Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Hotuba ya Rais Kikwete 30.6.2012

Rais JK kaongea kwa watafiti wa mambo ni wazi madaktari hawewezi kufanikiwa na wengi watapoteza kazi J, tatu Madaktari wengi wataripoti kazini...
Kwani madaktari jmosi na jumapili hawafanyi kazi mpaka useme j3
 
Umenikumbusha kuna jamaa alikuwa anahojiwa kwenye televisheni huku anamsukuma mgonjwa wake kwenye kibaiskeli pale maeneo ya MOI yeye japo mgonjwa wake alikosa matibabu lakini aliungana na madaktari na kuitupia lawama Serikali kwa kushindwa kushughulikia mgogoro wa madaktari huyo mtu sensible kweli mimi narudia kusema kwa mwananchi wa kawaida kuelekeza nguvu zake kulaumu madaktari ni kupoteza pumzi bure kwani hakuna sehemu daktari alipofunga mkataba na mwananchi kutoa huduma bora za afya na mengineyo lakini still hatustaili kadhia tunayopata kwa kukosa huduma za afya kutokana na mgomo so what should we do? Sahihi kabisa tukimwajibisha aliyepewa dhamana..........

Hakuna mkataba na mwananchi kutoa huduma ...yes mna mkataba ya kutoa huduma kwa wagonjwa kwa mujibu wa kazi zenu na vifaa vilivyopo..(japo pungufu)..

Yes, mna haki ya kuondoka na kuacha kazi incase mkiona vifaa na mashahara wa mwajiri haufikii matarajio yako

BUT, huna haki ya kukataa kuripoti kazini, kufanya kazi na kuwazuia wengine (mobilize) wengine wagome..ili kuikomoa serikalini..

Just go and leave goverment hospitals nenda private au jenga hospitali yako jilipe upendavyo..
 
Anza kupeleka barua na watuhumiwa; omba msaada US na washirika wako wote (mfanye vizuri vile vikao vyenu vya jumuia) ..

Tutakutana mahakamani ..au vipi?

Pole mwana JF. sisi siyo akina Rizi moja wanaofurukuta mahakamani-mahakamani halafu hawaonekani.

Tanguliza Udini, tukana au mtetee filauni, lakini fact ni kwamba Duniani hatujawahi kuwa na martial plan iliyopangwa na mwaarabu au mwafrika na ikaleta maendelea popote. Inabidi ukubali ubora wa madikteta wa ulaya wameendeleza baadhi ya nchi.

Ni kweli kwamba tukio la Dr. Stephen kuna mizengwe toka serikalini jambo ambalo huanyika kwa siri kila mmoja wetu anajua serikali po pote zina intelijensia katika kuzima mambo fulani, lakini jambo hilo limefanyika wakati mbaya ambapo serikali inatoa tamko la kuwafukuza madaktari walio kwenye migomo na kuwasitiri wenye kujali wajibu wa taaluma yao kulinda uhai wa raia.

Kwa hotuba ya Rais inaonyesha wazi serikali imejitahidi sana katika kusikiliza madai yao, lakini kwa akili ya kawaida tu huwezi kutegemea kwamba madai yote yatekelezwe kadiri unavyotaka kwa kuwa chunguni kule chakula si cha madaktari tu, wote wanatumbulia macho chungu kile, na mwenye kutunza chungu anajua mgao mwingine, anabidi bakishe kwa ajili ya mgao mwingine vinginevyo wengi watakufa njaa wakijali mmoja tu.

Milioni 7 wanazodai madaktari ni mno ukilinganisha na uwezo wa serikali, na hata kama chama kingine kiingie madarakani katu hawatawaze kutoa dau hilo kwani kuna kazi hadi kufikia huku kitu ambacho kitatuchukua muda mrefu.

Rais alitakiwa kuyaweka wazi haya hadharani mapema wengi tungeelewa ukweli wa pande zote mbili, kwani kwa muda mrefu tumekuwa na uelewa wa madai ya madatari tu bila kuona upande wa pili.

