Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Uamsho mnataka madaktari wa Iran waje ili baadae nao watake kulipwa fadhila ili ianzishe mahakama ya 'hedhi' na sharia za kishetani ndani ya Tanzania kwaajili ya kusuluhisha ndoa, talaka na kukatana viungo. Kwa hilo mmefeli jaribuni strategy nyingine.

Saa hizi ndiyo mtabaki kutukana tu, tunawajua kuwa hamna hoja. Wenzako wamesharukia hoja ya Pinda, kisha tangaza mwisho cc 3000 wao wanajifanya hoja yao, eti mashangingi! kawaunge mkono huko, hii ya mgomo tumeshamaliza hoja zote.

Jakaya Mrisho Kikwete kishafunga kazi kwa hilo la madaktari. Asiyetaka kufanya kazi aende kwa muajiri ataemlipa zaidi na tunamtakia kila la heri. Siku hizi Hospitali za binafsi ni nyingi sana na wanalipa vizuri. Na kama hapa unaona hapakufai unaenda duniani, mbona madokta wengi sana wapo nje ya Tanzania.

Saa hizi ni povu tu linawatoka hamna zaidi. Kwi kwi kwi teh teh teh!
 
Indeed zomba JK ndiye Rais wa jamhuri yetu...and that is a huge responsibility. He takes with him the good and bad things of the government he leads.

I admire his abilities. He has achieved higher standards in every aspect of development within a very short time. He is the best ever!
 
Hakuna jipya,ni hotuba iliyojaa habari za uongo,za kidhaifu,hotuba ya unafiki tupu,hotuba ya ubabe,lakini hajaja na strategy ya kumaliza mgomo na mzizi wa mgomo.
Nilichojifunza kwenye hotuba hii ni kutumia nguvu ya umma tu,maana kauli alizotoa ni za kejeli sana,kauli za dharau,kauli zenye kutujuza kuwa tayari wameshafanya maamuzi na utumishi wameshaanza kuchukua hatua wakati shauri lao halijaanza hata kusikilizwa,leo wamejidhihirisha ya kuwa wanafanya ubabe tu hata huko bungeni.

Natoa wito suala hili ili kupata suluhu ni kutumi nguvu ya umma tu.
 
Mkuu wa nchi kaamua sasa unataka kazi endelea hautaki acha, kumbe ndo mana walimu wanaogopa migomo kupata kazi ishu jamani nyie acheni tu hadi leo watu wanasota mtaani miaka mitatu alafu wengine mnaleta masihara kwenye kazi..
 
I admire his abilities. He has achieved higher standards in every aspect of development within a very short time. He is the best ever![/QUOTE

I agree to disagree with you...mambo si kama vile unavyosema hapa unless wewe ni miongoni mwa wateule wachache ambao mambo yao yako pouwa kwenye hii inflation ya kutisha tuliyonayo.
 
Aache kuwadanganya watanzania, jk hana jipya! Kawaita wakina Michuzi na kuwapa hiyo hotuba waiweke kwenye blogs. Kwa nini hakuwa na uso wa kusimama mbele ya camera tuuone uso wake akiisoma hotuba hiyo? Tumeacha shughuli zetu muhimu na kusubiri mpaka usiku sana hakuhutubia! Siku zenu zinahesabika!

Kiwi ilikuwepo leo tbc. tofauti ni kwamba badala ya kutoka mwisho wa mwezi imetoka mwanzo wa mwezi, labda ndo kilichokuchanganya.
 
Last edited by a moderator:


  • Mwaka 2004/2005, mshahara wa kuanzia wa daktari ulikuwa shilingi 178,700/=,
  • mwaka 2005/ 2006 tuliupandisha na kuwa shilingi 403,120/=. Tuliendelea kuupandisha
  • mwaka hadi mwaka mpaka kufikia shilingi 957,700/= wanazolipwa s
    • Ongezeka lipo lakini linaendana na hali halisi ya maisha, 2004/05, nikumbushe petrol ilikuwa sh ngapi vile, sukari ilikuwa sh ngapi, nyumba za kupanga zilikuwa sh ngapi vile. kada nyingine nadhani mshahara unawatoshandio maana hawadai. Hata hivyo madai ya madaktari sio mshahara tu bali na mazingira mazuri ya kufanyia kazi, ikiwemo upatikanaji wa vifaa tiba na rasilimali watu vile vile. Mr presidentplease try as much as you can to make the doctors comfortable for them to properly serve ur people.
 
