HOJA MBADALA: Tuhamasishe CCM imsimamishe Membe 2015?

HOJA MBADALA: Tuhamasishe CCM imsimamishe Membe 2015?

Nadhani kwa kuwa alikuwa huko USA mtakuwa mmeonana na amekusainisha rasmi. Kwa sasa umeanza kazi kwa kuja kupima upepo hapa jamvini ili ujue wapi uanzie kibarua chako.

kweli unafikiri ana ubavu huo?
 
kweli unafikiri ana ubavu huo?

Why not? Kama umefikia hatua ya kumpa hadhi ya Presidency material bila kutupa sifa zinazotuthibitishia pasi na shaka kwamba anaweza kukalia kiti hicho na kwamba hana kashifa ya ufisadi kwa nini tusiamini kuwepo wa kikao baina yako na yeye huko USA? Ni suala la muda tu.
 
Ni bora kumchagua fisadi Lowassa mwenye maamuzi na sauti,kuliko Membe goigoi na mfuata upepo. tutakua tunakaribisha miaka kumi mingine ya kuipoteza nchi yetu..maana hapa tulipo jk nchi imemshinda tupo mteremkoni na breki zimekatika..2015 tunahitaji raisi ambaye ataweza kuokoa nchi isidumbukie korongoni, kama mtu mwenyewe ndio Membe basi itabidi nianze mapema kuililia nchi yangu Tanganyika.!
 
Why not? Kama umefikia hatua ya kumpa hadhi ya Presidency material bila kutupa sifa zinazotuthibitishia pasi na shaka kwamba anaweza kukalia kiti hicho na kwamba hana kashifa ya ufisadi kwa nini tusiamini kuwepo wa kikao baina yako na yeye huko USA? Ni suala la muda tu.

mnawaendekeza sana; ni wapi nimesema kuwa ni "presidential material"? usije kuwa unafikiria kuwa mgombea wa CCM ni presidential material.
 
Mkuu Mkandara: Tafadhali angalia hapo nilipoweka red!! Kwa kutumia hiyo kauli mbiu inaashiria ufanisi bora? Hili la kusema kuwa wanawake wakiwezeshwa wanaweza bado ni kitendawili kwa hapa Tanzania. Wanawake watendaji wamewezeshwa kielimu na kwa semina elekezi lakini mazingira ya kazi si rafiki kwao. Je wanawake walio madarakani wamewezaje kuwakomboa wananchi kutokana na mateso ya umaskini, ujinga na maradhi. Tuchukulie mfano wa wabunge, viongozi wanawake kwenye mawizara, wakuu wa mikoa na wilaya na wakurugenzi wa wilaya hivi wameonyesha utendaji uliotukuka tofauti na wanaume wenye nafasi kama hizo? Swali moja tu je, ubadhirifu wa mali ya umma haupo kwenye sehemu ambazo wanawake wanaongoza? Bila kubadilisha mfumo uliopo hata wanawake wakipewa nafasi zote za uongozi bado ni tabu na shida tu.
Dah mkuu wangu mimi natoa tahadhari tu sio navyoamini miye. Unajua ktk mijadala siku zote unatakiwa mtu ujitoe pembeni halafu utazame ile picha ukutani na kuizungumzia. Hivyo nachosema mimi ni jinsi wanawake wanavyoweza kutumia kauli mbiu ya - Tukiwezeshwa, Tunaweza. Walifanya hivyo bungeni na wakapewa viti maalum. Je, walifanikiwa kupata viti japokuwa watu hawakubaliani na nadharia hiyo? Jibu litakuwa NDIO walifanikiwa yanayofuata ni baada ya ushindi.. Hivyo tazama kwanza uwezekano wa ushindi kwa kupitia kumsimamisha mwanamke wa kwanza, kauli mbiu, nafasi ya Umoja wa wanawake ktk jamii na si uwezo wa AshaRose..

Ebu nambie Mkapa au JK walipita uchaguzi kwa vigezo gani?. wameweza kuondoa Ujinga na Umaskini? - laa! na hakuna isipokuwa wametupiga bao kwa maandalizi na UONGO UNAOKUBALIKA. Na sijasema AshaRose Migiro atakuwa rais atakayetufaa! isipokuwa ni mtu ambaye anaandaliwa kuwaletea Ushindi CCM mwaka 2015 and thats all what they need - Ushindi. Kumbukeni tu ya kwamba huwezi kumchagua mtu ambaye ni msafi, hodari na mchapakazi lakini hana Umaarufu mtashindwa uchaguzi na mkishindwa mtasubiri miaka 5 ijayo na pengine isirudi tena. Maswala ya kuwaletea wengine maendeleo hufuata baada ya kushinda..

