HOJA MBADALA: Tuhamasishe CCM imsimamishe Membe 2015?

HOJA MBADALA: Tuhamasishe CCM imsimamishe Membe 2015?

Membe anaonekana anaweza lakini affiliates wake je? decendant wa nani? kusave interest za nani? hapo ndo shughuli. Kama Jk akiweza kuweka mgombea basi Membe sawa, lkn je? ndani ya ccm watalikubali hilo? na wananchi watakubali tawi la JK litawale? akifaulu hapo mi sidhani.

Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?
 
"Nyoka wa Mdimu" awe Rais si tutakufa wote...Kasomea kufitinisha na ufitinishaji plus kujikombakomba pengine atawafaa MAGAMBA wasiaibike sana 2015...
 
Ukishamaliza huko kwa Membe kumpigia kampeni, uje umuhamsishe na Shibuda kuja kugombea Urais kupitia CDM.
 
Mzee Mwanakijiji,
Sintopendekeza mtu isipokuwa kwa manufaa ya taifa na japokuwa Membe ni kichwa, muweza ukiachana na habari za Ufisadi wake maana huko CCM hakuna msafi kihivyo. Wayahudi walilaaniwa tena na Mungu mwenyewe lakini bado wanaitawala dunia.

Hivyo pamoja na utetezi wako bado nakuhakikishia kwamba CCM wataweza tu kushindana ikiwa watamsimamisha Asha Rose Migiro na hii itatokana na WANAWAKE kutumia kauli mbiu ya TUKIWEZESHWA TUNAWEZA. Itakuwa sio swala la chama bali wanawake against the rest...Na amini maneno yangu watu hawatatazama tena nyuma wala kutazama uwezo wa AshaRose isipokuwa ni mageuzi ambayo kwao yatawalemaza akili..

Kwa upande wa ushindani na hasa Chadema wanatakiwa kuanza mapema sana kumtafuta na kumwandaa mgombea japo kwa siri lakini nawatahadharisha mapema - KAZI IPO 2015 wajipange mapema na vizuri sana laa sivyo itakuwa aibu maana elimu ya Uraia haijazama vichwani mwa wananchi hivyo SHIDA na MATATIZO yanatangulia Mapenzi yao..
This might be out of topic ila hapo kwenye red umeongea kinyume chake...
Wanao walaani Wayahudi ndio wana laaniwa....
 
duuuh mkuu nahisi umekosa topic ya kupost kumsimamisha membe itakuwa bora hata arudi white hair

Naona labda hujamwelewa; Angalia scenarios hapa;

Slaa/ZZK/Mbowe Vs White Hair/Membe/Mwandosya/Sumaye/Sitta/Mwakyembe
Slaa/ZZk/Mbowe Vs White Hair/Membe/Mwandosya/Sumaye/Sitta/Mwakyembe
 
Sidhani kuwa CCM inachukiwa kwasababu ya Rais fulani, kinyume chake Rais amebaki kuwa anapendwa na CCM inachukiwa.Chuki dhidi ya CCM si kutokana na watu au haiba zao, si kutokana na sera, ni kutokana na mfumo uliokiuka maana nzima ya chama, kanuni, taratibu na sheria n.k.
Chuki dhidi ya CCM ni kutokana na chama kupoteza umiliki wa wananchi kwa kundi dogo lenye nia tofauti na ile ya CCM.

Uchaguzi wa 2015 hautaongozwa na sura au kashfa za mtu mmoja mmoja. Utaongozwa na dira ya kitaifa na mtazamo.
Kikubwa zaidi ni kuchoshwa kwa wananchi na kundi teule kuiweka nchi ilipo kwa miaka 50.

Hakuna kiongozi aliye ndani ya CCM au serikali yake anayeweza kuja na hadithi tofauti.
Membe kama walivyo wengine hajaweza kusimama katika masilahi ya taifa.
Hajakwepa kashfa kwasababu anaposhindwa kuueleza umma nini kimetokea kwa kujificha nyuma ya bunge na serikali hana maadili, uthubutu au utashi wa kisiasa.

Lakini hatuhitaji kiongozi wa uchumi na siasa tu, tunahitaji kiongozi atakayewaunganisha Watanzania na kurudisha Tanzania isiyo na makundi ya kikabila au kidini. Membe ameshindwa mtihani huo kwa kuanzia.

Naamini kuwa ili CCM ijirudishie hadhi ni lazima mgombea wa 2015 atoke nje ya 'system' iliyopo.
Na sidhani kuwa ni suala la nani atakuwa rais, bali chama gani kinaweza kututoa hapa tulipo!
 