I agree to disagree with you...mambo si kama vile unavyosema hapa unless wewe ni miongoni mwa wateule wachache ambao mambo yao yako pouwa kwenye hii inflation ya kutisha tuliyonayo.

Inlation isikutishe, wenye ujanja wa biashara wanaitumia hii chance ku export kwa wingi na wanawekeza kwenye uzalishaji wa kuuza bidhaa nje. Mbaya kukiwa na inflation halafu hatuwezi ku afford, mpaka sasa Bar zinajaa kila siku.

Kumbuka Tanzania kuna mzunguko mkubwa wa fedha zisizolipiwa kodi, hiyo inasababisha sana kukuwa kwa inflation. Measures zipo jikoni, usiwe na shaka.
 
mamayeyo, hv hizi ni nyingi kuliko mil 10 na kidogo wanazolipwa watu dodoma kwa ajili ya kugonga meza na kupigana vijembe? Mbona hamsimami kukemea? Ok basi budget ijayo tunaongeza 5m zaid hapo kwe mishahara ya wagonga meza kwa kuwa bunge letu ndo linalipa mishahara midogo kuliko mabunge yote Afrika!

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
ZIDUMU "FIKRA SAHIHI" ZA WATUNGA SERA WA CCM!
MDAU JR, Kwa hiyo ni sahihi kuwatoa kafara wagonjwa eti kwa sababu wabunge wanapewa mil10? Hakuna njia nyingine za kufanya hadi wagonjwa wafe? Kwani hizo pesa wanazofaidi wabunge ni za madaktari tu? Ni za wananchi wote. Itafutwe njia sahihi ya kukomesha mpango wa wachache kufaidi keki ya taifa wakati wengine wanaumia na si njia hii ya kuchezea roho za watu wasio na hatia. AMKA MDAU JR.
 
Acha kufuata mistari ya DHAIFU eti Serikali haina uwezo wa kuwalipa madaktari.....uwezo upo sana tu, usifuate nyimbo za mafisadi alias viongozi ambao uwezo wao wa kufikiri ni finyu. Kama tunaweza kutengeneza mabilionea nchini mwetu kila mwaka kwa kukwapua mali za Watanzania basi tunaweza kabisa kuwalipa madaktari mishahara waliyoiomba na kwa wafanyakazi wengine Serikalini ili kuboresha maisha ya Watanzania walio wengi. Kwenye miaka ya sitini uchumi wetru ulikuwa sawa sawa na nchi za Singapore na South Korea na hawa hawana utajiri wa mali asili ambao Tanzania tumejaliwa lakini angalia wenzetu walivyopata mafanikio makubwa katika kunyanyua uchumi wao na kuboresha maisha ya Wananchi wao...sie bado tumejikiita kuimba nyimbo za Viongozi DHAIFU eti Serikali haina uwezo!!!!


Hapo ndipo umakini unaotakiwa kuangalia. Ni sawa na mfanyakazi anayeangalia mmiminiko wa pesa shirikani bila kufahamu mtiririko wa matumizi ya kampuni. Yeye anachoangalia ni mshahara wake tu si vinginevyo.

Kwa akili yako madaktari wakipata pesa hizo na wewe unayehitimu sasa uendelee kusona na laki nne imekaa sawa? Barabara tunalalamika zijengwa, hospitali ziboreshe, kuimarisha mashirika ya umma kama ATC na Reli, na mengineyo, na bado watumishi wengine wa umma wanadai nyongeza za mishahara. Tunapojadili tuangalie mambo kwa upana si kuangaliwa tu kulipwa madaktari, je watumishi wengine? Bora kuongeza kidogo kidogo kwa awamu na wote wataridhika kidogo wanachopata kuliko wachache wawe na maisha peponi na wengine ndi hivyo tena kuedlea na ulalahoi.
 