Hivyo ndani ya chama kuhusu Uchaguzi USHINDI ndio picha mbele yenu. Swali kubwa huwa Kati ya wagombea wote ni nani ataleta Ushindi na kwa sababu gani ili mbinu na propaganda za kutafuta kura ziambatane na mgombea. Hiki ndio nachozungumzia miye sio uwezo wa mtu kama anatufaa Watanzania. Binafsi yangu kama alivyosema Nguruvi3, namtafuta kiongozi ambaye ataweza kurudisha UMOJA wa Watanzania, kurudisha sifa ya UTU wetu na sio mtu yeyote atakaye tugawa zaidi. Bila shaka chaguo langu atatoka Chadema au Upinzani..
 
si ccm si chadema c kafu hakuna mtu wa kuwa rais pale,its beta tukawa bila rais kama sasa hivi na maisha yakaenda,,,,,membe atauweza uraisi wakat kajimbo kake kanamshinda?????
basi simama wewe mkuu!maana naona hujui maana ya taifa wala hujui maana ya familia!!!wa wapi wewe mkuu,duh,pole tanzania.
 
Mkuu Bajabiri, hii inaitwa "negation"!, kukanusha kitu ambacho ni facts!.
Huwezu kukanusha hard facts ili tuu ku ji please nafsi yako!.
  1. CCM ni chama cha siasa chenye usajili wa kudumu, na ndicho chama klilichopata certficate of registration as Nambari One Tanzamnia political Party!. This is a fact, you can't deny it!, unless ni kujifurahisha!.
  2. CCM ndicho chama tawala Tanzania kwa sasa, uwe ulikichagua or not, CCM ndicho kinachotawala and this is a fact!, you can't deny it unless unajifurahisha!.

Mkuu Bajabiri na wengine, tujenge utamaduni wa kuwa wakweli toka kwenye nafsi zetiu kwa kuzikubali hard facts
kuwa CCM ni chama, kipo, ndicho chama tawala!, sasa suala la kuendelea kuwepo baada ya 2015, au kuendelea
kutawala baada ya 2015, hivyo ndio debatable subject subject based on political probabilities!.

P.

Hilo la CCM kuwa chama kinachotawala lina ugumu gani kulielewa hilo? Wala halihitaji kupigiwa debe kama unavyofanya. Ukishaona mwanaume anarudia rudia yeye ndiye mume na baba hapo nyumbani ujue kuna mushkeli katika kukubalika kwake. Ana tatizo. Anyway CCM ndicho chama kinachoiongoza nchi 'fine'. Kipo katika jitihada za kujibakisha madarakani 2015 kama chama chochote cha siasa ambavyo kingefanya 'fine'. Swali ni hili (na pengine uliyekuwa unamjibu alilenga hapo) CCM baada ya hayo iliyoyafanya inataka kujibakisha madarakani 2015 kwa maslahi ya nchi au ya chama? Ikiwa ni kwa maslahi ya chama wanayo sababu nzuri. Na wakilisema hilo wazi wazi angalau kwa mara ya kwanza wataonekana wamesema ukweli. Lakini ikiwa wanajibakisha kwa maslahi ya nchi wana kibarua kigumu kuipeleka hiyo hoja kwa wananchi. Wanamhitaji mtu mahiri aliyejitofautisha nao (kama alivyokuwa Mrema alipogombea uraisi) anayeweza kuwashawishi kuwa hautafuti uraisi ili kuwalinda walaji wenzake.