Kwa sasa ukweli ni serikali ipo sahihi katika kutoa hitimisho la mgomo huo, na madaktari vichwa ngumu waende wanaokoona watapata mafao hayo, na wadaktari wazalendo wenye kujali uhai wetu ndio tubaki nao hata kama ni wachache bora kuliko kuwa na kundi lisilojali uhai wetu.

ni leo ndio umeyajua haya? yana tofauti gani na yale aliyosema mwezi wa 3 kwa wazee wake?
hivi kusema madaktari wanaotaka kuondoka waondoke ndo kutoa hitimisho la mgomo?hivyo?
usilowanishe msimamo wako kwa hii hotuba chonganishi...
 
Ni kweli kwamba tukio la Dr. Stephen kuna mizengwe toka serikalini jambo ambalo huanyika kwa siri kila mmoja wetu anajua serikali po pote zina intelijensia katika kuzima mambo fulani, lakini jambo hilo limefanyika wakati mbaya ambapo serikali inatoa tamko la kuwafukuza madaktari walio kwenye migomo na kuwasitiri wenye kujali wajibu wa taaluma yao kulinda uhai wa raia.

Kwa hotuba ya Rais inaonyesha wazi serikali imejitahidi sana katika kusikiliza madai yao, lakini kwa akili ya kawaida tu huwezi kutegemea kwamba madai yote yatekelezwe kadiri unavyotaka kwa kuwa chunguni kule chakula si cha madaktari tu, wote wanatumbulia macho chungu kile, na mwenye kutunza chungu anajua mgao mwingine, anabidi bakishe kwa ajili ya mgao mwingine vinginevyo wengi watakufa njaa wakijali mmoja tu.

Milioni 7 wanazodai madaktari ni mno ukilinganisha na uwezo wa serikali, na hata kama chama kingine kiingie madarakani katu hawatawaze kutoa dau hilo kwani kuna kazi hadi kufikia huku kitu ambacho kitatuchukua muda mrefu.

Rais alitakiwa kuyaweka wazi haya hadharani mapema wengi tungeelewa ukweli wa pande zote mbili, kwani kwa muda mrefu tumekuwa na uelewa wa madai ya madatari tu bila kuona upande wa pili.

Kwa sasa ukweli ni serikali ipo sahihi katika kutoa hitimisho la mgomo huo, na madaktari vichwa ngumu waende wanaokoona watapata mafao hayo, na wadaktari wazalendo wenye kujali uhai wetu ndio tubaki nao hata kama ni wachache bora kuliko kuwa na kundi lisilojali uhai wetu.

Kusema ukweli hakuna nchi yoyote inayoendesha mambo yake kwa hotuba za kwenye luninga. Leaders are there to serve people. Sidhani kama anachosema JK ndio kitu ambacho wasaidizi wake walikuwa wanawaambia madaktari. Ubabe na vitisho ndio lugha watawala wanayopenda kuitumia bila hata sababu za msingi. Halafu worse of all ni hii ya kujaribu kumsilence one of theirs...it was a terrible mistake!
Turudi tena kwenye basics. JK akaze uzi kuzuia wizi wa mali ya umma na matumizi mabaya ya fedha za umma ili wakati wa kujenga hoja kwamba nchi haina uwezo, watu wawe wanamuani kama anasema ukweli. Sasa hivi ni kama vile kuna usanii unaendelea.
 
Pamoja mkuu. Ni kweli kabisa. Hakuna anayewalazimisha kubaki kwa mwajiri asiyetaka kuwaongeza mshahara wanaotaka wao. Naunga mkono kabisa kuwa waende wakatafute green pastures. Na usemavyo kuwa nchi nyingine wafanyakazi wanafanya part time baada ya saa za kazi ni kweli. Na hawa wetu wanafanya sana tu lakini si baada ya saa za kazi bali wakiwa ndani ya saa za kazi na hakuna anayewauliza. Pia wamejiajiri, wana maduka ya madawa, dispensary, na miradi mingi tu. Sijui kwa nini hawaridhiki jamani? Hii pesa iliyomuua nabii ISSA haijai mfuko ndugu zangu. Ridhikeni na mnachopata na kama hamridhiki, achieni ngazi! Shs 7,700,000/ ni mshahara wa walimu takribani 20 wenye shahada ya kwanza baada ya kukatwa kodi. Wacheni hizo jamani! Jaribuni kwenda kuajiriwa hospital za binafsi muone utalipwa sh ngapi kwa mwezi, na uthubutu kuwa na kazi za part time nje ya kituo ulichoajiriwa wakati wa kazi uone kama hujafukuzwa kama mbwa bila majadiliano. Mmebembelezwa saaaaaana sasa mnajiona ninyi ni MUNGU anayeshikilia uhai wa watu. Lakini muogopeni MUNGU MUUMBA aliyewapa uhai mlionao. Mnavyofanya msifikiri mnaikomoa serikali, mnajikomoa wanyewe kwa sababu kwake yeye BWANA MUNGU mtajibu kuhusu kila roho mliyoiacha ikatoka kwa migomo yenu.

