Hoja za Waitara - Je, CHADEMA watajibu?

Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
13,928
2,000
Umewahi kumsikia magufuli anazungumzia matrilioni ya ununuzi wa ndege na ujenzi wa airport chato na upotevu wa zile 1.5tn?.......
Tuanzie hapo kwanza kwa maslahi ya taifa
 

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
6,863
2,000
Hoja za Lijuakali ukijumlisha na hizi za Waitara zinashawishi kuonyesha kuwa huko CHADEMA kuna matatizo makubwa ya matumizi ya pesa.

Hivyo ni muhimu kwa CHADEMA kujibu hizi hoja kwa ushahidi wa stakabadhi, juu ya matumizi ya pesa wanazopata toka vyanzo mbalimbali.

Wasi wasi wangu mkubwa si matatizo yanayotokea katika hicho chama, bali ni pale kitapofanikiwa kuingia madarakani na kuiharibu nchi kwa kuifilisi mpaka kile kidogo kunachorambaramba. Kimsingi kimefanikiwa kuwashawishi kiasi kikubwa cha watanzania kuamini kuwa CHADEMA ndio chama mbadala. Hivyo kama watanzania tukateleza na kuwachagua wasije wakatuharibia nchi.

Cha msingi ni kwa wale viongozi waliochadema kuunda timu na kuyasema hayo wakiwa ndani ya CHADEMA. Wanapoyasema nje ya chadema, hayana uzito sana uzito kwani tulio nje tunafikiri kuwa kwa vile mmefukuzwa ndio mnalipiza kisasi.

Kinachonishangaza ni kimoja tu, yaani kwa makosa yote mnayoyaeleza mnashindwa kuunda umoja ndani ya CHADEMA utaofanya mapinduzi humo ndani bila ya kungoja kutoka nje. Hilo litakuwa jambo jema sana hasa kwa waliobaki CHADEMA, vinginevyo ni vigumu sana kuaminika. Na kwa udhaifu huo yawezekana ndio huyo Mwamba anawashinda kirahisi sana. COME ON!!!!!!
Kuna pia hoja za Wabunge wawili wanawake, pamoja na madai ya matumizi mabaya ya fedha, kuna rushwa ya ngono.
Vyama vingi vyenye ushawishi mkubwa kama NCCR na CUF vilifuatiliwa kwa propaganda na kupandikizwa wasaliti mpaka baadaye vikafa ama kupunguzwa nguvu. Inaweza kuwa ni kweli kuwa Mbowe ana mapungufu yake lakini ushawishi mkubwa wa kiasiasa alionao kwa wanachama na wananchi wengine unawapa kazi sana ccm namna ya kumwondoa ili kufanikisha lengo kama lililofanywa kwa vyama vingine ili ccm isiwe na upinzani mkubwa.

Kwa maoni yangu naona Mbowe akiondoka au kuondolewa uenyekiti basi CHADEMA nacho kitafuata nyayo za NCCR na CUF kwani imagine watu hao wanao hama ndiyo wangekuwa wenyeviti. Chama nafikiri kina waanzilishi wenye uchungu navyo na pengine wale ambao wana affiliation na waasisi wanaweza kuwa na uchungu na chama kuliko wengine ambao pengine malengo yao hayaeleweki na yanaweza kuyumbishwa na ushawishi wa kifedha ambapo wanaweza hata kutumiwa kuua chama.

Mzee Mbowe kama yasemwayo ni kweli pengine kuna haja ya kujirekebisha na kuruhusu demokrasia ishamiri. Mifumo pia ya kiutawala iwe wazi ikiwemo ya manunuzi ambayo ina ushawishi mkubwa wa kifedha. Nafikiri pia Chadema inatakiwa kuwa na Kamati ya Tenda pamoja na mtaalam wa ununuzi ambaye anatakiwa atumie kanuni za wazi za ununuzi (Best practices).
Mh Mbowe atumie busara kuweka wazi matumizi ya fedha za chama kwa wanachama kupitia Baraza Kuu la chama, kabla ya kuanza mchakato wa kuteua wagombea wa chama kwenye Uchaguzi Mkuu. Asipofanya hivyo atawapa mtihani wagombea hao kujibu tuhuma dhidi yake, wakati wa kampeni. Hakuna shaka wagombea wa upinzani watabeba tuhuma dhidi ya Mbowe kama agenda.
 

