Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,723
Wanabodi,
Hii hoja ya wasomi wahitimu wa vyuo vikuu kwenda kusoma VETA.
Shuhudia hizi Testimonials....
View: https://youtu.be/Rzr6coD9ihs?si=ZKYzt1V9FZFITszQ
kauli ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majaliwa, kuwa wahitimu wa Chuo Kikuu, wakasome VETA, imepokelewa kwa hisia tofauti, zenye sintofahamu fulani fulani.
Kauli hiyo imepokelewa vibaya na wasomi wa vyuo vikuu, wanaoringia usomi wao, hata kama usomi huo, hauwasaidii kitu, hivyo kitendo cha kuambia wakasome VETA, wanajiona kama wamedharauliwa!.
Wahadhiri wa vyuo vikuu nao wameipokea vibaya kauli hiyo, kwa kuona Waziri Mkuu, ni kama ametangazia taifa kuwa elimu ya chuo kikuu kwa sasa, ni kama haina maana tena, mambo yote ni elimu ya ufundi stadi inayotolewa na VETA, hivyo kuogopa kuitikiwa kwa wanafunzi badala ya kuomba udahili wa vyuo vikuu, bora waende VETA!.
Ukweli utabaki kuwa ukweli, watu wanaongoza kwa kutegemea ajira za maofisini, ni wasomi wa vyuo vikuu, wanaojiona wao ni wasomi sana, wamesema sana, na wanastahili kazi za maana, huku wakuwaona wahitimu wa VETA kama ni wale Darasa la saba, waliofeli na kushindwa kujiunga sekondari ndio wanategemea VETA!.
Hapa ukumbini, zimetolewa shuhuda 10 za wahitimu wa vyuo vikuu, waliokosa kazi baada ya kuhitimu, na walipoamua kujiunga VETA kusomea ufundi standi, sasa ni matajiri wakubwa, sio tuu kwa kujiajiri, bali pia kwa kuajiri wengine.
Ukweli mchungu kuhusu elimu yetu ya chuo kikuu inawafundisha watu kutegemea ajira, hivyo wahitimu wa vyuo vikuu wanaweza kukosa ajira kwa vile hazipo, lakini wahitimu wa VETA, hakuna kabisa hoja ya kukosa ajira, kwasababu wahitimu wa VETA, hawahitaji kuajiriwa, bali VETA inawajengea uwezo wa kujiajiri!.
Pascal