T2015CCM
JF-Expert Member
- Sep 13, 2012
- 7,930
- 990
Rais hatoki tena miji ya mwambao...safari hii ni zamu ya nyanda za juu, kaskazini na ziwa jitihada za kuumiliki u-rais mwambaoni safari hii hazita weza lbd kwa force.
unaota au
Rais hatoki tena miji ya mwambao...safari hii ni zamu ya nyanda za juu, kaskazini na ziwa jitihada za kuumiliki u-rais mwambaoni safari hii hazita weza lbd kwa force.
Mkuu Nsanu, jf was meant for ma gt, ila hata sisi watu wa kawaida tusio ma great thinkers pia tupo, utakapo kuwa kuwa mkubwa zaidi kidogo kiakili, nawe utakuwa great thinker hivyo nawe ndio angalau utanielewa namaanisha nini!.Hivi unaposema hayo maneno hapo ktk red huwa una maana gani? Aaaaaaggggggg
Kwa kweli mkuu umepoteza heshima yangu Kwako.
Time will tell,siku utakaposikia kuhusu huyu jamaa ndio utajua kuwa Tanzania ni nchi ya maajabu saba ya duniani.Hiki kinachoitwa kashfa ya fedha za Libya tumeisubiri muda mrefu lakini nafikiri huyo producer wa hiyo filamu mitambo yake imeungua na umeme wa Tanesco. Niwaambie hivi, and you can take this to the bank, Membe has what it takes to be the next President na kama kuna wanaodhani uadilifu siyo sifa ya uongozi basi labda mnazungumzia uongozi wa Freemasons au kwa TB Joshua. For once Mwanakijiji umeona mbali!
MM naomba nichakachue thread yako kama inavyoendelea kuchakachuliwa.
Mara nyingi natatizika sana kila ninaposoma habari za fulani ni best candidate.
Hapa ndipo nakubaliana na Mkandara kuwa elimu ya uraia bado ni tatizo kubwa sana.
Wenzetu wanaojua kuchagua viongozi huangalia kigezo kimoja hadi kingine:
Maadili ya mtu, misimamo yake kisiasa, anasimamia nini, mahusiano na wenzake, mahusiano na chama chake, ushiriki katikashughuli za kijamii, maadili yake, mahusiano kati yake na wananchi, mtazamo wake kuhusu nchi, historia ya utendaji wake, maamuzi aliyowahi kuayafanya huko nyuma, uthubutu katika kusimamia anachokiamini n.k.
Tunatakiwa twende mbali zaidi ya hapa pa kusema fulani atatusaidia.
Labda nitoe mifano kidogo, ni Membe aliyetuambia kuwa tumeibiwa katika Radar, ni Membe aliyekataa kutuambia nani ni wezi. Alichotaka ni ku-score political point kuwa pesa zimerudi! Sasa huyu mtu kimaadili unamweka kundi gani?
Nina nani miongoni mwetu anayejua misimamo ya Membe kuhusu masuala ya kitaifa?
Mfano wa pili, ni Lowasa huyu aliyetuambia hakuna wizi Richmond, ni Lowasa huyu aliyejiuzulu kwa dhambi anayosema hakuitenda, ni Lowasa huyu anayesema alifanya hivyo kuilinda serikali, ni Lowasa huyo asiyetuambia nani alibofoa Richmond hadi leo tunapata hasara. Ushujaa wa kusema huyu ni best candidate unakuwa katika misingi gani?
Ni nani anayeweza kunishawishi kuhusu uadilifu wa Lowasa hadi apewe ofisi kubwa kiasi hicho?Ni nani anayeweza kutumia vigezo ilivyoweka kumpa pasi Lowasa japo 60%?
Kama ni suala la kusema tu fulani anafaa basi mimi nasema Sophia Simba anafaa kama best candidate.
Msiniulize kwa vigezo gani kwasababu lengo ni kutaja tu.
...Kama ni suala la kusema tu fulani anafaa basi mimi nasema Sophia Simba anafaa kama best candidate.
Msiniulize kwa vigezo gani kwasababu lengo ni kutaja tu.
ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"
Magamba wasahau 2015
Enzi za uchaguzi ule wa picha ya mgombea mmoja upande mmoja na sehemu nyingine kuwekwa kivuli, hapo angeweza kuuchukua ki-urahisi kabisa. lakini katika siasa za sasa hivi zilizojaa uana harakati nafikiri amepoa sana hana mvuto hata wa kushawishi. Labda kura za kupikwa tu.Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho. Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"
CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.
Ni kweli?
Why blame in on one only?, kwa nini waliofuatia AHM, BWM na JMK nao wasipate sehemu yao ya blame?!. Usitumie kisingizio cha msingi dhaifu, hivyo nyumba dhaifu!, kama JKN aliacha msingi dhaifu, hao waliompokea kwa nini waliendelea kujenga kwenye ule ule msingi dhaifu na kuachwa hivi hivi, wakati walipaswa kwanza kubomoa huo msingi dhaifu ndipo wajenge msingi mpya imara ili nyumba yetu isimame imara?!.Siasa zetu bado sana, mtaji ni elimu dhaifu ya asilimia kubwa ya watanzania blame it on JKN trust me.
