk Alisema:- Rais Bush alikuja kuwathibitishia wananchi wa Marekani kuwa sera yao ya misaada Afrika ni sahihi na kwamba mafanikio yaliyotarajiwa yanapatikana. Kwa ajili hiyo, aliamua kukaa hapa kwetu kwa siku nyingi kwa sababu, katika misaada yao ya kupambana na malaria na UKIMWI barani Afrika, hapa Tanzania kumekuwepo na mafanikio ya kutolewa mfano.
Nachotaka kufahamu hiyo sera mwanzoni tulipewa kiasi gani kiasi kwamba aje kwa siku tatu kuonyesha mafanikio?
Je, ni mafanikio yapi yamepatikana ktk kuondoa maradhi haya HIV na hasa Maleria toka mradi huu umeanzishwa. Nilichokiona zaidi hapa ni rais wetu kuwashukuru baadhi ya watu kwa maandalizi mazuri ya kumpokea Bush... kazi ambayo nchi za Kiafrika ni mahodari sana ktk maandalizi ya kumfumba mtu ukweli na hali halisi. Ni katika mtililiko wa mazingaombwe haya Hospital kama Amana zilipigwa soap soap na huduma kuboreshwa ktk siku hizo tatu, hivyo hivyo sehemu zote walizotembelea kuna kila dalili kuwa watu waliandandaliwa kuonyesha mafanikio badala ya hali halisi.
Jambo jingine ningependa kuelewa nalo ni kwamba hivi kama sio ziara ya Bush na ahadi alizotoa ina maana sisi wenyewe hatukuwa na mpango wala hesabu za kutengeneza barabara, umeme wala viwanja vyetu isipokuwa kwa msaada wa Millenium?..
Nje ya misaada hii ya Millenium ni kiasi gani cha fedha za misaada toka nchi nyinginezo ambazo zimeweza jenga miundombinu yetu na kwa gharama inayokubalika kimahesabu. Kwa sababu tusiwe tunazungumzia figures yaani dollar millioni 700 macho yakatutoka kwa uroho, kumbe wazee wanavuta karibu nusu yake. Tukazungumzia matukio ya jirani zetu, Ujio wa Bush na maswala ya EPA hali kuna mambo mengine mazito zaidi yanazidisha chuki ya wananchi kwa serikali yao. Chanzo cha vurugu zozote zile ni ubadhilifu wa serikali iliyopo madarakani. Ubaguzi wa rangi ama kikabila hutokana na kutokuwepo kwa haki ama uongozi bora wa serikali inayo tawala laa sivyo viamsho hivi ubakia kama volcano iliyolala (dormant).
Ni rahisi sana kuwadanganya wageni kuhusu maendeleo yetu lakini sii rahisi kuwadanganya raia wenyewe ambao wanafahamu uchovu wa serikali ama viongozi wao. Tatizo la Kenya halikutokana na makabila, laa hasha limetokana na ushindi ama uongozi wa Mwai Kibaki. Nina hakika kabisa kuwa kama Mwai Kibaki angekubali kushindwa na kuachia ngazi haya matatizo ya Ukabila Kenya yasingetokea...
Hivyo basi ni muhimu kutazama chanzo cha kila tukio badala ya kutibu gonjwa, matatizo ya Kenya yataendelea ikiwa Mwai ataendelea kuwa rais wa nchi hiyo sawa na tatizo la aMaleria nchini haliwezi kwisha kwa viandarua millioni 5 ama 10 ila litakwisha ikiwa madimbwi ya maji machafu na yaliyosimama yatafukiwa kuhakikihsa MBU hawapati sehemu za kuzaliana.
Mwisho, nimeona ktk Youtube, kumbe Bush aliwahi kuja TZ kabla ya safari hii (sio kama mgeni rasmi).
Tazama Youtube:- President Bush remembers Tanzania
Tutakuwa tunatoka nje ya mada.
NInajua hilo kuwa Tanzania katika ulimwengu haijulikani kabisa hata huna haja ya kwenda ulaya-Amerika-China- Japan nk. Tanazania hata haijulikani kwa baadhi ya nchi za Kiafrica.
Sijui sasa hivi umeisha faya analysis ukajua kuwa Baada ya Bush kututembelea tumeisha julikana kama unavyotaka tuamini?
Mkuu MtanzaniaKakindomaster,
Hapo ndipo unapokosea, unapotaka kuniweka maneno yako mdomoni mwangu. hakuna hata sehemu moja nilipoandika sasa wanadunia wanaijua Tanzania na wala jambo hilo haliwezi kufanywa na ziara moja.
