Hizi pongezi Kwa Rais Samia zina nini nyuma yake kama sio kumbeza na kutweza utu wake?

Desprospero

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
887
2,201
Imezoeleka Rais Mpya aliyeko madarakani kuadhimisha siku 100 Ikulu, utaratibu ambao nchi nyingi zimeiga kutoka Marekani. Baada ya hapo Rais anaachwa kuchapa kazi.

Hata Joe Biden baada ya zile siku 100 hatukusikia tena akipongezwa Kwa mwaka mmoja au miwili au vinginevyo. Siku 100 imewekwa mahuksusi kwamba inatosha umma kufahamu mwelekeo, mtizamo, dira na visheni ya Kiongozi huyo na si vinginevyo.

Kama ni pongezi kila baada ya muda fulani basi tungekuwa tunatoa pongezi kila mwezi au miezi sita. Kwa maoni yangu wanaokimbilia kumpongeza Samia kuongoza Kwa miaka miwili ama ni ambao hawakuamini kwamba mama ni jembe na anapiga kazi au wanalo lao jambo kwamba imekuwaje akamaliza miaka miwili?

Tuachane na hizi pongezi za kinafiki zenye husda ndani yake na hila Kwa mbali. Samia piga kazi hata kama walamba asali wamekuzunguka na joto jingi la upigaji kupitia miradi bunifu hewa kama lile la kuwafunda Arusha. Nadhani umeletewa bili "ukafurahi na roho yako'.

Hivi kama Hadi Bashiru Ally, Prof. Kabudi, Job Ndugai, Ditto James, Bernard Kalimani, Charles Kitwanga na Bashite wanakupongeza kutimiza miaka miwili madarakani hushituki?

Kiongozi Mao Ze Dong wa China aliwahi kusema, "ukiona adui yako anakusifia kufanya jambo fulani achana na jambo hilo haraka sana, ni hatari. Na ukiona anakupinga kufanya jambo, basi lifanye
 
Wanasiasa wa Tanzania ni wachumia tumbo sio CCM wala upinzani hapo wamelipwa fedha za umma anashangilia viazi vitamu hao

USSR
 
Back
Top Bottom