Chama, Kanoute kuikosa Singida Fountain Gate Tanga

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891
KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Simba Clatous Chota Chama, ataukosa mchezo wa ufunguzi wa michuano mifupi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate, kutokana na kufungiwa michezo mitatu iliyo chini ya shirikisho la soka nchini TFF.

Chama alifungiwa kutokana na kuwa na adhabu hiyo aliyopewa baada ya kutenda tendo lisilokua la kiungwana baada ya kumkanyanga mchezaji AbalKassim Seleman wa Ruvu Shooting katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu nchini ambao Simba sc waliibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Adhabu hiyo ya michezo mitatu itamfanya staa huyo kukosa mchezo huo pekee kutokana na kwamba alishaitumikia msimu uliopita alipokosa michezo miwili dhidi ya Polisi Tanzania na Coastal Union hivyo ataungana na kikosi katika mchezo wa ama fainali ama mshindi wa tatu katika michuano hiyo mifupi itakoyohusisha timu nne za Simba, Azam FC,Yanga pamoja na Singida Fountain Gate FC.

Katika mchezo huo, Simba pia itamkosa pia kiungo wao Sadio Kanoute aliyeoneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA) dhidi ya Azam FC.

Hata hivyo kukosekana kwa wachezaji hao hakutajwi kuwa kama ni pengo kubwa kwa timu hiyo kutokana na aina ya wachezaji wapya iliowasajili ambapo kwa sasa mastaa kama Fabrice Ngoma, Saido Ntibanzokiza, Aubin Kramo, Leandre Onana wanaweza kuziba pengo hilo bila wasiwasi.
 
Kusema kuwa kukosekana kwa hao watu hakuna pengo sijui una maana gani, unless umzungumzie Chama ila sio Sadio, Sadio ndio uti wa mgogo wa ukabaji Simba.
 
Back
Top Bottom