Mh.mwanakijiji hakika pasipo kumumunya maneno Membe amekutuma,toa hiyo thread.
Kwa nini nasema hivyo mkuu wangu?.
1:Membe hakubaliki ndani ya CCM na hasa wale ambao watakwenda kufanya uchaguzi wa kumpata mgombea kupitia chama hicho,na kama kuna kosa ambalo amelifanya na kutokujipanga kwenye uchaguzi unaomalizika hivi sasa ndani ya chama hicho.
2:Lowasa ni mtu ambaye ni popula sana ndani ya ccm na hata wewe unalijua hilo,na hata kwenye uchaguzi huu unaomalizaika ametengeneza kura nyingi hilo halina ubishi mkuu.
kwa hiyo ka tathmini tu hiyo ya awali nadhani umeona ni namna gani ambavyo Lowassa atamshinda Membe,na nataka nikwambie kwamba hata mimi ukinishindanisha na Membe ndani ya CCM namshinda kwa sababu nina watu ndani yake kuliko yeye.
Naungana na yule aliyesema kwamba wewe ni mfuasi wake na humu umekuja kupima tu upepo,na nina hakika upepo utauona.