kiroba
JF-Expert Member
- Sep 10, 2011
- 324
- 114
Mzee mwanakijiji hapa umechemsha kabisa. Kama kigezo ni kashfa na wala si uwezo basi tunaweza kupata raisi ambaye atakuwa dhaifu sana kushinda hata huyu tuliyenaye kwa sasa. Kumbuka huyu tuliyenaye sasa wapambe wake walimnadi kuwa ni mtu safi hana kashfa za kutisha.Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"
CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.
Ni kweli?
Binafsi natamani raisi ajaye awe ana uwezo mkubwa sana wa kuongoza kwani atakuwa ana mambo mengi sana ya kutekeleza ukizingatia nchi yetu ipo nyuma sana kwa maendeleo. Huyu aliyepo sasa hajafanya mambo mengi sana, kwa hiyo ajaye inabidi akave na haya aliyeyaacha huyu wa sasa.
Kwa mantiki hii basi tusiangalie sana usafi wa mtu kwani kuwa safi bila kuwa na uwezo ni hatari sana kuwa na raisi wa namna hiyo. Inabidi awe na uwezo mkubwa sana wa kuwajibika kama raisi na pia awe mtu anayechukia sana rushwa.
Kama ni usafi basi atatufaa tena kama waziri ifikapo 2015 na wala si uraisi. Kumbuka ndugu yangu mzee mwanakijiji, uraisi ni mzigo mzito sana. Uraisi anahitajika mtu ambaye ni hodari na mchapakazi na pia jasiri sana wa kukemea maovu.
Mh Membe si mtu wa aina hiyo kabisa. Ni kweli unampenda sana mh membe lakini huna haja ya kumpigia debe awe raisi. Jaribu kuweka mbele maslahi ya taifa na upenzi weka kando kabisa. Hii ni nchi yetu sote, hivyo ni jukumu letu sisi kuipigania iweze kusonga mbele. Tulishakosea kwa huyu tuliyenaye kwa njia hii hii ya kuwalaghai wananchi kuwa wamchague kwani ni mtu safi. Sasa tunapiga kelele hana uwezo. Kuwa mtu safi haimaanishi kuwa basi wewe unaweza kuwa raisi. Uraisi unataka mtu safi na sifa nyingine za msingi nyingi sana.
Hitimisho langu mimi kama mtanzania ninayeipenda sana nchi yangu, mh membe hafai kabisa kuwa raisi. Kama ni uwaziri basi angoje 2015 atakayeingia madarakani ampe huo uwaziri.
Tuache ushabiki usio na tija kwa maslahi ya taifa letu. Tuijenge tanzania yetu kwa kuepeuka ushabiki na mapenzi kwa mtu au kikundi cha watu ili mradi tu anakupatia maslahi yako.
Je maslahi ya taifa nani anayapigania? Chukua hatua ndugu na amka katika usingizi huo mbaya na hatari sana kwa taifa letu.