Rais Samia Afanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC)

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,209
4,706
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzay Mheshimiwa Samia Suluhu leo Mei 22, 2021 amekutana na kufanya Mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania ( TRC) Masanja Kadogosa

Katika mazungumzo hayo muhimu yaliyofanyika Ikulu pamoja na mambo mengine walijadili maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ( SGR)

Mkurugenzi Mkuu wa TRC alimshukuru sana Mama Samia kwa kuidhinisha fedha tshs bilion 372 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya SGR kipande cha kuanzia Mwanza Hadi Isaka chenye urefu wa kilometa 341

Rais Samia alimueleza Mkurugenzi wa TRC kuwa Serikali itahakikisha kuwa Mradi wa SGR utakaounganisha Bandari ya Dar es salaam na Kanda ya Ziwa, Kanda ya Magharibi na Nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na DRC unakamilika kwa wakati

===

TBC Taifa - Serikali kukamilisha ujenzi wa reli ya kati...

Serikali kukamilisha ujenzi wa reli ya kati

Rais Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa, mazungumzo ambayo yamehusu maendeleo ya miradi ya ujenzi wa reli na maendeleo ya shirika hilo.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam, Kadogosa ameishukuru Serikali kwa kuidhinisha shilingi Bilioni 372.34 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kipande cha tano cha reli ya Mwanza – Isaka chenye urefu wa kilometa 341 kwa kiwango cha kisasa.

Amesema ujenzi wa reli katika vipande viwili unaendelea vizuri ambapo hadi mwezi Aprili mwaka huu kipande cha Dar es salaam hadi Morogoro chenye urefu wa kilomita 300 kilikuwa kimefikia asilimia 91 na kile cha Morogoro hadi Makutupora chenye urefu wa kilomita 422 kilikuwa kimefikia asilimia 60.02.

Mkurugenzi Mkuu huyo wa TRC amemueleza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa, majaribo ya treni ya abiria yanatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu kwa kipande cha Dar es salaam hadi Morogoro.

Kwa upande wake Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imedhamiria kuhakikisha ujenzi wa reli ya kati utakaounganisha bandari ya Dar es salaam na mikoa ya kanda ya ziwa na kanda ya magharibi unakamilishwa ili kuzifikia nchi za Uganda, Burundi, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Amemuagiza Kadogosa kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo ya ujenzi vizuri ikiwa ni pamoja na kujipanga kwa ajili ya ujenzi wa vipande vya Makutopora – Tabora, Tabora – Isaka na Kaliua – Mpanda – Kalema.

Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza TRC chini ya Kadogosa pamoja na wote wanaoshiriki katika ujenzi wa reli kwa kazi nzuri wanayoifanya, na ameeleza kuridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo.

1621933274109.png
 
Muda siyo Mrefu tutasikia KISHINDO CHA AWAMU YA SITA.
Haa😆😅😄😃😂😁😀
Kuna Jamaa Wanakemea Hapo
Najua Watakuja Na Kwako Watasema
Shindwa Shindwa 😥😣😏🙄😶😑😐
Ulegee Kama Mlenda 😆😅😄😃😂😁😀
Tanzania Ni Tajiri Sana
Pesa Zipo Hao Waturuki Ni Vibarua Watu
 
Badala aombe hizo 370bn za kumalizia Dar Moro treni ianze kujivinjari ndipo Moro Makutupora, sasa Mwanza Isaka kabla ya Tabora ni wapi na wapi Kadogosa hapo?
Binafsi Huu Mradi Ni Mzuri Umegubikwa Na Mambo Ya Hovyo Hovyo Sana. Kulikuwa Na Haraka Gani Kutangaza Mpaka Isaka


Ulitakiwa Dar es Salaam ~Morogoro Treni Ianze Kazi
Sasa Wao Kila Wakati Wanasogeza Mbele Tu Mara Itaanza April Mara September.

Baadaye Ndiyo Wangekuja Na Morogoro ~Dodoma
Ikikamilika Wanakwenda Mbele

Mpaka Sasa Hivi Dar es Salaam ~Morogoro Wamesogeza Mbele Mara Nyingi Mno
 
Back
Top Bottom