Ongezeka lipo lakini linaendana na hali halisi ya maisha, 2004/05, nikumbushe petrol ilikuwa sh ngapi vile, sukari ilikuwa sh ngapi, nyumba za kupanga zilikuwa sh ngapi vile. kada nyingine nadhani mshahara unawatoshandio maana hawadai. Hata hivyo madai ya madaktari sio mshahara tu bali na mazingira mazuri ya kufanyia kazi, ikiwemo upatikanaji wa vifaa tiba na rasilimali watu vile vile. Mr presidentplease try as much as you can to make the doctors comfortable for them to properly serve ur people.
[/LIST]
[/B]
[/LIST]
[/B]


Tunapojadili hili tunaangalia watumishi wengine wa umma au madaktari tu? Wenye matatizo ya maisha ni madaktari tu au na watumishi wengine wa umma? Pesa hiyo kwa masha ya bongo inatosha kwa vile kuna nyongeza ya posho mbalimbali ambazo madaktari hwa wanapata, pengine zote jumla zinafikia karibu 2,000,000. Tatizo binadamu wengi hawaridhika na kipato kama kitabu fulani cha alflela ulela kilivyo sema: "Zaidi mtu apatavyo ndivyo atamanivyo." Pesa hiyo hiyo wengine inawatosha na wengine hata wangepata milioni 10 bado zisingewatosha.

Every doctor get enough money, how to manage them thats is
the big problem .
 
Hakuna jipya,ni hotuba iliyojaa habari za uongo,za kidhaifu,hotuba ya unafiki tupu,hotuba ya ubabe,lakini hajaja na strategy ya kumaliza mgomo na mzizi wa mgomo.
Nilichojifunza kwenye hotuba hii ni kutumia nguvu ya umma tu,maana kauli alizotoa ni za kejeli sana,kauli za dharau,kauli zenye kutujuza kuwa tayari wameshafanya maamuzi na utumishi wameshaanza kuchukua hatua wakati shauri lao halijaanza hata kusikilizwa,leo wamejidhihirisha ya kuwa wanafanya ubabe tu hata huko bungeni.

Natoa wito suala hili ili kupata suluhu ni kutumi nguvu ya umma tu.

kwenye vitisho ni kweli, maana kasema doc akifukuzwa kazi itabidi aachie nyumba ya serikali within 24 hrs. kama sio kutishana ni nini? lakini pia nimepata point nyingine, hivi mtu anaweza kupata nyumba ya kupanga within 24hrs? inabidi hili nalo liangaliwe.
 
Huu mgogoro una pande mbili: serikali na madaktari. Amri ya mahakama ni kwamba pande mbili hizi zikae kwenye meza ya mazungumzo, lakini pia hata wapambe wa CCM wanashauri hivyo na serikali yenyewe inarudiarudia kuwa bado mazungumzo yanaendelea.

Sasa kuna mambo yanahitajika ili kufanya mazungumzo yaende vizuri: sincerity, confidenctiality & trust. Haya mambo yakikosekana mazungumzo yatavunjika. Tangu mwanzo serikali imekuwa ina-behave kama watoto wadogo, kila kukicha wanalilia mbele ya vyombo vya habari, na mbaya zaidi wanatoa details za kile wanachosema kinaoongelewa! Tafsiri yake ni kwamba wanataka to-weaken the other side which in effect inaharibu kabisa trust kati ya pande hizi mbili.

Sijui ni busara gani imetumika kwa serikali ku-publicize hiki wanachokiita madai ya madaktari? Utaongeaje na mtu ambaye tayari unashinda kwenye vyombo vya habari kumtangaza kama mkorofi na mlafi wa malipo manono? Kulikuwa na haraka gani kwa serikali kuongelea in details haya madai, tena huku kukiwa na amri ya mahakama?