JOHNKEKE

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
944
1,000
Mimi sishangai, nilishasema muda mrefu Mbowe ni msanii!
Najua kwa akili yake ndogo anafikiri akilipa vijana watukane JF na kumtukuza yeye basi atapata uraisi!
 

JOHNKEKE

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
944
1,000
Propaganda tu nilidhani ana nyaraka kumbe anatutuma kwa Gwajima!!

Anadai Mbowe ametapeli pesa za kampeni ilihali Waitara bado alikubali kugombea kupitia CHADEMA!!

Hvi tuhuma nzito hivi unadhani Dr Slaa asingezimwaga siku anasepa ama Zitto?

Dr Mashinji alikua katibu mkuu hajayasema hya sembuse hyu aliyekua subordinate tu.

Ifike mahala hawa waropokaji wafaiwe nyaraka kuthubitisha maana kma CAG anakagua mahesabu afu haoni huu ubadhirifu ila wanasiasa ndio wanauona basi nchi yetu ina matatizo mazito zaidi.

CCM jaribuni zaidi, Kma Dr Slaa alifeli sidhani kuna press conference ya kuivunja CHADEMA.

Kuna yule Naibu waziri alisema CHADEMA walimdhuru Lissu nashangaa polisi haijamuita kusaidia upelelezi na kosa la kuiba evidence eneo la tukio.
Wewe ni msukule wa Mbowe, tunajua ni miongoni mwa BAVICHA wanaolipwa kuchafua JF. Ndiyo maana muda wote kuanzia asubuhi na usiku unashinda JF kutukana na kutoa matusi badala ya hoja. Ukiona hujibiwi manaake umedharaurika!
 

kipande

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,268
2,000
Propaganda tu nilidhani ana nyaraka kumbe anatutuma kwa Gwajima!!

Anadai Mbowe ametapeli pesa za kampeni ilihali Waitara bado alikubali kugombea kupitia CHADEMA!!

Hvi tuhuma nzito hivi unadhani Dr Slaa asingezimwaga siku anasepa ama Zitto?

Dr Mashinji alikua katibu mkuu hajayasema hya sembuse hyu aliyekua subordinate tu.

Ifike mahala hawa waropokaji wafaiwe nyaraka kuthubitisha maana kma CAG anakagua mahesabu afu haoni huu ubadhirifu ila wanasiasa ndio wanauona basi nchi yetu ina matatizo mazito zaidi.

CCM jaribuni zaidi, Kma Dr Slaa alifeli sidhani kuna press conference ya kuivunja CHADEMA.

Kuna yule Naibu waziri alisema CHADEMA walimdhuru Lissu nashangaa polisi haijamuita kusaidia upelelezi na kosa la kuiba evidence eneo la tukio.
Fanya tu evaluation. Kama umetumia muda wako kutetea uovu halafu umepata like mbili tu. Ujue kuna shida mahali. Watu wameanza kuujua upande wa pili wa CDM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
11,484
2,000
Fanya tu evaluation. Kama umetumia muda wako kutetea uovu halafu umepata like mbili tu. Ujue kuna shida mahali. Watu wameanza kuujua upande wa pili wa CDM.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukweli hauwi determined na likes ama maoni ya jamiiforums bali facts.

CAG ametoa hati safi ikimaanisha madeni yamehakikiwa sasa tumuamini waitara ambaye ametutuma kwa Gwajima ama CAG report?

Tujaribu kuwa objective tuache ushabiki, wwe binafsi nkikuuliza uprove hoja hta moja hapo utaweza? Eti Mbowe alitumia 300m kupambana na Waitara? Ssa alishindwa kumuundia kesi amvue uanachama hadi atumie pesa yote hyo kumpora jimbo?
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
11,484
2,000
Wewe ni msukule wa Mbowe, tunajua ni miongoni mwa BAVICHA wanaolipwa kuchafua JF. Ndiyo maana muda wote kuanzia asubuhi na usiku unashinda JF kutukana na kutoa matusi badala ya hoja. Ukiona hujibiwi manaake umedharaurika!
Mkuu jibu hoja acha kuzunguka

Je kwanini Waitara hajatoa uthibitisho zaidi ya maneno?