NI vizuri watu wakasoma actually nimeandika nini... maana wengine wanachangia wakidhania kuwa nimeandika nini.

hapa mzee unajikosha tu, lakini within the context, we know who you are and what you actually meant katika andiko lako la kwanza, kuna watu walikuwa wanakusubiri kwa hamu sana provided that you have started showing your hidden agenda, the saga is with you wait a bit. TANZANIA Si Kiongozi, ama Tajiri, ama Mchambuzi nguli( mwanakijiji), ama CCM ama UPINZANI, ama Masikini ambaye ni wa kumwamini wengi wao wanahubiri , kuishi na kusema wasichokiamini ndani ya mioyo yao.
 
Kaka mara hii umeishakachuliwa hadi kuwa kuwadi wa mafisadi kama si nepi yao? Huyo Membe amekupa nini hadi umzimie na kumuabudia hivyo ndugu yangu? Kweli adui yako muombee njaa na penye udhia penyeza rupia. Yaani mihemko yako yote ya miaka yote umeishia hapo? Kwanini siku hizi watu wanashabikia uchanguuu hadi kwenye mawazo yarabi? Heri ungenyamaza kuliko kuvua nguo mtoni usijue kuna watu. Heri kuamini kwenye unachohubiri hata watu wakakucheka kuliko kuramba matapishi yako. Pole sana bwana mdogo. Je huduma yako unauza bei gani?

Kila mtu ana bei yake inapofika huwa ananunuliwa...
 
Membe atatupotezea muda watanzania,tuweke pembeni hisia dini,rangi,kabila,jinsia na muonekano wa mtu.Tunapaswa kufikiria jinsi ya kupata kiongozi ambae atatutoa katika taifa lililoanza kujengwa katika hali manunguniko na kukata tamaa aje kiongozi atakaelijenga taifa letu imara lenye matumaini na maendeleo.
 
Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwanza asante kwa sasa kukubali ukweli halisi kuwa determinant factor ya ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, lies with mgombea wa CCM na ndio maana mimi siku zote nimempigania EL!, na nikasema wazi, kama sio yeye then ni Membe!.

Siku zote nimempigania EL nikiamini he is the one and only asset ya kuinusuru kifo CCM, 2015!. Lakini baada ya kuisoma ile "safety net" ya bilioni 400, nimekubali matokeo kuwa 2015, ni CCM tena, with or without EL!. Hivyo by now EL is not an asset anymore!, has turned into a liability, just waiting to be dispossed off!. Mimi niliamini wange tumia nyundo ya ujumbe wa NEC kumcrush off!, kumbe wamerealise wafuasi wake lukuki!, the need them kwanza awa rally behind Membe ndipo "disposal" process ifuatie!.

Kwanye ule mtandao wa JK wa 2005, RA was not the brain behind, he was just a "cash cow"!. Kinana was just a figure head!, there were "the opparatives" who were the "think tank"!. Nikiwa Dodoma juzi kwenye budget ya Membe, nimewaona hawa "opperatives" wamesha ji "line up" behind Membe!.

Miongoni mwa silaha kubwa kabisa za kutumia ni "the control" of "print media"!. Ile elevation ya "mwana jf mwenzetu" aliyoipata toka "mbeba mikoba wa Membe" turned into a "print media regulator", "overningt"!, sio kwa mahati mbaya, its a part of the plan!. With "print media" on safe hands!, e-media doesnt matter much!. The the man for 2015 is "Membe"!.

Nawashauri, wale wote, wenye mapenzi mema na taifa hili, lets rally behind EL, or Membe for CCM candidate, 2015, ili taifa letu lipate, ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!.

EL for 2015!, if not then Membe!.

Pasco.
 
Sidhani kuwa CCM inachukiwa kwasababu ya Rais fulani, kinyume chake Rais amebaki kuwa anapendwa na CCM inachukiwa.Chuki dhidi ya CCM si kutokana na watu au haiba zao, si kutokana na sera, ni kutokana na mfumo uliokiuka maana nzima ya chama, kanuni, taratibu na sheria n.k.
Chuki dhidi ya CCM ni kutokana na chama kupoteza umiliki wa wananchi kwa kundi dogo lenye nia tofauti na ile ya CCM.

Uchaguzi wa 2015 hautaongozwa na sura au kashfa za mtu mmoja mmoja. Utaongozwa na dira ya kitaifa na mtazamo.
Kikubwa zaidi ni kuchoshwa kwa wananchi na kundi teule kuiweka nchi ilipo kwa miaka 50.

