Hospitali ya Mzena inamilikiwa na nani? Kwanini iitwe Mzena?

krava

JF-Expert Member
Nov 17, 2016
225
287
Hii hospitali inayoitwa Dr. Mzena iko wapi na inamilikiwa na nani, na huyo Dr Mzena ni nani hasa? Yupo au alikuwa hospitali gani?

=========

Kwanini hospitali ya Usalama wa Taifa inaitwa Mzena?

Emilio Mzena, alikuwa Mkurugenzi wa kwanza wa Idara ya Usalama wa Taifa, na aliongoza idara hii kuanzia mwaka 1961 hadi 1975, akiwa ndiye Mkurugenzi wa TISS aliyeongoza miaka mingi zaidi kuliko wengine (miaka 14).

Emilio Mzena, aliaminiwa sana na Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, baada ya Idara yake kuzima majaribio kadhaa ya kumpindua. Na hiyo ikapelekea Mwl. Nyerere, kumpa heshima ya kuiita hospitali hiyo kwa jina lake.
 
Ni hospitali muhimu kwa viongozi wa kitaifa.

Pia kwa usalama wa taifa , wao na watoto wao

Imepewa jina hilo kuenzi kazi kubwa aliyofanya mzee kuijenga taasisi ya usalama wa taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
Malizia maswali, iko wapi na inamilikiwa na nani?

Inatibu viongozi tu wa kitaifa na usalama na familia zao? Au mtu yoyote anakuwa admitted? Toa location tukapime malaria hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ipo eneo la Makumbusho, imepakana na kijiji cha Makumbusho upande wa kushoto ukiwa unaelekea eneo la Victoria.

Ni kwa ajili ya viongozi na maofisa usalama na familia zao, ingawa nasikia wenye bima wanatibiwa.

Ni hospitali nzuri kwa maana ya huduma, vifaa na utaalamu. Inamilikiwa na serikali, na imepewa jina la Mzena ikiwa ni kumbukumbu ya aliyewahi kuwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Emilio Mzena
 
Ni ile ile ambayo alilazwa Mjane wa Baba wa Taifa miezi kadhaa mwaka huu na kila ilipokuwa ikitolewa taarifa za Kumhusu ikawa haitajwi katika Maelezo na inafichwa. Na leo tena nimeona Mtu mwingine Muhimu na Nyeti kabisa nchini Tanzania nae amelazwa hapo hapo tena katembelewa na Mheshimiwa Namba Moja lakini Jina la hiyo Hospitali limefichwa tena.

Nikiwa kama Mtanzania naomba Kuijua hiyo Hospitali ili nami nikamtembelee Kiupendo huyo Mgonjwa Kesho mapema tu.
 
Back
Top Bottom