Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Kwanini imechukua muda mrefu kufikia uamuzi huo? Hili suala siamini kabisa lingefika hapa lilipofika kama kila mtu angekuwa genuine. Ila ndo hivyo tena. By the way, kumbe hata rais anasikitika na kuumizwa kwa Dr. Uli ingawa sio mfanyakazi wa serikali?

Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Rais wa wote.
 
Dai la kupinga nyongeza ya madai ya wabunge ni tofauti na hili la madaktari? Pengine wabunge lilikuwa na hoja kwamba wao ni muda mfupi na hawana mafao zaidi baada ya kuacha ubunge kuliko hawa madaktari ambao taaluma yao ni ya maisha. Wabunge tulivimbisha iishipa usoni, lakini la madatari tunanywea hii imekaaje?

Kwa sababu madaktari wanastahili kupata mishahara inayoendana na Taaluma zao. Si Serikali hii hii inayodai kila inapokutana na Watanzania nci za nje kwamba inajaribu kuweka mazingira mazuri mbali mbali ikiwemo mishahara ya watalaamu mbali mbali ikiwemo madaktari ili kuakikisha hawaendi kuajiriwa ncgi za nje na wale walio nje wavutiwe kurudi nyumbani. Sasa inakuwaje tena kauli zao zinapingana? Wako radhi kuwalipa mavuvuzela wa magamba kule Bungeni mishahara na marupurupu manono kule bungeni lakini wakati huo huo kuwalipa mishahara viduchu madaktari. Eti yule mganga wa kienyeji aliyeishia darasa la sana sasa hivi anapata mshahara mkubwa kuliko daktari ambaye anaokoa maisha ya Watanzania!!!
 
Wakuu sentensi hii niliyowekea red ni kwamba rais anakubali kuwa ni watu dani ya serikali wamefanya unyama huo halafu anawakana, yaani anaiepusha serikali kuwa si kazi yake, ila ni kazi ya mtu ndani ya serikali?

Au ana maana kuwa ni mahakama ndio imefanya hivyo?

Siwezi kuamini kama kweli rais alisoma hiyo, kama kuna mtu alimwandikia rais hotuba hiyo anatakaiwa kukatwa kichwa. You can not send people to kill and then you abandon them.

ukiunganisha na hapa unapata jibu kuwa jamaa amehusika'' Ni kweli kwamba yeye si mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya. Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa na Serikali.''

huwa anaropoka tu
Nadhani wakati mwingine tuwe na kile kinachoitwa fair comment, ninachokiona ni udhaifu mkubwa wa kufikiri miongoni mwa wana-JF na nitathibitisha kama ifuatavyo. Mnyika amewahi kusema Rais ni dhaifu, ingawa kwa namna fulani naye (Mnyika) alikuwa dhaifu kifkra wakati anatamka hiyo, sasa basi kwa kuwa alisema Rais ni dhaifu maana halisi Rais awe imara katika masuala yanayohusu maisha ya Watanzania, wiki kadhaa kuna mgomo wa madaktari usiofuata sheria za nchi wala maadili ya kidaktari lakini kubwa zaidi ni mgomo unaoua Watanzania wasio na hatia na hapo hapo ni mgomo unaoshabikiwa kwa chini chini na wanaharakati pamoja na chama kimoja cha upinzani kilichowahi kutamka wanaweza kuifanya nchi isitawalike, sasa Rais ameamua (uamuzi mgomo) madaktari wachague kuacha kazi au kuendelea na kazi ili Serikali iwe na uhakika kuhusu kuziba nafasi na pia kuokoa maisha ya watanzania wanalioko hatarini kufa kwa kukosa huduma (hawa watanzania hawajumuishi wanaharakati au madaktari wenyewe kwa sababu wakiumia wanatibiana). Najiuliza uamuzi huu wa Rais kwa nini unawakera watu? Au kwa vile ni uamuzi unaoelekea kuhitimisha mgomo huu wa kuua raia wasio na hatia ambao Kikwete yuko tayari kuwalinda kwa gharama zozote kwa sababu kura zao ndizo zimemuweka madarakani? Kwanini kuna watu wanakerwa au ni kwa sababu mbinu za "nchi isitawalike" zinakwamaba? Niwaulize mnataka mgomo uendelee kwa sababu zipi zenye nguvu ya hoja zaidi ya kunusuru maisha ya Watanzania? Mawazo yenu hayo yanawavua uzalendo. Je, nanyi si mauaji?
 