Jamani, nilikuwa nawaza kwa sauti!

DSCF0557.JPG

Uneona mpaka ndani, na ukweli haupingiki. Madaktari madai yao ni dhidi ya watu kama hawa ambao ndo serikali ya nchi yao na sio Kikwete ambaye anapita na watu hawa wanabaki. Madaktari wameamua kuwekea rahani uhai wa maskini kama hawa, inatisha kwani ni kinyume cha kiapo cha taaluma ya utumishiwa wao wa kulinda uhai wa binadamu. Bora tuwe na wachache ieleweke kuliku kundi kubwa lisilotoa huduma stahiki.
 
Huna hoja.

Waliyokubaliana kayasema na ambayo serikali imekataa na hayo kayasema waziwazi na ambayo hawajakubaliana kayasema waziwazi na kasema asiyeyataka hayo ambayo serikali imeyakataa aache mwenyewe kazi. Nini zaidi usichokielewa?

Kama huna hoja kaa kimya kama wenzako.

zombie acha kelel bana, support jf uwe hata bronze premium member!!!
 
Pole mwana JF. sisi siyo akina Rizi moja wanaofurukuta mahakamani-mahakamani halafu hawaonekani.

Tanguliza Udini, tukana au mtetee filauni, lakini fact ni kwamba Duniani hatujawahi kuwa na martial plan iliyopangwa na mwaarabu au mwafrika na ikaleta maendelea popote. Inabidi ukubali ubora wa madikteta wa ulaya wameendeleza baadhi ya nchi.

Unda kundi la kipinzani liite Lord resistance army, wapelekee hao madikteta wa ulaya waliofanikiwa, watakupa pesa nzuri sana; utamuondoa JK haraka sana na utampeleka hague...OK..

Fanya hivyo mkuu
 
Kusema ukweli hakuna nchi yoyote inayoendesha mambo yake kwa hotuba za kwenye luninga. Leaders are there to serve people. Sidhani kama anachosema JK ndio kitu ambacho wasaidizi wake walikuwa wanawaambia madaktari. Ubabe na vitisho ndio lugha watawala wanayopenda kuitumia bila hata sababu za msingi. Halafu worse of all ni hii ya kujaribu kumsilence one of theirs...it was a terrible mistake!
Turudi tena kwenye basics. JK akaze uzi kuzuia wizi wa mali ya umma na matumizi mabaya ya fedha za umma ili wakati wa kujenga hoja kwamba nchi haina uwezo, watu wawe wanamuani kama anasema ukweli. Sasa hivi ni kama vile kuna usanii unaendelea.

Watanzania wengi hatujui lugha yenye mjengo wa diplomatic, Rais kaongea wazi kuwa serikali haitarudi kwenye meza ya mazungumzo bali ni kutekeleza yale tu ambayo serikali imeyafanya mpaka sasa, zaidi ya hayo serikali haina uwezo.

Kwa hiyo daktari asiyekuwa tayari yupo huru kuondoka, asisubiri kufukuzwa na kupewa masaa 24 kuachia nyumba wanazoishia ambazo watapangiwa madaktari wengine ambao wako tayari kufanya kazi na serikali.

Utekelezaji huo wa serikali umeshafanyika kuwafukuza madaktari, kwani sekta za mashirika ya dini ambayo mfumo ni wa direct wameshafukuzwa, serikalini ni kwa sababu ya mfumo wa mzunguko unachukua muda, kitu ambacho kinaweza kuwapa nafasi madaktari ambao wako tayari to-swing back wafanye hivyo kabla nyundo haijawapitia. Wafanye kazi mitaani watajuta kufanya migomo safari nyingine.

Kadriki ya taaluma yao na kiapo chao cha kazi wangetakiwa kufunguliwa mashtaka, ila tu serikali ina huruma.
 