Kinachofanyika ni process nzima na kuja kwa Bush ni kitu kimoja tu kwenye hiyo process. Sasa ukiunganisha mambo yote kwa pamoja, mwisho wake ni kwa Tanzania kujulikana duniani.
Naona unafikisha conclusions zako kwa data kidogo sana, matokeo yake unapata garbage, si unajua garbage in garbager out? Sijaandika popote kwamba baada ya Bush kuja, basi sasa watu wakitaka kufungua ofisi, watafungua Dar. Mkuu, soma tena hoja na kama kuna kitu hujaelewa, basi uliza. Hii ya moja jumlisha moja ni tatu, yalimponza Jumbe. Nilichomaanisha ni kwamba hiyo image ya a democratic and stable Tanzania ambayo inakuja kwa kujumlisha mambo chungu nzima, kukiwemo kuja kwa Bush, mafanikio ya JK Kenya, ndio inaleta hiyo perception ya vyombo vya dunia ku prefer Dar kuliko Nairobi wakati huko nyuma ilikuwa ni kinyume chake.
Mkuu Bin Maryam
Alichotaka kuonyesha ni kuwa kujulikana siyo tu kuja Bush Tanzania, kwa kipindi Bush amefika Bongo inawezekana kuna watu lukuki ambao hawakujua suala hilo, na baada ya miaka mitano ijayo linaweza lisiwe katika kumbukumbu za watu.
Hila huyu anatuonyesha ni jinsi gani mambo mbalimbali kama riadha, Kandanda, Mashirika ya ndege, na vitu vingine vidogo vidogo vinavyoweza kuchangia kusababisha nchi kujulikana.
Mkuu Mtanzania
Nafikiri kwa la kwanza sasa tunaelekea kuelewana mimi nilikuwa nakupinga baada ya kuona unashikilia suala la Bush kama ndo Basi tumeisha piga bao, ungeeleza vizuri mwanzoni tusingelitofautiana.
Lakini sasa tunaweza kuelewana baada ya kuonyesha kuwa hili suala la kujulikana linachangiwa na vitu vingi sana. Kwa Mfano wakati nasoma watu waliijua Kenya na Nigeria kwa sababu kulikuwa na Walimu kutoka Kenya na Nigeria basi. Hapa naona tunaelewana kuwa siyo Bush tu hila ni process kama nilivyoweka hata pale juu.
Suala la Dar umelitolea Mfano sina haja ya kuelezea hili Mkuu.
Ni vizuri sasa baada ya kukuulizia sana na kukupinga umeliweka vizuri. Nafikiri pia pale ambapo hujaelewa unaweza kupoint naweza kukutolea ufafanuzi Mkuu.
Hapa hatugombani Mkuu.
Bin Maryam,
I mean vyandarua millioni 5 bure kwa watoto kweli vinaweza kusaidia ikiwa mbu watazidi kuzaliana?...hivi kweli Maleria hupatika tu pale watu wanapolala ama ni swala la mazingira mazima. Je ni kiasi gani kati ya fedha hizo zimetengwa ili kuboresha mazingira yanayohusiana na chanzo cha maradhi hayo?.. zero!
Hata hivyo sina maana Bush hakufanya la maana isipokuwa nionavyo mimi hii ni biashara zaidi ya kusaidia.
Komredi Mkandara:
Wewe sasa masikini jeuri. Maswali mengi kama vile tushawahi kujitegemea miaka iliyopita.
Bin Maryam,
Hapana mkuu wangu sio masikini jeuri ila kama umenielewa mimi nayaweka maslahi ya Taifa mbele...
Bush kesha kuja na ahadi zimetolewa sawa! tunazipokea lkwa mikono miwili akini humu ndani mwetu kweli hizo fedha zinapewa huduma na thamani inayotakiwa!... hatujawahi jitegemea lakini sii ndio malengo yenyewe mkuu?..
Inakuwaje vibaya kujiuliza kama huko nyuma tumeweza tambua matatizo yanayotukwamisha ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya fedha hizi za misaada. Vijimila vya kuwa wasafi anapokuja mgeni ama mtu kuvaa suti yake siku ya harusi, kula chakula kizuri siku za harusi na maulidi..is this healthy kweli ktk maendeleo ya nchi yetu?