Wakuu sentensi hii niliyowekea red ni kwamba rais anakubali kuwa ni watu dani ya serikali wamefanya unyama huo halafu anawakana, yaani anaiepusha serikali kuwa si kazi yake, ila ni kazi ya mtu ndani ya serikali?

Au ana maana kuwa ni mahakama ndio imefanya hivyo?

Siwezi kuamini kama kweli rais alisoma hiyo, kama kuna mtu alimwandikia rais hotuba hiyo anatakaiwa kukatwa kichwa. You can not send people to kill and then you abandon them.

Na, kuhusu mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kusitisha mgomo. Anayekaidi amri ya Mahakama ananunua ugomvi na mhimili huo wa dola ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu mtu huyo. Hivi baada ya kufika hapo Serikali iwe na ugomvi na Dkt. Steven Ulimboka kwa sababu ipi na jambo lipi hata iamue kumdhuru? Kama kuna mtu wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa kutumwa na Serikali.

Nini kisichoeleweka kwako kama Rais amesema "kama kuna mtu wa serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake bnafsi na si Serikali au kutumwa na seikali." Hii imeeleweka wazi.
 
Wewe ndio huna cha kuzungumza kazi kuitetea Serikali inayowaua raia wake wasio na hatia kila siku siku,mbona Serikali haikuzungumzia kuhusu uboreshwaji Wa mazingira ya kazi/vitendea kazi vinavyomuwezesha daktari kumtibu binaadamu mbona hii point Serikali inaikwepa sana na matokeo yake wanazungumzia mishahara na posho za madaktari?

Katika mambo 12, 11 yanahusu maslahi ya madaktari na si maslahi ya mgonjwa, na hilo unalouliza wewe limejibiwa, ulikuwa unataka jibu lipi zaidi ya hili:

Jambo la sita ni kuhusu mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na madaktari kuhusu kuboresha huduma ya afya. Mapendekezo hayo yalihusu kutathmini sera na mpango wa afya ya msingi, bajeti ya afya kuwa asilimia 15 ya bajeti ya Serikali, kuwepo na utaratibu mzuri wa kuajiri madaktari na kuboresha viwango vya ubora wa madaktari na kadhalika. Serikali imeyaafiki mapendekezo hayo na yatafanyiwa kazi.
 
Nasikitika kupoteza muda wangu kusoma propaganda hizi ndefu za DHAIFU, I thought angekuja na suluhisho kumbe mmmhhhh....
Mahakama nataka ilalamike kwa hili la swala ambalo liko mahakamani kuendelea kuzungumzwa na JK
Inawezekanaje swala ambalo liko mahakamani huku mamlaka nyingine zinaendelea kufukuza watu kazi?
Nakosa imani na kila kitu; Serikali, Bunge na mahakama
 
Suala la madaktari naona Mkuu ameendeleza propanganda zilezile za kwamba kulikuwa na makubaliano. Makubaliano gani wakati mazungumzo yalikuwa hayajakamilika, hebu tuwekeeni haya makubaliano yakiwa na sahihi za pande zote mbili tuone.

Na JK ameendelea kuudanganya umma na kuufitinisha na madaktari kwa kuonyesha kuwa madaktari tatizo kubwa waling'ang'ania mshahari wa mil 3.5 wakati walikuwa wanajadiliana na kabla ya makubaliano serikali ikatangaza hizo 15% na labda sasa wanafikiri kuongeza mpaka 20% maana hii haikuwepo mwanzo. JK bila aibu anautangazia umma nyongeza ya posho ya kuchunguza maiti, dai ambalo halikuwepo kati ya yale waliyokuwa wanajadili.

JK acha kutishia nyau, hamuwezi kufukuza madaktari wote walioko kwenye mgomo, mnajidanganya, wasikilizeni madaktari na mfikie muafaka warudi kazini, kuendeleza vitisho na kuwakamata na kutesa viongozi wao haitawasidia.