ZombaAsiyetaka ajitoe, asietaka kujiondoa anabaki akiwa na chuki kazin nan anateseka raia au kikwete?

Ni maamuzi ya kipuuzi na ya kitoto, hayapaswi kutoka kwa rais wa nchi.
Je umejuwa hao
Wagen malipo yao/head kiasi gan? Huko
na kwanin. Mtoto mgonjwa anapokataa kula unamwacha afe kwa hasara ya nani? Kama sio mzazi.

Wamegoma watu wanakufa, anasema asietaka aende je ametoa suluhisho gan? Hakuna, is he a man to make and give critical decision? Or a
Normal citizen? What distinguish
him as a president from the least of us? Ni ujinga kutegemea wagen badala kuendeleza wako.

Tengeneza wako wakuhudumie utaomba vingapi? Fedha uombe, technology uombe, vifaa uombe, hata madakitari na waalimu pia?

Ni upuuz kuzan wagen wataziba pengo
-hakuna vifaa wala madawa
-lugha kikwazo
-hawajui tamadun zetu
-watahudum katika hospital ngapi?

-watatoa bure huduma mpaka lin

-tutawalipaje hizo gharama

-Watafika mpaka vijijin au?

Hekima nikutatua mgogoro kwa faida ya watanzania na ajira bora kwa madakitari wetu
 
Pumba tupu umeandika.

Ningependa kujadili zaidi suala la Madaktari kufanya uamuzi wa kusitisha mgomo na kuamua kubaki kuendelea na huduma, la sivyo hawakubaliani na ridhaa ya seriakali, basi waondoke na kwenda huko wanaokofikiria watapata mafao yanayodai. Kwamba serikali imehusika katika kifo cha Dr. Stephen au la mimi sijui, na kinachoongelewa hapa ni tetesi zisizothibitishwa mpaka sasa.

Serikali ina idara nyingi na njia mbalimbali za kumaliza matatizo, ukianza kufatili utaumiza kichwa bure kwani hayo ni mipango migumu kuifumbua wakati waliopanga wana njia zote za kufifisha kiini cha ukweli. Cha kumshukuru Mungu waliomteka Dr. Stephen hawakumwua na imesaidia kupata ukweli fulani. Huenda hao watekaji wamekiuka kagizo la wakuu wao, mkinzano huo wanaujua wao na kwa sababu zao wenyewe. Ndio maana serikali ye yote duniani ina kitendo cha siri cha inteligensia, hakuna asiyejua hili. Tutalalamika hatimaye tutapoa. Kwa wenye uelewa hatupotezei muda kujadili hilo, na kama madaktari wangekuwa na uungwana na utu katika kudai haki zao na kupima kwa busara hayo pengine yasingetokea.

Kosa ambalo madaktari wamelifanya kuwekea rahani uhai wa wagonjwa ili kuishinikiza serikali jambo ambalo halikubaliki. Utaona hospitali za mashirika ya dini ndizo za kwanza kutekeleza uamuzi wa sirikali kuwafukuza madaktari walio kwenye mgomo kwa vile mashirika ya dini yanajali kwanza uhai wa binadamu na dhana nzima ya kuwajibikaji.

Kadiri ya Hotuba ya Rais, kiasi kikubwa cha madai ya madaktari yalishashatekelezwa, na sitegemea kwamba madai yote yangekubalika kwa vile mengine yako nje ya uwezo wa serikali. Kumbuka unaporatibu mishahara ni kitu cha kutumu kwa maisha, katu siku serikali haiwezi kupunguza kiwango cha mishahara ila kukipaisha. Kwa hiyo busara na uratibu wa kiuchumi katika idara ya utumishi na hazina ndio wenye kupima kiwango sahihi kinachoweza kulipwa kadiri ya uwezo wa serikali, hali ya uchumi wa nchi na uwezo wa idara ya utumishi kadiri ya uchumi wa nchi. Vinginevyo ni kudai bila kujua taratibu na sheria za ajira na uchumi wa nchi. Tukumbuke pesa nyinzi zinazoahidiwa toka kwenye bajeti ya serikali haziko hazina bali ni pesa hewa zinazotegemewa kutoka matarajio ya vyanzo mbalimbali, kwa maana hiyo malengo yanaweza kufikiwa au yasifikiwe.
 