Wampate wapi mtu kama huyo katika CCM kwa wakati huu? Pengine hilo ndilo swali la Mwanakijiji ambalo amelileta kwa namna isiyoeleweka vizuri kwa wengine. CCM imeendelea kupungukiwa na watu wenye sifa hiyo. Siyo kwamba hawakuwa nao. Walikuwepo kina Mwakyembe, Mwandosya, Lowassa, Sitta, Magufuli n.k. ambao ukiwaona na kuwasikiliza unapata matarajio kuwa hawa wanaweza kutuvusha hapa tulipokwama. Lakini kadri siku zinavyokwenda wanapungua kwenye mizani. Watu wasioguswa katika kashfa zinazofahamika sana huenda ni hao kina Membe, na huyo dada yetu Migiro. Lakini hawa wakipanda jukwaani na kwenye midahalo ya uchaguzi watahimili vishindo mbele ya watu machachari wasiotabirika kama Dr. Slaa (sijajua kama ndiye atakayesimamishwa na CHADEMA) au Tundu Lisu au hata Kibamba yule mwanaharakati - watu wenye uwezo wa kupanga hoja na kuzitoa kwa kasi ya ajabu?

Mtu hahitaji kumpigia debe Lowassa kwa sababu kwa vyovyote vile iwavyo ndiye mtu anayekubalika na wana CCM kwamba anaweza kuhimili mikiki ya kampeni za uchaguzi (kama asingekuwa amechafuka) na ambaye atalinda madudu yaliyofanywa na wanaoondoka kwa makubaliano ya kuweka kando ile sera ya kuvua gamba na kuanza kumsafisha kwa matarajio ya 'kukinusuru chama'. Nani anataka kupelekwa 'The Hegue' Na kama njia ya kuepuka huko ni kumwandaa mtu anayekubalika hata kama anasafishika kwa taabu nani hatajaribu njia hiyo. CCM watatafuta mtu atakayewaponya kwa hayo na mengineyo wakilenga maslahi yao zaidi. Wenye sauti ya mwisho watakuwa wananchi ambao watanunuliwa kadri wanavyoweza kununuliwa, watatishwa kwa kutumia vyombo vyote vya dola, na kuibiwa kura kutumia mfumo ule uliotumika huko nyuma ukiwa umeongezewa ustadi.

Ikiwa wananchi wameelimika vya kutosha (na mimi naamini wameelimika) na kuamua kushikamana kwa gharama yoyote ile dhidi ya mikakati hiyo niliyoitaja patatokea mlipuko mkubwa. Utakuwaje na utafanana na nini ni mapema sana kujua. Ila ukweli mmoja unabaki. Wanaotaka kung'ang'ania kutawala wakiwa hawatakiwi wasidhani kazi hiyo ni rahisi. Itawagharimu. Na wale wanaotaka kuwaondoa watawala wasiotakiwa na umma wasidhani kuwa kazi hiyo ni nyepesi. Itawagharimu.

Silaha ya walio madarakani ni nguvu ya dola katika kutumia mabavu, kununua watu na kuiba kura. Nguvu ya wanaotaka kuwaondoa walio madarakani ni NGUVU YA UMMA. Anayetaka kushinda kupitia nguvu ya Umma ana watu wengi nyuma yake na ana Mungu upande wake. Anayetaka kushinda kupitia watawala, ana nguvu ya dola ambayo haijashikamana (nusu chuma nusu udongo) na fedha za kununulia watu na kura. Lakini kwa kuwa watawala wana makundi yanayoendelea ndani yao makundi hayo yatamhujumu sana huyo atakayepitishwa kama ilivyotokea kwa mgombe ubunge wa kule Arumeru. Awe Lowasa, awe Mkapa awe nani atahujumiwa tu na wenzake. Mgombea sahihi wa CCM anatakiwa awe mtu anayekubalika na makundi yote yanayohasimiana ndani ya chama kwanza ndipo sifa zingine za uadilifu zifuate. Mtu huyo yupo?
 
mwambei huyo,,,,,ishu si kashfa ishu ni uwezo,,,,,,,kwa hiyo kama hana kashfa awe rais,,,,duh.
Basi hata KOMBA hana kashfa ya rushwa
Mkuu kwa style Hii tutaambiwa hata Ndugai anafaa kuwa Presidential material
 
Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?
Mkuu MM, vp Ndugai
 
mnawaendekeza sana; ni wapi nimesema kuwa ni "presidential material"? usije kuwa unafikiria kuwa mgombea wa CCM ni presidential material.

Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?

Hapo kwenye red, Unasema Membe yuko safe kwenye mlolongo wa kashfa za Ufisadi. How? Can you prove? Sasa kama hujatuletea ukweli wa usafi wake katika hili na kwa kweli ukweli tupu (Maana tumeshoka na UFISADI) utaanzaje kumpigia chapuo kati ya wengine?