Je CAG kwanini katoa hati safi ilihali kuna madeni hewa ya Mbowe?

Kwanini Dr Mashinji na Dr Slaa pamoja na kujua siri zote za chama hawajawahi dai Mbowe amekula ruzuku ila waitara ambaye hajawahi hta kufagia ofisi ya Mbowe ndio azushe bila ushahidi?

Je ni lini Ushahidi umekua "kamuulize Gwajima..... Fulani anajua?"

Embu naomba ujibu hoja na CCM wenzio kwa mtiririko huu if at all una hyo IQ?
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
3,263
2,000
Toeni walaka wa kupinga maana nyie kwa kusema wengine hamjambo
Ngoja niwasaidie watu wa CCM wanaopiga propaganda mfu hapa.

Waitara asingehitaji kamwe kutengeneza video na kuileta hapa JF; kwa sababu haisaidii kitu.
Waitara yupo desperate ile mbaya, anatafuta njia ya kutokea, na anajuwa njia hiyo sio hapa JF.

JF haitoi shukrani kwa yeyote na wala haimzawadii chochote Waitara kutokana na taarifa yake kuwa hapa.
Anapaelewa vizuri sana, ambapo kama akiwasilisha taarifa za kummaliza Mbowe anazawadiwa mara dufu.

Sasa kwa nini asiende huko na ushahidi mzito, na badala yake aje hapa JF, itamsaidia kitu gani yeye?

Mbowe amepambana na kuzishinda njia nyingi za kumwondoa alipo. Mwita Waitara awe na ushahidi wa hakika wenye tuhuma za kummaliza Mbowe, halafu ashindwe kuzipeleka kwa watu ambao wanazitafuta usiku na mchana? Watu anaojua Waitara watamzawadia maradufu kwa taarifa zake zitakazotimiza malengo ya kumwondoa njiani Mbowe!

Mara nyingi Jukwaa hili la JF linatumika kama jalala vile.
Kuna watu wanadhani JF hakuna watu wenye akili timamu!
Sent using Jamii Forums mobile app
 

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
3,263
2,000
Mkuu yote haya yanasababishwa na ujinga wa watanzania yaani MIJITU mijinga mpaka kichefuchefu.sasa Jinga kama hili waitara nalo kwa sababu linajua kuna majinga zaidi yake yataamini lolote analosema yatakubali basi linalopoka tu. Na tatizo kuu ni Mbowe kugoma kuabudu kimungu chao.
Hii hoja haijaanza na waitara ilianza tangu mwigamba sio ya leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

kipande

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,268
2,000
Ukweli hauwi determined na likes ama maoni ya jamiiforums bali facts.

CAG ametoa hati safi ikimaanisha madeni yamehakikiwa sasa tumuamini waitara ambaye ametutuma kwa Gwajima ama CAG report?

Tujaribu kuwa objective tuache ushabiki, wwe binafsi nkikuuliza uprove hoja hta moja hapo utaweza? Eti Mbowe alitumia 300m kupambana na Waitara? Ssa alishindwa kumuundia kesi amvue uanachama hadi atumie pesa yote hyo kumpora jimbo?
Nadhani Wewe ni mgeni humu jamvini. Siku zote hoja inayoletwa humu kama ni nzito lazima itakua na idadi kubwa ya wachangiaji. Kama ni mchango unaoungwa mkono lazima uwe na likes za kutosha. Na huwezi kuungwa mkono kama huna facts. Sema siku hizi tu JF imeingiliwa unaweza ukapiga porojo na ukapata likes za kutosha. Lakini wewe hata hilo limeshindikana kwenye hoja yako. Inabidi unishukuru hata mimi niliekujibu.

