Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,157
- 166,115
Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Mama Gift, mkazi wa Kitongoji cha Mbugani, Kijiji cha Magugu wilayani Babati, amenusurika kushambuliwa baada ya kudaiwa kukutwa usiku akifukia dawa zinazohusishwa na imani za kishirikina katika nyumba ya jirani.
Mwanamke huyo mara baada ya kugundulika na kijana anaye fahamika kwa jina la Idrisa Mohamed amesema alimkuta Mama huyo akiwa tayari ameshafukia dawa kisha akaondoka na kurudi tena huku akipewa maelekezo ya sehemu alipo fukia dawa hiyo hapakuwa sahihi mara baada ya kugundulika mwanamke huyo alianza kumshambulia kijana huyo kwa kutaka kumchoma na kisu,
Baadhi ya wananchi waliofika katika eneo hilo wameshtushwa na tukio hilo kwani mwanamke huyo amejikita sana katika Maombi pamoja na uimbaji wa kwaya tukio lililowaacha wanananchi wengi midomo wazi wamesema mwanamke huyo amekuwa msumbufu kwa matukio kadhaa huku wakikemea vikali tabia hizo,
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha mbugani Jonasi Daudi amekiri kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema alipokea taarifa hizo majira ya saatisa kasoro za usiku ndipo alipofika katika eneo la tukio na kumkuta mwanamke huyo akiwa utupu na mara baada ya kuhojiwa mwanamke huyo alikiri kwa kusema alikuja kuroga na kuhisi kuwa alitupiwa magonjwa na jirani yake ndipo alipo chukua jukumu la kwenda kuchimbia dawa hizo.
View: https://www.facebook.com/share/v/1EJfSL1Ztg/