Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 313
Serikali imewapokonya Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga na Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka walinzi dakika chache zilizopita.
Aidha Wabunge sita akiwemo Opiyo Wandayi vilevile wamepokonywa walinzi.
Kawaida Viongozi wa ngazi za juu serikalini wanapostaafu hupewa walinzi kwa ajili ya usalama wao.
Hatua hii inakuja baada ya Viongozi mbalimbali wa serikali kumuomba Inspekta Jenerali wa Polisi Japheth Koome kuwapokonya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, Raila Odinga na Kalonzo Musyoka walinzi wao, kwa tuhuma kuwa ndio wafadhuli Wakuu wa vuguvugu la maandamano linaloshuhudiwa nchini.
Aidha pia kuna wito mkubwa kutoka kwa Wabunge wa Kenya Kwanza kumokonya Uhuru Kenyatta mafao yake ya pensheni.