Huduma gani zimeboreshwa kwenye hospitali za mikoa eti na sasa wanageukia wilayani, hii sio era ya kusema uongo na ukafikiri utapata watu. Ukifika mahospitalini sasa hivi hakuna dawa, hakuna vifaa tiba, hakuna watumishi. Hospitali eti zimepandishwa hadhi ya kuwa za rufaa zikiwa hazina madaktari bingwa, sasa nashangaa kama rufaa inatoka kwa MD inakwenda Kwa MD sijui itakuwa rufaa ya namna gani hiyo. Hospitali kuzitaja kwa uchache ni mfano hospitali ya mkoa wa rukwa ambayo ina bingwa mmoja tu ambaye ni surgeon nae yuko kwenye administration. JK usitupige changa la macho hakuna maboresho yoyote yalofanywe. Nchi imekushinda step down.

mkuu sio kwamba utashindwa kwenda Jamaica kubembea.Mnafiki Mkubwa dhaifu, TISS na mwanao ndio ulowatuma kumfanyia unyama Ulimboka, utalipa hapahapa duniani.

Mkuu hakuna anaetishiwa Nyau, kila jambo lazima liwe na Mstari wake, haliwezi kwenda/kuendeshwa bila kuwa na "Limitation" yake.
The so called dhaifu amefikia yake now its up to the Doctors, tha ball is in Doctors court!

Hii hapa kwa kiswahili Chepesi:
"Kutokana na ukweli huo basi kama daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo. Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo wa kumlipa anachokitaka. Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi. Kwa nini upate usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24. Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo, mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na sheria za kazi na maadili ya kazi ya udaktari."

Raisi wangu ana busara sana.. hata mtoto mdogo akisomewa hiyo hotuba ataelewa tu..
 
Naona unajikanyaga kanyaga tu eti Serikali haina uwezo wa kuwalipa madaktari mishahara waliyoiomba. Hivi umefanya tathmini ipi iliyokuwezesha kutoa hitimisho kwamba Serikali haina uwezo wa kuwalipa madaktari mishahara ya sh 3.5 millioni kwa mwezi?

Hapo ndipo umakini unaotakiwa kuangalia. Ni sawa na mfanyakazi anayeangalia mmiminiko wa pesa shirikani bila kufahamu mtiririko wa matumizi ya kampuni. Yeye anachoangalia ni mshahara wake tu si vinginevyo.

Kwa akili yako madaktari wakipata pesa hizo na wewe unayehitimu sasa uendelee kusona na laki nne imekaa sawa? Barabara tunalalamika zijengwa, hospitali ziboreshe, kuimarisha mashirika ya umma kama ATC na Reli, na mengineyo, na bado watumishi wengine wa umma wanadai nyongeza za mishahara. Tunapojadili tuangalie mambo kwa upana si kuangaliwa tu kulipwa madaktari, je watumishi wengine? Bora kuongeza kidogo kidogo kwa awamu na wote wataridhika kidogo wanachopata kuliko wachache wawe na maisha peponi na wengine ndi hivyo tena kuedlea na ulalahoi.
 
Nadhani wakati mwingine tuwe na kile kinachoitwa fair comment, ninachokiona ni udhaifu mkubwa wa kufikiri miongoni mwa wana-JF na nitathibitisha kama ifuatavyo. Mnyika amewahi kusema Rais ni dhaifu, ingawa kwa namna fulani naye (Mnyika) alikuwa dhaifu kifkra wakati anatamka hiyo, sasa basi kwa kuwa alisema Rais ni dhaifu maana halisi Rais awe imara katika masuala yanayohusu maisha ya Watanzania, wiki kadhaa kuna mgomo wa madaktari usiofuata sheria za nchi wala maadili ya kidaktari lakini kubwa zaidi ni mgomo unaoua Watanzania wasio na hatia na hapo hapo ni mgomo unaoshabikiwa kwa chini chini na wanaharakati pamoja na chama kimoja cha upinzani kilichowahi kutamka wanaweza kuifanya nchi isitawalike, sasa Rais ameamua (uamuzi mgomo) madaktari wachague kuacha kazi au kuendelea na kazi ili Serikali iwe na uhakika kuhusu kuziba nafasi na pia kuokoa maisha ya watanzania wanalioko hatarini kufa kwa kukosa huduma (hawa watanzania hawajumuishi wanaharakati au madaktari wenyewe kwa sababu wakiumia wanatibiana). Najiuliza uamuzi huu wa Rais kwa nini unawakera watu? Au kwa vile ni uamuzi unaoelekea kuhitimisha mgomo huu wa kuua raia wasio na hatia ambao Kikwete yuko tayari kuwalinda kwa gharama zozote kwa sababu kura zao ndizo zimemuweka madarakani? Kwanini kuna watu wanakerwa au ni kwa sababu mbinu za "nchi isitawalike" zinakwamaba? Niwaulize mnataka mgomo uendelee kwa sababu zipi zenye nguvu ya hoja zaidi ya kunusuru maisha ya Watanzania? Mawazo yenu hayo yanawavua uzalendo. Je, nanyi si mauaji?

