Hongera sana Yericko Nyerere

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Mwana JF mwenzetu Bwana Yericko Nyerere amesaini leo mkataba na kampuni ya MJ Printing Press kwa ajili ya kuandika kitabu cha UJASUSI WA KIDOLA NA KIUCHUMI, hii ni hatua nzuri sana ukiwa kama mtu mwenye kipaji cha uandishi lakini pia uwezo wa kujenga hoja.

Mara nyingi hoja zako hapa zimekuwa zikitatiza kama ni fiction au ni za kweli, lakini haiondoi ukweli kuwa una uwezo mzuri sana wa kujenga hoja na kuzitetea hoja hizo, hasa zile za jikoni.

Ifike wakati sasa tuone wana JF wenzetu wenye uwezo mkubwa wa kiunadishi pia kama Pasco , Mzee Mwanakijiji , Manyerere Jackton , Mchambuzi, Mtambuzi na wengineo wengi ambao ni mazao ya hapa JF wakichapisha vitabu vyao.

Ningependa kutoa ombi kwa uongozi wa JF kutafuta uwezekano wa kumfanyia interview Yericko mara kitabu kitakapo toka kama sehemu ya kumpa support member mwenzetu, lakini pia kuenzi michango yake mingi humu JF, na hii itatia sana hamasa kwa members humu kujiingiza katika tasnia hii.
Binafsi kitabu hicho kikitoka nitakinunua, kwa kuwa ni msomaji mzuri pia wa vitabu.

CgALHM6UkAE73SY.jpg


Hongera sana na All the best, ila usisahau kuitaja JForums kwenye dibaji maana najua pia imekujenga sana katika tasnia hii ya uandishi.
 
teh teh, shindano gani hilo tena mkuu.?
Kuna shindano Yericko alianzisha la matumizi sahihi ya kiswahili na kuna dogo alifaulu ila Yericko akamdhulumu pesa yake na Yericko alikili (dogo aliandika lalamiko hilo JF). Sikufuatilia mpaka mwisho kama jamaa alimlipa, so kama hajamlipa ajue anakula laana
 
Kuna shindano Yericko alianzisha la matumizi sahihi ya kiswahili na kuna dogo alifaulu ila Yericko akamdhulumu pesa yake na Yericko alikili (dogo aliandika lalamiko hilo JF). Sikufuatilia mpaka mwisho kama jamaa alimlipa, so kama hajamlipa ajue anakula laana
Ngoja, atakuja kujibu hizi tuhuma zake.

Ila kwa hili la kitabu nampa hongera sana
 
OMBI LANGU vitabu hivyo visiwe ghali kwani hali ya kiuchumi kwa sasa na kuendelea ni ngumu vinginevyo hongera kwake .
Ni kweli mkuu, japo watanzania nao hatuna utamaduni wa kusoma vitabu, na utafiti uliozinduliwa leo unaonesha kuwa 71% ya muda wa watanzania unatumika kwenye mambo yasiyo na maana.

Inaonekana tuna mentality ya kupenda kuchart kuliko kusoma, tunapenda tetesi kuliko ripoti au uchambuzi.
 
Ha ha ha, mkuu huo uongo wake na uchonganishi ndio umemfungulia fursa.

Isije siku moja ukasikia kaandika kitabu kikubwa zaidi ya hiki au kafanya documentary kabisa
Kama jamaa ana hizo tabia za uongo na uchonganishi si ishara kwamba hata kitabu chake kitakuwa kimejaa uongo?
 
Back
Top Bottom