Watatupa hadi lini ikiwa sisi wenyewe hatuna malengo zaidi ya kutegemea misaada ambayo haiwafikii wananchi. Trust me, Bin Maryam, fedha za mabarabara na Umeme ambazo tumewahi pewa.. ni billion of dollars lakini tazama tumefanya nini?...na imekuwaje tumekuwa wazuri sana ktk kupokea misaada ya kuponya magonjwa yaliyokwisha ingia badala ya kuzuia magonjwa hayo!
I mean vyandarua millioni 5 bure kwa watoto kweli vinaweza kusaidia ikiwa mbu watazidi kuzaliana?...hivi kweli Maleria hupatika tu pale watu wanapolala ama ni swala la mazingira mazima. Je ni kiasi gani kati ya fedha hizo zimetengwa ili kuboresha mazingira yanayohusiana na chanzo cha maradhi hayo?.. zero!
Hata hivyo sina maana Bush hakufanya la maana isipokuwa nionavyo mimi hii ni biashara zaidi ya kusaidia.
Kadiri yangu, msaada wa vyandarua ni wa aibu. lakini hii Bongo bwana. Watawala wetu wamesifia, wadanganyika tumepiga makofi, maisha yanaendelea.
Ninavyoamini misaada hutumika tu kama daraja au stepping stone kuelekea kwenye sustainable something(maendeleo).
Nchi inapoendeshwa kwa misaada miaka nenda rudi, hii ndio nini?
Muafaka wa Kenya JK did nothing labda la kukaa na Bush na kuchekacheka naye
Mimi na Mkandara tunafanana kwa moja, wote naona tulikuwa waumini wazuri wa ujamaa na wapenzi wa Mwalimu Nyerere. Ila sasa tofauti inakuja, Mkandara hataki kukubali kwamba yule mpenzi wake wa utotoni sasa hayupo tena, inatakiwa aachane naye na kutambua reality iliyopo. Amheshimu mpenzi wake wa sasa na kuacha kukumbushia mambo yake ya nyuma, vinginevyo atawakosa wote.
Mimi naona ndugu yangu tukubaliane na the reality ya dunia tunayoishi sasa na kwamba kujikomba kwenye maslahi ndio reality ya dunia ya leo. Mmarekani akitaka mafuta Saudi, basi huenda na kila lugha ya kusifia. Mwingereza akitaka kuwavuta wawekezaji wa Kichina anaenda kuwaona bila hata kutaja neno human right. Sisi tukitaka 600M za Mmarekani inabidi tukubali kumweka Bush matakoni kwetu (According to Chemi Che-Mponda)na pia tutabasamu mpaka magego yaume. Nani anajali? Ni siku tatu tu, baada ya hapo unaweza kwenda Ruvuma ukawaambia wananchi dawa ya ukimwi inakuja, barabara inakuja, una uhakika wa makofi na kura 2010. Hiyo ndio reality ya dunia ambayo kama tunataka kufanikiwa inabidi tuikubali.
MkuuKadiri yangu, msaada wa vyandarua ni wa aibu. lakini hii Bongo bwana. Watawala wetu wamesifia, wadanganyika tumepiga makofi, maisha yanaendelea.
Ninavyoamini misaada hutumika tu kama daraja au stepping stone kuelekea kwenye sustainable something(maendeleo).
Nchi inapoendeshwa kwa misaada miaka nenda rudi, hii ndio nini?
Kikwete na waandishi wake wa hotuba ni zero kabisa.
Kasema kuna mambo matatu lakini kaongelea mawili tu, lile la tatu kaliogopa!
What a joke!
Niliandika "anaweza kudeliver" nikiwa na maana the jury is still out. Anaweza kuwa ana struggle mpaka sasa lakini kuna uwezekano akafanikiwa kwenye baadhi ya mambo labda kuliko hao walimtangulia na mifano ni hilo la Kenya na kumleta Bush.
Huenda mpaka sasa haya mambo hayatusaidii kama taifa maana hayaongezi pato wala shibe ya Mtanzania lakini pia yanaweza kuwa nguzo kubwa ya kuiletea baraka TZ siku za mbele through employment na investments zingine. Message kubwa hapo ni kwamba Tanzania ni democratic and stable, vitu viwili ambavyo ni muhimu mno kwa investors wa maana.
Sikuwa na maana JK amedeliver maana mambo mengi aliyosema atafanya, hajafanikiwa kuyafanya mpaka sasa.
Mkuu,
Naamini dunia na watu wengi wa dunia akiwemo Annan, wanaamini JK kasaidia.