Mchambuzi ndiyo maana tumekuwa tunakemea mambo ya kufanya siasa ''unilaterally'.Mimi nadhani tunapoteza tu muda wetu mwingi sana kujadili majina ya wagombea wa CCM wakati ni dhahiri kwamba hata asimamishwe nani kwa tiketi ya CCM, chini ya kanuni ya sasa ya Mshindi ni Mshindi, atakayeshinda Uchaguzi Mkuu ngazi ya Urais 2015 ni CCM, kwa mfano hata mgombea wa CCM akipata 50.01% dhidi ya mgombea wa Chadema 49.99%, mshindi atakuwa ni CCM, labda kama katika kipindi kilichobakia Chadema watafanya juhudi za ziada katiba mpya ibadili Uchwara huu;
Vinginevyo ushindi wa Chadema utakuwepo zaidi majimboni. Ni muhimu tu katika kipindi hiki (hasa iwapo kanuni ya mshindi ni mshindi itabakia intact):
- Chadema wakaanza kujiandaa kisaikolojia juu ya uwezekano wa kualikwa kuunda serikali ya Umoja kutokana na Chadema kushinda viti vingi sana vya Ubunge, huku ikijua wazi kwamba itakuwa ni kula matapishi yake kwani ndoa ya Vyama Chadema imeikataa kama vile ni ndoa ya Jinsi Moja;
- Huku nao CCM waanze kujiandaa pia kisaikolojia kuwa na Rais ambae atapita uchaguzi mkuu kwa just above 50%, kwa mara ya kwanza katika historia ya chama hiki;
Ni muhimu pia Chadema isijidanganye na matokeo ya uchaguzi Zanzibar 1995, 2000, 2005, 2010 ambapo CUF inasemekena ilishinda mara zote; Hii ni kwa sababu kama ilivyokuwa kwa uwepo wa mabaki ya TANU bara, yapo mabaki ya ASP Zanzibar, na CCM ni ndoa tu ambayo Suala la yupi ni mke na yupi ni mume baina ya TANU na ASP, is very much open to debate;
My answer to your question and quote is entirely based on this this sentence of my post. Kwa maana hiyo nitajibu kuzingatia kipengele hicho tu or else correct me.Siasa zetu bado sana, mtaji ni elimu dhaifu ya asilimia kubwa ya watanzania blame it on JKN trust me.
Why blame in on one only?, kwa nini waliofuatia AHM, BWM na JMK nao wasipate sehemu yao ya blame?!. Usitumie kisingizio cha msingi dhaifu, hivyo nyumba dhaifu!, kama JKN aliacha msingi dhaifu, hao waliompokea kwa nini waliendelea kujenga kwenye ule ule msingi dhaifu na kuachwa hivi hivi, wakati walipaswa kwanza kubomoa huo msingi dhaifu ndipo wajenge msingi mpya imara ili nyumba yetu isimame imara?!.
P.
Wakati anaaga, alisema wazi, "kutenda kosa, sii kosa, kosa kurudia kosa!".Waliofuata wametumia ulemavu aliouwacha to advance their courses for their selfish purposes. Na sasa we have to pay the price, by motivating the young ones for the large part to see uozo wa CCM for what it is.
Ndio maana wenzake wazalendo wa vyama vyote wanajaribu kurekebisha makosa yake, kwani makosa aliyoyafanya hayakuwa madogo wachilia mbali kutowapa elimu ya haki zao za msingi watanzania.Wakati anaaga, alisema wazi, "kutenda kosa, sii kosa, kosa kurudia kosa!".
Yeye katawala kwa miaka 23, by 2015 tutatimiza miaka 30!, hivi kweli, is fair mtoto anazaliwa mpaka anatimiza miaka 30, amekosa haki zake za msingi toka kwa baba yake na mama yake ambao wako hai, na kuja kutupia lawama kwa babu yake aliyemwachia baba yake kila kitu miaka 30 iliyopita?!.
Mkuu Nguruvi3, hapa ndipo mimi ninalia napo!. Hizi nondo mnazozimwaga humu ni darasa tosha, niko kwenye mchakato wa kurudi rasmi hewani na program ya elimu kwa umma kwa njia ya "vox pop" ili baadhi ya hoja zinazomwagwa humu, ziwafikie watu wa mbali zaidi, hata wale wasio na access ya mitandao au magazeti.Elimu ya umma inahitajika sana!
Kama baba yako yupo, naye hakusomesha wewe eti kwa vile na yeye hakusomeshwa na baba yake ambaye ndie babu yako!, kumlaumu babu yako marehemu, kwa makosa ya kutomsomesha baba yako, na kujustify ndio sababu ya wewe kutosemeshwa, doesn't help!. Wewe mtoto unatakiwa ubanane na baba yako!, leave your late grand alone!. Umenikumbusha story ya Kalumekenge aliyekataa kwenda shule!.Ndio maana wenzake wazalendo wa vyama vyote wanajaribu kurekebisha makosa yake, kwani makosa aliyoyafanya hayakuwa madogo wachilia mbali kutowapa elimu ya haki zao za msingi watanzania.
Kumbuka ni wanagapi waliokuwa wana elimu ya hadhi yake wakati Tanganyika inapata uhuru, kuwa mkweli na wangapi leo wana elimu ya hadhi yake. Point hapa ni kwamba viongozi wengi leo wenye madaraka wamepata elimu yao chini ya mwalimu, chini ya chama kimoja na wakijengwa kutetea sera za chama kimoja. Walichojifunza hawa watu ni kutumia miguvu ya kujilinda chini ya mwalimu wao 'JKN' lakini si uzalendo wa taifa lao ambao aliufikiria yeye.
Since walikuwa chini ya uongozi wake it says he did not just fail the social but his future leaders, unaona ndipo hapo kazi yetu ya kurekebisha makosa yake ambayo ni mengi, dont let me go into his economical policies, the guy failed us miserably. usiku mwema