Anyway turudi kwenye hoja yako. Sasa hivi msahafu wa CDM kumsafisha mwenyekiti wenu mbowe ni hati safi za CAG. Kumbuka CAG anakagua mahesabu tu kwa maana ya matumizi ya fedha zilizototolewa na Serikali Lakini maamuzi wa hizo fedha zinatumika vp hawezi kuingilia ni maamuzi ya chama na hapo ndo mbowe anapowapigia. Kwa mfano, chama kilikua na madeni na inaonekana kwenye mahesabu hayo madeni yamelipwa na stakabadhi zipo, unadhani CAG atasemaje? Lakini watu wanachohoji ni uhalali wa hayo madeni. Lakini vipi kuhusu michango na misaada ambayo chama inapokea nani anakagua?

Tuhuma za mbowe kuhusu ubadhirifu wa fedha za chama hazikuanza Leo wala jana. Chacha Wangwe aliongea, Zitto Kabwe aliongea, Mwigamba aliongea, Kitila aliongea. Na sasa wanaongea wabunge kina lijualikali na Waitara. Hawa wote wanamsingizia mbowe? Toka gizani fungua akili yako. Utajikuta unatetea kitu usichokijua kutokana tu na mahaba uliyonayo kwenye hicho chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

geordan

Member
May 28, 2014
15
45
CHADEMA hamna haja ya kuwajibu hawa wapuuzi ni wa kupuuzwa waaachwe wabwabwaje maana ndio kazi walioitiwa kwenye Chama Cha Manunuzi
 

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
6,863
2,000
Mimi sishangai, nilishasema muda mrefu Mbowe ni msanii!
Najua kwa akili yake ndogo anafikiri akilipa vijana watukane JF na kumtukuza yeye basi atapata uraisi!
Mbowe hajawa, hana na hatakuwa na nia ya kugombea Urais. Kwake yeye falsafa ni ya "hapendwi mtu ila fedha tu". Kuthibitisha hoja hii alimkaribisha Lowassa akiamini angeweza kuwa Rais na yeye akateuliwa kuwa Waziri wa Fedha au Wizara yoyote yenye kuhusika na pato kubwa la Taifa. Pamoja na kukosa nafasi hiyo, alifanikiwa kupata Wabunge wengi na kuongoza Halmashauri za miji mikubwa nchini. Ruzuku na michango ya Wabunge, hakika si kipato haba.

Kufanikisha azima yake ya utajiri (ati anachukia umaskini, huwaambia wanachama wake), anakiongoza chama kama kampuni yake ya biashara na si SACCOS, ambavyo wengi wanavyosema. Mkurugenzi Mkuu Mtendaji ni Katibu Mkuu wa chama. Viongozi wengine ni Wakurugenzi na Mameneja katika Idara mbalimbali ndani ya Chama. Wanachama na wafuasi ni "sales persons", wengi wao wakiwa machinga wa kuuza bidhaa zake. Bidhaa anazotengeneza na kuuza ni hizo kauli zake za kuigonganisha Serikali na wananchi. Kuthibitisha hoja hii, Mbowe ni mmoja wa Viongozi wa vyama vya upinzani aliyepinga, kwa nguvu zake zote, mabadiliko ya Sheria ya Vyama vya Siasa [The Political Parties (Amendment) Act, 2019] kwa kuwa yanampa madaraka Msajiri kufuatilia mienendo ya vyama vya siasa, hasa katika matumizi ya fedha.

Ushahidi mwingine, anashupalia kuwepo kwa Tume ya Uchaguzi ambayo anaweza kuweka mkono wake, kwa kutumia nguvu yake kipesa, kubadili matokeo ya kura. Kama anadai CCM hubadili matokeo ya kura, kwa nini yeye asiweze kufanya hivyo. Tunajua fika kuwa pesa ina nguvu sana kubadili tabia ya mtu yeyote.

Ukweli kwamba CAG hajaweza kubaini matumizi mabaya ya fedha za chama na ufisadi wa Mbowe, ni wazi kuwa watumishi wa ofisi ya CAG (siyo CAG mwenyewe), wanaotumwa kukagua hesabu za CHADEMA, hupewa rushwa.

HAKIKA MBOWE NI MJASIRIAMALI WA KISIASA BINGWA HASA
 
Top Bottom