Hakuna kiongozi aliye ndani ya CCM au serikali yake anayeweza kuja na hadithi tofauti.
Membe kama walivyo wengine hajaweza kusimama katika masilahi ya taifa.
Hajakwepa kashfa kwasababu anaposhindwa kuueleza umma nini kimetokea kwa kujificha nyuma ya bunge na serikali hana maadili, uthubutu au utashi wa kisiasa.

Lakini hatuhitaji kiongozi wa uchumi na siasa tu, tunahitaji kiongozi atakayewaunganisha Watanzania na kurudisha Tanzania isiyo na makundi ya kikabila au kidini. Membe ameshindwa mtihani huo kwa kuanzia.

Naamini kuwa ili CCM ijirudishie hadhi ni lazima mgombea wa 2015 atoke nje ya 'system' iliyopo.
Na sidhani kuwa ni suala la nani atakuwa rais, bali chama gani kinaweza kututoa hapa tulipo!
Mkuu wangu katika hili kusema kweli nitatofautiana na wewe..Nitarudia kusema kwamba Wadanganyika bado kabisa hawajaelimika ktk elimu ya Uraia na siku zinakwisha..Na uloyasema hapo juu kwao ni miujiza ya Mussa kwa sababu wana njaa, wana shida na meli yetu inazama hivyo kila mtu leo yupo ktk kupoteza maisha kama asipopata boya ya kuelea. Hivyo sii rahisi kuupata UMOJA ktk hali hii na pengine sii rahisi pia kumpata rais unayemzungumzia..

Wananchi leo hii bado wanakatiwa umeme wanaenda kununua magenereta, wanalala kizani na wengine kuilalamikia Tanesco lakini wanalala kiza na kesho mwendo mdundo..Nchi haina maji bado wanachimba visima kila sehemu wasifikie kuiadhibu serikali lawama zote kwa JK ambaye bado anapendwa na kutetewa kwa madai kwamba wanaompa ushauri ndio hovyo. JK hana wasaidizi wazuri nakadhalika, hii ndio Tanganyika yetu.

Kina mama wajawazito na watoto wanakufa, migomo ya madaktari yaani yote haya yanakuonyesha wazi kwamba bado kabisa Wadanganyika hawajafikia mahala wakaiadhibu serikali kwa kukosekana vitu muhimu ktk maisha yao. Kuna msemo wanasema kama wewe huna sema wewe huna au maskini, sio watu wote maskini!..Wadanganyika wanaamini ktk UBINAFSI na hakika watapiga kura zao ktk UBINAFSI..

Mkuu wangu inatisha sana kuona hapa tulipofikia na hasa baada ya nchi kuuzwa..SIJUI na wala siwezi kusema mengi isipokuwa mwaka 2015 tutajifunza mengine mapya ama pengine kujitambua sisi ni wanyama gani ktk kundi la wanadamu.
 
URAISI si lele mama,si kili mtu tu anaweza kuwa raisi,MEMBE uyouyoyuko karibu na KIKWETE na pia aasimamia sera hizohizo DHOOFU NA DHALIMU ZA CCM ambazo ndizo kikwazo cha maendeleo ya wananchi iweje leo mtu kama uyo aongoze nchi???hkutokuwa na kashfa tu haitoshi bali ni kipi cha ajabu alichokifanya katika jimbo lake???CCM NA WASHIRIKA WAKE HAWAFAI KUONGOZA NCHI HII NA 2015 NDO KIFO CHAO!!!
 
Nadhani Mzee Mwanakijiji amewalinganisha kwa "usafi" Lowassa na Membe na amefikia hitimisho kwamba kama hoja ni CCM kuchagua mtu safi basi kwa kigezo cha usafi wa Ki- CCM basi mtu huyo ni Membe kwani ni yeye ambaye anaweza kuwa "safi" kwani kwa mtazamo wa Mzee Mwanakijiji Lowassa amechafuka na hawezi kuwa Mgombea atakayeweza kushindana na mikiki ya Kampeni kwani Umma wa Tanzania wanaamini kwamba yeye si msafi na ni FIsadi MKubwa au Papa kama anavyopenda kusema Prof: Lipumba au mzee Mengi.

Mzee Mwanakijiji hajasema kwamba Membe anafaa kuwa Rais bali anafaa kuwa Mgombea Urais kupitia CCM kuliko wenzie wote wanaotajwa. Kama kushinda au kushindwa hilo ni suala jingine kabisa linalohitaji mjadala wake!!
 
Back
Top Bottom