Hongera Kikwete

Chuo chenyewe ni chuo hicho!!!!! Hiyo ni sehemu ya watu kupotezea muda tu!!

Vijana wetu wa mwanzo kuhitimu UDOM leo wanahitimu baada ya kujituma kwa miaka mitatu, wanafaa waandikwe kwenye historia kuwa wamejituma kwa mazingira magumu, huku chuo kinajengwa huku wao wanachimba, mpaka Mwenyeezi Mungu kawasaidia wamehitimu, hawa"kupoteza muda tu" kama unavyofikiria. Wamechakarika na wanastahili kila sifa na nawapa Hongera sana kwa kuwa wastahamilivu.
 
Udom haikuwa concept ya Mkapa, kwa matamshi yake Mwenyewe Kikwete katika uzinduzi hapo jana, ilikuwa ni "kiherehere" chake binafsi na ahadi binafsi aliyoitowa wakati wa kampeni za 2005, anasema, aliogopa hata CCM wasije wakamuuliza hii sera ya kujenga chuo kipya ilitoka wapi? Na Bajeti yake iko wapi.

Kuhusu rekodi ya Dunia. Hilo ni wazo langu binafsi, kwani mpaka sasa sijasikia, wazo, ahadi, kujenga chuo kipya, mpaka kudahili within 2 years na kutowa wahitimu wa mwanzo within 5 years. Sijawahi kuona au kusikia zaidi ya UDOM. Jee wewe umewahi?

Usiwe unaongelea rekodi za dunia wakati ujafanya utafiti wa kina,swala zito kama hili halipaswi kuongelewa kwa hisia tu!hii inaweza kukuaibisha mbele ya watu makini!ona sasa ulivyojiaibisha!kuwa makini na maelezo yako!acha ushabiki wa mitaani!
 
Aaaah, hayo utangoja wewe, mimi napongeza kwa dhati kabisa na namtakia kila kheri Kikwete, kwani bila elimu hatuna badiliko ya kweli na Kikwete anajitahidi katika kuwafunguwa macho wa Tanzania, kwa elimu na mengi mengine.

Sijapinga kumpongeza Mh Kikwete ila vile vile ubora wa wahitimu nao ni muhimu isijekuwa tunatoa wahitimu wa kuwa waratibu kata wasioweza kushindana na wahitimu wengine kwenye kazi za kimataifa
 
Vijana wetu wa mwanzo kuhitimu UDOM leo wanahitimu baada ya kujituma kwa miaka mitatu, wanafaa waandikwe kwenye historia kuwa wamejituma kwa mazingira magumu, huku chuo kinajengwa huku wao wanachimba, mpaka Mwenyeezi Mungu kawasaidia wamehitimu, hawa"kupoteza muda tu" kama unavyofikiria. Wamechakarika na wanastahili kila sifa na nawapa Hongera sana kwa kuwa wastahamilivu.

Nahisi na wewe ni mhitimu wa chuo hicho!Nasikitika kukufahamisha kwamba ubora wa chuo hicho uko chini sana!swala la kumaliza nafikiri hilo ni la kawaida tu,kwa kuwa hata wale wanaosoma vyuo vikuu feki,pia humaliza!
 
Labda ni mimi ndiyo nachanganya mambo lakini UDOM haikuwa conceptualized na kujengwa wakati wa Mkapa kisha ika malizika kipindi cha JK na yeye kuki zindua mwaka 2007?

Je hiyo rekodi ya dunia umeipimaje mkuu? I mean ume research ukaona ni rekodi ya dunia au ume fikiaje hiyo conclusion?

Otherwise hongereni wahitimu wa UDOM.

nadhani, mkuu huelewi maana ya "rekodi" especially ya dunia
 
Usiwe unaongelea rekodi za dunia wakati ujafanya utafiti wa kina,swala zito kama hili halipaswi kuongelewa kwa hisia tu!hii inaweza kukuaibisha mbele ya watu makini!ona sasa ulivyojiaibisha!kuwa makini na maelezo yako!acha ushabiki wa mitaani!

