HOJA MBADALA: Tuhamasishe CCM imsimamishe Membe 2015?

HOJA MBADALA: Tuhamasishe CCM imsimamishe Membe 2015?

Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?
Mzee Mwanakijiji, red on bold umeisemea vizuri. but on the blue marked, hatuko tayari kujiunga na oic
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwanza asante kwa sasa kukubali ukweli halisi kuwa determinant factor ya ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, lies with mgombea wa CCM na ndio maana mimi siku zote nimempigania EL!, na nikasema wazi, kama sio yeye then ni Membe!.

Siku zote nimempigania EL nikiamini he is the one and only asset ya kuinusuru kifo CCM, 2015!. Lakini baada ya kuisoma ile "safety net" ya bilioni 400, nimekubali matokeo kuwa 2015, ni CCM tena, with or without EL!. Hivyo by now EL is not an asset anymore!, has turned into a liability, just waiting to be dispossed off!. Mimi niliamini wange tumia nyundo ya ujumbe wa NEC kumcrush off!, kumbe wamerealise wafuasi wake lukuki!, the need them kwanza awa rally behind Membe ndipo "disposal" process ifuatie!.

Kwanye ule mtandao wa JK wa 2005, RA was not the brain behind, he was just a "cash cow"!. Kinana was just a figure head!, there were "the opparatives" who were the "think tank"!. Nikiwa Dodoma juzi kwenye budget ya Membe, nimewaona hawa "opperatives" wamesha ji "line up" behind Membe!.

Miongoni mwa silaha kubwa kabisa za kutumia ni "the control" of "print media"!. Ile elevation ya "mwana jf mwenzetu" aliyoipata toka "mbeba mikoba wa Membe" turned into a "print media regulator", "overningt"!, sio kwa mahati mbaya, its a part of the plan!. With "print media" on safe hands!, e-media doesnt matter much!. The the man for 2015 is "Membe"!.

Nawashauri, wale wote, wenye mapenzi mema na taifa hili, lets rally behind EL, or Membe for CCM candidate, 2015, ili taifa letu lipate, ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

EL for 2015!, if not then Membe!.

Pasco.

Mkuu Pasco kuna tatizo hapa.

Look, to be a Print Media regulator does not guarantee someone presidency or whatever the glory. Serikali na hata CCM yenyewe ndiyo regulators wenyewe kwa sasa lakini tunaona nini kwenye media? Unataka kuaminisha kwamba, kuwa regulator basi utaamka asubuhi na kufungia magazeti yaliyo against Membe? Au utahakikisa Membe aandikwe vizuri tu? Don't forget the media indutry is much diversified in such a case it has ownership complexity with different ideological and interests stands. Sasa sidhani kama kuwa na Rugulator wa Print media basi ni guarantee ya kuwa rais.Lakini pia kama ni suala la media control hata Wagombea wengine wanaweza si Membe peke yake.

Lakini, sidhani kwa Dunia ya sasa na mabadiliko ya ICT yaliyoikumba Tanzania siku za karibuni unaweza kusimama na kupuuza nguvu ya e-media. JF tu ina members karibu 100,000, hatujazungumzia FB, Twitter, BBM, Quepassa nk. nk. Ni wazi e-democracy ni kubwa kwa sasa hapa nchini hasa baada ya simu nazo kumwagika kwa kasi. Unaweza kuzungumzia Watanzania wengi si consumers wa e-media lakini nakuhakikishia nguvu yake kwa sasa si ya kupuuza. Uchaguzi mdogo wa Arumeru East ulinipa somo kubwa sana kuhusu hili.
 
Comrade,kwa wakati huu sio wakati wa kuwa na raisi tena kutoka mabwepande. Kumbuka wasaidizi wake ni wale wale. wewe unataka kuniambia membe anaamika zaidi kuliko alivyoaminika chaguo la Mungu??????????? Si unajua chaguo la Mungu aliaminika mpaka basi, leo sijui amegeuka kuwa chaguo la shetani!!!!!! Kumbuka mabwepande wanasema wasaidizi wake ndio wanaomuangusha!!!!!!!!!!!!!!sasa kuna sababu gani kujadili hoja ya Membe wakati wasaidizi watokanao na sisiem sisiem watamuangusha? jadili namna gani wanainji watafanya mageuzi kama ilivyokuwa Zambia over yeras ago na juzi kwa Satta, Kenya na Malawi. Tumebaki Tanzania na Uganda.
 
Nina uhusiano na Membe? naomba muweke wazi ili watu wajue. You HAVE MY PERMISSION, DARING AND BLESSING.

