Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula amjibu Yericko Nyerere

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
898
Reaction score
1,947
ASKOFU HAKATISHWI TAMAA KWA UWONGO!

Wiki chache zilizopita, aliyekuwa mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Kigamboni kupitia tiketi ya CHAUMMA, Yericko Nyerere alijirekodi na kusambaza video katika ukurasa wake ikiwa na maudhui kadhaa kuhusu Askofu Mwamakula.

Katika video ile, Yericko alisikika akisema kuwa kipindi cha mwaka 2024, Askofu Mwamakula amekuwa na safari za mara kwa mara kwenda Nairobi. Yericko alidai kuwa safari hizo ni zile za kukutana na Maria Sarungi-Tsehai kwa kile alichokiita yeye kuwa wanapeana fedha! Lakini ilitushangaza sana kwani askofu hajawahi hata siku moja kukutana na Maria Sarungi na wala hata kuongea naye! Na sijui hata Maria anajua kama askofu akifurahi anakuwaje maana naye hajawahi kumuona.

Baada ya kuona na kuisikiliza video ile, tulifikiri kuwa Yericko angepata muda wa kuirekebisha au kusahihisha kauli zake hasa kama atakuwa aligundua ya kuwa hakusema kweli. Tulifikiria hivyo kwa kuwa tuliamini kuwa Yericko ni mtu anayejenga hoja zenye ukweli uliopatikana kwa njia ya kuzifanyia utafiti na kuzihakiki taarifa.
Lakini kwa kuwa hadi sasa hajasahihisha kauli yake, sisi tumeona vema tuweke kumbukumbu sahihi ili kizazi kijacho kisirithi kumbukumbu iliyopotoka na isiyo sahihi. Hii pia itakuwa fursa ya pekee kwa Yericko kujifunza namna nzuri ya kujenga hoja za kisayansi katika siasa ili aweze kuaminika katika jamii.

Kwa kipindi cha miaka minne mfululizo kutoka 2023, 2024, 2025 na 2026; Askofu Mwamakula hajawahi kutoka nje ya nchi. Kumbukumbu za Idara ya Uhamiaji zitathibitisha ya kuwa askofu alitoka nje ya nchi kwa mara ya mwisho mwezi Desemba 2022 kupitia mpaka wa Namanga na pia alirudi kupitia mpaka huo huo. Hiyo ilikuwa ni safari ya Kanisa ambapo alikwenda kufanya ibada katika Kanisa lao la Ruiru iliyo karibu na Nairobi.
Lakini kabla ya hapo alitoka Septemba 2019 na baada ya hapo ugonjwa wa Covid 19 uliziathiri safari zake ambazo zilitegemea sana kukutana pia na umati wa watu huko alikokuwa akienda.

Lakini kama Yericko Nyerere atakuwa na jinsi nyingine ya kuthibitisha kama askofu anamiliki paspoti feki basi atauambia umma kuwa jina la hiyo paspoti ni lipi na alipitia ruti ipi kutoka nje ya nchi na kurudi tena nchini kwa paspoti hiyo na Uhamiaji watathibitisha jina hilo.

Tunasikitika sana kuwa Mhe. Yericko Nyerere alijiruhusu kujirekodi, kusema na kusambaza uwongo dhidi ya Askofu Mwamakula pasipo ya kujiridhisha. Hatujui lengo lake lilikuwa ni nini. Sisi pia tunafikiri na kuamini ya kuwa uwongo haujawahi kumjenga mwanasiasa yeyote zaidi ya kubomoa taswira na haiba yake. Lakini pia ni ukweli kuwa tuhuma za uwongo hazimbomoi mtu, lakini mtu anayejali utu anatafuta namna kumsaidia mtu anayetaka kujenga utamaduni wa kujenga hoja zisizo na ukweli.

Na kama watu wanamuamini kiongozi mkweli, basi ni wajibu wa viongozi waliotangulia kiumri ili kuwaasa viongozi vijana kuepuka kujenga au kuunda hoja zisizo kuwa na ukweli wowote na kisha wakaziremba ili waaminike.

Siasa ni sayansi - kwa maana ya kuwa hoja za kisiasa hufanyiwa utafiti wa kina kuhusu ukweli wake na faida yake kwa jamii kabla ya kuzitoa hadharani. Siasa ni sanaa, kwa maana ya kuwa hoja na taarifa za kisiasa zilizofanyiwa utafiti hutafutiwa njia nzuri na bora ili ziwasilishwe

kwa umma kwa urahisi zaidi. Lakini pia siasa ni ushawishi, kwa maana ya kuwa umma huweza kushawishiwa na kuvutiwa na hoja ambazo pia zimefanyiwa utafiti juu ya ukweli wake kabla ya kuwasilishwa kwa ustadi.
Siasa ni maisha halisi ya watu. Kwa sababu hii, mwanasiasa makini huepuka kujenga uadui na watu kwa kupika maneno ya uwongo dhidi ya watu wengine. Mwanasiasa anaweza kujijenga au kujibomoa kutokana na anavyojenga hoja zake hadharani kuhusu watu wengine.

Tunatarajia pia kuwa kama Yericko hataweza kuthibitisha juu ya safari za mara kwa mara za askofu kwenda Nairobi kwa kipindi hicho cha mwaka 2024, basi ataweza kuomba radhi kwa kitendo cha kujirekodi, kusema na kusambaza taarifa zisizo kuwa za kweli. Hii itamsaidia pia yeye mwenyewe binafsi katika maisha yake ya kisiasa kwa kuwa yeye bado ni kijana mdogo aliye na miaka mingi mbele ya kufanya siasa.

Askofu amekuwa akiwatetea watu wengi sana wakiwemo wanaharakati na viongozi wa vyama vya upinzani, na katika harakati hizo hajawahi kulipwa fedha na kiongozi yeyote yule au pia taasisi yeyote ile. Ni aghalabu sana akialikwa anaweza kulipiwa gharama za usafiri na wale waliomualika lakini hiyo inakuwa mara chache.
Kutetea watu nchini Tanzania ni zoezi gumu na lenye gharama nyingi sana. Lakini pia gharama iliyo kubwa kupita zote ni ya kusalitiwa na watu uliowahi kuwatetea. Inasemekana kuwa watu watu wengi waliacha kutetea haki mara baada ya kukatishwa tamaa na wenzao. Inawezekana pia mambo haya yanakuja ili pia tuweze kukata tamaa. Lakini kwa nini mtu ukate tamaa wakati wa kushuka Mlima Kitonga wakati unajua kuwa muda sio mrefu utaingia Mikumi uende Ifakara na Kilombero kula 'pepeta'?

Tunaweka haya ili baadaye Yericko akija kupata kuwa kiongozi, tusijisikie vibaya kumkosoa kwa kwani tutakuwa na historia ya kumrekebisha.

Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 2 Machi 2026; Saa 7:12 mchana.
 
Mpeleke mahakamani ajute kuzaliwa
 
Back
Top Bottom