Kwenye hayo madai ya Madaktari wapi yamemtetea wananchi wa kawaida kama tunavyoaminishwa humu JF du kumbe jamaa wanataka 7,7000,000 kwa mwezi halafu masaa 2 Regency, masaa 2 TMJ, masaa 2 Agha Khan..kuonana na Dr sh 40,000 hivi kuna kumtetea Mtanzania kweli.
 
Pamoja mkuu. Ni kweli kabisa. Hakuna anayewalazimisha kubaki kwa mwajiri asiyetaka kuwaongeza mshahara wanaotaka wao. Naunga mkono kabisa kuwa waende wakatafute green pastures. Na usemavyo kuwa nchi nyingine wafanyakazi wanafanya part time baada ya saa za kazi ni kweli. Na hawa wetu wanafanya sana tu lakini si baada ya saa za kazi bali wakiwa ndani ya saa za kazi na hakuna anayewauliza. Pia wamejiajiri, wana maduka ya madawa, dispensary, na miradi mingi tu. Sijui kwa nini hawaridhiki jamani? Hii pesa iliyomuua nabii ISSA haijai mfuko ndugu zangu. Ridhikeni na mnachopata na kama hamridhiki, achieni ngazi! Shs 7,700,000/ ni mshahara wa walimu takribani 20 wenye shahada ya kwanza baada ya kukatwa kodi. Wacheni hizo jamani! Jaribuni kwenda kuajiriwa hospital za binafsi muone utalipwa sh ngapi kwa mwezi, na uthubutu kuwa na kazi za part time nje ya kituo ulichoajiriwa wakati wa kazi uone kama hujafukuzwa kama mbwa bila majadiliano. Mmebembelezwa saaaaaana sasa mnajiona ninyi ni MUNGU anayeshikilia uhai wa watu. Lakini muogopeni MUNGU MUUMBA aliyewapa uhai mlionao. Mnavyofanya msifikiri mnaikomoa serikali, mnajikomoa wanyewe kwa sababu kwake yeye BWANA MUNGU mtajibu kuhusu kila roho mliyoiacha ikatoka kwa migomo yenu.

Jamani, nilikuwa nawaza kwa sauti!

mamayeyo, hv hizi ni nyingi kuliko mil 10 na kidogo wanazolipwa watu dodoma kwa ajili ya kugonga meza na kupigana vijembe? Mbona hamsimami kukemea? Ok basi budget ijayo tunaongeza 5m zaid hapo kwe mishahara ya wagonga meza kwa kuwa bunge letu ndo linalipa mishahara midogo kuliko mabunge yote Afrika!

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
ZIDUMU "FIKRA SAHIHI" ZA WATUNGA SERA WA CCM!
 
Last edited by a moderator:

Milioni 7 wanazodai madaktari ni mno
ukilinganisha na uwezo wa serikali, na hata kama chama kingine kiingie madarakani katu hawatawaze kutoa dau hilo kwani kuna kazi hadi kufikia huku kitu ambacho kitatuchukua muda mrefu.

Uwezo gani huo wa Serikali unaozungumzia hapa? Huu wa kugawa rasilimali zetu kwa wageni kwa mfano dhahabu na kuwaacha wachukue 96% na kutuachia 4% wakati nchi za jirani kama vile Botswana wanagawana 50% kwa 50%? au uwezo ambao mafisadi ndani ya Serikali wanakwapua mabilioni ya pesa na kuzificha nchi za nje na pia kununua majumba ya kifahari katika nchi mbali mbali duniani zikiwemo UK, US, SA, Dubai n.k.? Ufisadi wa rada $42 millioni, Ufisadi wa Dowans Sh 96 billioni, ufisadi wa Meremeta $155 millioni, ufisadi wa kagoda haujulikani hadi hii leo ni wa kiasi gani, yule gavana wa BoT alijenga jumba la shilingi 1.5 billioni na wakadai anastahili. Ufisadi wa mashangini miaka nenda miaka rudi shangingi moja gharama yake ni zaidi ya shilingi 200 milioni na yananunuliwa mashangingi chungu nzima kila mwaka.

Uwezo wa kulipa madaktari upo ila kuna wajanja wachache ambao ndio wanatumia nyadhifa zao mbali walizopewa kuifaidi keki ya Taifa kupitia ufisadi huku wafanyakazi wengine chungu nzima ndani ya Serikali wakiwemo Madaktari, Manesi, Waalimu na wengineo wakilipwa mishahara viduchu ambayo haiendani kabisa na gharama halisi za maisha.

