El'son
JF-Expert Member
- Jun 3, 2012
- 380
- 324
Siku ya leo kumetokea tukio la kustaajabisha ktk tasnia ya siasa nchini tanzania. Tukio hilo limetokea dar es salaam wakati aliyekuwa waziri wa michezo na tamaduni Nape nauye akitaka kuongea na waandishi wa habari baada ya kuondolewa katika nafasi yake ya uwaziri. Nape ameondelewa leo hii katika nafasi yake baada ya mh rais kufanya marekebisho madogo katika wizara mbili.
Baada ya mh Nape kuwasili maeneo ya Pritoria hotel kulitokea tafrani baada ya watu walitambuliwa kuwa ni maafisa usalama kumzuia asiongee na waandishi na kumtaka arudi ndani ya gari. Wakati sakata hilo likitokea mmoja wa maafisa usalama alitoa bastola na kumtishia Mh Nape ambaye naye hakustuka . Afisa huyo aliirudisha silaha hiyo kiunoni kisha kuanza kumsukuma Mh nape kumrudisha ndani ya gari. Pasipo kutarajiwa kijana mmoja mtanashati aliyevaa koti jekundu alionekana kujongea kujua kinachoendelea baada ya kuona tafrani ikitokea.
Kijana huyo aliweza kutambuliwa kuwa ni mtangazaji maarufu Maulid Kitenge. Kijana huyoo aliweza kuingilia kati na kumtoa afisa usalama kwa nguvu eneo la tukio huku akimsukuma bila kuogopa. Hakika alifanikiwa akamuondoa eneo hilo na afisa huyo alitii bila shurti. Wengi tumeona na kustaajabu na hatuna budi kumpa hongera maulidi kitenge kwa ujasiri aliouonesha.
ILA
Nimejaribu kujiuliza kwa hali ya kawaida kuna raia wa kawaida anaweza kuwa na ujasiri wa namna hiyoo. Nikapata jibu inawezekana na yeye ni wale watu wanaovaa suti nyeusi(mashushu).mpaka sasa bado sijapata jibu sahihi .
Waungwana ninyi mnaonaje nawasilisha