Ms Judith
JF-Expert Member
- Dec 24, 2010
- 2,563
- 919
nianze kwa kuweka wazi kuwa sina hakika na imani ya huyu ndugu yetu Mohamedi Shossi, sijui kama ni mwislamu, mkristo ama muumini wa dini nyinginezo.
aliweka wazi kuwa babu si size ya Yesu na alisema kuwa Yesu ni "world icon" na babu hawezi kulinganishwa naye hata kidogo. baadhi walimkosoa kumwita Yesu "world icon" na walikuwa na sababu zao. pia ametoa michango mingi tu mingine ila hapa nataka niungane naye na kumpongeza kwa kuhoji hiyo bei ya babu.
Mungu wetu afikie mahali apange bei!! tena ya huduma itokanayo na karama aliyotoa mwenyewe? kweli hapo pagumu kuingia akilini. tena mungu wake huyo akampa na mchanganuo wa namna atakavyozigawa hizo pesa, eti 300/- kwakanisa, yatima na wajane na 200/- za wahudumu wanaomsaidia kazi! kwa kweli naona kama hizi ni kashfa kwa Mungu wetu.
neema ya Mungu wetu ni kubwa na pana sana, na kamwe huyu babu asiichezee kiasi hiki. yeye atangaze kuwa ni mganga aliyekuja na dawa ya mti wa mrigariga, afuate taratibu za serikali za kujisajili kisheria ili serikali itambue kazi zake na aweke bei yake kama wawekavyo waganga wengine na tutamchukulia kama tunavyowachukulia waganga wengine.
hongera tena Mohamed Shossi, hoja yako ni njema na ya kweli. Mungu wetu hahitaji hata senti yetu moja. karama zake hutoa bure. michango kwa ajili ya kazi ya Bwana ni ya hiyari na kadiri mtu alivyojaaliwa kutoa.
ukishaweka bei (hata kama ni sh.10/-) maana yake ni kwamba asiye nayo hapati huduma! kumbuka madukani kuna pipi za sh.10/- na usipokuwa na hiyo sh.10/- hupati hiyo pipi. ndiyo maana ya bei. sasa babu anasema kama huna sh. 500/- kaa pembeni mwenye hela aje apate kikombe! hata akiamua kuwasamehe wengine kulipa, manake atakuwa kakiuka utaratibu wa huyo mungu wake anayedhibiti bei! sasa hii nayo bado ni huduma ya kiroho kweli kwa mujibu wa dini ya kikristo? mungu gani huyu anayepanga hesabu hivi?
tuendelee kutafakari na kuliombea kanisa
Mungu akubariki sana ndugu Mohamedi Shossi,
Glory to God!