Nakuunga mkono.
Mgomo umepatiwa majibu. Bravo Rais tulihitaji msimamo wa mkuu wa nchi hata kama hautawafurahisha wote
Kwanza madaktari mmesindwa kuwin public sympathy. Viongozi wenu wamewakana mbele ya mahakama. Ina maana MAT haiungi mkono mgomo. Na hiyo inayoitwa “Jumuia ya madaktari haina uhalali wowote”. Sasa haijulikani nani anaongoza mgomo. So madakatari wanaachwa solemba kila mtu aamue mwenyewe. This was predicted before.
Hotuba hii ya Rais ya maandishi imetulia. Madaktari wao wenyewe walianza kuchoma daraja kabla hawajalivuka. Mkidhani mkuu wa nchi hawezi kufukuza madaktari. Sasa amesema anaweza.
Kwa kutumia mgomo ambao sanasana umewaumiza wananchi walio wa chini ambao hawajahamasishwa vya kutosha kuelewa lengo la mgomo ni vigumu kuwaunga mkono. Mmekosa sympathy kotekote, serikalini na kwa wananchi. What a pitty.
Kipigo cha Ulimboka ambacho hakijathibitishwa aliyemuumiza ni nani mlitaka kukitumia kuongezea mafuta katika mgomo ambao ulishaanza kudorora kwa kutokuwa na mashiko. Sasa Ulimboka kaenda nje ya nchi mgomo utakolezwa na nini….?!
Mkuu ambaye mlidhani ni dhaifu kayaweka wazi . Anayetaka kuendelea na kazi aendelee asiyetaka aache. Hilo la wananchi watatibiwa na nani hiyo muachie yeye. Haikuhusu. Hiyo sympathy kama mlikuwa nayo mbona hamjajali maumivu ya wagonjwa wakati wa mgomo.
Wanaojiita jumuia ya “specialist wa Dar es salaam” nao wawe waangalifu. Wao kama seniors wangepashwa kuongoza vijana madaktari wachanga katika fani badala ya kuchochea unethical behaviours. Acheni kucheza na maisha ya watu.
 
Nasikia ndo anasoma hotuba hii sasa hivi ?
ni kweli kwa nyie mnaangalia TV
 
Huyu bwana Juma Mgaza ndo nani wakuu.Inaonekana yeye ndo alimwokoa Dr Ulimboka.Na kama ni kweli i think he will be the next to follow the foot step.Manake chini ya hutuba ya mkuu kamrusha yangu macho
Mkuu huyu Juma Mgaza ndiye aliyemuokota Dk Ulimboka kwa mara ya Kwanza mstuni Pande na kumpeleka Polisi.
 
Huna hoja.

Waliyokubaliana kayasema na ambayo serikali imekataa na hayo kayasema waziwazi na ambayo hawajakubaliana kayasema waziwazi na kasema asiyeyataka hayo ambayo serikali imeyakataa aache mwenyewe kazi. Nini zaidi usichokielewa?

Kama huna hoja kaa kimya kama wenzako.

watoa roho za watu utawajua tu jinsi wanavyoteteana,wenzake wapi waliokaa kimya?
 