Kama kweli huyu mkuu kaya anaweza kusimamia haya anayoyasema.Tangu mwanzo mbona hakuweza kusema haya,amesubiri watoto wameshakomaa ndio anakuja na kauli za juzi.
 
Watanzania wengi hatujui lugha yenye mjengo wa diplomatic, Rais kaongea wazi kuwa serikali haitarudi kwenye meza ya mazungumzo bali ni kutekeleza yale tu ambayo serikali imeyafanya mpaka sasa, zaidi ya hayo serikali haina uwezo.

Kwa hiyo daktari asiyekuwa tayari yupo huru kuondoka, asisubiri kufukuzwa na kupewa masaa 24 kuachia nyumba wanazoishia ambazo watapangiwa madaktari wengine ambao wako tayari kufanya kazi na serikali.

Utekelezaji huo wa serikali umeshafanyika kuwafukuza madaktari, kwani sekta za mashirika ya dini ambayo mfumo ni wa direct wameshafukuzwa, serikalini ni kwa sababu ya mfumo wa mzunguko unachukua muda, kitu ambacho kinaweza kuwapa nafasi madaktari ambao wako tayari to-swing back wafanye hivyo kabla nyundo haijawapitia. Wafanye kazi mitaani watajuta kufanya migomo safari nyingine.

Kadriki ya taaluma yao na
kiapo chao cha kazi wangetakiwa kufunguliwa mashtaka, ila tu serikali ina huruma.

Kama ni kuwapeleka mahakamani kwa sababu ya viapo vyao, wasiishie hapo tu....wamepeleke kila anayeapa na kufanya mambo kinyume na kiapo. Wananchi wataipenda serikali yao trust me. Vinginevyo, wata collapse kabisa health system in the country. Busara lazima itangulie mbele na sio ubabe na dharau.Wewe na mimi kama watanzania tunataka kuiona Tanzania yenye neema kwa wote. Tumekosea kujenga madaraja ya wateule na wanaotawaliwa. Huu mgomo ni moja tu ya kielelezo cha ubaya wa kujenga matabaka kwenye jamii.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Huyu jamaa anadhiirisha kweli ni dhaifu! Naona hamna lolote zaidi ya ku ''peti peti'' hii midaktari ya bongo isiyojua hata ethics za udaktari. Alifanya vizuri kusafisha uongozi (waziri, katimbu, nk). Safari hi alitakiwa asitishe ajira ya hii midaktari mara moja.
 
Umenikumbusha kuna jamaa alikuwa anahojiwa kwenye televisheni huku anamsukuma mgonjwa wake kwenye kibaiskeli pale maeneo ya MOI yeye japo mgonjwa wake alikosa matibabu lakini aliungana na madaktari na kuitupia lawama Serikali kwa kushindwa kushughulikia mgogoro wa madaktari huyo mtu sensible kweli mimi narudia kusema kwa mwananchi wa kawaida kuelekeza nguvu zake kulaumu madaktari ni kupoteza pumzi bure kwani hakuna sehemu daktari alipofunga mkataba na mwananchi kutoa huduma bora za afya na mengineyo lakini still hatustaili kadhia tunayopata kwa kukosa huduma za afya kutokana na mgomo so what should we do? Sahihi kabisa tukimwajibisha aliyepewa dhamana..........

Ha ha ha ha, sooooo misguided! Kumbe kuelewa pia ni kuchagua.
 
Kwenye hayo madai ya Madaktari wapi yamemtetea wananchi wa kawaida kama tunavyoaminishwa humu JF du kumbe jamaa wanataka 7,7000,000 kwa mwezi halafu masaa 2 Regency, masaa 2 TMJ, masaa 2 Agha Khan..kuonana na Dr sh 40,000 hivi kuna kumtetea Mtanzania kweli.

Mbona Rais tunamlinda, halipi kodi, tunalinda mkewe, tunalinda mwanaye mpendwa, kwa ujumla tunanunua hata toilet paper yake au kopo lake la chooni, lakini bado anapata muda wa kwenda kubembea asia na kuacha kazi za nchi?
 
Back
Top Bottom