Hoja za Waitara - Je, CHADEMA watajibu?

Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
13,674
2,000

========
Mh. Waitara amesema kuwa baada ya wabunge wa CHADEMA kutangaza kuwa watahamia CCM na wengine wataenda NCCR Mageuzi basi wameshambuliwa sana na hasa Mh, Lijualikali.

Amesema kuwa miongoni mwa watu ambao anawafahamu ni pamoja na Lijualikali, anadai alipoenda Mlimba na Kilombero wakati Lijualikali anagombea udiwani na Lijualikali hakuwa mtumishi wa CHADEMA ila alikuwa ni mwanachama wa CHADEMA.

Anadai kuwa wakati huo yeye ndie aliekuwa mtu wa sera na utafiti na alifanya utafiti nchi nzima hivyo kusema Lijualikali hana nguvu Kilombero sio kweli kwa kuwa alichaguliwa kugombea kati ya wengi waliokuwa wanataka kugombea.

Anasema kwenye siasa ukitaka kushinda, chama cha siasa kinapomchangua mgombea mwenye sifa basi wanahesabu asilimia 30 kuwa tayari wameshashinda.

Anasema katika nchi hii mtu ambaye amebahatika kukaa kwenye siasa mda mrefu lakini ni tapeli wa kisiasa na alipaswa afungwe kwenye ile timu ya wahujumu wa Uchumi ni Mh. Mbowe lakini Mungu wake ni mkubwa sana.

Anadai kuwa kwenye matumizi ya pesa Mh. Mbowe anatumia pesa za chama kwa matumizi yake binafsi na hakuna maendeleo ya chama kama ofisi nk.

Anadai Kuna pesa ambazo CHADEMA ilipewa kutoka Japani kwa ajili ya kusaidia mchakato wa kampeni mwaka 2014 lakini pesa hizo hazijulikani ziliwekwa kwenye akaunti gani wala matumizi yake ni yapi na Mh. Mbowe hajatoa majibu kuhusu pesa hizo.

Anasema kuwa watu wanahama chama kwa kuwa wanagundua madhaifu yaliyopo kwenye mfumo wa kiuongozi wa Mh Mbowe kwa maana Mh Mbowe ndie anae fanya manunuzi peke yake na yeye ndie mwenye maamuzi ya mwisho na ikitokea mtu amelalamika au kusema kuhusu jambo lolote lisilo kuwa sawa kwa upande wa Mh. Mbowe basi anachukuliwa hatua kali.

Mbowe anatumia pesa za ruzuku kwa shughuli binafsi na kuwachangisha wabunge wake kila mwezi kwa matumizi binafsi. Huyu ni Dictator mkubwa sana wakati hata Ofisi ameshindwa kujenga licha ya kuwa Chama kinapata pesa nyingi.
 

byeyombo

JF-Expert Member
Sep 3, 2015
1,189
2,000
Waitara amemwaga ugali lakini hiyo Video ipo you tube JF wameizuia kwa sababu za msingi zinazojulikana. Ukiingia you tube imewekwa about 3 hrs hujuma zote za Mwamba ie Mbowe.
SABABU GANI ZA MSINGI MKUU??
 
Top Bottom