Madaktari wamekuwa na attitude ya grown up sana kwenye huu mgogoro. Hatujasikia wakililia kwenye redio au television, lakini kila mgonjwa anayekwenda kwenye hizi hospitali zinazosifiwa na serikali anajua tabu wanayopata madaktari.

Kwa maoni yangu, a third party is needed. Spika wa Bunge angeruhusu sasa report ya kamati ya bunge inayohusika na huduma za jamii kuweka mezani report waliyoandika mara baada ya kukutana na pande zote mbili. Naamini list ya madai ni tofauti na hii tuliyopewa na serikali.

Pia ningeshauri viongozi wetu wavute pumzi, wa-relax na waachane na dhana/hisia kwamba wakikubali kukaa chini na kujadili kwa kina madai ya madaktari wataonekana dhaifu. Kushuka chini ni kielelezo cha ukomavu. Naona kama kuna 'ukubwa' fulani kwa upande wa serikali lakini kama wangechukua attitute ya kwamba migomo ni sehemu ya demokrasia basi wangepata solution. Inawezekana kabisa madaktari wako tayari kupata chini ya huo mshahara wa 3.5m kama wataona upande wa pili wana nia ya dhati ya kuborosha mazingira ya kazi.

Hivi ni kiongozi gani atakubali kulipwa Tsh 1m kwa kufanya kazi chumba kilichojaa wagonjwa tena wengine wanajinyea? Everyday unakumbana na hali kama hii. Hujui wagonjwa wametoka wapi, risks za kuambukizwa magonjwa ni kubwa sana maana wakati mwingine hata gloves ni shida! Ifike mahali tuelewe wanachosema madaktari hata kama hawapigi kelele kwenye vyombo vya habari.
 
LIWALO NA LIWE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:wacko:
 
Sio MGOMO, madaktari WAACHE kazi! Usijifanye chizi huelewi!
 
Acha kufuata mistari ya DHAIFU eti Serikali haina uwezo wa kuwalipa madaktari.....uwezo upo sana tu, usifuate nyimbo za mafisadi alias viongozi ambao uwezo wao wa kufikiri ni finyu. Kama tunaweza kutengeneza mabilionea nchini mwetu kila mwaka kwa kukwapua mali za Watanzania basi tunaweza kabisa kuwalipa madaktari mishahara waliyoiomba na kwa wafanyakazi wengine Serikalini ili kuboresha maisha ya Watanzania walio wengi. Kwenye miaka ya sitini uchumi wetru ulikuwa sawa sawa na nchi za Singapore na South Korea na hawa hawana utajiri wa mali asili ambao Tanzania tumejaliwa lakini angalia wenzetu walivyopata mafanikio makubwa katika kunyanyua uchumi wao na kuboresha maisha ya Wananchi wao...sie bado tumejikiita kuimba nyimbo za Viongozi DHAIFU eti Serikali haina uwezo!!!!

:cheer2:Zamani nilikuwa nafikiri hivi hivi kwa vile sikujua kinogaubaga. Nilipokabidhiwa jukumu katika kampuni fulani na majukumu na kuingia na kutoka unashtukia unababaika namna ya kupata za kuwalipa wafanyakazi. Rahisi kumnyooshea kidole mchezaji uwanjani ukaonekana ni mchezaji mzuri, laini kama ungeingia wewe pale uwanjani kingekuwa kichekesho cha kuwavunja mbavu watazamaji kukaba miguu ya mtu wakati mpira ulishaondoka zamani.:cheer2:
 
Sio MGOMO, madaktari WAACHE kazi! Usijifanye chizi huelewi!

Mbona povu linakutoka namna hiyo, hivi unadhani Ma Dr. ni kama walimu. Ngoja wakutane watoe tamko lao baada ya hutuba ya rais utalipenda tu.
 
Back
Top Bottom