Nakuunga mkono.
Mgomo umepatiwa majibu. Bravo Rais tulihitaji msimamo wa mkuu wa nchi hata kama hautawafurahisha wote
Kwanza madaktari mmesindwa kuwin public sympathy. Viongozi wenu wamewakana mbele ya mahakama. Ina maana MAT haiungi mkono mgomo. Na hiyo inayoitwa "Jumuia ya madaktari haina uhalali wowote". Sasa haijulikani nani anaongoza mgomo. So madakatari wanaachwa solemba kila mtu aamue mwenyewe. This was predicted before.
Hotuba hii ya Rais ya maandishi imetulia. Madaktari wao wenyewe walianza kuchoma daraja kabla hawajalivuka. Mkidhani mkuu wa nchi hawezi kufukuza madaktari. Sasa amesema anaweza.
Kwa kutumia mgomo ambao sanasana umewaumiza wananchi walio wa chini ambao hawajahamasishwa vya kutosha kuelewa lengo la mgomo ni vigumu kuwaunga mkono. Mmekosa sympathy kotekote, serikalini na kwa wananchi. What a pitty.
Kipigo cha Ulimboka ambacho hakijathibitishwa aliyemuumiza ni nani mlitaka kukitumia kuongezea mafuta katika mgomo ambao ulishaanza kudorora kwa kutokuwa na mashiko. Sasa Ulimboka kaenda nje ya nchi mgomo utakolezwa na nini….?!
Mkuu ambaye mlidhani ni dhaifu kayaweka wazi . Anayetaka kuendelea na kazi aendelee asiyetaka aache. Hilo la wananchi watatibiwa na nani hiyo muachie yeye. Haikuhusu. Hiyo sympathy kama mlikuwa nayo mbona hamjajali maumivu ya wagonjwa wakati wa mgomo.
Wanaojiita jumuia ya "specialist wa Dar es salaam" nao wawe waangalifu. Wao kama seniors wangepashwa kuongoza vijana madaktari wachanga katika fani badala ya kuchochea unethical behaviours. Acheni kucheza na maisha ya watu.

Bora wewe umekuwa na upeo wa kuangalia pande zote za shingilingi na side effects. Tatizo wengi wetu mambo ya kiitikadi za kisiasa tunazieta kwenye mfumo wa kazi za kitaaluma zenye kufuata sheria katika utendaji. Kiburi nacho walichoonyesha madaktari si cha kawaida na chenye kwenda kinyume kabisa cha maadili ya kazi yao. Serikali imefanya kazi kwa upole sana hadi kupeleka suala kwenye mahakama ya kazi ya usuluhishi, hata hivyo madaktari wameendelea na kichwa ngumu.

Kama serikali ingechukua rungu lake lingeanzia na utafiti wa wagonjwa walioathirika na mgomo huo na kisha kufunguliwa mashtaka mahakamani madaktari ambao wangesombwa na karandika na kwenda kusweka kule Keko. Lakini serikali imekuwa na uungwana mkubwa sana tu.

Kwa yeyote mwenye uelewa mpana hotuba ya Rais imetulia, ametumia zaidi lugha ya kidiplomasia kufikisha ujumbe uliokamilika. Si madaktari wote ambao wanaafiki migomo hiyo kwani wengine wamefanya kwa kushinikizwa tu kama ilivyotokea KCMC baadhi ya madaktari waliokuwa kazini kutolewa kwa vitisho na wale waliokuwa katika mgomo.

Narudia kusema tena serikali inazo taasisi na idara mbalimbali za usalama katika kuendesha shughuli zake, na baadhi ya taasisi au idara ziko independence katika utendaji wake ambao hata mkuu wa nchi wakati mwingine hawezi kuzinyooshea kidole. Ndiyo maana yalikomkuta kiongozi wa mgomo wa madaktari Dr. Stephen ni jambo nyeti na wenye kulifanya wana njia zote za kulififisha uchunguzi usikamilike kwa sababu za wanazojua wao katika utendaji wao, na hatuna hakika ni nani.

Cha msingi madaktari wasitishe migomo na kuendelea na kazi, wasiokubali waende kutafuta ajira sehemu nyingine kufikia ndoto zao za kufikirika.

Rais katoa hutuba iliyotulia na kilichozunguzwa amekifafanua kwa tahadhari na busara ya hali ya juu, mwenye kuelewa anajua ninachojadili katika post hii.
 
hi serikali ya nani? Je madaktari hawana haki kusema katika mazingira hayo magumu, je kuwafukuza ni dawa swali kwako je wanasiasa wanalipwa kiasi gani na ukilinganisha wao na madaktari wetu ni nani wana kazi ngumu?:deadhorse:
 
Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Rais wa wote.

Indeed zomba JK ndiye Rais wa jamhuri yetu...and that is a huge responsibility. He takes with him the good and bad things of the government he leads.
 
kawajibu vuzuri madaktari....kama muajiri wa sasa hawezi kukulipa unachotaka ai unachostaili huitaji kugoma ....ni kuacha kazi ns kumfuata muajiri anayekulipa vizuri.....madaktari acheni kusumbua vichwa vyetu.....labda mtubainishie kuwa pesa hizo zipo mahala mmeziona...after all mlipwe m 3.5 kea lipi?....
 
Back
Top Bottom