Mzee mwenzangu kuna vitu labda huwa navitafsiri vibaya lakini nachelea kusema nitaishikilia tafsiri hiyo kama msimamo wangu kwenye mahusiano.
Naamini watu wanachanganya sana vitu vitatu katika mahusiano (hii ni kwa mujibu wa uelewa wangu finyu.). Mie naamini kuna Mapenzi, Mapendo (Upendo) na Kutamaniana. Kwangu mie ni vitu tofauti.
1. Mapenzi: Kwangu mie hii makitu inahusisha upendo na ngono ndani yake. Kwa mantiki hii kale ka maiwaifu kangu kanaangukia hapa. Nna mapenzi naye. Hata ikatokea kwa namna yoyote ile nimechepuka, hiyo itakuwa ni bahati mbaya na hakika kwake nitarudi tu. Hii inahusisha kupendana, kujaliana, kusikilizana, kuheshimiana, kuridhishana, kusameheana, kusaidiana na vitu kama hivyo.
2. Upendo: Huu ndio ule wa Agape sasa. Hauna uhusiano na ngono. Bahati nzuri kwenye upendo, hata yule uliye na mapenzi naye anaingia. Kwahiyo hapa wanaingia watu wengi sana, mke, marafiki, wazazi, watoto, majirani et el.
3. Matamanio: Hii ya kutamani ndio kama hiyo red hapo juu. Ni kutamaniana kuvuliana chupi na kubanjuka. Baada ya muda kila mtu anachukua time yake. Hisia zikirudi tena mnajikumbushia then kila mtu anachukua time. Hii inaweza sababishwa na tamaa za kimaumbile, sura, fedha, ulevi, misifa na vitu kama hivyo.
Hivi leo jumangapi vile?