Hongera Maulid Kitenge

Hongera Maulid Kitenge

hahaahah kwa kuwa kazi zao wanafanya kwa siri basi tumejenga picha ni watu wenye akili za hali ya juu, kumbe ukiwaleta hadharani ni ma bashite sana. amini mkuu ndo hao vilaza
Umeongea point sana kwasababu hatujawazoea hadharani tunahisi wanaakili lakini ukweli ni mamburula kama tulivyoona jana very shame swali dogo nionyeshe kitambulisho anatoa bastoramaybe kitambulisho chake ni pisto
 
Nilishangaa yule ofisa anachomoa bastola Kwa mkono wa kushoto halafu anaishika Kwa mkono wa kulia.....nikajua moja Kwa moja jamaa hana mafunzo..... mmmmh
 
Povu la nini tena mkuu

Sijakipinga Kitendo cha Kishujaa alichokifanya Maulid Baraka Kitenge ila najaribu tu kumtahadharisha kuwa siku zingine ajitahidi kuwa makini sana kwani katika matukio kama yale umakini huhitajika mno kuliko kujipendekeza kwani huwezi jua temper ya Mtu ipoje pale hasa ambaye ameshapewa maagizo maalum kutoka kwa Mtu au Taasisi maalum.

Laiti ungekuwa angalau tu umepitia JKT kidogo au umeiva katika Sanaa za Kimapigano nadhani ungenielewa hicho nilichokiandika hapo ila kwa povu lako Kwangu nimegundua Wewe ni mtupu Kimedani ya Kivita au ya Kimapigano. Leo tunamsifi Kitenge ila nikuhakikishie tu Mkuu kuwa Kitendo chake kile cha jana kilikuwa ni cha hatari na alikuwa anajihatarishia pia na yeye.

Tuwe makini sana hasa katika Emotional gatherings kwani huwezi jua adui yako hapo ni nani.

Kila la kheri Mkuu.
 
Yule jamaa ni boya sijapata kuona.

Kama yule mpumbavu ndio usalama wa Taifa kama nchi tuna hasara sana.
 
Angalau sasa tumefahamu shimoni ni wapi anakotishia watu bashite kila siku.
 
Kinga ni bora kuliko tiba, usalama alikuwa sahihi kutoa silaha bila kuitumia ili kupunguza uwezekano na ulazima wa kuitumia. watu wakijuu kuwa kuna silaha wanabadilisha tabia.
Silaha inakaa kishamba vile. Mbona ingechomolewa na yeyote wa nyuma. Sio mwana usalama wala nini, ni lofa tu wa Bashite.
 
ILA
Nimejaribu kujiuliza kwa hali ya kawaida kuna raia wa kawaida anaweza kuwa na ujasiri wa namna hiyoo. Nikapata jibu inawezekana na yeye ni wale watu wanaovaa suti nyeusi(mashushu).mpaka sasa bado sijapata jibu sahihi .


Hilo linaitwa kuipenda Nchi kuliko unavyojipenda. Unadhani kifo cha Daudi Mwangosi ilitokeaje?. Afisa yule wa Polisi alikuwa tayari amekosa mwelekeo na hakustahili kuendelea na zoezi lile. Alichokifanya Kitenge ni kwa mkono wa Mungu. Fikiri Nape angepaniki nini kingetokea?? Gun Shooting >>>????
 
hongera kitenge tunahitaji watanzania majasiri kama wewe umeonyesha njia
 
Kwa kweli jana Maulid Kitenge alikuwa shujaa kwa kuamua kuingilia kati, maana amejitahidi na ndiye aliyemaliza kila kitu.
 
Kwangu kafanya Kosa Kubwa Sana na la Hatari kwake .
Unapokwenda Kuoka Tukio la Mtu anayefanyiwa Attack kwa Kutumia Silaha ya Moto ..nilazima uwe Umejiandaa na Silaha Mfanano wa adui anayoitumia , iki pakitokea mazungira ya Matumizi basi uweze kujihami .

Yeye kaenda na koti la Suti la Pink na simu Kubwa Kama Bomu , Halafu anakaribiana na Adui almost Zero Distance.

Mnaomsifia Shame on You
Ule mguu wa kuku hakuuona alikuta umesharudishwa, waliuona walimbia hadi Mtwara.
 
Wenye akili walikuwepo enzi za mwalimu, siku hizi wanapeana nafasi kidugu hasa wamu ya nne imeingiza mabashite wengi wasio na vigezo
Naunga mkono kwa hili, ndio maana tulikuwa tukikaa nao kwenye moja moto moja baridi walikuwa wanakauli zao " unajua mimi ni nani", hakuna maadili tena kwenye hili.
 
Siku ya leo kumetokea tukio la kustaajabisha ktk tasnia ya siasa nchini tanzania. Tukio hilo limetokea dar es salaam wakati aliyekuwa waziri wa michezo na tamaduni Nape nauye akitaka kuongea na waandishi wa habari baada ya kuondolewa katika nafasi yake ya uwaziri. Nape ameondelewa leo hii katika nafasi yake baada ya mh rais kufanya marekebisho madogo katika wizara mbili.

Baada ya mh Nape kuwasili maeneo ya Pritoria hotel kulitokea tafrani baada ya watu walitambuliwa kuwa ni maafisa usalama kumzuia asiongee na waandishi na kumtaka arudi ndani ya gari. Wakati sakata hilo likitokea mmoja wa maafisa usalama alitoa bastola na kumtishia Mh Nape ambaye naye hakustuka . Afisa huyo aliirudisha silaha hiyo kiunoni kisha kuanza kumsukuma Mh nape kumrudisha ndani ya gari. Pasipo kutarajiwa kijana mmoja mtanashati aliyevaa koti jekundu alionekana kujongea kujua kinachoendelea baada ya kuona tafrani ikitokea.

Kijana huyo aliweza kutambuliwa kuwa ni mtangazaji maarufu Maulid Kitenge. Kijana huyoo aliweza kuingilia kati na kumtoa afisa usalama kwa nguvu eneo la tukio huku akimsukuma bila kuogopa. Hakika alifanikiwa akamuondoa eneo hilo na afisa huyo alitii bila shurti. Wengi tumeona na kustaajabu na hatuna budi kumpa hongera maulidi kitenge kwa ujasiri aliouonesha.

ILA
Nimejaribu kujiuliza kwa hali ya kawaida kuna raia wa kawaida anaweza kuwa na ujasiri wa namna hiyoo. Nikapata jibu inawezekana na yeye ni wale watu wanaovaa suti nyeusi(mashushu).mpaka sasa bado sijapata jibu sahihi .

Waungwana ninyi mnaonaje nawasilishaView attachment 485865View attachment 485866View attachment 485867View attachment 485868
Actually ni kinyume chake. Hongerah kijana wa Usalama wa Taifa kwa ni alitumia tu Busara na ukumbuke hakuwa peke yake. They are trainded usifikirie alishindwa bali alitumia tu busara ya kumuachia kitenge na kiduku chake!
 
Kwani kuna mtu asiyejua kwamba kitenge ni usalama. Yule yupo katika ivi vyombo vya habari kwa kazi maalum. Jezi nambari 9 mgongoni Maulidi mbaraka wa kitenge
Bongo buana, ndio maana hata Bashite sasa amebatizwa kuwa TISS!
 
Kama yule Jamaa ni Usalama wa Taifa aliyetoa bastora basi nakubali yale maovu yanayofanyika watu mara nyingi usema kwamba wahusika ni Usalama
 
Back
Top Bottom