Je, ni kweli Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ndiye mfadhili mkuu wa maandamano au ni 'cheche' za Serikali tu

Kenyan

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
414
313
Kwa muda sasa Viongozi wengi wanaomuunga mkono Rais William Ruto wamekuwa wakimkemea Rais mstaafu Uhuru Kenyatta wakidai ndiye mfadhili mkuu wa vuguvugu la maandamano linaloshuhudiwa Kenya.

Madai haya yamezua maswali mengi miongoni mwa watu wengi ikizingatiwa kuwa Viongozi wengi wanaomkemea Kenyatta wanatokea kaunti zilizoko Mkoa wa Kati anakotokea Rais Kenyatta. Kwa lugha nyepesi (na wala sikusudii kuingiza nukta ya ukabila hapa), Wakikuyu wenzake wamekuwa wakimkemea Aliyekuwa ndiye Kiongozi wao Mkuu. Bingwa wa Kabila Hilo.

Ni Jana tu Jumapili ambapo Waziri wa Biashara na Uwekezaji Moses Kuria, ambaye anatokea Jimbo sawa na Rais mstaafu Kenyatta alimweleza maneno yafuatayo katika tamasha Moja kaunti ya Kiambu:

"Wewe Uhuru Kenyatta kubali tulikushinda wewe na Mzee wako Odinga. Achaa kutusumbua. Na ukicheza na Mimi nitakuja nyumbani kwako nikojoe kwenye geti na hakuna lolote kubwa utanifanyia Mimi." Alisema Moses Kuria kwa lugha ya Kikuyu ambayo ndiyo lugha ya kwanza ya Uhuru Kenyatta.

Ikumbukwe pia yapata wiki chache zilizopita Shamba la Uhuru Kenyatta la Northlands lililoko kaunti hiyo hiyo ya Kiambu lilivamiwa na watu wasiojulikana na kuondoka na mamia ya mbuzi.

Madai yote haya hasa kutoka kwa waliokuwa waandani wake wa karibu tena wa kutokea kabila lake ambalo Mila na tamaduni zake ni tofauti kabisa na kabila analotokea Rais Ruto yanaibua maswali haya muhimu:

(a) Iweje Viongozi wa kabila la Kikuyu Wadai Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, Mkikuyu mwenzao, ndiye anafadhili vuguvugu la maandamano kwa kumtumia Raila Odinga?

(b) Iweje bado Rais Uhuru Kenyatta bado anatekeleza wajibu wake wa kuongoza ujumbe wa kusaka amani DRC, kazi aliyopewa na Rais Ruto na akaridhia kufanya?

(c) Iweje Kenyatta hajawahi kujitokeza hadharani na kulaani maandamano?

(d) Iweje Kiongozi Mkuu kama Raila Odinga akaridhia kutumika na Mwanasiasa aliyewahi kushindana naye mara mbili kusaka kiti cha urais 2013 na 2017 bila kufanikiwa?

Maswali ya mwisho mawili nitayaweka hivi;

(e) Iwapo ni kweli Uhuru Kenyatta anayafadhili haya maandamano, lengo lake Kuu la mwisho ni lipi hasa?

(f) Iwapo si kweli, Je lengo la Raila basi ni lipi ikizingatiwa alipataa uungwaji mkono wa Rais Aliyekuwa akiondoka lakini akagonga mwamba.

Nimehisi ni busara nihoji mambo yote haya kwani sio jambo dogo kwa uongozi ulioko madarakani kudai Rais aliyewakabidhi madaraka anapanga njama kubwa ya kuwahujumu, tena kwa kumtumia Kiongozi mwandamizi wa Upinzani Raila Odinga, ambaye pia anajivunia kuwa na mamilioni ya wafuasi kote nchini.

Natanguliza shukran
 
Back
Top Bottom