Hoja ya kusitisha Mafao ya Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta yatua Bungeni

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
uhuru_has_a_right_to6218e83c70cdc.jpg
Bunge la Kitaifa la Kenya linahitaji kura za walio wengi kusitisha mafao ya kila mwezi na marupurupu mengine ambayo Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta anapata kwa kinachoelezwa kuwa anajihusisha na siasa baada ya kustaafu.

Mbunge wa Gatundu Kusini, Gabriel Kagombe amewasilisha hoja katika Bunge la Kitaifa Jumanne Mei 2, 2023 akitaka Kenyatta anyimwe marupurupu yake ya kustaafu.

Hoja hiyo pia inalenga kusitisha mafao na marupurupu mengine ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga na aliyekuwa Makamu wa Rais, Kalonzo Musyoka.

Hoja hiyo inaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wabunge wanaounga mkono Muungano wa Kenya Kwanza wa Rais William Ruto.

Uamuzi wa kusitisha mafao ya Odinga na Musyoka utaamuliwa na si chini ya nusu ya wabunge, kwa mujibu wa Sheria ya Mafao ya Kustaafu (Naibu Rais na Maofisa Walioteuliwa).

Kagombe pia anataka Hazina ya Taifa kurejesha angalau Sh844 milioni ambazo zimelipwa kwa maofisa watatu wa zamani baada ya kuondoka ofisini.

Mbunge huyo wa awamu ya kwanza anawatuhumu watatu hao kwa kujihusisha na siasa kali huku wakiendelea kupokea mafao yao ya kustaafu, jambo ambalo anasema ni kinyume na vifungu vya Sheria ya Mafao ya Kustaafu ya Rais ya mwaka 2003 na Sheria ya Mafao ya Kustaafu (Naibu Rais na Maofisa Wateule) ya mwaka 2015.

MWANANCHI
 
Hiki sasa ni kisasi na kitawafikisha pabaya
 
Tuangalie na sheria zetu hapa Bongo tuna wasiwasi kwamba kuna mtu ameshika remote, tukimtolea uhalali wa kupata mafao nchi itaenda vizuri. Inasemekana mtu wetu ndo amebuni mkakati wa kulambisha asali.
 
uhuru_has_a_right_to6218e83c70cdc.jpg
Bunge la Kitaifa la Kenya linahitaji kura za walio wengi kusitisha mafao ya kila mwezi na marupurupu mengine ambayo Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta anapata kwa kinachoelezwa kuwa anajihusisha na siasa baada ya kustaafu.

Mbunge wa Gatundu Kusini, Gabriel Kagombe amewasilisha hoja katika Bunge la Kitaifa Jumanne Mei 2, 2023 akitaka Kenyatta anyimwe marupurupu yake ya kustaafu.

Hoja hiyo pia inalenga kusitisha mafao na marupurupu mengine ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Raila Odinga na aliyekuwa Makamu wa Rais, Kalonzo Musyoka.

Hoja hiyo inaungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wabunge wanaounga mkono Muungano wa Kenya Kwanza wa Rais William Ruto.

Uamuzi wa kusitisha mafao ya Odinga na Musyoka utaamuliwa na si chini ya nusu ya wabunge, kwa mujibu wa Sheria ya Mafao ya Kustaafu (Naibu Rais na Maofisa Walioteuliwa).

Kagombe pia anataka Hazina ya Taifa kurejesha angalau Sh844 milioni ambazo zimelipwa kwa maofisa watatu wa zamani baada ya kuondoka ofisini.

Mbunge huyo wa awamu ya kwanza anawatuhumu watatu hao kwa kujihusisha na siasa kali huku wakiendelea kupokea mafao yao ya kustaafu, jambo ambalo anasema ni kinyume na vifungu vya Sheria ya Mafao ya Kustaafu ya Rais ya mwaka 2003 na Sheria ya Mafao ya Kustaafu (Naibu Rais na Maofisa Wateule) ya mwaka 2015.

MWANANCHI

Kwani katiba mpya inasemajeee?
Kastaafu urais pekee, au kastaafu urais na siasa pia??
 
BrazaJ unaitwa huku....
Brazajeeeeeei
Waandamane😅😅😅😅😅😅😅
 
Back
Top Bottom