Rais Mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta nusura arushiwe bomu la Machozi

Kenyan

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
414
313
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Uhuru Kenyatta ameibua hisia mseto miongoni mwa raia wengi wa Kenya, wakihoji ni sababu gani hasa inamfanya Kiongozi huyo mstaafu kugoma kustaafu siasa kama walivyofanya watangulizi wake, Hayati Rais Moi na Hayati Kibaki.

Hili ni kutokana na kitendo cha Jana, ambapo Kenyatta alijitokeza eneo la Kileleshwa na kuwataka maafisa wa polisi waliokuwa wakipiga doria nje ya Ofisi za Chama chake cha Jubilee kuondoka.

Kwa mujibu wa Kenyatta, serikali ya Rais Ruto inalenga kukikandamiza Chama cha Jubilee kwa kuwafurusha eneo hilo.

Ikumbukwe makao makuu ya Chama hicho yaliyomo katika Barabara ya Thika yalishapigwa mnada kufuatia ugumu wa kulipa kodi.

Aidha Kenyatta amewasihi Polisi kutotumika vibaya na Serikali na badala yake kuzingatia kiapo cha kulinda maisha na mali ya wananchi.

Haya yanajiri huku Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga akitarajiwa kuwasili nchini leo akitokea Dubai, ambapo pia anatarajiwa kutangaza vuguvugu jipya la maandamano ya kupinga serikali ya Rais William Ruto
 
Ruto anamhangaisha Uhuru.....
 
Attachments

  • Kabila mbili Kenya.mp4
    11.2 MB
Rais mstaafu wa awamu ya nne, Uhuru Kenyatta ameibua hisia mseto miongoni mwa raia wengi wa Kenya, wakihoji ni sababu gani hasa inamfanya Kiongozi huyo mstaafu kugoma kustaafu siasa kama walivyofanya watangulizi wake, Hayati Rais Moi na Hayati Kibaki.

Hili ni kutokana na kitendo cha Jana, ambapo Kenyatta alijitokeza eneo la Kileleshwa na kuwataka maafisa wa polisi waliokuwa wakipiga doria nje ya Ofisi za Chama chake cha Jubilee kuondoka.

Kwa mujibu wa Kenyatta, serikali ya Rais Ruto inalenga kukikandamiza Chama cha Jubilee kwa kuwafurusha eneo hilo.

Ikumbukwe makao makuu ya Chama hicho yaliyomo katika Barabara ya Thika yalishapigwa mnada kufuatia ugumu wa kulipa kodi.

Aidha Kenyatta amewasihi Polisi kutotumika vibaya na Serikali na badala yake kuzingatia kiapo cha kulinda maisha na mali ya wananchi.

Haya yanajiri huku Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga akitarajiwa kuwasili nchini leo akitokea Dubai, ambapo pia anatarajiwa kutangaza vuguvugu jipya la maandamano ya kupinga serikali ya Rais William Ruto View attachment 2602180View attachment 2602181

Kenya wako vizuri, Kenyatta Yuko vizuri, wakenya wako vizuri na hata polisi wao wako vizuri.

Wapi Uhuru kanisurika tear gas?

Polisi wameelewa somo na kuondoka.

Wajameni shida iko wapi?
 
Back
Top Bottom