Hongera sana Yericko Nyerere

Hongera sana Yericko Nyerere

Mwana JF mwenzetu Bwana Yericko Nyerere amesaini leo mkataba na kampuni ya MJ Printing Press kwa ajili ya kuandika kitabu cha UJASUSI WA KIDOLA NA KIUCHUMI, hii ni hatua nzuri sana ukiwa kama mtu mwenye kipaji cha uandishi lakini pia uwezo wa kujenga hoja.

Mara nyingi hoja zako hapa zimekuwa zikitatiza kama ni fiction au ni za kweli, lakini haiondoi ukweli kuwa una uwezo mzuri sana wa kujenga hoja na kuzitetea hoja hizo, hasa zile za jikoni.

Ifike wakati sasa tuone wana JF wenzetu wenye uwezo mkubwa wa kiunadishi pia kama Pasco , Mzee Mwanakijiji , Manyerere Jackton , Mchambuzi, Mtambuzi na wengineo wengi ambao ni mazao ya hapa JF wakichapisha vitabu vyao.

Ningependa kutoa ombi kwa uongozi wa JF kutafuta uwezekano wa kumfanyia interview Yericko mara kitabu kitakapo toka kama sehemu ya kumpa support member mwenzetu, lakini pia kuenzi michango yake mingi humu JF, na hii itatia sana hamasa kwa members humu kujiingiza katika tasnia hii.
Binafsi kitabu hicho kikitoka nitakinunua, kwa kuwa ni msomaji mzuri pia wa vitabu.

CgALHM6UkAE73SY.jpg


Hongera sana na All the best, ila usisahau kuitaja JForums kwenye dibaji maana najua pia imekujenga sana katika tasnia hii ya uandishi.
Naona unajipigia chepuo mambo ya kijasusi na Uchumi Yericko kayajulia wapi yeye ateleze mambo ya jela zetu na mahabusu ziko vipi maana ametoka huko juzi tu.
 
Familia ya Nyerere ina vipaji vingi
Jina Nyerere ni la utani tu, alipewa sababu ya ubishi wake na uwezo wake wa kujenga hoja na kuzitetea.
Sasa kwanini anatumia majina ya utani kwenye vitu serious?
Tupe jina lake la ukweli.
Asigwa na Jungle, Yeriko Nyerere ni jina lake halisi na sii jina la utani!.
Ushahidi ni huu kutoka kwake mwenyewe.
Mimi ninae Baba yangu mzee Yohanesy Nyerere kwa sasa marehemu
Nyerere ni jina la ukoo tu halina hati miliki...Mimi ni Mhehe ...
Naitwa Yericko Nyerere, je sio damu ya nyerere?
,baba yangu ni Yohanesy nasio Julius
Naungana na wengine kumpongeza Yeriko.

Pasco
 
Ikiwa huyo ana 'kipaji cha kuandika".

Nnahaki ya kusema "if such are the priests, God bless the congregation".

Sasa hicho kitabu kama hakijafundisha ujinga kitafundisha nini zaidi.
 
Kwanza keshamlipa yule dogo pesa zake za shindano aliloanzisha la Kiswahili? Dhurma si nzuri aisee, kama hajamlipa afanye hivyo ili abarikiwe na mauzo yake yapae...
Hahahaaaa.... Nilimfahamu Yericko kipindi kile dogo kaanzisha uzi wa kudai chake. Kwa wasio jua sakata hili fuatilia Uzi huu.. Yericko Nyerere tafadhali sana naomba nipe zawadi yangu Namalizia kwa kumpongeza Yericko kwa hatua hii ya kuandika kitabu... Mwisho kabisa namwita Oluoch hapa.
 
Ikiwa huyo ana 'kipaji cha kuandika".

Nnahaki ya kusema "if such are the priests, God bless the congregation".
Nilitegemea maneno haya kutoka kwako.
Sasa hicho kitabu kama hakijafundisha ujinga kitafundisha nini zaidi.


Duc In Altum.
 
Back
Top Bottom