Nadhani kwa kuwa alikuwa huko USA mtakuwa mmeonana na amekusainisha rasmi. Kwa sasa umeanza kazi kwa kuja kupima upepo hapa jamvini ili ujue wapi uanzie kibarua chako.
 
mzee mwanakijiji's independence is being impaired...
 
pasco is opposition hater from the start..hivi huyu ni mwandishi wa gazeti gani anyway,i hear stories that he is a journalist
 
Kuna ile KANUNI iliyojificha ya CCM ya kumteua mgombea URAIS wa Tanzania kutoka jamii ndogo za Kitanzania. Kama kanuni hiyo bado inatufaa katika mazingira yetu tuendelee nayo tu. Kanuni hiyo inampitisha Membe moja kwa moja kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CCM.

Ninaposema jamii ndogo nina maana kabila ndogo zisizo na nguvu kubwa za kiuchumi, kielimu, kidini na kitabaka. Kanuni hii imechangia vizuri kupunguza ukabila na udini nchi hii. JIrani zetu hapa Kenya linawapa taabu sana hili. Wakikuyu hawaelewi mtu wa kabila ingine kuwa Rais wa Kenya.

Sio siri kwamba baadhi ya watu hawawezi kuhimili nguvu kubwa ya makabila na dini zao. Tuwaepuke hawa kama ukoma au ukimwi.
 
You always act as if you were a lecturer in jf,always attacking members capability to analyse issues,..mr.know it all
 
Oh! please..here we go again. can you cut the bull...for once!
 
Kuna thread ambayo ilikuwa inahusu urais 2015. Mwanakijiji alichangia, sikumbuki vizuri neno kwa neno lakini alikuwa against Membe kwamba tunataka kurudia makosa tuliyoyafanya 2005.

Hapa ni kutafuta ukweli wa maoni ya watu wengine.
 
Maoni ya Mwanakijiji kwenye thread nyingine dhidi ya Membe ni tofauti kidogo na nilichosema hapo juu.Alichokiandika
Membe angeweza kabisa (kama angetaka) kutengeneza mechanism ya kuspring kuelekea Urais. Bahati mbaya sana amechagua njia isiyo sahihi sasa hivi na hii support inayotengenezwa itatuleta kwenye matatizo ya mwaka jana au 2005. Ninafuatilia vizuri sana wigo la support yake inatoka wapi - japo najua kwanini. He will have to deal with IT.
 
Naona itawasaidia sana cdm kushinda! Hizi enzi si tu mtu anabebwa na chama kama ilivyokuwa kwa Mkapa "95, bali pia mtu nae anakibeba chama kama Dr Slaa "10! Membe doesnt fit in any how!

kwanza membe ni m2 wa visasi!, hawezi kuongoza nchi. Membe ni uchochoro wa cdm kushika nchi.
 
Membe anaweza kulete maafa zaidi ya jk maana huyu jamaa sijaona msimamo wowote alionao kweli hana kasoro nyingi lakini kutokana na na kutokuwa na misimamo imara ndio kigezo kitakachoiweka tena nchi rehani mwa mafisadi kama EL, RA, AC aka gwiji la Bariadi
 
Badilisha heading iwe CCM tuhamasishe...... kwa sababu sisi tusioipenda CCM Hatuna mchango hapo kwa sababu CCM wote ni walewale hakuna wa afadhari.
 
Tutaona mengi ya wanaotafuta ulaji 2015. Watu kama MM wanapenda kuandika kwa staili inayoficha misimamo yao na kujifanya kuwa 'great thinkers' wameelewa, ila wasiyo na 'great thinking capabilities' hawajaelewa. Hakuna 'rocket science' hapa, hii iko wazi, umri umesogea na matumaini yenu yako ukingoni na hapa mnatapatapa tu.

MM na wenzako, speculation zenu ziko wazi, msifikiri hamuonekani kwa sababu ninyi hamuoni. Mmeficha vichwa vyenu kwenye nyasi na viwiliwili vyenu viko hadharani. Mnatafuta pa kushika ili 2015 kieleweke. Desperation zenu zitawapeleka kwenye 'dead end'.

Si unaona jamaa yenu WM anavyohaha, mara EA, mara DSM, uchuro tu wa kutafuta ulaji kwa kujificha kwenye maandishi. kha!!!
 
Inaonekana kwa uchangiaji wa hii mada kuna watu wanataka CCM iweke mtu ambaye atamshinda mgombea wa CHADEMA!!Hili ni Jambo la ajabu kabisa!!
 
Back
Top Bottom