Unaposema miaka hii iliyobaki akijiandaa anaweza kuwa na Presidential material na unasema anaweza kushinda maana yake nini? Automatic you see Membe as a true presidential candidate hayo masuala ya yeye kujipanga hayawezi kumshinda MMKJJ
 
pasco is opposition hater from the start..hivi huyu ni mwandishi wa gazeti gani anyway,i hear stories that he is a journalist
Mkuu Nyabhingi, I hate opposition vibaya sana!. I love CCM from the bottom of my heart na hizi hapa chini, ni baadhi ya thread zangu nilizo zianzisha ili kuifagilia CCM!.
Yes Pasco wa jf is a journalist reporting for jf!. Yaani gazeti ninaloliandikia ni media inayojulikana kama jf. Nimeripoti matukio mengi tuu humu ukiwemo uchaguzi mkuu!.

Need more?.

Pasco.
 
hivi huyo atakayempa Membe urais atakuwa ni kichaaaaaaaaaaaaaaa.....jaman nyie mlioleta hii mada ata kama membe anawapa pesa za kuishi anazopora nchi msimdanganye awe rais kwa sifa zpi hiv mmeshawahi kufka jmbo la mtama na kuona jinsi ufukara ulivyoipindukia na jmbo lenyewe ni dogo,elmu duni,huduma za afya ,barabara etc..nani aliyewaloga enyi wagalatia..membe ata ubunge haumfai kwanza ata dini yake ya ukrsto ameiasi na kuslimu...na ni kinara mkubwa wa kupgia DEBE tanazania kujiunga OIC umoja wa nchi za kiislam(Zinazoongozwa kwa kupitia SHARIA Inayopiganiwa na BOKO HARAMU NA ALSHABAAB Kuingzwa ktk nchi zao ambazo hazitak mfumo huu kandamizi ambao mwanamke haruhusiwi kutawala ata kijiji na wanafunz wa kike hawaruhusiw kwenda shule na mitaala ya shule ifate sharia(quruan),ata waislam wengne hawaitak ila membe aliyehasi ukrsto anaitaka...hiv mna habari kuwa cardnal alshamfukuza ofsni kwake alpotaka kumpelekea hii ajenda ya Tanzania kujiunga na IOC...Tumuepukee Membe kama ukmwi ni ndumilakuwili atatuuza oman.
 
naheshimu michango ya MM, humu JF bt kwa hili mzee umeenda chaka
 
Mkuu Mwanakijiji,Subiri kashfa ya pesa za Libya ndio utawajua vizuri wanasiasa wetu wana sura gani ni mapema mno kumjadili huyu nyoka wa mdimu.Ni bora mchawi Lowasa tumkabidhi mwana.

Hiki kinachoitwa kashfa ya fedha za Libya tumeisubiri muda mrefu lakini nafikiri huyo producer wa hiyo filamu mitambo yake imeungua na umeme wa Tanesco. Niwaambie hivi, and you can take this to the bank, Membe has what it takes to be the next President na kama kuna wanaodhani uadilifu siyo sifa ya uongozi basi labda mnazungumzia uongozi wa Freemasons au kwa TB Joshua. For once Mwanakijiji umeona mbali!
 
Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?

Mkuu,Mbona unaturudisha kulre kule tena?hatujadili tena ni platform gani itatoa candidate tumeamua kwenda easy way out kwa kujadili candidates?

Membe anasimamia nini tofauti na hao wengine?Je kashfa itatumika kama kigezo?Ninahofia kama suala ni kuchafuaka ama la basi 2015 hata huyo Membe atakuwa kama aliyetoka kwenye sewage kwa siasa zetu hizi
 
Nawashauri, wale wote, wenye mapenzi mema na taifa hili, lets rally behind EL, or Membe for CCM candidate, 2015, ili taifa letu lipate, ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

EL for 2015!, if not then Membe!.

Hivi unaposema hayo maneno hapo ktk red huwa una maana gani? Aaaaaaggggggg
 
mwambei huyo,,,,,ishu si kashfa ishu ni uwezo,,,,,,,kwa hiyo kama hana kashfa awe rais,,,,duh.
Basi hata KOMBA hana kashfa ya rushwa

Issue ni kuwa na uwezo, mwadilifu asiyekuwa na kashfa.
 
Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?
Kwa kweli mkuu umepoteza heshima yangu Kwako.
 
Back
Top Bottom