Hayo ni mawazo yangu binafsi, wewe uko huru kuwa na mawazo yako binafsi, jee wewe ulifanya utafiti kuona hii siyo rekodi ya dunia? Mimi sijafanya utafiti, lakini, mpaka leo sijasikia rekodi iliyoipita hii. Wewe kama una utafiti wa kulipinga hilo, uweke hapa, kama hauna, funga bakuli.
 
Nahisi na wewe ni mhitimu wa chuo hicho!Nasikitika kukufahamisha kwamba ubora wa chuo hicho uko chini sana!swala la kumaliza nafikiri hilo ni la kawaida tu,kwa kuwa hata wale wanaosoma vyuo vikuu feki,pia humaliza!

Mimi si mhitimu wa chuo hicho. Ubora wa chuo? chuo ni kipya, fresh, brand new, waalimu waliobobea, kama uliisikia hotuba ya uzinduzi jana, mpaka Dr. Mohamed Gharib Bilal anafundisha hapo, au unataka kusahili na uhodari wa Dk. Gharib Bilal? na wengi wengineo. Nadhani hiki chuo kitakuwa cha kwanza kwa ubora katika Afrika si muda mrefu kuanzia sasa. Hiyo ndio aim ya JMK na ataweza. Tunaona jitihada zake, kwani hata makamu wake wa Raisi kisha mwambia asiache kufundisha pale na asiache kusimamia wanafunzi wa Phd. Jee, yote hayo huyaoni. Au mradi tuu, uponde, hata mema basi?
 
Kizuri chajiuza..nini mpaka mmkampenie "sifa"..

Kampeni wakati uchaguzi usha-kwisha, na Jakaya Mrisho Kiwete ndio Rais wa JMT na Dr. Mohamed Gharib Bilal ndio Makamu wa Rais na Dr. Mohamed Shein ndio Rais wa Zanzibar na Seif "Double" au "Square" ndio makamo zake wa kwanza na wapili. Kampeni ipi tena?
 
Natoa pongezi na hongera zangu za dhati kabisa kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Toka wazo hadi udahili wa mwanzo mpaka leo tunashuhudia wahitimu wa mwanzo wa UDOM, yote haya katika kipindi kifupi. Hii ni rekodi ya Dunia.
Hongera wahitimu, hongera Tanzania.

Unajua mie nawashangaa sana watu humu JF . JF imekuwa kama Chama Cha Upinzani dhidi ya serikali hata pale mazuri yanapofanywa. Kama ni hivyo si tusajili Chama kiwe officially known basi. Kwani kila kitu nikupinga kupinga tu. Hata kama wamchukia mtu , kwenye mema apewe sifa zake. Mie nadhani JF tunapoteza mwelekeo kabisa, na hata globu zingine kama Facebook etc zimeanza kutupita kwa ku analyse mambo vizuri kuliko sie, tutabaki tu na neno la GREAT THINKERS kumbe hatutumii weledi wetu ku prove hiko kitu,

Hayo ni mawazo yangu binafsi, wewe uko huru kuwa na mawazo yako binafsi, jee wewe ulifanya utafiti kuona hii siyo rekodi ya dunia? Mimi sijafanya utafiti, lakini, mpaka leo sijasikia rekodi iliyoipita hii. Wewe kama una utafiti wa kulipinga hilo, uweke hapa, kama hauna, funga bakuli.

Oh!kumbe mambo ya mtaani!basi sikuwezi!lakini hoja yangu ya msingi ilikuwa kwenye rekodi ya dunia!kwa kawaida mtoa hoja hanapaswa kuonyesha chanzo cha habari yake,pale anapoongelea habari ambayo ameinukuu,na kwa kuwa wewe ndiye mtoa mada ulipaswa kutoa chanzo cha habari ili kuchochea udadisi zaidi!mimi kama mlaji wa habari yako si wajibu wangu kutoa chanzo cha habari,na kwa kuwa nilikuwa sijafanya utafiti ndiyo maana sikutoa habari hii.Tukana uwezavyo lakini hapo umeteleza,truth shall prevail forever!!
 
Chanzo Cha habari ni mimi mwenyewe na unaweza kuninukuu.
 
