Hongera Chama kioo cha Soka la Bongo. Utakuwa ukilinganishwa na kila Mchezaji ajaye. Chama babalao

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
7,621
16,700
MABAO mawili aliyofunga dhidi ya Power Dynamos huko Zambia, yamemfanya Clatous Chama azidi kuinyemelea rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ligi ya Mabingwa Afrika inayoshikiliwa na nyota za zamani wa TP Mazembe na DR Congo, Tresor Mputu.

Kwa kufunga katika mchezo huo uliochezwa Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Levy Mwanawasa jijini Ndola, Chama sasa amefikisha idadi ya mabao 20 ambayo amepachika katika mashindano hayo, akidaiwa mabao 19 ili aifikie rekodi ya Mputu na mabao 20 ili aivunje kabisa.

Chama ambaye alikuwa anashika nafasi ya 11, katika chati ya wafungaji bora wa muda wote wa mashindano hayo, kwa sasa amesogea hadi nafasi ya tisa akimfikia nyota wa zamani wa TP Mazembe, Dioko Kaluyituka na staa aliyewahi kutamba katika timu za Moghreb Tetouan, Wydad Casablanca na Raja Casablanca, Mouhcine Lajour.

Nyota huyo kutoka Zambia, anahitajika kufunga mabao manne tu ili aweze kuingia katika tano bora kwani aliyepo nafasi ya tano ni mchezaji wa zamani wa Al Ahly, Emad Moteab aliyepachika mabao 24 na akifunga mabao manane tu ataingia katika tatu bora kwani atamfikia Mahmoud El Khatib ambaye amefunga mabao 28.

Idadi kubwa ya mabao yanayomfanya Chama atambe katika Ligi ya Mabingwa Afrika ameyapata akiwa anaitumikia Simba na ameifungia timu hiyo mabao 16 katika misimu mitano tofauti alivyoichezea Zesco aliyoitumikia kwa msimu mmoja, ameifungia mabao manne.

Nyota ya Chama ndani ya Simba ilianza kung’aa katika msimu wa 2018/2019 ambapo alifunga mabao matano, kisha katika msimu uliofuata wa 2019/2020 hakufunga bao ambapo Simba iliishia katika hatua ya awali ikitolewa na UD Songo.

Msimu wa 2020/2021, Chama alifufuka upya ambapo alipachika mabao matano katika mashindano hayo, mawili akifunga katika hatua za mwanzoni na matatu akapachika katika hatua ya makundi.

Katika msimu uliopita, staa huyo wa Zambia alifunga mabao manne na safari hii ambapo Simba imeanzia katika raundi ya kwanza, ameanza kwa kupachika mabao hayo mawili dhidi ya ndugu zake wa Power Dynamos.

Viwanja vya Benjamin Mkapa Dar es Salaam na Levy Mwanawasa, Ndola ndivyo vinaonekana kuwa na bahati zaidi kwa Chama kwani ndivyo amefungia mabao mengi kulinganisha na vingine vitatu ambako pia alipatia mabao yake.

Chama amefunga mabao 10 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, sita katika Uwanja wa Levy Mwanawasa, mawili katika Uwanja wa Mavuso, Swaziland huku moja akifunga katika Uwanja wa New Jos, Nigeria na lingine akifunga katika Uwanja wa Novemba 11, Angola.

Wachezaji WAFUATAO WAMEKUWA wakilonganishwa na chama Na wanaendelea kuangukia PUA.

1. Feisal Salum
2. Saido Ntibazonkiza.
3. Raly Bwalya.
4.Azizi ki Stephen.
5. Pakome Zoazoa.
6. Max Nzegeli nk.

CHAMA BABALAO.
 
MABAO mawili aliyofunga dhidi ya Power Dynamos huko Zambia, yamemfanya Clatous Chama azidi kuinyemelea rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Ligi ya Mabingwa Afrika inayoshikiliwa na nyota za zamani wa TP Mazembe na DR Congo, Tresor Mputu.

Kwa kufunga katika mchezo huo uliochezwa Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Levy Mwanawasa jijini Ndola, Chama sasa amefikisha idadi ya mabao 20 ambayo amepachika katika mashindano hayo, akidaiwa mabao 19 ili aifikie rekodi ya

CHAMA BABALAO.
Ndio tatizo la kujiona smart halafu kichwani hamna kitu.

Hivi unashindwa vipi hata kuelewa kua magoli rasmi ya CAF wanaanza kuyahesabu kuanzia Group stage.

Huku preliminary na 2nd round hata mchezaji afunge magoli 100+ hayahesabiwi.
 
Ndio tatizo la kujiona smart halafu kichwani hamna kitu.

Hivi unashindwa vipi hata kuelewa kua magoli rasmi ya CAF wanaanza kuyahesabu kuanzia Group stage.

Huku preliminary na 2nd round hata mchezaji afunge magoli 100+ hayahesabiwi.



Sent using Jamii Forums mobile app

Jiulize mwenyewe Halafu tafakari.
Ukikosa majibu Nitakusaidia.

Huwa napenda sana WATU waelimike na Kujifunza KUPITIA kwa kile kidogo nilichonacho.
 
Back
Top Bottom