Udom haikuwa concept ya Mkapa, kwa matamshi yake Mwenyewe Kikwete katika uzinduzi hapo jana, ilikuwa ni "kiherehere" chake binafsi na ahadi binafsi aliyoitowa wakati wa kampeni za 2005, anasema, aliogopa hata CCM wasije wakamuuliza hii sera ya kujenga chuo kipya ilitoka wapi? Na Bajeti yake iko wapi.

Kuhusu rekodi ya Dunia. Hilo ni wazo langu binafsi, kwani mpaka sasa sijasikia, wazo, ahadi, kujenga chuo kipya, mpaka kudahili within 2 years na kutowa wahitimu wa mwanzo within 5 years. Sijawahi kuona au kusikia zaidi ya UDOM. Jee wewe umewahi?
UDOM ilikuwa ni concept ya Mbowe katika kampeni zake za 2005, kwamba wataigeuza Dodoma kuwa jiji la vyuo vikuu
 
Tanzania tuna tatizo la kupenda kuona kitu kipya na wingi wake bila ya kuangalia quality/ubora wake.

Sasa hivi UDOM inashamiri wakati UDSM ndiyo inazidi kufa. Ila huwezi kujisifu kwa kupanua UDSM.

Kujenga Chuo kipya inauzika safi sana kuliko kuvifanyia matengenezo vilivyopo na kuvipanua.

Mashule ya Kata ndiyo kabisa. Eti Secondary ina walimu 3, WTF!!!!!????

Mtu ukihoji, jitu linakuja na hoja ya Mipasho ya "...Una wivu wa kike....".

Sasa aliyetowa hela kwa ajili ya ujenzi wa chuo ni nani? Iran? Mashirika ya Bima ya Tanzania au Bill Gates?

Isije kuwa safari zote hizo za nje zimeishia kupata chuo cha UDOM. Angelikaa na kudhibiti kodi, angelijenga UDOM na UDSM kuiboresha kwa kuleta walimu safi na wa maana.

Jana nimekutana na kijana mmoja kutoka Rwanda na anasema "Kagame analipa Dola 75 kwa saa kwa walimu wa University." Sikuuliza kwa walimu wa grade ipi ila hiyo ni pesa nzuri sana na nina imani watu wengi walioko nje na haswa Watanzania, wangelirudi nyumbani ili kuja kusaidia vyuo vyetu. Mtu akijikusanya kwa masaa 20 kwa mwezi, basi ana hela yake nzuri tu kwa mwezi na unakuwa na muda wa kujiandaa na masomo na kufanya tafiti mbalimbali na wanafunzi wako/practical.

Ifike sehemu Watanzania tuanze kudai UBORA na siyo WINGI. Tatizo ni kuwa, kumtembeza kiwete wa akili ni kasheshe.
 
Natoa pongezi na hongera zangu za dhati kabisa kwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Toka wazo hadi udahili wa mwanzo mpaka leo tunashuhudia wahitimu wa mwanzo wa UDOM, yote haya katika kipindi kifupi. Hii ni rekodi ya Dunia.
Hongera wahitimu, hongera Tanzania.
Kweli ni recodi ya dunia, unaanzisha chuo bila walimu wa kutosha!? walimu wa kuungaunga tunategemea kupata product gani kwa wanafunzi wanaograduate leo? Scrap!!
 
Sasa aliyetowa hela kwa ajili ya ujenzi wa chuo ni nani? Iran? Mashirika ya Bima ya Tanzania au Bill Gates?

Isije kuwa safari zote hizo za nje zimeishia kupata chuo cha UDOM. Angelikaa na kudhibiti kodi, angelijenga UDOM na UDSM kuiboresha kwa kuleta walimu safi na wa maana.
.
Safari za nje hakuna kitu alichopata, ametumia hela zetu za pension, halafu anajisifia
 
Kweli ni recodi ya dunia, unaanzisha chuo bila walimu wa kutosha!? walimu wa kuungaunga tunategemea kupata product gani kwa wanafunzi wanaograduate leo? Scrap!!

Wakuungaunga, something is better than nothing.
 
Back
Top Bottom